RIWAYA: Black star

Black Star 28
Tariq Haji
0624065911

Sehemu fulani jukwaani.

"Hamelin, nahisi ni muda muafaka wa kumzuia Chaka. Atamuua kweli".

"Tulia Kendra, muache Chaka atoe hasira zake. Si unajuwa juzi tu kachezea kichapo"

"Hata kama lakini hatuwezi kuacha akamuuwa, lazima na sisi tumfaidi akija katika ligi zetu"

Wakati wanaongea ghafla wakanyamaza, baridi ilitembea katika miili yao kama shoti ya umeme. "Hamelin usinambie Chaka anatumia Agomenti" aliongea Kendra akiangalia uwanjani.

"Una bahati sana kwa kuona jambo zuri kama Agomenti. Inaufanya mwili wangu kuwa mgumu kama chuma" alijisifu Chaka.

"Ago.. sijui ndio nini haitakusaidia. Nitakuonyesha nini maana ya kuwa na mwili wa chuma siyo kama chuma" aliongea Fahad na kujibonyeza sehemu katika kifua chake.

"Ngoja nikupe siri, misuli ya binadamu kawaida hutoa nguvu kwa asilimia thalathini tu katika maisha yote ya uhai wa binadamu. Ni wachache sana wanaoweza kuzalisha nguvu mpka asilimia hamsini, na ndio hao ambao wametamba zaidi duniani na kuwa tishio.

Watu kama kina Bruce Lee, Mohammed Ali na Mike Tyson miongoni mwa wachache waliokuwa na uwezo huwo. Ila kwangu ni tofauti, nitukuonyesha nguvu ya kweli ni ipi" aliongea Fahad kubonyea kidogo.

"Black Star Original: steel pagoda" alinuia, misuli yake ikaanza kutanuka damu nyingi ikaanza kusafiri kwa wingi. Mwili wake utanuka kidogo, "asilimia hamsini" alimwambia Chaka.

"Hahaha, nakupa nafasi moja ufanye shambulizi" aliongea Chaka. Fahad akatabasamu kidogo na "bariked" alikuwa tayari mbele ya Chaka na ngumi yake ilikuwa ishagusa kifua cha mtu huyo. Hakuna aliefahamu nini kimetokea lakini Chaka alijikuta ukutani, sehemu ya kati ya kifua chake ilikuwa imebonyea. "Koh koh" alikohoa na kucheuka damu nyingi.

"Haiwezekani mwili wangu ni mgumu kama chuma nikiwa katika hali ya Agoment lakini mbona unauma kama kawaida" alijisemea huku akishika kifua. Macho yalikuwa yamemtoka mithili ya mjusi aliebanwa na mlangoni.

Chaka akajizoa na kumvamia Fahad kwa nguvu zake zote. Aliweka uwezo wake wote kwenye ngumi hiyo akiwa na lengo la kumaliza pambano hilo. "Kang!" Ngumi hiyo ililia kama iliyokutana na chuma. "Kama mwili wako ni mgumu kama chuma, basi mwili wangu ni chuma chenyewe" alionge Fahad.

Akirudisha mguu nyuma na kuvurumisha ngumi kali sana. Chaka alipoona hana uwezo wa kuikwepa, akakaza misuli yake yote ya mwili ili kustahimili uzito wa ngumi hiyo. "Ikiwa hutakufa basi hutaweza kucheza martial arts tena" aliongea Fahad pindi tu ngumi ilipogusa mwili wa Chaka.

"Aaaaaaah!" Chaka alipiga kelele akijitahidi kukaza zaidi misuli ya kifua na tumbo. Mbavu zikavunjika pamoja na uti wa mgongo, Fahad akaamuwa kulegeza misuli ya mgongo pamoja na mkono. "Bazuka" akanena.

Chaka akatupwa na kujibamiza ukutani. "Koh!" Akakohoa mara moja tu, hata viini vyake vya macho vikapotea. Akaanguka chini na kupoteza Fahamu.

