Secrets of Swiss Banking - Kitabu

Zomba,
Kikwete kayafanyia kazi kinafiki sana haya. Asingeteua watu kama Lowasa, Chenge kuwa kwenye Cabinet yake huku akijua wazi hawa jamaa kwa money laundering hawana mbadala nchi hii.

Shutma bila ushahidi ndio maana huwa mnashindwa kesi na kuambiwa mlipie gharama kubwa kubwa. Vitu kama hivi inabidi uende "scientifically" sio kufukuzana na kubambikiana tu kwa kuwa fulani kasema. Kama kuna ushahidi wewe unao usingoje Kikwete, unakwenda tu mahakamani, hujaona Mtikila anavyoonesha mfano?
 
zomba Mkuu, nadhani umeona baadhi ya title za hizo nyuzi bila ya kujisumbua kuzisoma, na kama ulisoma, niambie unajisifia nini katika maelezo yaliyopo hapa chini?: zomba Mkuu, kwa maelezo yako na maneno ya Kikwete, ni kuwa Rais wetu angalau kwa hili la wizi wa mali za umma, anasema asichokifanya na kufanya asichokisema. Kama ingekuwa kinyume chake, kwa nini igunduliwe na nchi za nje kuwa kuna mijizi inavusha pesa kupeleka Uswisi? Hakuchukii mtu kumpenda Kikwete kwani mapenzi kipofu.

Itazame hiyo ripoti ya lini? na mpaka leo ni lini? na in between kimetendeka nini? Hiyo siyo ripoti ya leo niliiweka kuonesha kuwa Kikwete kaanza kulifanyia kazi hili zamani na leo tunaanza kuona matunda, kuna wengi tumewaona wakifikishwa mahakamani, kuna waliofungwa kuna wanaoendelea kuchunguzwa kuna hizi habari sasa zinapatikana kutoka uswiss, yote hayo ni matunda ya kazi njema za Kikwete, hatuwahi kuyaona kabla ya Kikwete
 
Hata hivyo, naelewa sheria zetu zinavyochelewesha maamuzi! Inafurahisha kuwa walau Jeshini kuna hatua zimeanza kuchukukiwa...

zomba, am well informed juu ya alichofanya majuzi ndugu Shimbo, nipende kusema kuwa kwenye 'hili' la majuzi alilofanya huko China ni la kizalendo na karibuni wananchi watamwona kuwa ni 'hero'. Muhimu, ajiweke kando na wanasiasa!

Kamanda,

Kipi hicho kilichotokea? Au unataka kuh-hint juu ya kibomu unachotaka kulipua?

That is why I am in love with JF!
 
Nyuzi kama hii ndipo nnapopata fursa ya kumsifu Kikwete, kabla Invisible hajatuwekea humu hiki kitabu, Kikwete kaanza kulifanyia kazi zamani sana na nivyema mpaka leo (2008) elimu imewafikia kina Invisible na wanaanza kuwatanabahisha na wengine, ingawa Invisible yupo miaka miwili nuyma lakini hii ni kazi ya kuendelea na nampongeza kwa kuiunga mkono kwa kutowa elimu kama hii aliyotuwekea.

Kikwete hii kazi aliianza na kuifanya kwa kubadilisha sheria humu ndani ya nchi zinazohusiana na utoroshaji wa fedha na rushwa, hakuishia hapo akakazania sana kuhusu sheria ya Umoja wa Mataifa itakaruhusu fedha zilizopo nje ya Afrika za Waafrika ziwekwe wazi na kurudishwa ikigundulika hazijapatikana kihalali, hata juzi juzi alilisemea sana alipokuwa Arusha kwenye mkutano wa majaji wa jumuiya madola.

Alilitilia mkazo pia walipokutana na wakuu wa kuzuia rushwa afrika mashariki.

Sasa japo tunaona manufaa ya kazi yake, angalau tunajuwa ziko ngapi hapo Uswisi tu na bado zipo nje kwingine kwingi na nyingi tu nna uhakika Kikwete haziachi hizo, kama alivyorudisha fedha za rada na hizi zitarudi tu.

