Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,420
- 3,480
Kauli zozote za kishujaa kuhusu muungano ni nakili kutoka kwa waasisi wa mataifa haya mawaili. Huenda labda kwa wakati huo muungano ulikuwa na manufaa lakini sio sasa. Kama nyumba ya zamani inaweza kuvunjwa na kujengwa mpya inayoendana na wakati, basi hata muungano kwa sasa ni jumba la kale linalotakiwa kuvunjwa na kujengwa upya kwa mahitaji ya sasa.
Kama wazanzibar walio wengi wanaunung'unikia muungano basi kuna hatari kubwa kizazi kijacho kikaja kuingia vitani kudai uhuru wao. Yapo mengi ambayo wazanzibar wanaamini muungano unawakosesha.
Kwa mfano Zanzibar wanabendera lakini bendera yao haitambuliki popote zaidi ya wao wenyewe. Zanzibar ilikuwa nchi na sio Kijiji kwa hiyo Zanzibar ilipaswa kuwa na kiti kwenye mabaraza yote ya umoja wa Afrika! Kwa sasa hawana.
Zanzibar hawana muwakilishi hata katika mashindano ya kimataifa, Zanzibar kama wanaona muungano hauna manufaa tena kwao tusiwalazimishe. Ndoa yoyote huwa inavunjwa kwa hiyari serikali ione umuhimu wa kuruhusu kura ya maoni, ili wazanzibar waamue kwa sababu kizazi kilichopo sasa sio kile Cha mwanzo mwa 1965.