"Nilitegemea hii ngumi ikuuwe lakini inaonekana nimelegeza kidogo" aliongea na kuanza kumfata. "Nakuomba msamehe kakaangu, mimi ndio mwenye makosa. Kama unataka kuuwa niuwe mimi" alishikwa mguu na Monk. Alikuwa akilia mpaka kamasi zikimtoka.

"Siku nyingine mnaponunua ugomvi, jueni kwanza kwanini mumeuziwa" aliongea na kuachia pumzi. Akajitoa mikononi mwa Monk, na kuendelea kutembea alipo Chaka. "Black Star inatosha" Hamelin aliruka kutoka juu na kuingia uwanjani. "Mimi nishamaliza pambano ninachotaka kufanya ni kumsaidia tu. Hatoweza kuishi kama mpiganaji lakini angalau ataweza kuishi maisha ya kawaida" aliongea.

Hamelin alipoona hahisi kiu ya damy kutoka kwa Fahad akasogea pembeni. Fahad akafika mpaka alipo Chaka na kumuinamia kisha akamuweke mkono wa kifua. Baada kama dakika tano Chaka akazunduka. "Ishi vizuri, usipoteze nafasi hii niliyokupa" akainuka na kuondoka. Watu waliyoshuhudia hilo wakapiga makofi.

Don Pizallo akatoka jukwaani na kukimbilia katika chumba cha maandalizi cha Fahad. "Bosi, nipeleke nikapumzike" aliongea Fahad akihisi macho kupoteza nuru. Don Pizallo akamsaidia na kumtoka mpaka nje ya uwanja. Dereva wake akaja kumsaidia, wakumuingiza kwenye gari na kumkimbiza katika nyumba waliofikia.

"Nikilala tu sijui nitaamka lini. Mwili wangu wote unauma kama kidonda kilichochunwa ngozi angali kibichi" aliongea kwa tabu.

"Sawa wewe pumzika, nitamleta daktari akuwekee drip ya chakula" alijibu Don Pizallo. Fahad akajibwaga kitandani na papo hapo usingizi mzito ukamchukuwa.

"Hivi huu ndio uwezo wako wote, master Ge amekupa mafunzo gani. Master Ge umezalisha balaa gani" alijisemea akiwa chumbani kwake. Akato siga na kuwasha, akapiga pafu kubwa. Akiwa katika mawazo hayo simu yake ikaita.

"Don Pizallo, unahitajika makao mkauu ya Indra na Asura".

"Sawa" aliitika na kukata simu. Akairudisha mfukoni na kutoka. Alipofika nje akaacha magizo yote, kisha yeye akaondoka.

"Ohoo! Kijana umerudi tena" aliongea mzee Karakantha. Fahad alipofunguwa macho akajikuta mbele ya mtu huyo. Alikuwa na kikombe cha chai mkononi. "Habari za muda Master" aliongea Fahad. "Unaonekana umefanya vurugu sana huko ulimwenguni".

"Hapana, nilikuwa nanyoosha misuli kidogo tu ila nahisi nimeenda mbali kidogo" alijibu. "Ahahahaha! Hujaenda mbali. Mara ya mwisho tulivyokutana. Nilizifunga meridian zako zote. Nilibakisha mbili tu ili kuzuia uwezo wako" aliongea Mzee Karakantha. "Ndio maana nilikuwa napata tabu sana" alijibu Fahad.

"Nahisi sasa ni muda muafaka wa wewe kujuwa historia ya ulimwengu wa Dao" aliongea mzee Karakantha na kusimam. "Nifuate" aliongea.
 
Black Star 29
Tariq Haji
0624065911

Miaka mingi sana katika kijiji kidogo mbali sana miji mingine. Katika kijiji hicho watu walikuwa wakiendelea na mambo yake kama kawaida. Miongoni mwa hao alikuwa kijana mmoja mwenye umrinkati ya miaka kumi na sita mpaka kumi na nane. Alikuwa amevaa kikapu mgongoni na kilikuwa na matunda aliyokuwa anapeleka sokoni kuuza.

