Mtikila anaonekana alikuwa na information nyingi sana. Kwanza mmoja wa hao kina Haidery ndiye jina lake linaonekana katika kampuni ya Isenegeja iliyonunua magazeti ya Rai na Mtanzania (si kampuni yote ya Habari Corporation).Mafisadi walionufaika na mtaji huo wa Sakarir Aziz ndio waliofanya uhaini wa kumpa Ubunge wa Igunga alipofariki hayati Charles Kabeho. Wazee wa Kiajemi waliolowea hapa, Hussein Heidari na Hassan nduguye ndio waliompokea kijana Sakarir Aziz kule Igunga, kwa sababu wanao uhusiano na mkewe Aziz yaani mama yake Sakarir au Rostam.
Hawa wazee ndio waliomnadi huyu Mwajemi kwa wazee wa Igunga katika kuiba Ubunge wa Nchi ya watu ambao anawachukulia kuwa 'mataahira'. Sakarir Aziz anao nduguze wa kiume wawili yaani Jahangir Aziz ambaye alipigana kizalendo kabisa ile vita ya nchi yao dhidi ya Iraq, na wa pili ni Akram Aziz.
sasa mtu siyo raia wa tanzania, je passport ya tanzania amepataje?
sasa mtu siyo raia wa tanzania, je passport ya tanzania amepataje?
Wana Jamii,
Hivi hakuna Investigative Journalism hapa kwetu? Nyaraka hizi za uthibitisho wake kweli haupatikani? Mbona mie wananijua? Mambo ya ndani(uhamiaji)
Dawa ya mwizi ni mwivi..Nyaraka zinazonuka ufisadi zinakuja hapa, hata harufu haijaisha zinatua kabla hata kinyesi hakijakauka hapa...Kulikoni?
Kulikoni za Idara ya Uhamiaji? (Msije kuniambia ule moto uliowaka wakati ule hapa uliondoa nyaraka hizo aidha kwa maji ya zimamoto au moto wenyewe!) Yale yale, twin towers.
Nilifikiri ka nzi kana uwezo wa kupenya penya, ama uhamiaji hakunuki?
Wamemshinda huyu Jeetu watamweza huyo RA?
Tutashuhudia...ka nzi kapewe vinyesi vya ufisadi uhamiaji(hakuna vyandarua pale)kama ushahidi unatakikana, tetesi mpaka lini?
Nitathubutu kumuuliza mkuu wa kaya mwenyewe, ikibidi(wewe unamjua Rosatm, alisoma wapi-ni rafiki yako, ulimpa uraia? Unaweza kumfungulia kabrasha ya uchunguzi yakinifu?
Jioni njema
Je na hii ni muendelezo wa yale masaa 72 ya Vodacom?.
Kwa maoni yangu, hata kama ukweli halisi ndio huo, lazima atakuwa alikuja nchini zamani zaidi ya hiyo hoja ya Mtikila maana anazungumza lafudhi ya Kiswahili safi cha ndani na si polished.
Mtikila alipewa pesa na Mangi kuyafanya hayo anayoyafanya, nadhani hata kubeba gharama za baadhi ya kesi zake ikiwemo ili ya mgombea binafsi, ni kazi ya Mangi, uzuri wa Mtikila, haaminiki, siku ya siku itafika, atasema yote.
Kwa vile madai hayo ni mazito na hajachuliwa hatua yoyote, enda ikawa yana kwa ukweli, na kama ni kweli, hiyo ina maana wahusika wakuu wote hayo wanayajua na kwa vile ndio amewafikisha hapo walipo kupitia pande la Kagoda, panya gani anaweza kujitolea kumvisha paka kengele?.
Tuendelee kujadili changamsha jamvi nyingine hii, lakini King Maker will remain safe until the end of the kingdom he made. Tuendelee kupiga kelele tuu, tupige kelee wee, tupige kelele wee kwa matumaini hatimaye mwenyenyumba ataamka toka usingizini.
Ukweli wenyewe kumbe anachosikia mwenye nyumba, ni kelele tuu za mlango haziwezi kumkosesha usingizi wake.
Maneno mazito hayo Mkuu. Niliwahi kusema, lazima kuwe na UASI ndani ya TAASISI ZOTE NYETI IKIWAMO UHAMIAJI. Uwe UASI takatifu kwa Wazalendo kuamua kuanika uozo wote wa hawa wanaoivuruga nchi yetu. Maslahi ya Taifa yanavunja nguvu zote za kihalifu ikiwa TUTAAMUA. Wengi wamejaribu na wamepata kinga, wachache wameumia, lakini ndio gharama za UKOMBOZI. Hii ni VITA ya UKOMBOZI TUSIFANYA UTANI. Yataibuka mambo mazito na tutaanza kushangaa na kulaumiana. Tuchukue hatua NOW
Kazi kwenu.
Wewe una uhakika ameipata kienyeji ? Au unafuata mkumbo tu
Mkuu Pasco, maneno yako mazito, lakini yenye kupooza uhalisia. Inawezekana kuna ukweli ya kuwa Mchungaji amekuwa akitumika mara kadhaa lakini hata wewe ukitumika, haina tatizo, HOJA hapa tujadili facts kama ulivyosema kwamba "King Maker will remain safe until the end of the kingdom he made" na hapo ungesaidia/tusaidiane kujadili solution, maana linagusa maslahi yetu na vizazi vyetu, na historia itatuhukumu na watoto wetu watafukua makaburi yetu, kuangalia kama vichwa vyetu vilikuwa na tofauti gani na vya kondoo!!!
Kinacho ni shangaza ni je utunzaji wa rekodi mbali mbali za wakazi wa Tanzani(siyo lazima raia) ukoje mpaka ishindikane kujulikana mtu katokea wapi na vipi? Kwa nini asi chunguzwe? Iweje mtu apate passport ya Kianzania kienyeji enyeji? Basi tuna "watanzania" wengi. Kuna maswali mengi ya kuulizwa na yalipaswa yachunguzwe ukkweli ujulikane. Mimi naona jamaa ana lindwa sana maana haya maswali siyo vigumu sana kuchunguza na kupatamajibu yake. Tanzania tuna tia huruma kama hata wageni wana kuja na kutuibia chini ya "mwamvuli" wa utanzania. Na mtu kama huyu akiulizwa defense yake ya kwanza kuwa kuna ubaguzi. Tanzania ina tia huruma. Nawa laumu vhao watanzania wajinga walio kubali kutumiwa ili kum patia anacho taka.