Secrets of Swiss Banking - Kitabu

Zomba,
Kikwete kayafanyia kazi kinafiki sana haya. Asingeteua watu kama Lowasa, Chenge kuwa kwenye Cabinet yake huku akijua wazi hawa jamaa kwa money laundering hawana mbadala nchi hii.

Shutma bila ushahidi ndio maana huwa mnashindwa kesi na kuambiwa mlipie gharama kubwa kubwa. Vitu kama hivi inabidi uende "scientifically" sio kufukuzana na kubambikiana tu kwa kuwa fulani kasema. Kama kuna ushahidi wewe unao usingoje Kikwete, unakwenda tu mahakamani, hujaona Mtikila anavyoonesha mfano?
 

Itazame hiyo ripoti ya lini? na mpaka leo ni lini? na in between kimetendeka nini? Hiyo siyo ripoti ya leo niliiweka kuonesha kuwa Kikwete kaanza kulifanyia kazi hili zamani na leo tunaanza kuona matunda, kuna wengi tumewaona wakifikishwa mahakamani, kuna waliofungwa kuna wanaoendelea kuchunguzwa kuna hizi habari sasa zinapatikana kutoka uswiss, yote hayo ni matunda ya kazi njema za Kikwete, hatuwahi kuyaona kabla ya Kikwete
 

Kamanda,

Kipi hicho kilichotokea? Au unataka kuh-hint juu ya kibomu unachotaka kulipua?

That is why I am in love with JF!
 

Mpwa,

Unaponishangaza wewe ni kuwa mabaya ambayo yamefanyika chini ya Kikwete hutaki na hupendi yeye awe na responsibility! Like the same old line: "Kikwete ana nia nzuri ila anaangushwa na watendaji wake...."
 
Bado waliowekeza india kwa kutumia Wahindi walioko hapa.ICICI Bank,Bank of Baroda nk.
 
zomba Mkuu, naomba mifano ya angalau watano tu ya hao wengi waliofungwa. Ninalokubaliana nawe ni hilo la kuchunguzwa kwani "uchunguzi unaendelea" ndio kauli mbiu ya viongozi wetu.
 
Last edited by a moderator:
Tena hao majina yanafahamika! ICICI Bank wakibanwa na watu wetu wanaweza kutoa siri za kushangaza!

yeah....Tena nilifanya Internship hapo wakati nasoma bachelor kisha wakati nasubiri kuanza Masters nikafanya kazi hapo kwa muda.Kaka yaani si kwa Tanzania tu Kenya,Uganda na Nigeria ni hatari.mbaya zaidi hata wanaoweka fedha hizi wamekuwa wakila dili na maofisa ubalozi na wanapokelewa na Management kama vile ni halali kabisa

Dili hizi ndizo zilizosukuma Benki hii kuelekeza harakati zake kwenye offshore service.
 
Zomba,
Sheria ile ya rushwa enzi za Mwalimu ingebaki kama ilivyokuwa suala la ushahidi lisingeleta shida. Zamani mtu kama Chenge angesimama kizimbani tu akatueleza yeye vile vijisenti vya kule Jersey alivipataje. Kwa kweli sheria ile isiporudishwa kama ilivyokuwa, kauli yako hii itawaokoa wengi.
 

Shimbo Huyu Huyu ambaye wewe mwenyewe ushawahi kumreport hapa jamvini au mwingine?
Dah, I am tired with how things goes in this country, kesho kutwa hata ACP Msangi atafanya kitu cha kishujaa na kuonekana HERO.
 
Yameanza kutimia...Asante maana hii kitu sikuwahi kuiona labda kwa kuwa nilikuwa mpya mpya kipindi hicho...
 

Na yeye zake alizoficha Arabuni, je?
 

Shimbo Huyu Huyu ambaye wewe mwenyewe ushawahi kumreport hapa jamvini au mwingine?
Dah, I am tired with how things goes in this country, kesho kutwa hata ACP Msangi atafanya kitu cha kishujaa na kuonekana HERO.
Niliwaona maofisa wakubwa tu wa SUMAJKT wakiingia mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. Ndio kazi ya Lt Gen Shimbo hiyo? Au hawakumgawia nini!
 

ni sawa na kuomba uamsho afunge novena

siamini hadi nione...
 
zomba Mkuu, naomba mifano ya angalau watano tu ya hao wengi waliofungwa. Ninalokubaliana nawe ni hilo la kuchunguzwa kwani "uchunguzi unaendelea" ndio kauli mbiu ya viongozi wetu.

Kufungwa au kutokungwa sio kazi ya Kikwete, ni kazi ya mhimili wa dola unaoitwa Mahakama. Mimi hapa naongelea anayoyafanya Kikwete.

Isitoshe, wapo wengi tu, zaidi ya hao watano uwatakao. Kwa kuanzia tu haraka haraka kabla sijaenda mbali nakupa sita, ni mmoja zaidi ya uwatakao, ukitaka nikuongeze wengine sema tu.:

hawa wanne:

Hawa wawili:
 
yah, ila kesi kama za babu seya na yule mangi pale moshi ni kazi ya nani?
 

Sheria ipi hiyo na wangapi walisamamishwa kwa rushwa kizimbani wakati wa Nyerere? usiandikie mate kama wino unao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…