SoC04 Serikali ianzishe wizara maalumu ya saikolojia na utatuzi wa migogoro ili kuzipunguzia wizara zingine mzigo wa kushughulikia migogoro

Tanzania Tuitakayo competition threads

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,102
1,919
Bwana Yesu ASIFIWE ....
Assalamualaikum......

Serikali ianzishe wizara maalumu ya saikolojia na utatuzi wa migogoro ili kuzipunguzia wizara zingine mzigo wa kushughulikia migogoro

Kwanza nianze kwa kuwashukuru Jforum kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kuweka majukwaa mbalimbali yanayoibua mawazo mapya kila kukicha. M/Mungu awabariki zaidi na mtandao huu udumu zaidi. Baada ya shukrani hizi, Wacha nijikite kwenye mada yangu kama inayoonekana hapo juu kwenye title.

Kwamba, ninapendekeza serikali kupitia viongozi wetu na kwa kushirikiana na Bunge, ianzishwe wizara moja itakayokuwa inashughulikia maswala ya saikolojia na utatuzi wa migogoro katika jamii, maeneo ya biashara na kwa wafanyakazi. Yaani, katika harimashauri zetu, kutakuwa na ofisi maalumu itakayokuwa chini ya waziri wa saikolojia na utatuzi wa migogoro nchini. Wizara hii tutapanga namna bora itakavyokuwa ila inatakiwa isambae kila harimashauri, na kata zetu.

Nasema hivi kwasababu, dunia kwa sasa na serikali zetu za kidunia zinachangamoto ya migogoro mikubwa ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiimani. Kila eneo linachangamoto zake na kusema ukweli mahakama zetu zimezidiwa, na ndiyo maana tunaona baadhi ya migogoro inakuwa inatolewa na wananchi mbele ya wanasiasa na viongozi wengine hata kama migogoro hiyo haiwezi kutatuliwa na viongozi hao. Hii maana yake nini, jamii imekosa platform nzuri yakuweza kutatua migogoro Yao. Nasema hivi kwasababu, viongozi wetu kuanzia ngazi ya kata, kama vile wenyeviti wa vijijini, watendaji, maafisa mifugo, waratibu elimu nk. Wanashindwa kutatua baadhi ya migogoro kulingana na namna inavyokuja.

Mfano, inatokea migogoro ya kiimani baina ya dhehebu Moja au dhehebu jingine, uongozi wa kata hushindwa kutatua migogoro hiyo kwasababu pia, kiuhalisia, viongozi wetu hawana ujuzi wa utatuzi wa migogoro. Na hapa nataka kusema kwamba, kabla ya kuianzisha wizara hii niliyoipendekeza, inatakiwa kule vyuoni ianzishwe kozi maalumu ya saikolojia na utatuzi wa migogoro, iwe inatoa cheti Cha psychology and problem solving skills.

Cheti cha saikolojia na utatuzi wa migogoro. Najua kwasasa hakuna cheti hiki maana yake hatuna pia wabobezi wa saikolojia na utatuzi wa migogoro nchini isipokuwa baadhi ya wataalamu wanachopekewa maarifa ya namna ya kushughulikia migogoro katika fani wanazozisomea. Na hao ndiyo wanatumika kutatua migogoro mbalimbali katika maeneo yetu, kiuhalisia hawana ujuzi wa kutosha wa kushughulikia migogoro katika maeneo yetu. Mtu mwenye uelewa na ujuzi wa kutosha kuhusu utatuzi wa migogoro, anapaswa kuingia darasani na kusoma zaidi ya mwaka mmoja, ndiyo maana, chuo Cha Georgia kilichopo Atlanta, kinatoa kozi hii na kutoa cheti Cha utatuzi wa migogoro, certificate of problem solving skills.

Ninachokieleza hapa, ukiwadha harakaharaka, unaweza ukaona nichakawaida sana, lakini ukitulia, utakubaliana na Mimi kwamba, migogoro katika jamii zetu, katika taasisi zetu na maeneo yetu ya kazi ni mingi sana. Migogoro imekuwa ndiyo chanzo Cha watu kupoteza kazi, migogoro imekuwa ndiyo chanzo Cha kupoteza watu muhimu katika kazi zetu, migogoro imekuwa ndiyo chanzo Cha watu kufariki, migogoro ndiyo inafanya taasisi kuzorota katika uzalishaji na matokeo chanya.

