Rostam Aziz kuvuliwa Uraia?

sasa mtu siyo raia wa tanzania, je passport ya tanzania amepataje?
Magezi,
Kuna rafiki yangu World Bank anatoka Lebanon. Aliniambia mdogo wake alinunua pasipoti ya Tanzania kwa dola elfu mbili. Kwa hiyo sishangai kama kuna watu wasio Watanzania wana pasipoti za Tanzania.
 
Heee......mbona wamemuuzia bei mbaya hivyo? duh watu wabaya kweli...wakati angeweza kupata hata kwa dola mia mbili tu.......! Mjomba ni utani tu..
 
Sio Rostam athibitishe uraia, mwenye kupinga uraia wa Rostam na atoe vithibiti, sio yeye Rostam ajibu maswali, no, wewe prove. Hakuna jipya, acha wanakijiji wapotoshwa wasaidie wanakijiji wapotoshwa wao.

Aya ya kwanza ya toleo la CHECHE linasomeka kana kwamba kuna new development kuhusu uraia wa Rostam na potentially anaweza kuvuliwa uraia:

``Bw. Rostam Aziz anaweza akajikuta katika matata mengine kabisa endapo atashindwa kuthibitisha uraia wake wa Tanzania kufuatia tetesi ambazo zimekuwa zikizagaa tangu...``

Lakini ukisoma kwa undani - na usijaze bandwith kuchangia hapa kama hujasoma CHECHE - ukisoma utagundua kwamba mwandishi si mkweli kwa sababu yeye mwenyewe kadokeza kwamba Rostam is not in any trouble, hakuna kinachofanyika. Ukurasa wa tatu wa CHECHE:

``Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa kwa muda mrefu vyombo mbalimbali vya serikali haviko tayari kufanya uchunguzi juu ya Rostam kwani endapo ukweli utajulikana unaweza kukitikisa chama na nchi.

...kutokana na ukaribu wa Rostam na maraia Kikwete pamoja na Mkapa na jinsi alivyoshiriki katika kukisaidia Chama cha Mapinduzi nawabunge mbalimbali uwezekano wa uchunguzi huru kufanyika haupo.``

Kwa hiyo hakuna assertion yeyote ku substantiate kwamba Rostam is potentially in trouble kama aya ya ukurasa wa kwanza ya CHECHE inavyoashiria. Halafu "dossier" ya Mtilika nayo pia ni old chestnut. Hivyo Mwanakijiji anapotosha anapodai Rostam anaweza kuvuliwa uraia, hajaonyesha kuna any new development.
 
Last edited:
Dilunga,
Lakini ile ya kuvuliwa uraia Mwanakijiji kaiwekea question mark. It was just another way of drawing your attention to the article.
 
Dilunga,
Lakini ile ya kuvuliwa uraia Mwanakijiji kaiwekea question mark. It was just another way of drawing your attention to the article.

Sawa kabisa Jasusi, absolutely right, kichwa cha habari ni swali, lakini ndani aya ya kwanza mwandishi ametoa assertion kwamba huenda Rostam akavuliwa uraia halafu, badala ya kuonyesha kuna nini kimetokea, unakuta mwandishi huyo huyo anasema hii status quo hii haiwezi kumfanya kitu Rostam.

Sasa, which is which, Jasusi hebu nisaidie, maana mimi ni "mkaanga sumu." Wewe you are as fair-minded as they come, we nambie, Mwanakijiji ana speculate kwamba Rostam may be in trouble au anasema Serikali haiwezi kumgusa Rostam? Kipi ni kipi?

Halafu unapotoa nukuu mia nne za sources bila kutaja hata mmoja, mi msomaji nitajueje hujatunga? Kwa nini nikuamini wewe? Wafuasi wako watakuamini, ndio, lakini kama unataka ku convince wengi zaidi ili twende tukapige kura kuondoa status quo basi jaribu ku reach beyond the kwaya, wana kwaya wameshakubali somo, katoe injili Jangwani ku convert wengine upanue zizi la kondoo wa bwana. Au basi angalau hao wafuasi wako waambie ukweli. Ukweli wenyewe tabu. Rostam yuko matatani, nani kamtia matatani, Mtikila? Kesha lipa deni?
 
..yaani shukurani za CCM kwa Rostam, kwa kuwanunuliwa Ubunge na Uraisi, iwe kumvua uraia?

..halafu mimi i am getting exasperated here...sidhani kama wananchi wanaelewa hili somo la ufisadi. ndio maana bado wanaendelea kuipigia kura CCM ktk hizi chaguzi ndogo.
 
