Serikali ifanye nini ili uchumi wetu uipiku Kenya na mataifa yenye uchumi mkubwa kuliko sisi?

Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi na fulsa nyingi kwa nchi za afrika Mashariki.Tuna eneo kubwa la ardhi inayoweza kutumika kwa kilimo na ufugaji,tuna bahari, maziwa na Mito yenye samaki wa aina mbalimbali,tunayo madini ya aina mbalimbali nk.Karibu asilimia 60 ya wananchi wanajishughulisha na kilimo Cha kujikumu (njaa) na siyo kilimo biashara.wakulima wetu wanapambana Sana kutaka kufanya kilimo Cha kisasa na chenye Tija lakini wanakwamishwa na nyenzo za kufanyia kazi,(tractor au power tiler),pembejeo,miundo mbinu ya kusafirishia mazao kutoka mashambani na kufikisha sokoni bidhaa /mazao Yao au viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani nk.Hali ilivyo ni kwamba vijiji bado hawana wataalamu wa kilimo au mifugo na wakulima bado wanatumia majembe ya mikono ,mbolea au viatifu havipatikani kwa wakati/ havitoshelezi mahitaji ya wakulima.Bado kilimo chetu kinategemea mvua badala ya kuanza scheme za umwagiliaji,kilimo Cha kutegemea jembe la mkono na mvua,inakuwa vigumu kukopesheka na mabenki kutokana na uncertainty.Nini kifanyike: serikali iongeze bajeti ya kilimo kwa maana kilimo ni UTI wa mgongo na kinatoa ajira nyingi kwa watanzania Kama Kuna uwezekano kila Kijiji wapatiwe tractor ambalo litakodishwa kwa wahitaji kwa gharama nafuu( kwa ajili ya gharama za uendeshaji,) serikali kupitia Tarura wafanye matengenezo/maboresho ya barabara za vijijini ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima wakati wa kupeleka sokoni au viwanda vya kuchakata mazao,wizara ya viwanda na biashara kwa kushirikiana na wizara ya uwekezaji wahamasishe wawekezaji kujenga viwanda vidogo vidogo vya kimkakati katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kutafuta masoko vya mazao,vyama vya ushirika vilishiriki katika mchakato wa kuongeza thamani mazao na kutafuta masoko.Kuhusu upande wa bahari na maziwa,serikali ihamasishe wavuvi kutumia vyombo vya kisasa /Meli kufanya uvuvi na kuwa na vyombo vya kuhifadhia samaki.Benki ya kilimo na tib ziwe zinakwenda mikoani/wilayani kuangalia fulsa na kuwashawishi au kutoa elimu kwa vikindu mbalimbali juu ya huduma wanazotoa na faida zake kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu
 
Kwa jinsi mama anavyoupiga mwingi kiutopolo, mda sio mfupi tutakuwa kama Malaysia 😋
 
CCM under MagufuliJP tulikuwa na speed ya hatari. Hata wao waliona kabisa speed yetu wakaanza chuki. Ila kwasasa na speed ya mama. Tusahau kabisa tutanyonywa. Mshindani wako unatakiwa kuweka urafiki wenu kwa akili ila sisi tumekwemda mazima. Tutapigwa hatari sana
1628510983699.png

Unategemea nini kwa kushikwa shikwa hovyo?
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Wamekwama Miaka 60 ya UHURU kama WAMESHINDWA hakuna JIPYA

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ukitaka kujipima na mataifa yaliyotuzidi angalia tunauza nini nje ya nchi
Hata kama ni nyanya lakini zinaingiza fedha za kigeni pindi zinapoliwa Ulaya au Uarabuni

Sisi tunashindwa kwa sababu hatutaki kwenda na wakati na serikali imelala
 
Huwezi kujenga uchumi wa nchi yako wakati wananchi wamegawanyika makundi mawili - sahau.

Kenyatta aliyaona hayo akaamua kufanya kazi na Ondinga, wakenya walau sasa ni wamoja, uchumi wao unasonga na Rais Kenyatta hajabadilika sura au kapungukiwa madaraka yake sababu tu ya kukaa meza moja na mpinzani wake.
 
