Uchaguzi 2025 LGE2024 Serikali, Bunge, Ziheshimu Mahakama! Kwanini Serikali na Bunge Hazijatekeleza Hukumu ya Mahakama kuhusu Ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,340
120,865
Wanabodi
Hii ni makala yangu ya Gazeti la Mwananchi Wiki hii
Katiba Inavyobatilisha Sheria Batili.png

Leo naendelea na hizi makala elimishi kuhusu katiba ya JMT kwa jicho la mtunga katiba, alidhamiria nini. Wiki iliyopita nilizungumzia ukuu wa katiba na jinsi wakuu wa mihimili, ya serikali, Bunge na Mahakama marais wa awamu zilizopita walivyo jiinua juu ya katiba na kufikia kiwango cha kuikanyanga katiba.

Declaration of Interest ya Nia Njema
Naomba kutoa declaration of interest ya nia njema, kuuhusu ukuu wa katiba, maana Mihimili mitatu ya dola, Serikali, Bunge na Mahakama, inapotimiza majukumu yake, zinapaswa kutimiza majukumu hayo kwa mujibu wa katiba, zikiongozwa na kusimamiwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, hivyo anapojitokeza mtu mdogo kama sisimizi mimi, nikaonyesha makosa kwenye tafsiri ya katiba kwa kuonyeshea nia ya mtunga katiba, naweza kutafsiriwa kuwa huyu ni mpinzania wa Serikali, Bunge na Mahakama!, ningewaomba wakuu hao, nao kuitumia fursa hii kujifunza nia ya mtunga katiba, ili nao wajifunze, kama mimi nimekosea, nikosolewe, ila kama Serikali, Bunge na Mahakama zilikosea, ni turekebishe katiba yetu, sheria zetu ili twende salama, hivyo mimi sio mpinzani, bali ni muelimishaji umma mwenye nia njema na ya dhati ya kulisaidia taifa langu!.