Kuna vitu tunavisema kama kuviweka kwenye rekodi ili ijulikane vimesemwa na vimejulikana. Lakini zaidi tunaviweka kama ushahidi ya kuwa siku ya siku ikifika watu wasiseme wanaonewa.

Sijui kama kuna mtu yeyote ndani ya CCM ambaye anaelewa implication ya kuwa Rostam si raia. Ninachoona ni kama watu waliofunika vichwa vyao mchangani kama mbuni. Wanaombea tu kuwa hawa watu "wataacha majungu, kupandikiza chuki, uzushi na madai yasiyo na msingi".

Hakuna mwandishi anayeweza kumuuliza Rostam alisoma shule ya msingi ya wapi, na alisoma Chuo Kikuu cha wapi na mwaka gani? Hakuna ambaye anaweza kumuuliza wazazi wake ni raia wa wapi na wako wapi. Sababu ni kuwa kufanya hivyo kutamfanya mwandishi huyo aangaliwe vibaya na wengine!!
 
Mkuu wangu Mwanakijiji, hili siyo swala rahisi, lingekuwa hivyo akina Ulimwengu wangekuwa wamesha muuliza. Kumbuka kuwa Kamati ya Mwakyembe ilishindwa kumpata ili ajibu kuhusu Richond na Dowans. Hivyo, si rahisi kumhoji huyu jamaa, ni aina fulani ya mafia. Kinachonishangaza ni vyombo vya dola (TISS, Uhamiaji na Polisi) na CCM kutokuwa tayari kumchunguza. Kelele hizi si bure, zitamtoa nyoka pangoni.

Naunga mkono signature yako "Thank you Ka "nzi", this one is very good!"
 
Moto unazidi kuwaka na kumsogelea fisadi papa Rostam Azizi. Ninafurahi kuona joto ndani ya jiko lake likizidi kuongezeka. Hii issue ya uraia, Rostam anatamani sana ife na isitokee kabisa kwenye habari za Tanzania. Kila mara akidhani kuwa amefanikiwa (kama vile alivyofanya kwa Mtikila) ndio mwanzo inakuja kwa kasi kubwa zaidi.

Mwanakijiji, swali zuri kabisa .... kwa kuongezea tu mshangao wangu binafsi kwenye swali lako la msingi (kichwa cha habari hii).... je mtu aweza vipi kunyangwanya uraia ambao hakuwa nao in the first place?
 
Mwafrika, nadhani wanachofanya ni kumtoa "mask" ambayo kaivaa yenye kuitwa "Mtanzania" na kumuacha aonekane katika sura yake halisi. Mask hiyo inaonekana kwa kupewa Ubunge, Umeneja wa Kampeni, n.k

Fikiria mtu ambaye ameshiriki kuchangisha fedha na kusimamia fedha zilizomuingiza Rais wa nchi hakimiya madarakani kuwa si rais wa nchi hiyo.. what does is say about such a country?
 
Mwanakijiji,
mmm, hapa naona umeamua kumvua chupi RA, na kumwacha kengele zinagongana zenyewe ha ha ha
 
Yaani, tumeshindwa kum-nail RA kwa ufisadi wake sasa tunaangalia uraia? What difference does it make?
Fisadi+Tanzanian, Fisadi+Non-Tanzanian they all deserve to be locked up and the key thrown away.

Huyu RA tunamjadili kwa yote ambayo anatufanyia watanzania walipa kodi, Na hapa tunataka kujua ni RA anahaki gani ya kuwa na raia mbili? na ni kwanini ananakuwa na raia mbili? bila shaka ni ufisadi wake. RA anatuhuma nyingi sana kwanini awe yeye tuuuu na si mwingine? mkuuu kaa ukijua kwamba wewe mwenyewe unaibiwa na huyu RA.
 
....Mtikila hii game yake ya kutumia uraia/uzawa kusukuma agenda zake sio kitu kipya,ndio mwanzilishi wa siasa za ********* akasababisha baadhi ya watanzania kutokana na rangi zao kuishi kwa wasiwasi,huu ni ufashisti wa hali ya juu ambao ndio mwanzo wa matatizo na vita kwenye nchi nyingi,this fool mtikila lisipoangaliwa litaleta vita na chuki tuu...kama RA kaiba kwanini inakuwa ngumu sana kumfikisha mbele ya sheria wakati mawaziri kibao wamepigwa ndani na wengine kujiuzuru na hata Waziri mkuu kuachia ngazi,hana uchungu wowote na nchi zaidi ya kuganga njaa tuu!
 
