Serikali na Polisi sasa waanze kujibu uzuri madai na tuhuma zinazorushwa mitandaoni na Vyombo vya Habari vya kimataifa

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,501
22,351
Mitandao ya kijamii ni eneo pana na lenye kuweza kuwekwa picha mbambali za video iwe za miaka ya nyuma, miaka hii au hivi karibuni.

Kwasababu la kiusalama inawezekana kabisa kuzuia mitandao isiwezeshe video za namna hii kutumika kueneza uchochezi na uvunjifu wa amani katika nchi yetu bila kuwezesha kupatikana ushahidi wa video hizo

Picha na video za zamani zimeweza kutumika katika mitandao ya kijamii katika nchi kadhaa na nchi hizo waliweza kubaini kuwa picha na video hizo zilikuwa ni za uongo

Kwa mtazamo wangu ni kwamba serikali ina uwezo kabisa wa kugharamia teknolojia ambayo itaruhusu mitandao kuendelea kutumika wakti wa uchaguzi kwa kuzuia au kuchuja habari na ujumbe usofaa na wenye lengo la kuleta taharuki kwa jamii ya watanzania

Lakini licha ya hilo, serikali ya Tanzania na vyombo vya usalama vinawajibika kujibu tuhuma zozote na vielelezo vya picha na video mbalimbali zinazozagaa mitandaoni ambazo zinatumika kipropanda

Kwa mfano, picha na video za watu walokufa kuzikwa imewezekana kusambazwa mitandaoni na hadi kufika katika vyombo vya habari vya kimataifa lakini majibu ya jeshi la polisi yamekuwa kuwa "hakuna kitu kama hicho".

Mpaka hivi sasa serikali haijajibu tuhuma za kuzima mitandao ili kufanya maovu ya kuiba kura na kubinya shughuli nzima za kidemokrasia na ukimya wake waweza kuhalalisha madai hayo.

Pia hadi sasa bwana Robert Amsterdam akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni amedai kuwa na ushahidi wa mauaji kule Zanzibar na ushahidi wa kura feki zilizokuwa tayari zimepigwa.

Ilitegemewa kwamba ofisi ya msemaji mkuu wa serikali kupitia TCRA ingekuwa iko makini kuhakikisha inasoma yanoandikwa na yanotumwa mitandaoni na kujibu tuhuma hizo kwa vyombo vya habari vya Tanzania na vile vya kimataifa ikiwemo Aljazeera ambayo imekuwa ikifuatilia mchakato mzima wa uchaguzi wa mwaka huu.

Serikali ina sheria yake ya mitandao ambayo ilipitishwa miaka mitano ilopita kwanini isitumie sheria hii kuwadhibiti wale wanaokiuka sheria hii kwa kufuatilia simu zao zinazotumika kutuma picha mitandaoni.

Mfano wa matumizi ya sheria hii kiufanisi ni kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa vijan amabo walitoa kauli za matusi kwa kiongozi wa nchi na wakahukumiwa.

Pamoja na mitandao kuzimwa, bado mitandao ya kijamii iliweza kuendelea kurusha video na picha mitandaoni zinazoonyesha watu walouliwa huko Zanzibar na mabeki matupu ambayo yanasadikiwa kuwa yalitumika kubeba kura feki.

Isitoshe kule Zanzibar kituo kimoja cha televisheni binafsi ambacho hutumia mtandao wa facebook kiliweza kurusha video za kuwepo maandamano, picha za watu walojeruhiwa na ghasia na pia kuzirusha video hizo mitandaoni na pia kwenda nje ya nchi.

Ningependa kushauri kwamba kwenda mbele serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mambo ya nje, msemaji mkuu wa serikali na jeshi la polisi wajifunze kujibu tuhuma na kuelimisha wananchi.

Hii pia inahusisha utaratibu wa kuwajibu watu kama Robert Amsterdam ambae amekuwa akiongoza kueneza sumu ya chuki dhidi ya taifa letu.

Hii itasaidia kueleza kwamba hizi video au picha zilizosambazwa mitandaoni kuhusu mauaji kama ilivyoelezwa na chama cha ACT ni uongo na kwamba zinakusudia kuleta mtfaruku katikajamii wakati wa uchaguzi.

Tuondoe nadharia kuzibwa midomo kwamba chombo cha ndani kikirusha video na picha hizo au habari za kuwepo mauaji Zanzibar, basi mara moja kinakumbana na sheria ya mitandao na vyombo vya habari.

Vyombo vya habari vya kimataifa kama New York Times, BBC na Aljazeera vimekuwa vikiripoti habari hizo siku moja kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Hivyo serikali ya Tanzania ilipaswa kuviandikia barua ya malalamiko vyombo hivyo kwamba vinaripoti habari ambazo si za kweli.

Kuvijibu vyombo hivi serikali inapaswa kusema kuwa hizo picha ni zipi, je watu 10 walouawa ni kweli? na je, walotuma video hizo niwatu wa aina gani?

Serikali isikae kimya sana imekuwa kimya mno hadi kuogopa kumruhusu raisi Magufuli asiendelee kuwasiliana na wafuasi wake katika mtandao wa twitter.

Serikali iache uoga iwe tayari kukabiliana na hekaheka za mitandaoni na iwe inafanya "engagement" kwa polisi, msemaji wake, wizara ya mambo ya ndani na wizara zake zote kuwasiliana na watanzania wote jambo linaloweza kuwapa imani watanzania kwamba wappo salama na kuwawezesha kuripoti masuala yote mabaya.

Pale penye kuhitaji ufafanuzi serikali ijitokeze kifua mbele kujibu kwa uwazi na kwa kujiamini.

Kitendo cha kukaa kimya kinaendelea kulea kidonda ambacho kikija kuwa ni kidondandugu itakuwa vugumu kukitibu.

Dah!! haya mambo mtu waandika kwa harakaharaka lakin mtanielewa wakuu.
 
Unataka kuhalalisha unyama huu kwa kuishauri serikali itafute namna ya kuzuia video zisitumwe mtandaoni? Kwamba vyombo vya nje vionywe? Kwamba serikali izikane video za watu waliouawa Zanzibar? Kwamba tv zilirusha video hizo zishughulikiwe?

Hivi wewe unayasema haya kwasabbb tu unafaidika na udhalimu huu? Ficha ujinga wako huu kwa kukaa kimya.
 
Hutaki kuamini serikali imezima mitandao ili wafanye hujuma zao kwenye uchaguzi, unasubiri serikali ikwambie tatizo hilo lilitokea bahati mbaya likawa nje ya uwezo wao, kwanini litokee wakati huu wa uchaguzi tena likitanguliwa na ile kauli ya "ningekuwa na uwezo ningetuma malaika wazime mitandao"?

Kweli mahaba hupofua akili.
 
Fikra za kidikteta. Ukweli siku zote utakuwa ukweli kama ilivyo kwa uongo. Haiingii akilini kwamba mtu auliwe nduguye mbele ya macho yake halafu anyamaze Kimya. Mawazo ya kibabe.
 
Awamu ya 5 wameua somo la Kiingereza na kuwakataza watu kutumia ki English sasa watawezaje kuufahamisha ulimwengu ukweli kufuatana na simulizi zao za 'uhakika' toka vyombo vyao vya usalama na idara zake
 
Mtoa mada una uhakika na maisha pasi kujua kesho yako endapo tutapata kiongozi aina ya PK, vinginevyo andiko lako ni zero maana uthibitisho wa video na picha zoote toka Zanzibar zimechukuliwa kwa wakati na muda muafaka, so utetezi wako ni 🍺!!
 
Back
Top Bottom