  1. Leo nakuletea jinsi katiba ya JMT ilivyo kiukwa na serikali, Bunge na Mahakama, kwa kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT, Mahakama Kuu ikaitengua, serikali ikakata rufaa ikashindwa, serikali ikaamua kuinajisi katiba ya JMT kwa kuchomekea kiubatili kipengele batili ndani ya katiba, Mahakama Kuu ikashikilia msimo kuwa mabadiliko hayo ya katiba ni batili. Lakini Mahakama ya Rufani ikaulinda ubatili huo ambao mpaka leo ubaliti huo bado uko ndani ya katiba yetu!.
  2. Kwa vile sheria ya uchaguzi iliishabatilishwa na hukumu ya Mahakama Kuu, kwa kuelezwa ni sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, hukumu hii haikuwahi kubatilishwa, japo serikali ilikata rufaa ikashindwa, swali la ajabu ni kwanini sasa serikali yetu ya sasa imetunga sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu?!.
  3. Bunge letu Tukufu lilisha amriwa na huku ya Mahakama ya Rufaa, kuwa Bunge lilifanya ubatili , kwa kanuni ya mihimili kuheshimiana, Mahakama ya Rufaa, kwa kuliheshimu Bunge, Mahakama ya Rufaa, ukalihukumu Bunge, kuuondoa ubatili huo!, Kwanini mpaka leo Bunge letu tukufu, mpaka leo, halijatekeleza huku hiyo ya Mahakama ya Rufaa?!, hili ni jambo la kushangaza sana!.
  4. Bunge letu tukufu, sio tuu mpaka leo, limepuuza kwa kugomea kuitekeleza hukumu ya Mahakama ya Rufaa, kuuondoa ubatili huo ndani ya katiba yetu, bali sasa limetunga tena sheria batili nyingine ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule unaokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Rais wa JMT ameisha isaini sheria hiyo batili, na imeanza kutumika!, kitu ambacho ni muendelezo wa mhimili wa serikali na mhimili wa Bunge kuidharau mahakama na kujiinua juu ya katiba ya JMT!, kitu ambacho sio kitu sahihi, hivyo kama hakutafanyika mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms, hii maana yake tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa za uchaguzi mkuu kwa katiba yenye ubatili, kwa kutumia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977.
  5. Ubatili huo ni lile shurti la kumlazimisha mgombea uongozi wa umma, kujiunga na chama cha siasa, ili kudhaminiwa na chama cha siasa, kuweza kugombea, shurti ambalo ni kinyume cha katiba ya JMT, kinyume cha Universal Declaration of Human Rights, kinyume cha The United Nations Human Rights Committee, kinyume cha African Chatter of People and Political Rights.
  6. Ibara, 5 ya katiba yetu inatoa haki kwa kila Mtanzania anapofikisha umri wa miaka 18, anakuwa huru kupiga kura kumchagua kiongozi anayemtaka. Kitendo cha wagombea wa vyama tuu ndio wanaoruhusiwa kuchaguliwa, kinawanyima haki Watanzania kuwachagua viongozi wanaowataka, wamelazimishwa kuwachagua viongozi waliodhaminiwa na vyama vya siasa!. Ile haki kuu ya kwanza ya haki ya kila Mtanzania kumchagua kiongozi anayemtaka, imeporwa kwa wananchi na kukasimiwa vya vyama vya siasa ndio pekee vyenye haki ya kuchaguliwa!.
  7. Ibara ya 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatoa haki ya kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 21, ana sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa na uongozi kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote kama inavyoelezwa hapa Uhuru wa kushiriki shughuli za umma 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
  8. Ibara hizo mbili ndio dhima ya mtunga katiba, Watanzania wawe huru kuchagua na kuchaguliwa lakini serikali yetu tukufu, ikachomekea shurti batili la kumlazimisha mtu kudhaminiwa na chama cha siasa kwenye ibara ya 39 na ibara ya 67, ya katiba, hivyo sasa ibara ya 21 ya katiba yetu inasomeka hivi 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.[/I][/B]
  9. Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 5 na ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na Ibara ya 67 (b)(c) kwa kuweka shurti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa hivyo lazima adhaminiwe na chama cha siasa!. Haki kuu ya kisiasa kwa za kuchagua na kuchaguliwa zinatolewa na ibara moja halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo! Huu ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya JMT kwa kuweka masharti yanayokwenda kinyume cha katiba.
  10. Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya juhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi.
  11. Baada tuu ya Mchungaji Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, jambo la kwanza ni serikali ilikata rufaa!. Hili ndilo kosa la kwanza la mhimili wa Mahakama. Dhima ya mtunga katiba aliposema katiba ni sheria Mama, na sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili, mtunga katiba alidhamiria hakuna mamlaka yoyote ndani ya JMT inaruhusiwa kutunga sheria yoyote inayokwenda kinyume cha katiba, na ikitokea sheria hiyo ikatungwa, mtunga katiba alidhamiria sheria hiyo ni batili.
  12. Anayebatilisha sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT kwa dhima ya mtunga katiba, ni katiba yenyewe na sio Mahakama Kuu ya Tanzania. Jukumu la Mahakama Kuu kwenye ukuu wa katiba, ni kujiridhisha tuu na kuthibitisha tuu kuwa sheria fulani inakwenda kinyume cha katiba, hivyo uamuzi wa Mahakama Kuu ni kuuthibisha na kuutangaza ubatili wa kwenda kinyume cha katiba, na sio kuibatilisha! Anayebatilisha sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ni katiba yenyewe na sio Mahakama Kuu.
  13. Serikali Bunge na Mahakama, zina wajibu wa kuheshimiana, mahakama ikitoa hukumu, bunge na serikali zinapaswa kwanza kutekeleza hukumu husika, ndipo taratibu za kukata rufaa ziendelee, lakini kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977, dhima ya mtunga katiba ni sheria yoyote batili, sio sheria, kwa lugha ya kisheria ni "void ab initio", yaani haipo!.
  14. Toka Mahakama Kuu ilipotoa uamuzi wa ubatili huo, ubatili huo unakuwa umebatilishika pale pale!, hivyo serikali haikupaswa kukata rufaa, lakini serikali yetu ilikata rufaa na wakati huo huo serikali ilipeleka Bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa, ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!. Hapa ndipo ubatili wa kuinajisi katiba yetu ulipoanzia serikali yetu kuchomekea ubatili ndani ya katiba yetu kiubatili!.
  15. Je Mchungaji Mtikila alikubali katiba yetu inajisiwe kwa kuchomekewa kiubatili, kifungu batili kinachokwenda kinyume cha Katiba ya JMT?. Jiunge nami Jumatano Ijayo kwenye gazeti la Mwananchi.
Paskali.
 
Hivi mgombea huru akiruhusiwa,

Wakajitokeza wagombea Urais 1000,

Hiyo karatasi ya kura itakuwaje?
Vigezo vya Urais ndio vitawaengua,
  • ili kugombea urais, unapaswa kupata wadhamini 1000, katika mikoa 15 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 ya Zanzibar, na mmoja Pemba.
  • Uwe na elimu ya Masters ya Chuo Kikuu
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 10,000,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 100,000,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
individuals hawawezi.

