Sasa ni rasmi Rais wa TFF, Jamal Malinzi amehusika na upangaji matokeo

NA KWA HABARI NILIZOZIPATA HIVI PUNDE TU ZINASEMA KWAMBA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA KUNA MJUMBE MMOJA AMBAYE KUTOKANA NA USHAHIDI ALIOKUWA NAO TENA WA KIMAWASILIANO YA SAUTI YA RAIS MALINZI AKITOA MAELEKEZO NA AMBAO ALITAKA KUUTOA MBELE YA ILE KAMATI YA UCHUNGUZI WA HILI SAKATA LAKINI AKAZUIWA HADI KUTISHWA SASA ANATAKA KUWAITA WAANDISHI WA HABARI ILI AWEKE KILA KITU HADHARANI KWANI ANASEMA KWAMBA KWA KUWA KAMATI YA AKINA TARIMBA ABBAS ILIYO CHINI YA TFF YA MALINZI IMEAMUA KUMWAGA UGALI SASA YEYE ANATAKA KUMWAGA SI TU MBOGA BALI MAJI YA KUNAWA, VIJIKO, VIBAKULI NA HATA KULITUPILIA MBALI KABISA NA JIKO LENYEWE ILI KILA KITU KIWE HADHARANI. WAANDISHI WA HABARI WOTE WA MICHEZO HAKIKISHENI HAMKAI MBALI KWANI NYANGUMI SASA HIVI ANAKWENDA KUVULIWA!

NITOE WITO AMA OMBI KWA WAZIRI NAPE NA TAKUKURU KUWA FANYENI UPESI TOENI MAELEKEZO WATU WAENDE TCRA UPESI WAKAFUATILIE MAWASILIANO YA HAWA WATU WAWILI Rais Malinzi Na Huyu Bwana Chacha Kiongozi Wa Mashindano Wa TFF Ya Siku 9 Kabla Ya Mechi Ya Geita Gold FC Dhidi Ya KANEMBWA FC Kisha Mawasiliano Ya Hawa Watu Wawili Wakati Wa MAPUMZIKO Wa Hiyo Mechi Huko Mkoani Kigoma. TCRA Tafadhalini Sana TOENI USHIRIKIANO Wenu Kwani USHAHIDI WOTE SASA UPO HADHARANI Kwani Tumechoka KUFANYWA WAJINGA au WAPUMBAVU Na Kikundi Cha Watu Wanaotumia Jasho La Wachezaji Wetu KUJINEEMESHA.
 
alisema hivi

upload_2016-4-6_13-22-10.png
 

Sasa Kwakuwa AMEUDHIHAKI Kwa Namna Fulani Mtandao Wa JF Ila Hasa Hasa Sisi Members Tena Kwa DHARAU Kubwa Tunamwambia Ni Humu JF Ambako Sasa TUTAHAKIKISHA Tunapambana Kwa Nguvu Zote Ili Kuonyesha Kuwa Members Waliopo Humu HAWAPOTEZI Muda Humu Bali Nao Pia Wanawajibika Katika Kuipigania Nchi Yao Na Hasa Kupambana Na UFISADI. Hatutaki Longolongo Za Aina Yoyote Bali Tunataka Tu Rais Wa TFF Jamal Malinzi Atuachie TFF Yetu Na Mpira Wetu. Leo Hii JF Ni Mbaya Kwake Mbona Alipopata Huo Urais Alikimbilia Humu Kuja KUTUSHUKURU Na Kutuhaidi Mambo Mengi? Kwahiyo Leo Kusemwa JF Mbaya Ila Akisifiwa JF Ni Nzuri Kwake? AMESHIKWA PABAYA SANA NA HUO USHAHIDI AMBAO HUYO MJUMBE ANATAKA KUUTOA BAADAE Nina UHAKIKA Ndiyo UTAMFANYA Jamal Malinzi Arudi Kwao KAMACHUMU Akanywe Kahawa.
 
Mimi hata hiyo clip sihitaji kuisikiliza ushahidi wa matokeo tu unaniambia kuna mlungula umetumika kwa kiasi kikubwa so huwezi kunambia kuwa huo uozo hauna nataka za malinzi.
 
Mambo mapya yamezidi kuibuka kuhusu sakata la upangaji matokeo kwenye ligi daraja la kwanza ikiwa ni siku chache baada ya TFF kutoa hukumu kwa baadhi ya viongozi, wachezaji na waamuzi waliopatikana na hatia mbele ya kamati ya nidhamu ya Shirikisho hilo linalosimamia mpira wa miguu Tanzania.

Kubwa ambalo ndiyo habari ya ‘mujini’ kwa sasa ni kuvuja kwa sauti ambayo wanasikika baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa TFF pamoja na viongozi wa timu ya Geita Gold Sports wakipanga mikakati ya kupanga matokeo ambayo inahusisha rushwa ndani yake.

Sauti ya kigogo mmoja wa TFF inasikika akiomba rushwa ya shilingi milioni 25 kutoka kwa viongozi wa Geita ili aweze kuhakikisha anawasaidia katika baadhi ya matatizo ambayo miongoni mwayo ni pamoja na vibali vya wachezaji.

Sauti hiyo imeifikia www.shaffihdauda.co.tz na kutokana na kutaka kuwajulisha wadau wa mchezo huu pendwa, mtandao huu unakuletea moja kwa moja sauti hiyo ili upate kuwasikia vigogo hao wa TFF wenye dhamana kubwa ya soka la Bongo wanavyolihujumu na kulisambaratisha soka kwa kutumia vibaya mamlaka yao.

Jana (April 5) Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha alitangaza kujiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF mara baada ya kuvuja kwa sauti ya mjadala wa kupanga matokeo pamoja na kuomba rushwa.

Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha alieleza kuwa amepata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho.

Martin alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Afisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Hili ndiyo soka la Bongo sinema na mazingaombwe bado yanaendelea TFF, usiache kufatilia www.shaffihdauda.co.tz kujua mengi zaidi juu ya sakata hili, utaendelea kupata taarifa kadiri zinavyotufikia kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Hii hapa ndiyo sauti iliyonaswa kwenye mjadala huo wa upangaji matokeo uliowahusisha maafisa wa ngazi za juu wa TFF pamoja na viongozi wa timu ya Geita Gold Sports ya mkoani Geita.
 
Hiyo clip iko wap?umbea mi sipendi,weka clip watu waamini unataka tumchukie malinz kwa maneno yako?

Nadhani kwa Watanzania wapenda soka labda ni wewe tu pekee ndiyo huna hiyo au hujaisikia hiyo clip na hii inadhihirisha kabisa ni jinsi gani ulivyo mvivu wa kujibiidisha katika kupata kitu na pia mvivu wa akilini. Unasema kuwa namchukia Jamal Malinzi kisha nataka nanyi mumchukie. Huwa nadhani mtu akishakuwa na umri kama wako basi hata akili zake tu nazo zinachaji na anakuwa ni mchambuzi wa issue mzuri na aliyetukuka. Kwahiyo unataka kusema kuwa hata juhudi zote zinazofanywa na Serikali ya Rais Dr. Magufuli kwa wala rushwa na wabadhirifu wa nchi hii na yeye pia ana chuki nao? Mkuu kama nimekugusa wewe pengine ulikuwa na maslahi nae basi hapa kwangu sirudi nyuma ng'o na bahati nzuri mno sifa yangu kubwa ni kujiamini, kutoogopa na kuwa tayari kwa lolote. Utabaki hivyo hivyo kusema " weka clip " huku wenzako tunasonga mbele!
 
Back
Top Bottom