"Minhe, umefika" aliongea mzee mmoja, "ndio mjomba, nimeleta matunda" alijibu Minhe na kuweka kikapu chini. Akayamwaga matunda kwenye gunia ilokuwepo chini. Mjomba ake akayahesabu na kumpa kiasi cha pesa. Minhe akapokea na kuaga akaanza kuondoka. "Masikini, baba ake amekufa amemuacha peke yake. Hata mama ake hamtaki" watu wengine walikuwa wakinong'ona alipokuwa akipita.

"Kazi yao kuongea mambo yasowahusu tu" alijisemea Minhe na kuachana nao. Akatoka nje ya kijiji hicho na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake. Pamoja na kuwa na umri mdogo tayari alishakuwa na mke na mtoto mmoja. Alinunua baadhi ya vitu na kuvitia kwenye kapu. Safari ya kutoka anapokaa ni mbali sana, na alikuwa akipeleka matunda sokoni kwa mwezi mara moja.

Akiwa kilometa kadhaa, ukatokea mlipuko mkubwa katika maeneo karibu na kijiji anachoishi. "Farah, Zayan" alitamka maneno hayo na kutupa kikapu. Akakkimbilia ulipotokea mlipuko huwo. Alipofika kijijini alishuhudia moto mkali ukiendelea kutetekeza nyumba. Miili ya watu ilikuwa imesambaa maeneo mbali mabli. Akakimbilia nyumbani kwake, alipofika akakuta nyumba yake ikiwa mawe tu.

"Farah" aliita kwa nguvu lakini hakukuwa na jibu. Akakimbilia kwenye fusi hilo la mawe na kuanza kuyaondoa. Mawe hayo yalikuwa ya moto lakini hakujali. Macho yalimtoka alipoona mkono wa mkewe. Ulikuwa umerowa damu. "Minhe" aliita Farah kwa sauti ya chini. "Farah usiongee kitu, ngoja nimalizie kutoa mawe".

"Hapana mume wangu, sidhani kama nitapona. Hata nikipona, sidhani kama nitaweza kuishi bila Zayan. Wamichukulia maisha ya mtoto wangu" aliongea huku akilia. "Nisikilize Farah, kama mtoto tutazaa mwengine. Nyamaza mke wangu, maisha hayatakuwa maisha bila uwepo wako" alisisitiza. "Nafurahi kusikia maneno hayo, nakupenda sana na kwa heri mume wangu" pumzi ikaachia mwili wa Farah.

"Farah, Farah amka mke wangu" aliita bila mafanikio. "Pole sana, halikuwa kusudio letu kuleta madhara katika kijiji chako. Tutakupa mali, ukaanze maisha upya sehemu nyingine. Hili eneo kuanzia leo litakuwa ni uwanja wa vita wa sisi miungu" alisikia sauti ikitokea pande zote.

"Hahahaha, mnajiona nyinyi ni miungu. Wapumbavu wakubwa, mnachezea maisha ya watu halafu mnadhani pesa inatosha. Mnadhani kuanza maisha upya ni rahisi kiasi hicho" aliongea Minhe huku akicheka na machozi yakimtoka.

"Wewe ni binadamu tu, sisi ndio tunaamuwa unaishije. Tukiamuwa tukuondoe katika huu ulimwengu basi huwezi kufanya chochote" ile sauti iliongea. "Hahahaha, kama mngekuwa ni miungu msingekuwa na kauli hizo" aliongea.

"Kijana umepewa nafasi ya kuanza maisha upya umeipoteza, kufa" ile sauti ilijibu. Mawingu meusi yakaanza kutanda, "kabla hujaniuwa ningependa kulifahamu jina lako Mungu wa uongo" aliongea Minhe na kujiegemeza mti. "Kuna faida gani ya kulijuwa jina langu wakati unakufa".

"Nataka huko kuzimu nikikutana na wewe nikuue"

"Hahaha, mimi ndio mfalme wa miungu. Mungu wa radi na vita, Mtakatifu Indra" alijitamba. Radi kali sana ikapiga ule mti na kusababisha shimo kubwa. Minhe alizama katika shimo hilo na kupotea kabisa. "Shenzi sana, unajaribu kujibishana na mungu. Sisi ndio tunaamuwa nani aishi na nani afe" alisema Indra. Yale mawingu meusi yakatoweka.