Hapo ndipo nnapompendea Kikwete, nyie semeni yeye anafanya.

Kuwakumbusha tu kuwa kazi hii kaianza zamani na leo mna matunda yake nimewawekea links tofauti hapa chini mjikumbushe:

http://www.google.com/url?sa=t&rct=j...vFP36w&cad=rja

Kenya: Kikwete calls for uniform tax system in East Africa

Zimefichuka » Blog Archive » KIKWETE'S CAMPAIGN AGAINST CORRUPTION PROMISING

Kikwete on money laundering and corruption - Google Search[+Arusha

Mpwa,

Unaponishangaza wewe ni kuwa mabaya ambayo yamefanyika chini ya Kikwete hutaki na hupendi yeye awe na responsibility! Like the same old line: "Kikwete ana nia nzuri ila anaangushwa na watendaji wake...."
 
Bado waliowekeza india kwa kutumia Wahindi walioko hapa.ICICI Bank,Bank of Baroda nk.
 
Itazame hiyo ripoti ya lini? na mpaka leo ni lini? na in between kimetendeka nini? Hiyo siyo ripoti ya leo niliiweka kuonesha kuwa Kikwete kaanza kulifanyia kazi hili zamani na leo tunaanza kuona matunda, kuna wengi tumewaona wakifikishwa mahakamani, kuna waliofungwa kuna wanaoendelea kuchunguzwa kuna hizi habari sasa zinapatikana kutoka uswiss, yote hayo ni matunda ya kazi njema za Kikwete, hatuwahi kuyaona kabla ya Kikwete
zomba Mkuu, naomba mifano ya angalau watano tu ya hao wengi waliofungwa. Ninalokubaliana nawe ni hilo la kuchunguzwa kwani "uchunguzi unaendelea" ndio kauli mbiu ya viongozi wetu.
 
Last edited by a moderator:
Tena hao majina yanafahamika! ICICI Bank wakibanwa na watu wetu wanaweza kutoa siri za kushangaza!

yeah....Tena nilifanya Internship hapo wakati nasoma bachelor kisha wakati nasubiri kuanza Masters nikafanya kazi hapo kwa muda.Kaka yaani si kwa Tanzania tu Kenya,Uganda na Nigeria ni hatari.mbaya zaidi hata wanaoweka fedha hizi wamekuwa wakila dili na maofisa ubalozi na wanapokelewa na Management kama vile ni halali kabisa

Dili hizi ndizo zilizosukuma Benki hii kuelekeza harakati zake kwenye offshore service.
 
Shutma bila ushahidi ndio maana huwa mnashindwa kesi na kuambiwa mlipie gharama kubwa kubwa. Vitu kama hivi inabidi uende "scientifically" sio kufukuzana na kubambikiana tu kwa kuwa fulani kasema. Kama kuna ushahidi wewe unao usingoje Kikwete, unakwenda tu mahakamani, hujaona Mtikila anavyoonesha mfano?
Zomba,
Sheria ile ya rushwa enzi za Mwalimu ingebaki kama ilivyokuwa suala la ushahidi lisingeleta shida. Zamani mtu kama Chenge angesimama kizimbani tu akatueleza yeye vile vijisenti vya kule Jersey alivipataje. Kwa kweli sheria ile isiporudishwa kama ilivyokuwa, kauli yako hii itawaokoa wengi.
 
zomba,

Sina neno na utendaji wa JK, napenda kuendelea kumsihi asiweke uswahiba wa aina yoyote katika kuwashughulikia wahujumu uchumi hawa.

He's nothing to lose, zaidi atatengeneza legacy yake kwa kuwashughulikia watu hawa.

Mwizi hana chama, si mtu wa kumchekea hata chembe... Ndo wanaosababisha wananchi (bila kujali itikadi zao za kisiasa/kidini) waishi maisha ya kubahatisha.

Nikuombe, fanya uwezavyo (kama utaweza) kuhakikisha unamfahamisha kuwa wananchi wangependa kuona hatua za haraka zinachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika.

