Naomba kutoa Rai kwa serikali!
"Ukicheka na nyani Utavuna mabua" TUCTA must watch out!
Kuna HAKI na WAJIBU wa kila MTU
Haki ya mfanyakazi ni kulipwa ujira wake kama kanuni zinavyosema! LAKINI wajibu wa mfanyakazi ni kufanya kazi bora ili mwajili awe na sababu ya kulipa ujira huo hata Zaidi.
Sakata la nyongeza ya mishahara liwe fursa kwa serikali kubadilisha sheria za mfanyakazi ili kuongeza uwajibikaji!
Tiba ya kudumu ya sakata hili iko kwenye mageuzi ya sheria mbili
1. Sheria ya kumlinda mfanyakazi itazamwe upya
2. Sheria ya kibenki kwa mfanyakazi kukopea mshahara iwekewe spidi gavana
Ni kweli walistahili kuongezwa lakini je kuna tija gani kwa serikali kuwaongezea mishahara?
1. Unawaongezeaje mishahara wafanyakazi wavivu?
2. Unawaongezeaje mishahara wafanyakazi watoro kazini?
3. Unawaongezeaje mishahara wafanyakazi wabadhilifu?
4. Unawaongezeaje mishahara wafanyakazi wala rushwa?
5. Unawaongezeaje mishahara wafanyakazi wanaotegemea makal** kama CV?
6. Unawaongezeaje mishahara wafanyakazi waolalamikiwa na kila mwananchi mnyonge anaehitaji huduma bora?
Hata siku moja SIJAWAHI kuona TUCTA wakisimama kidete kuwakumbusha na kuwaonya wafanyakazi kuwajibika!
Sheria za mfanyakazi Tanzania zina mpa ulinzi mkubwa mno mfanyakazi kiasi kwamba haoni sababu ya kuwajibika ipasavyo kazini!
Mfanyakazi anaweza asiwajibike kazini sheria inamlinda, anaweza kula rushwa na akahamishwa, anaweza lewa chakali kazini na asifukuzwe, anaweza kunyonya hata mafuta ya gari la serikali na asifukuzwe, utoro, umalaya, uchelewaji, uzembe wa kila aina n.k na bado serikali ikamkubatia au kumhamisha idara.
Sheria za wafanyakazi ziliundwa enzi hizo kulikuwa hakuna wafanyakazi wa kutosha! LEO HII Sioni sababu ya kukumbatia sheria zinazompa Amani mfanyakazi wakati SERIKALI ikitukanwa kila kona kwa kuwakumbatia WAZEMBE.
Ukichunguza taasisi nyingi sana zinabebwa na watu wachache waojituma, asilimia kubwa wengi ni bora liende.
Kama ni benki utashangaa anaechapa kazi ni mmoja au wawili, kama ni shirika anaejituma katika 100 utakuta ni wafanyakazi 10 tu!
Sasa kwanini serikali isiweke sheria za kuwaongezea mishahara wale wafanyakazi bora wanaojituma kuliko kuhangaika na wafanyakazi wasio na tija?
Wafanyakazi wa kima cha chini huenda wameonekana bora kwasababu wengi wao wanajitahidi kiasi chake, kama ni usafi maofisini wanafanya, chai wanawapikia n.k
Je ni kweli Kwamba mishahara HAUTOSHI?
Jibu ni rahisi sana, Mishahara haujawahi kutosha hata iwe milioni 100 kwa mwezi HAUTATOSHA!
Tatizo kubwa sasa ni sheria na kanuni za mikopo hizi ndizo zinawatesa wafanyakazi!
Wanakopa na kutop-up pesa asilimia kubwa ya mishahara na kubakiwa na kitu kidogo ambacho hakiwatoshi kwa mwezi!
Mfano mtu alipwa 1mil, anakopea benki kununua SUBARU anabakiwa na mshahara wa laki mbili. kwa mwezi!
Gari lake kwa siku linataka elf 30! Sasa mtu kama huyu unafikili atasema mshahara unamtosha?
Wekeni sheria za ukomo wa kukopea mishahara iwe ni 30% tu, ili abakiwe na hela ya matumizi.
Sakata la mishahara likawe fursa kwa selikali kufumua sheria kwa dharura kuongeza uwajibikaji.
Kelele za Tucta zikizidi ndugu zangu kina "Flamingo" mnajua kazi yenu! ombeni kibali mmalize mchezo.