Katibu Tarafa
JF-Expert Member
- Feb 16, 2007
- 989
- 54
Tatizo la watanzania ni kuongea bila vigezo, nyie wadau mnaozungumza maneno ya kashfa kuhusu Balozi nyanganyi na kusema yeye ni mbomoaji nadhani hamna vigezo. Kama unataka kujua mambo aliyoyafanya siyo Tanzania tu bali dunia nzima unaweza kwenda kwenye mtandao na kusearch by his name na utaona kazi kubwa aliyoifanya Marekani kuitangaza Tanzania na kujenga Umoja baina ya Watanzania wanaoishi huku, nenda World Bank na IMF na uone kiasi gani cha fedha alileta nyumbani kwa projects na misaada mbali mbali kipindi alichokuwa Balozi, namba ya watalii iliongezeka mara dufu kwa kipindi hicho. Alikwenda Uarabuni na akaendelea na hilo hilo. Hotel ya Kilimanjaro ilikuwa gofu na akaitangaza Tanzania na waarabu wakaja kufanya vitu vyao, akaanzisha umoja wa Watanzania wanaoishi huko UAE na kuunda katiba. Ukiacha haya yote ya nje ya nchi, aliicha wizara ya Mawasiliano ikiwa imesheehena ndege zikiruka Uarabuni, Uingereza na bara lot ela Afrika akiwa waziri wa Mawasiliano na uchukuzi.Mbona hamuongelei kilichotokea ni nini? Na ndege hizo zilienda wapi? Kakabidhiwa shirika halina hata helicopter ya kupaa!Sasa JAKAYA kumrudisha hapo kuwa mwenyekiti wa bodi haikuwa kwa sababu ya kujuana bali ni kwa ajili ya uzoefu alionao. Makosa hutokea lakini si vizuri watu kukashifu mtu kama hakufanya chochote katika nchi hii. Hawa ni viongozi wachache ambao wameitumikia nchi kwa uaminifu kwa kufanya kazi karibu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hadi alipostaafu! Tuwe wakweli na tujifunze kukumbuka Historia, na siyo kuendeleza gumzo lisilo na maaana.
Na wewe jikumbushe hiyo historia yako,huyo ndugu yako ndie alituletea pantoni mbovu pale magogoni,ufisadi hakuanza leo wala jana ila mamekubuu ktk fani