Vigezo vya Ubunge
  • ili kugombea ubunge, unapaswa kupata wadhamini 100, katika jimbo husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya Chuo Kikuu
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 1,000,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 10,000,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
Vigezo vya Udiwani
  • ili kugombea udiwani, unapaswa kupata wadhamini 100, katika kata husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya Sekondari
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 500,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 1,000,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
Serikali ya Mtaa
  • ili kugombea serikali ya mtaa, unapaswa kupata wadhamini 100, katika mtaa husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya kujua kusoma na kuandika
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 100,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 100,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
P
 
Sababu ni moja tu. Chama chako kiko juu ya katiba na sheria kwa kuwa mwenyekiti wake kupitia kofia ya urais yuko juu ya katiba na sheria.

Maono yake, maagizo yake na utekelezaji wake (rais) hauhojiwi na chombo chochote.
 
"Vigezo vya Ubunge

  • ili kugombea ubunge, unapaswa kupata wadhamini 100, katika jimbo husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya Chuo Kikuu"

- Nukuu
Vigezo vya Urais ndio vitawaengua,
  • ili kugombea urais, unapaswa kupata wadhamini 1000, katika mikoa 15 ya Tanzania ikiwemo
P
Mkuu Paskali, kwa wabunge tuliokuwa nao hivi sasa bungeni, hiki kigezo cha elimu kweli kimezingatiwa?
 
"Vigezo vya Ubunge

  • ili kugombea ubunge, unapaswa kupata wadhamini 100, katika jimbo husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya Chuo Kikuu"

- NukuuMkuu Paskali, kwa wabunge tuliokuwa nao hivi sasa bungeni, hiki kigezo cha elimu kweli kimezingatiwa?
No hivi ni vigezo vyangu
P
 
Vigezo vya Urais ndio vitawaengua,
  • ili kugombea urais, unapaswa kupata wadhamini 1000, katika mikoa 15 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 ya Zanzibar, na mmoja Pemba.
  • Uwe na elimu ya Masters ya Chuo Kikuu
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 10,000,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 100,000,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
individuals hawawezi.

Vigezo vya Ubunge
  • ili kugombea ubunge, unapaswa kupata wadhamini 100, katika jimbo husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya Chuo Kikuu
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 1,000,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 10,000,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
Vigezo vya Udiwani
  • ili kugombea udiwani, unapaswa kupata wadhamini 100, katika kata husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya Sekondari
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 500,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 1,000,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
Serikali ya Mtaa
  • ili kugombea serikali ya mtaa, unapaswa kupata wadhamini 100, katika mtaa husika ambao wamejiandikisha kupiga kura.
  • Uwe na elimu ya kujua kusoma na kuandika
  • Uwe na shughuli ya kueleweka inakuingizia kipato cha zaidi ya TZS. 100,000 kwa mwezi
  • Utawasilisha dhamana ya TZS. 100,000
  • Utawasilisha list ya wafadhili na gharama za kampeni.
  • Utawasilisha ilani yako ya uchaguzi.
P
Mkuu hapo kwenye kigezo cha elimu ni kweli au unapendekeza tu?
 
Nakuita tenaa Paschal ...narudia tena Paschal au Mayala.NI kipengere kipi kinasema kua ili kugombea Urais wa JMT lazma mtu awe na elimu ya masters?

Paskali....Katiba imeweka wazi kua chama kitakacho pata wabunge wengi ndicho kitaunda au ndicho chenye mamlaka ya kuunda serikali.Sasa ebu tuambie mgombea au wagombea wasio na chama wataunda serikali kupitia chama gani? KARIBU
 
Haki iwepo, tushindwe wenyewe na sio kutulazimisha kuyachagua matutusa, tunayoletewa na vyama!.
P
Ni serekali ipi ya kutii hiyo mahakama ambayo hakimu au jaji akipigiwa simu Moja tu anatoa hukumu kuendana na maagizo? Niliidharau sana mahakama wakati wa kesi ya kutungwa ya Mbowe ya ugaidi. Yaani upande wa serekali ulikuwa unatoa ushahidi batili kabisa, na hakimu anaona ni ushahidi wenye mashiko! Mahakama ya kipuuzi hivyo unawezaje kuitii ukiwa na Nia ovu?

Mahakama za Kenya wangalau zinajitambua. Ukitaka kujua mahakama hapa kwetu ni kanyaboya, hata ww mwenye elimu ya Sheria unaishia kuweka mabandiko marefu marefu huku kwenye social media na huendi huko mahakamani, maana unajua ni kupoteza muda.
 
Sasa kama HAKI hiyo haitekelezeki, kwanini kudai?

Mgombea binafsi awezaje kuandaa Ilani yake ya Uchaguzi?
Ilani ya uchaguzi ni mataraji yako ukipewa uongozi, si kitu kigumu kuandika
Hawa wagombea binafsi hutumia wasomi katika kupanga mipango yao
 
Back
Top Bottom