SoC03 Serikali iunde kanzi data moja itakayounganisha Wizara na Taasisi zake zote

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
2,154
3,243
UTANGULIZI.
Serikali imekuwa ikikumbwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ambapo ubadhirifu huu unasababishwa kwa kiwango kikubwa na maamuzi mabovu yanayofanywa na wizara ama taasisi zake kwa makusudi ili kutimiza adhma ya ubadhirifu, kuna maamuzi mengi yanafanyika katika wizara mbalimbali na ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri mkuu haijui.

Katika ngazi za wilaya na mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mikoa nao wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baadae yanaigharimu serikali kutokana na upotevu wa fedha kupitia miradi hewa ama miradi isiyoendana na gharama husika.

Sababu inayopelekea ubadhilifu huu ni usimamizi mbovu wa mali za umma unaosababishwa na mifumo mibovu ya kiserikali katika kusimamia fedha za umma, ununuzi wa mali za serikali nk.

Kila wizara,kila taasisi ya serikali kwa sasa ina kanzi data yake ambayo haiwezi kuingiliwa, kwamba kila taasisi kwa sasa ina uhuru wake wakufanya mambo yake kiholela holela, na ndio maana katika kila taasisi ya serikali kuna ubadhirifu mkubwa wa mali na fedha za umma, imefika sehemu mpaka baadhi ya viongozi wanajimilikisha mali za umma kuwa za kwao na familia zao.

NINI KIFANYIKE.
Ili kupunguza ubadhilifu katika taasisi, na wizara zote, serikali iunde Kanzi data moja ambayo itatumiwa kuanzia ngazi ya wilaya mpaka serikali kuu,kutakuwa na mipaka ya kiuendeshaji kulingana na ngazi,kiongozi wa juu ataweza kuingia katika mfumo wa ngazi ya chini kwa kuwa uongozi wa juu unamamlaka kwa uongozi ngazi ya chini,mfano mkuu wa mkoa ataweza kuingia katika mfumo wa wilaya yoyote iliyopo katika mkoa wake na kukagua taarifa zote kama zipo sawa,lakini mkuu wa wilaya hata weza kuingia katika mfumo wa wilaya nyingine ama mfumo wa mkoa,mkuu wa mkoa hataweza kuingia katika mfumo wa mkoa mwingine,waziri wa TAMISEMI ataweza kuingia katika kila mfumo wa mkoa na mkuu wa mkoa hataweza kuingia katika mfumo wa TAMISEMI nk.

Rais,makamu wa Rais na waziri mkuu wataweza kuingia katika mfumo wowote ule mpaka ngazi ya chini kabisa,pamoja na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG,CAG hatakuwa na uwezo wa kuingia mfumo wa Rais tu,ila sehemu nyingine zote ataingia.

NAMNA KANZI DATA UUNDWE.
Kanzi data iundwe kwa kuzingatia ngazi za ki-utawala,kuwepo na ngazi ya Wilaya,Mkoa,Wizara,Mwanasheria mkuu wa serikali,Waziri mkuu,Makamu wa Rais, Rais na CAG.

Katika sehemu ya wilaya humo ndani utapatikana uongozi wote wa wilaya,kadhalika katika mkoa kutapatikana uongozi wote wa mkoa ,katika kila ngazi miradi yote iwe imeorodheshwa katika sehemu ya miradi na taarifa zake zote za kina kuhusu kila mradi,pia kuwe na sehemu ya ugavi inayoonesha tenda zote na manunuzi yote yaliyofanyika ndani ya wilaya husika.

Katika ngazi ya mkoa wilaya zote zionekane humo,uongozi wake,miradi yote na taarifa zote kuhusu miradi ndani ya mkoa husika,pia kuwe na sehemu ya ugavi ikionesha taarifa zote za ugavi ndani ya mkoa husika .

Katika wizara zitaonekana wizara zote za serikali na uongozi wake,taasisi zote zilizopo chini ya wizara husika na taarifa zote za miradi zinazohusu wizara husika,taarifa za utendaji kazi za wizara husika,taarifa zote za fedha za wizara husika na taarifa zote muhimu zipatikane hapo.