Tukiichukulia kawaida migogoro, hatuwezi kuipata Tanzania tunayoitaka. Ili tuipate Tanzania tunayoitaka, kwanza tumalize au angalau tupunguze migogoro katika jamii zetu na taasisi zetu kwa kutumia wataalamu watakao andaliwa vyema kutatua migogoro, tuachane na kutumia wataalamu wa fani zingine kutatua migogoro. Mtaalam aliyesomea maswala ya utawala, bado anapungukiwa ujuzi wa utatuzi wa migogoro. Tunatakiwa kama taifa, tuwe wa kwanza kuwa na wizara ya saikolojia na utatuzi wa migogoro na wala siyo kuwa tunaunda kamati, hapana, tuwe na wizara kamili kabisa ambayo, bila kupitia kwayo, huwezi kufika mahakamani. Wizara hii itakuwa na vitengo kama zilivyo wizara zingine.

Mfano, wizara ya elimu sayansi na Teknolojia ina taasisi zake kama vile Taasisi ya elimu nchini inayoshughulikia ubora wa elimu na usambazaji wa vitabu, Kuna NECTA,Kuna taasisi ya vyuo vikuu nk, hawa wote wanamsaidia wizara ya elimu sayansi na Teknolojia. Tukiunda wizara ya saikolojia na utatuzi wa migogoro, tutaitengenezea taasisi ndogo ndogo zitakazobeba wataalamu tupu wa saikolojia na utatuzi wa migogoro. Mfano, tunaweza tukawa na vitengo vifuatavyo vitakavyokuwa chini ya wizara hii.
  • Taasisi inayoshughulikia migogoro ya wafanyabiashara tu
  • Taasisi inayoshughulikia utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji
  • Taasisi inayoshughulikia utatuzi wa migogoro ya watumishi serikalini na taasisi binafsi
  • Taasisi inayoshughulikia utatuzi wa migogoro ya kijamii ikiwemo migogoro ya ndoa, na mapenzi
Tukiwa na wizara kamili inayoshughulikia utatuzi wa migogoro, nakuhakikishieni, tutakuwa na Tanzania nzuri zaidi kwasababu, wizara zingine zitashughulika kubuni mambo mazuri kwa ajili ya serikali na taasisi zake. Kwenda mahakamani iwe ni shauri la juu na la mwisho kabisa. Tukifanya hivi na tukafanikiwa, naamini mataifa mengine watakuja kujifunza kwetu.
 
Kwamba, ninapendekeza serikali kupitia viongozi wetu na kwa kushirikiana na Bunge, ianzishwe wizara moja itakayokuwa inashughulikia maswala ya saikolojia na utatuzi wa migogoro katika jamii, maeneo ya biashara na kwa wafanyakazi
Nimepata swali hapa, kwamba hiyo wizara itahusu migogoro tu. Migogoro ya wizara ipi? Na je? kila wizara itaendelea kudili na migogoro yake au hii wizara ya migogoro ndiyo itakusanya gogoro zoote za kila wizara halafu itadili nayo?

Na hapa nataka kusema kwamba, kabla ya kuianzisha wizara hii niliyoipendekeza, inatakiwa kule vyuoni ianzishwe kozi maalumu ya saikolojia na utatuzi wa migogoro, iwe inatoa cheti Cha psychology and problem solving skills.
Nimeanza kukupata sasa, unapanga kuanzisha kitu mpya kabisa kama vile computer science hivii

Tukiwa na wizara kamili inayoshughulikia utatuzi wa migogoro, nakuhakikishieni, tutakuwa na Tanzania nzuri zaidi kwasababu, wizara zingine zitashughulika kubuni mambo mazuri kwa ajili ya serikali na taasisi zake. Kwenda mahakamani iwe ni shauri la juu na la mwisho kabisa.
Na kama hilo litashindikana chief je? Utaridhika na kuanzishwa kwa kozi lakini watu wake badala ya kujengewa wizara wanakuwa tu 'hot cake' kila mahala wanahitajika. Kila wizara inawaajiri, kila kampuni inawataka, kila kamati lazima wawemo na mwishoni wanakuwa na ofisi zao kama za mawakili kwa ajili ya kutatua migogoro binafsi? Je itatoshea?
 
Nimepata swali hapa, kwamba hiyo wizara itahusu migogoro tu. Migogoro ya wizara ipi? Na je? kila wizara itaendelea kudili na migogoro yake au hii wizara ya migogoro ndiyo itakusanya gogoro zoote za kila wizara halafu itadili nayo?


Nimeanza kukupata sasa, unapanga kuanzisha kitu mpya kabisa kama vile computer science hivii


Na kama hilo litashindikana chief je? Utaridhika na kuanzishwa kwa kozi lakini watu wake badala ya kujengewa wizara wanakuwa tu 'hot cake' kila mahala wanahitajika. Kila wizara inawaajiri, kila kampuni inawataka, kila kamati lazima wawemo na mwishoni wanakuwa na ofisi zao kama za mawakili kwa ajili ya kutatua migogoro binafsi? Je itatoshea?
Upo vizuri kiongozi, Mimi nimeanzisha wazo, ni wazo huru kuboreshwa
 
Back
Top Bottom