Iongeze TOZO

Kodi ni muhimu, ilu serikali iweze kujiendesha na kujenga miundombinu( umeme, maji, barabara) hospitali, shule, kuhudumia polisi, mahalama, jeshi walimu, nk.

Lakini kodi ziwe za kiasi kwa watu wengi. Sekta zingine ziwezeshwe ili ziweze kuchangia their fair share. Kama uvuvi, mifugo, kilimo. Kutanua wigo na pia serikali yenyewe kuonyesha mfano kwa kubana matumizi.

Vitu kama mbolea, vifaa vya umwagiliaji, trekta havitakiwi kuongezewa kodi. Ingekuwa busara kuwaalika wazalishaji wakubwa wa mbolea, watengeneja wa solar panels na matrekta vIfaa vya umwagiliaji, magari, bajaji, pikipiki kuwawekee mazingira mazuri wazalishe hapa TZ.

Kwa muda mfupi shuguli za kiuchumi, uzalishaji zitaongezeka sana hivyo kuongeza pato kwa Taifa na watu binafsi, ajira na kodi kwa serikali.
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Tuache mambo ya kishamba ya kupeana kesi za ugaidi. Tuitishe Mkutano wa kitaifa, tushikane kama Taifa
 
Muhimu ni kukuza sector binafsi.
Nchi zote zilizoendelea wananchi wake wanamiliki uchumi kwa asilimia kubwa na siyo serikali.
 
Serikali ipunguze kodi tu . Baasu

Uganda walikuja na kodi kama hizi za muamula ila ilibidi wapunguze, sababu matumizi yalipungua kwa 24%. Wakarudisha kuwa 0.5% kwa muamala.

Ikumbukwe hakuna benki vijijini, hii huduma inawasadia sana wakulima kwa mambo mengi sana. Kuna huduma vijijini huwezi kuzipata / kuzifanya bila mobile money.

Tozo kubwa itapungua na ajira, pesa kwa wakala na zitakuwa na unintended consequences in the whole ecosystem and whole chain.

Matokeo ni serikali haitapa pesa ilizokusudia, zinaweza hata kupungua watu wengi wakiamua kutotumia au kupunguza matumizi ya hizi huduma.
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Sababu kubwa ni sera ambazo hazina muelekeo (ambazo hazina tija) sera ambazo siyo shirikishi 'ineffective policies and uncertainty policies'
 
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi na fulsa nyingi kwa nchi za afrika Mashariki.Tuna eneo kubwa la ardhi inayoweza kutumika kwa kilimo na ufugaji,tuna bahari, maziwa na Mito yenye samaki wa aina mbalimbali,tunayo madini ya aina mbalimbali nk.Karibu asilimia 60 ya wananchi wanajishughulisha na kilimo Cha kujikumu (njaa) na siyo kilimo biashara.wakulima wetu wanapambana Sana kutaka kufanya kilimo Cha kisasa na chenye Tija lakini wanakwamishwa na nyenzo za kufanyia kazi,(tractor au power tiler),pembejeo,miundo mbinu ya kusafirishia mazao kutoka mashambani na kufikisha sokoni bidhaa /mazao Yao au viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani nk.Hali ilivyo ni kwamba vijiji bado hawana wataalamu wa kilimo au mifugo na wakulima bado wanatumia majembe ya mikono ,mbolea au viatifu havipatikani kwa wakati/ havitoshelezi mahitaji ya wakulima.Bado kilimo chetu kinategemea mvua badala ya kuanza scheme za umwagiliaji,kilimo Cha kutegemea jembe la mkono na mvua,inakuwa vigumu kukopesheka na mabenki kutokana na uncertainty.Nini kifanyike: serikali iongeze bajeti ya kilimo kwa maana kilimo ni UTI wa mgongo na kinatoa ajira nyingi kwa watanzania Kama Kuna uwezekano kila Kijiji wapatiwe tractor ambalo litakodishwa kwa wahitaji kwa gharama nafuu( kwa ajili ya gharama za uendeshaji,) serikali kupitia Tarura wafanye matengenezo/maboresho ya barabara za vijijini ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima wakati wa kupeleka sokoni au viwanda vya kuchakata mazao,wizara ya viwanda na biashara kwa kushirikiana na wizara ya uwekezaji wahamasishe wawekezaji kujenga viwanda vidogo vidogo vya kimkakati katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kutafuta masoko vya mazao,vyama vya ushirika vilishiriki katika mchakato wa kuongeza thamani mazao na kutafuta masoko.Kuhusu upande wa bahari na maziwa,serikali ihamasishe wavuvi kutumia vyombo vya kisasa /Meli kufanya uvuvi na kuwa na vyombo vya kuhifadhia samaki.Benki ya kilimo na tib ziwe zinakwenda mikoani/wilayani kuangalia fulsa na kuwashawishi au kutoa elimu kwa vikindu mbalimbali juu ya huduma wanazotoa na faida zake kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu

Point nzuri sana, weka paragraphs please.
 
Tanzania, Tanzania. Nchi ya Watu wavivu kupindukia, watu hawafanyi kazi ila wanataka maisha mazuri, Wenzetu wanafanya kazi, kwa bidii. Na kutunza kile kidogo wanachopata. Watanzania ni wagonjwa sana kifikra, wanatamani ni lini na yeye atapata nafasi ya kuiba.
 
Tuache mambo ya kishamba ya kupeana kesi za ugaidi. Tuitishe Mkutano wa kitaifa, tushikane kama Taifa

Muhimu, hapa wapinzani, wasio na chama kama ni wabobezi, wamequalify wapewe nafasi za uongozi. Hata mabeberu wanaweza kuwekwa kwenye sekta fulani kwa muda fulani.

Mfano sekta ya Utalii, kilimo, mifugo, kutafuta masoko, hizi zinaweza kukuzwa haraka, with change of mindset, attitude, utaalamu, ubunifu, kujitangaza, great services na incentives, sera wezeshi.

Lengo liwe kufikia watalii 10 millioni, kùuza mifugo, nyama na samaki wa kutosha.

Kufungua biashara iwe ndani ya muda mfupi, kodi ziwekwe kutokana na mapato halisi mfanyabiashara.

Urasimu kutoa export licenses uondolewe.
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Mada nzuri umeiweka kishambakishamba sana, kiasi kwamba hata wewe ungepewa nafasi muhimu ya kutoa mapendekezo kifanyike kipi uchumi wetu ukue haraka, pengine ndiyo ungetudidimiza kabisa kuliko tulivyo sasa.

Kiufupi, naona kama watu wenye fikra kama zako ndio waliojaa huko serikalini na kushindwa kutupeleka mbele haraka.
 
Wanaweza kubadilisha mentality za wananchi wake?wanaweza kuboresha system ya elimu nchi nzima?
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
KWANZA katiba mpya ,sambamba na sheria kali kwa wenzi wa fedha za umma,

Pili mshikamano wa Taifa,kunzia kwenye siasa bora , maendeleo ya Taifa yataletwa na wananchi WENYEWE palipo mshikamano na UTULIVU wa kisiasa
 
CCM under MagufuliJP tulikuwa na speed ya hatari. Hata wao waliona kabisa speed yetu wakaanza chuki. Ila kwasasa na speed ya mama. Tusahau kabisa tutanyonywa. Mshindani wako unatakiwa kuweka urafiki wenu kwa akili ila sisi tumekwemda mazima. Tutapigwa hatari sana
Ninyi ndio mlioporwa akili na Magufuli.

Magufuli alidondisha ukuaji wa uchumi toka 7.5% mpaka 2%. Aliangusha ukuaji wa uwekwzaji toka 28% mpaka 4%. Aliangusha ukuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%. Aliangusha thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo iwa 50%, halafu kuna wehu wanaamini marehemu alikuza uchumi kwa kasi.

Magufuli alikwishafariki, rudisheni akili ja mzitumie msibakie na vichwa makopo.
 
Back
Top Bottom