Katika sehemu ya mwanasheria mkuu hapo wapatikane wanasheria wote wa ngazi zote za serikali,mikataba yote katika ngazi zote za serikali iliyoidhinishwa na wanasheria wa ngazi zote,na mikataba kutoka wizara zote inayohitaji kuhidhinishwa nayeye ili mikataba yote mikubwa iweze kufika ofisi ya Rais,Makamu na Waziri mkuu ni sharti ipite kwakwena iidhinishwe,na aipeleke sehemu husika.

Sehemu ya waziri mkuu ,makamu wa Rais na Rais ioneshe ngazi zote za serikali,na taasisi zake,iruhusu kuingia sehemu yeyote ile,ziwe na sehemu maalumu ambazo zitaonesha miradi yote iliyoidhinishwa na inayosubirir kuidhinishwa,kuwe na sehemu inayoonesha mikataba yote iliyohidhinishwa na inayosubiri kuidhinishwa,iweze kuonesha taasisi zote muhimu za serikali na taarifa zake zote muhimu.

Sehemu ya CAG yeye aweze kuona taarifa zote za kihasibu katika ngazi zote za serikali.

UTENDAJI KAZI WA KANZI DATA .
Kazi kubwa ya KANZI DATA iwe ni kuhakikisha ,maamuzi yote yanafanyika katika uwazi na yanafuata utaratibu uliowekwa.

Kuanzia ngazi ya wilaya, mkurugenzi ama, DAS na wengine masuala yote ya chini yataidhinishwa na wao kisha mkuu wa wilaya,baada ya mkuu wa wilaya kuidhinisha taarifa itatumwa kwa mkuu wa mkoa ambaye atakuwa na mamlaka ya kuidhinisha ama kubatilisha kwa kuainisha sabababu,taarifa haitaweza kupanda ngazi ya juu kama haijaidhinishwa na hatua ya chini, taarifa ikisha idhinishwa na mkuu wa mkoa basi itaweza kuonekana kwa ngazi za juu kama wizara zinazohusu taarifa hiyo, Mwanasheria mkuu wa serikali na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali,kwa kuwa taarifa zinazohusu miradi zinakuwa na mikataba ,mikataba hiyo iweze kumfikia mwanasheria mkuu wa serikali,kwa ajili ya rejeo na uhakiki.

Katika wizara zote taarifa hasa za miradi yote, manunuzi na masuala mengine ya fedha, itakuwa ni lazima yaidhinishwe na Rais na ni lazima yawe yamepitiwa na mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais ndiye atakuwa mtu wa mwisho kuidhinisha mikataba yoteiliyopitishwa na mwanasheria mkuu wa serikali ikitokea ofisi ya Rais haijaridhia basi ataukataa kupitia mfumo na kuacha sababu za kuukataa na kwa wakati huo atakakuwa ameshawasiliana na washauri wake na wahusika wa chini,ikitokea tu umekataliwa basi taarifa zote za chini zinatenguliwa na kuondolewa katika mtiririko mpaka pale zitakapo rekebishwa kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na ofisi ya rais.

Uidhinishwaji ama ubatilishwaji wa kila hatua utahushisha sahihi ya kidijitali kupitia skana maalumu sabambamba na alama za vidole kuzuia muingiliano.

Taarifa zote za juu zinaweza kuhizinishwa na Rais ,Makamu au Waziri mkuu kulingana na wapi imetoka,taarifa zinazowez kuidhinishwa na makamu wa rais ni zile zinazohusu ofisi yake,kazalika na waziri mkuu atahizinisha zile zinazohusu ofisi yake.

Kanzi data iweze kuweka hesabu zote kulingana na ngazi husika,hazina wataizinisha fedha kutoka kulingana na taarifa waliyopewa na hawataweza kuizinisha tofauti na taarifa kutoka juu .

FAIDA YA KUTUMIA KANZI DATA MOJA.
  • Taarifa zote zinakuwa wazi.
  • Uizinishwaji wa mikataba na fedha utafuata utaratibu kwa lazima.
  • Ubazilifu ngazi ya chini hautakuwepo maana taarifa zote zitakuwa wazi mpaka ofisi ya Rais.
  • Ufuatiliaji wa taarifa za maendeleo ya miladi utakuwa wazi na haraka maana kila taarifa itakuwa ni lazima iwekwe katika kanzi data
  • Hakutakuwepo na uchakachuaji katika taasisi za kiserikali kama TRA, Bandari na kadhalika maana taarifa zote zitaonekana na kufuatiliwa kupitia kanzi data kwa urahisi.
 
Back
Top Bottom