Viongozi wa nchi yetu na haswa Wizara husika wanatakiwa kufanya kazi ya kujibu haya maswali. Kwa jinsi mambo yanavyozidi kufichuka inaonekana siyo tu kwamba akiwa si raia amewezaje kupata pasi ya kitanzania, bali uchunguzi thabiti ukifanyika pia itathibitika kuwa ameshawaombea na kuwadhamini raia kadhaa wa nje kupata uraia na pasi. Sitashangaa ukikuta na sahihi za viongozi kwenye kumbukumbu za kupewa pasi wasio rahia halali au kinyume na sheria kwa kushinikizwa na RA. Hii si bongo tena ni Bongolala! kama alivyoiita mwandishi wa Kulikoni hivi karibuni.
 
Sawa kabisa Jasusi, absolutely right, kichwa cha habari ni swali, lakini ndani aya ya kwanza mwandishi ametoa assertion kwamba huenda Rostam akavuliwa uraia halafu, badala ya kuonyesha kuna nini kimetokea, unakuta mwandishi huyo huyo anasema hii status quo hii haiwezi kumfanya kitu Rostam.

Sasa, which is which, Jasusi hebu nisaidie, maana mimi ni "mkaanga sumu." Wewe you are as fair-minded as they come, we nambie, Mwanakijiji ana speculate kwamba Rostam may be in trouble au anasema Serikali haiwezi kumgusa Rostam? Kipi ni kipi?

Halafu unapotoa nukuu mia nne za sources bila kutaja hata mmoja, mi msomaji nitajueje hujatunga? Kwa nini nikuamini wewe? Wafuasi wako watakuamini, ndio, lakini kama unataka ku convince wengi zaidi ili twende tukapige kura kuondoa status quo basi jaribu ku reach beyond the kwaya, wana kwaya wameshakubali somo, katoe injili Jangwani ku convert wengine upanue zizi la kondoo wa bwana. Au basi angalau hao wafuasi wako waambie ukweli. Ukweli wenyewe tabu. Rostam yuko matatani, nani kamtia matatani, Mtikila? Kesha lipa deni?
Dilunga,
Naona Mwanakijiji amekujibu maswali yako katika bandiko lake #67.
Anajua, na sote hapa tunajua kuwa CCM ya sasa haiwezi kumgusa Rostum, lakini kuna umuhimu wa kuendelea "to keep this issue alive." Kwa sababu dunia si static, na Tanzania si static, kuna siku ya siku CCM inaweza kujikuta out of power. Na hapo ndipo Rostum anaweza kuvuliwa chupi, kama alivyosema Yomba Yomba--that is if he will still be in the country when CCM is out of power. Pia at the same time anachofanya Mwanakijiji, kupitia cheche zake, ni ku-preach beyond the choir. Wasomaji wa Cheche watajua kuna utata kuhusu aliposoma Rostum na uraia wake, na huenda ikawa, kama alivyosema Mao, cheche moja ya moto inaweza kuanzisha moto mbugani.
 
Mbona swali la Dilunga nalo halijajibiwa? "source" wetu kishalipa deni?
 
Hivi huyu jamaa ana nguvu kiasi gani?? Ni nini hasa kinapelekea serikari ye Tanzania kuendelea kumuacha?? Rangi yake au?? Tumechoka jamani hebu angalieni watoto wenu wanasoma chini ya miti mpaka leo hii wakati huyu mtu anatuibia pesa zetu ambazo zingeweza kujenga mashule kibao, Walimu wanatishia kuandamana kwani nyie setrikali mnashindwa kumfilisi huyu jamaa mkawalipa walimu?? Naandika haya nikijua wazi kuwa mpo mnaochungulia humu na muwapelekee taarifa hao wakubwa huko juu kwamba tumechoshwa na mwenendo mnaoendelea nao wa kumlinda Rostam sasa bado kuukinai tu na tukikinai na nyie wote hamtarudi madarakani tutapiga magoti na kumlilia Mungu wetu then mtaona cha mtema kuni
 
Kwannini asifanyiwe kama Generali Ulimwengu ambaye tangu utoto wake kama sio kuzaliwa alikuwa Tanzania masikini? Au viongozi wetu wana mpango wa kukimbilia Iran baada ya 'ku-retire'?

Hawezi kufanyiwa kama Ulimwengu kwani yeye hajawatia sirikali vidole kwenye njia ya haja kubwa. Kilichomponza ulimwengu ni pale alipozidisha mashambulizi kwa serikali ya Ben Mkaa Hapa kupitia gazeti la Rai enzi hizo likiwa rai kwelikweli
 
Back
Top Bottom