Serikali Kufufua Usafiri wa Reli ya Kati Kiwango cha META GAUGE Kutoka Dodoma Mpaka Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961

SERIKALI KUFUFUA USAFIRI WA RELI YA KATI KIWANGO CHA META GAUGE KUTOKA DODOMA MPAKA SINGIDA

"Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua usafiri wa Reli kutoka Dodoma kwenda Singida? - Mhe. Martha Nehemia Gwau, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida

"Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) ina mpango wa ufufuaji na ukarabati wa miundombinu ya Reli ya Kati yenye kiwango cha Meta Gauge. TRC inaendelea na ukarabati na uboreshaji wa njia kuu kutoka Dar es Salaam - Isaka ambapo kwa awamu ya kwanza uboreshaji umefanyika kutoka Dar es Salaam hadi Tabora. Awamu ya pili Serikali ina mpango wa kuboresha kipande cha Tabora mpaka Isaka ikiwemo ukarabati wa kipande cha Dodoma - Manyoni kwa maeneo yaliyobaki ukarabati wakati wa utekelezaji wa awamu ya kwanza. Vilevile, Serikali inafanya tathmini ya ukarabati wa njia ya Reli ya Manyoni - Singida ili kuimarisha shughuli za kiuchumi kupitia usafiri wa Reli kwa kuunganisha ukanda huo" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Je, ni lini Serikali italipa fidia kwa wananchi waliopisha Maeneo yao kwaajili ya ujenzi wa SGR ambao ni wananchi wa Halmashauri ya Itigi na wananchi wa Halmashauri ya Manyoni? Ni lini Serikali italipa Service Levy kutokana na ujenzi wa Reli ya SGR kwa hizi Halmashauri za Itigi na Manyoni ambazo zimepitiwa na Reli ya SGR?" - Mhe. Martha Nehemia Gwau, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida

"Mfumo wa utoaji Ardhi Katika eneo umekuwa ukienda sambamba na kulipa fidia. Maeneo ambayo hayajalipwa fidia kwa sasa Maeneo ambayo tuna uchimbaji wa malighafi ya ujenzi ikiwemo ni pamoja na Mtambuka Reli, Centre pamoja na Milembela. Maeneo haya yataendelea kulipwa kulingana na hatua za Uthamini zitakapokamilika" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Mwaka 2023 Wizara ya Uchukuzi ilifanya vikao na Halmashauri ya Itigi na Manyoni, baada ya kukubaliana ikaonekana kwamba wanatakiwa kulipwa Shilingi Bilioni 1.5 kwa kila Halmashauri. Mpaka sasa wameshalipwa Shilingi Milioni 214 kila mmoja na malipo mengine yataendelea kulipwa kulingana na jinsi tutakavyokuwa tumechimba malighafi" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-05-03 at 19.30.14.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-03 at 19.30.14.jpeg
    32.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-05-03 at 19.30.14(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-03 at 19.30.14(1).jpeg
    35.7 KB · Views: 4
  • KIHENZILExcsder.jpg
    KIHENZILExcsder.jpg
    46.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom