Serikali ipige Marufuku Ajira za kujitolea. Ni Mbinu mpya ya kinyonyaji, dhulma na uhujumu uchumi wa Nchi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,541
64,032
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hatuwezi kuwa na Taífa la matapeli, wanyonyaji na dhulma tupu. Alafu serikali ibariki unyonyaji huo.

Inashangaza kumwona Kiongozi akishadadia na kuhamasisha Vijana wajitolee, wanyonywe, wadhulumiwe, wapotezewe Muda waô. Kwa kweli inasikitisha Sana

Kama ingekuwa Mimi ndiye Kiongozi, ningepiga MARUFUKU Kwa Kampuni, taasisi, na shirika kuchukua Vijana ili wajitolee katika makampuni Yao. Kwa Sisi Watibeli huo ni utapeli, wizi, dhulma, UHUJUMU UCHUMI.

Vijana Kwa nini wajitolee? Yaani kijana asome Miaka na Miaka anamaliza chuo alafu ahitaji tenà kujitolea ili apate uzoefu.

Ukitaka kujua utapeli ulivyo, waulize itamchukua Muda gàni Mtu kupata uzoefu? Miaka miwili, mitatu au mitano? Je kisayansi Mtu anapata uzoefu wa kitu Kwa Muda gàni?

Nini kinamfanya Mtu awe mzoefu wa Jambo Fulani. Bila Shaka uzoefu unaletwa Kwa kufanya Jambo Fulani mara Kwa mara. Je hiyo mara Kwa mara ni Muda gàni?

Nimemaliza Miaka kadhaa iliyopita.

Kuna Vijana wenzangu niliomaliza nao waliona wajitolee nikawaambia mnapoteza Muda wenu.
Walibisha. Huu Mwaka unaenda kama siô wa Saba Basi wasita. MTU anajitolea Miaka Sita

Alafu Huko wanapojitolea zikitokea Ajira hawaajiriwi wanaojitolea wanaajiriwa Watu Wengine Kwa sababu hata kwèñye usaili ukifika wanaojitolea siô ajabu wakakalishwa na wale ambao ni fresh from school au wale ambao hawajawahi kujitolea.

Mbaya zaidi wakiona Umefanya Kazi Miaka mitatu hivi wanatafuta namna ya kukuondoa Kisha wanaleta Watu Wengine wa kujitolea.

Pumbavu! Hivi hii dhulma mnayotumia jasho la Watu Wengine kujijenga na kujenga familia zenu mnajua ni Laana kwèñye vizazi vyenu.

Nami Mtibeli nawalaani wôte ambao hutumia jasho la Watu Wengine kujitajirisha pasipo kuwapa Watu hao Haki zao. Walaaniwe waô na Watoto waô, na wajukuu zào na vizazi vyao.

Watibeli tunajua kuwa, Mtu anatakiwa kujitolea kwèñye Jambo ambalo siô biashara Yaani Jambo ambalo haliingiza faîda ya Kifedha au kimali.

Mfano, Mtu anaweza kujitolea Damu Ikiwa damu hiyo haitauzwa.. Hiyo tunaita kujitolea. Lakini sio Watu wanatoa damu alafu damu hiyo iuzwe. Huku siô kujitolea.

Mfano, Mtu anajitolea kufundisha katika Shule ya Yatima wasiolipa Ada. Yaani Hakuna biashara inayofanyika. Huko tunaita kujitolea.

Huwezi kuwa msomi mzima uliyehitimu tenà chuo kinachoitwa chuo Kikuu. Alafu ATI ulifauli kidato cha nne na Sita alafu unasema unajitolea kwèñye Kampuni Fulani linalofanya biashara na kuingiza mamilioni ya Pesa lakini wewe unajitolea. Hivi wewe kama siô msukule au ndondocha ni nini?

Nilishawahi kuwaambia hata Kanisani waimba Kwaya lazima walipwe mishahara, kauli ya kujitolea ni utapeli, unyonyaji na dhulma kwa wanyonge wenye akili mgando, watumwa na msukule. Anayekuambia ujitolee mwambie ajitolee yeye.

Jambo lolote ambalo linaingiza faida kiuchumi yàani àmbalo ni biashara alafu MTU anakuambia ujitolee Jua Mtu huyo kakudharau na wéwe ukilifanya umejidharau.

Ni Bora ufe, Bora úwe Maskini kuliko ugeuzwe msukule, ndondocha au ujitolee.

Taikon nawaambia Huko tuendako kama hatua madhubuti hazitachukuliwa Taífa Hili Vijana wake wengi watakuwa misukule, mandondocha, na Watumwa.


HASARA ZA KUJITOLEA

1. Kujitolea ndiko kunapelekea ukosefu wa Ajira.
Mtu ataajiri vipi Wakati Watu wakujitolea wàpo?
Ukosefu wa Ajira athari Zake zinajulikana

2. Watu kulipwa mishahara Duni.
Mishahara ya kipunda. Yaani Fanya Kazi nikupe Pesa ya Kula kama punda àmbaye HUFANYA Kazi alafu apewe majani na Maji Basi! Sasa wewe si punda tuu Bora hata ungekuwa pundamilia.

Fikiria Daktari (medical doctor) ati analipwa Laki tatu unajua nilishangaa Sana nilipokutana na ràfiki yàngu yupo dhoofu ilhali. Yaani Mtu asome degree alipwe Laki tatu kweli?

Sijazungumzia walimu wa degree wanaolipwa Laki na Nusu hulu kwèñye Shule za binafsi.
Huo utapeli, dhulma, unyonyaji.

Kujitolea kunawafanya Wamiliki wa biashara kuwalipa wafanyakazi mishahara midogo. Sisi Watibeli tunaita mishahara ya Mbwa.

Ni akheri kijana ujiajiri mwenyewe au uende ukaishi porini ukale matunda kama hayawani usubiri Siku zako za Kufa kuliko uwekwe kwèñye banda na kufanyishwa Kazi kama punda.

3. UHUJUMU UCHUMI
Kujitolea ni uhujumu uchumi wa Raia pamoja na nchi Kwa ujumla.

Niliwahi andika kuwa, ni Bora tusiwe na kiwanda hata Kimoja kuliko kuwa na viwanda au makampuni au taasisi au mashirika yanayogeuza Watu wetu kuwa misukule.

Unapomwambia Mtu ajitolee unahujumu Ñguvu Kazi ya nchi.

Huyo Mtu Kama umeshindwa kumuajiri Kabisa bora umuache yeye atajua namna ya kuishi. Lazima azalishe tuu kwani hatakubali Kufa.

Unahujumu Muda wa Vijana.
Unahujumu serikali Kwa sababu serikali haipati Kodi kutoka Kwa huyo Mtu anayejitolea.

MTU anajitolea halipo Kodi, Hana Bima yoyote Ile. Yaani ni kama Mnyama Fulani hivi aliyevishwa Nguo. Huu ni udhalilishaji katika historia ya Dunia.

4. Kutawaliwa na Watu wa Nje.
Hakuna Laana mbaya kama mgeni kumtawala mwenyeji hata Wanyama Hilo hawakubali.
Lakini kujitolea hupelekea Wageni kuzidi Kutumia Ñguvu Kazi ya Taífa letu kuongeza utajiri waô.

Watu wanatoka arabuni, India Huko nje wanakuja huku Tanzania, wanalipa Watu mishahara ya Laana kinyume na Haki.

Mgeni mwenzao wanampa Vizuri ila mwenyeji Kwa vile ni zumbukuku anaambiwa aidha ajitolee na kama Sheria ikifuatwa kiasi Basi watamlipa kimshahara kidunchu. Dharau na kudhalilika Kwa wananchi wetu kunaongezeka

Siô ajabu hata wachezaji wa Mpira wa nje wanalipwa Pesa ndefu kuliko wachezaji wetu wa ndàni ati Kwa kisingizio kuwa ati wa nje Wana kiwango kuliko wetu. Hivi Mtu anayekuambia hivi unasubiri nini Kumtia hata kibao kikali anyamaze.

Hivi Taífa la nne Kwa idadi ya Watu Afrika lenye Watu takribani Milioni 65 likose wachezaji wa kiwango cha Kina Chama au Azizi Ki. Kweli?

Aiseeh! Laana ni mbaya Sana.Alafu Watu Wanaona kawaida tuu.

Tunahitaji wanasiasa na viongozi weñye AKILI yenye kujua na kuthamini Taífa letu na Watu wake.

Tunahitaji viongozi weñye HAKI na kujua watañzania wanauwezo wa kufanya Kazi íwe kujiajiri au kuajiriwa na siô KUJITOLEA.

Tunahitaji Watu weñye kupenda Ukweli kuwa nchi yetu inawatu Aina zote. Hivyo kusema Vijana hawana uwezo ni dalili ya kuonyesha msemaji ni Mwongo na ana hila ya kutaka kuhujumu nchi yetu

Serikali ifute Kabisa kujitolea Kwa Vijana kwèñye sekta Ambazo zinafanya biashara na kujipatia faîda. Hiyo tunaita dhulma, unyonyaji na usukule.

Mimi Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Screenshot_20241020-143812~2.jpg
 
  • P.O. Box 2890 Dodoma,Tanzania, Kazi Street,Government City, Mtumba
  • Mobile: 0655544489.
  • 1 Barabara ya Julius Nyerere, Chamwino, S.L.P. 1102, 40400 DODOMA
  • 026-2961500.
  • Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
    Wizara ya Katiba na Sheria
    Mji wa Serikali, Mtumba
    S.L.P. 315,
    40484 DODOMA.
  • Bandiko lako zuri sana kama utaweza liandike kwa mfumo wa barua kupitia anuani hizo juu alafu tulitume Kwa email hizi chini unaweza ukawa mkombozi wa wengi kupitia mawazo yako
Ps@kazi.go.tz
Press@ikulu.go.tz
km@sheria.go.tz
 
  • P.O. Box 2890 Dodoma,Tanzania, Kazi Street,Government City, Mtumba
  • Mobile: 0655544489.
  • 1 Barabara ya Julius Nyerere, Chamwino, S.L.P. 1102, 40400 DODOMA
  • 026-2961500.
  • Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
    Wizara ya Katiba na Sheria
    Mji wa Serikali, Mtumba
    S.L.P. 315,
    40484 DODOMA.
  • Bandiko lako zuri sana kama utaweza liandike kwa mfumo wa barua kupitia anuani hizo juu alafu tulitume Kwa email hizi chini unaweza ukawa mkombozi wa wengi kupitia mawazo yako
Ps@kazi.go.tz
Press@ikulu.go.tz
km@sheria.go.tz

Sawasawa
 
Back
Top Bottom