Hata hivyo, naelewa sheria zetu zinavyochelewesha maamuzi! Inafurahisha kuwa walau Jeshini kuna hatua zimeanza kuchukukiwa...
zomba, am well informed juu ya alichofanya majuzi ndugu Shimbo, nipende kusema kuwa kwenye 'hili' la majuzi alilofanya huko China ni la kizalendo na karibuni wananchi watamwona kuwa ni 'hero'. Muhimu, ajiweke kando na wanasiasa!

Shimbo Huyu Huyu ambaye wewe mwenyewe ushawahi kumreport hapa jamvini au mwingine?
Dah, I am tired with how things goes in this country, kesho kutwa hata ACP Msangi atafanya kitu cha kishujaa na kuonekana HERO.
 
Kuna watu walinifahamisha wangependa kupata kitabu ama dondoo juu ya kitu hiki. Huenda ukawa mwanzo wa wengi kujua kwa undani nini hasa chanzo cha watu kuweka ngawira katika taifa hili...

As a tip: Kuna 'mafia' kadhaa toka Tanzania wamelimbiliza fedha nyingi huku. Ni zaidi ya EPA. Kuna siku itafumuka tu, Mungu anipe uhai!

CONTENTS:
Chapter 1: Challenges and Threats
Chapter 2: Switzerland-Alpine Financial Oasis
Chapter 3: Where to Begin: Opening a Swiss Bank Account
Chapter 4: Investing through Your Swiss Bank
Chapter 5: Banking Policies and Regulations
Chapter 6: The Ultimate Investment Plan
Chapter 7: Alpine Retreat for Business and Pleasure
Chapter 8: The Best Alternatives to Switzerland
Yameanza kutimia...Asante maana hii kitu sikuwahi kuiona labda kwa kuwa nilikuwa mpya mpya kipindi hicho...
 
Nyuzi kama hii ndipo nnapopata fursa ya kumsifu Kikwete, kabla Invisible hajatuwekea humu hiki kitabu, Kikwete kaanza kulifanyia kazi zamani sana na nivyema mpaka leo (2008) elimu imewafikia kina Invisible na wanaanza kuwatanabahisha na wengine, ingawa Invisible yupo miaka miwili nuyma lakini hii ni kazi ya kuendelea na nampongeza kwa kuiunga mkono kwa kutowa elimu kama hii aliyotuwekea.

Kikwete hii kazi aliianza na kuifanya kwa kubadilisha sheria humu ndani ya nchi zinazohusiana na utoroshaji wa fedha na rushwa, hakuishia hapo akakazania sana kuhusu sheria ya Umoja wa Mataifa itakaruhusu fedha zilizopo nje ya Afrika za Waafrika ziwekwe wazi na kurudishwa ikigundulika hazijapatikana kihalali, hata juzi juzi alilisemea sana alipokuwa Arusha kwenye mkutano wa majaji wa jumuiya madola.

Alilitilia mkazo pia walipokutana na wakuu wa kuzuia rushwa afrika mashariki.

Sasa japo tunaona manufaa ya kazi yake, angalau tunajuwa ziko ngapi hapo Uswisi tu na bado zipo nje kwingine kwingi na nyingi tu nna uhakika Kikwete haziachi hizo, kama alivyorudisha fedha za rada na hizi zitarudi tu.

Hapo ndipo nnapompendea Kikwete, nyie semeni yeye anafanya.

Kuwakumbusha tu kuwa kazi hii kaianza zamani na leo mna matunda yake nimewawekea links tofauti hapa chini mjikumbushe:

http://www.google.com/url?sa=t&rct=j...vFP36w&cad=rja

Kenya: Kikwete calls for uniform tax system in East Africa

Zimefichuka » Blog Archive » KIKWETE’S CAMPAIGN AGAINST CORRUPTION PROMISING

Kikwete on money laundering and corruption - Google Search[+Arusha

Na yeye zake alizoficha Arabuni, je?
 
Shimbo Huyu Huyu ambaye wewe mwenyewe ushawahi kumreport hapa jamvini au mwingine?
Dah, I am tired with how things goes in this country, kesho kutwa hata ACP Msangi atafanya kitu cha kishujaa na kuonekana HERO.
Niliwaona maofisa wakubwa tu wa SUMAJKT wakiingia mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. Ndio kazi ya Lt Gen Shimbo hiyo? Au hawakumgawia nini!
 
zomba,

Sina neno na utendaji wa JK, napenda kuendelea kumsihi asiweke uswahiba wa aina yoyote katika kuwashughulikia wahujumu uchumi hawa.

He's nothing to lose, zaidi atatengeneza legacy yake kwa kuwashughulikia watu hawa.

Mwizi hana chama, si mtu wa kumchekea hata chembe... Ndo wanaosababisha wananchi (bila kujali itikadi zao za kisiasa/kidini) waishi maisha ya kubahatisha.

Nikuombe, fanya uwezavyo (kama utaweza) kuhakikisha unamfahamisha kuwa wananchi wangependa kuona hatua za haraka zinachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika.

Hata hivyo, naelewa sheria zetu zinavyochelewesha maamuzi! Inafurahisha kuwa walau Jeshini kuna hatua zimeanza kuchukukiwa...
zomba, am well informed juu ya alichofanya majuzi ndugu Shimbo, nipende kusema kuwa kwenye 'hili' la majuzi alilofanya huko China ni la kizalendo na karibuni wananchi watamwona kuwa ni 'hero'. Muhimu, ajiweke kando na wanasiasa!

ni sawa na kuomba uamsho afunge novena

siamini hadi nione...
 
zomba Mkuu, naomba mifano ya angalau watano tu ya hao wengi waliofungwa. Ninalokubaliana nawe ni hilo la kuchunguzwa kwani "uchunguzi unaendelea" ndio kauli mbiu ya viongozi wetu.

Kufungwa au kutokungwa sio kazi ya Kikwete, ni kazi ya mhimili wa dola unaoitwa Mahakama. Mimi hapa naongelea anayoyafanya Kikwete.

Isitoshe, wapo wengi tu, zaidi ya hao watano uwatakao. Kwa kuanzia tu haraka haraka kabla sijaenda mbali nakupa sita, ni mmoja zaidi ya uwatakao, ukitaka nikuongeze wengine sema tu.:

hawa wanne:
Wanne wafungwa miaka mitano kwa rushwa
na Jumbe Ismailly, Manyoni
MAHAKAMA ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, imewahukumu watu wanne akiwemo ofisa mtendaji wa Kata ya Ipande, Tarafa ya Itigi, kifungo cha miaka mitano jela baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh 650,000.

Soma zaidi: Wanne wafungwa miaka mitano kwa rushwa

Hawa wawili:
KESI YA EPA: Maranda, Farijala wafungwa miaka 5
Tausi Ally
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana iliwahukumu kifungo cha miaka mitano jela kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein baada ya kupatikana na hatia kwenye mashtaka sita kati ya manane ya kujipatia fedha katika Akaunti ya Madeni ya...

Soma zaidi: KESI YA EPA: Maranda, Farijala wafungwa miaka 5
 
Kufungwa au kutokungwa sio kazi ya Kikwete, ni kazi ya mhimili wa dola unaoitwa Mahakama. Mimi hapa naongelea anayoyafanya Kikwete.

Isitoshe, wapo wengi tu, zaidi ya hao watano uwatakao. Kwa kuanzia tu haraka haraka kabla sijaenda mbali nakupa sita, ni mmoja zaidi ya uwatakao, ukitaka nikuongeze wengine sema tu.:

hawa wanne:

Hawa wawili:
yah, ila kesi kama za babu seya na yule mangi pale moshi ni kazi ya nani?
 
Zomba,
Sheria ile ya rushwa enzi za Mwalimu ingebaki kama ilivyokuwa suala la ushahidi lisingeleta shida. Zamani mtu kama Chenge angesimama kizimbani tu akatueleza yeye vile vijisenti vya kule Jersey alivipataje. Kwa kweli sheria ile isiporudishwa kama ilivyokuwa, kauli yako hii itawaokoa wengi.

Sheria ipi hiyo na wangapi walisamamishwa kwa rushwa kizimbani wakati wa Nyerere? usiandikie mate kama wino unao.
 
Back
Top Bottom