*********
 
TO THE END (MPAKA MWISHO) Ni riwaya inayo fuata baada ya Black Star.

KIONJO KWA UFUPI.............


TO THE END (mpaka mwisho)

KITABU CHA KWANZA

Na Tariq Haji
0624065911



Kalenda ya stela mwaka mia nne na tisini na tisa tokea dunia ilivyobadilisha kalenda yake. Kalenda hiyo imebadilika baada ya dunia kupata wageni kutoka anga za mbali, wageni hao hawakuwa na nia njema na dunia hata kidogo. Hivyo vita kubwa ikazuka na baada ya binadamu kugundua hakuna uwezekano wa kushinda, wachache wakaamua kuungana na wavamizi ili kunusuru maisha yao.

Ni katika nyakati hizo ngumu binadamu wakafanikiwa kupiga hatua moja mbele kiteknolojia. Silaha ya kwanza yenye uwezo wa kuwaumiza wavamizi ikaundwa. Ilikuwa ni robot ambalo liliebdeshwa na binadamu, ilikuwa imebeba silaha nzito ambazo zilikuwa na uwezo wa kusababisha madhara kwa wavamizi.

Hata hivyo halikudumu sana kutokana na marekebisho yake kuwa magumu na yenye kuchukuwa muda. Hata hivyo taratibu binadamu wakaanza kuendelea kiakili na kimwili. Na ni katika huwo binadamu wakagundua uwepo wa chembechembe maalum katika hewa aina 'itharion'.

Chembechembe ambazo ziliwapa uwezo wa ajabu katika kupambana na wavamizi wao. Kwa kupitia majribio mengo hatimae binadamu wakafanikiwa kuunda seli maalum ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya itharion kutoka katika hewa na kuzisambaza katika mwili wa binadamu.

Hilo likapelekea kuzaliwa kwa kizazi cha kwanza binadamu wapya ambao walitumika kama wanajeshi katika vita dhidi ya wavamizi. Miaka baadae binadamu wakapiga hatua nyingine na kusababisha mageuzi makubwa ya kiteknolojia.

Kwa kutumia vyuma vilivyong'oka kutoka katika mashine za wavamizi walifanikiwa kutengeneza maroboti yenye uwezo wa hali na ustadi mkubwa. Na kutokea hapo vita ikawa nyepesi na pia binadamu wakafungua kurasa mpya katika maisha yao. Kalenda ikabadilishwa na kuitwa kalenda ya stela ikiwa na maana mwaka ambao dunia ilishuhudia uvamizi na pia milango mipya ikafunguka.
**********
Republic of Iron City (mji wa chuma).
Taratibu na maandalizi ya kushherekea siku ya uhuru mwaka mia nne na tisini na tisa ziliendelea. Kila mti alionekana kuzama katika maandalizi hayo.

"Mlemavu anapita" minong'ono ilisikika kila alipokuwa akipita, kijana mwenye nywele nyeusi kuliko na macho ya rangi hazel. Alikuwa akiburuza kitoroli ambacho kilikuwa na maji ya sabuni ndani kwa ajili kufanyia usafi.

"Oooow! Kama sio Baston" kija mmoja mwenye nywele za kijani kibichi akasimama mbele ya kitoroli hicho na kumfanya Baston ashindwe kuendelea na safari yake. "Edward, unataka nini" aliuliza Baston akimuangalia usoni kijana huyo aliesimama mbele yake.

"Inaonekana kipigo cha nyuma hakijakutosha, nilikwambia unaponiona mimi huruhusiwi kuniangalia usoni" aliongea Edward na kuwapa ishara vibwengo wake.

"Inatosha" sauti laini ya mtoto wa kike ikasikika ikitokea mbali kidogo na wakipokuwa wamesimama. Ikafuatiwa na harua za taratibu kabisa ambazo kila zilipokanyaga ardhi zilitoa tafsiri ya mtu huyo aliekuwa anakuja.

"Shanequeen, hilo halikuhusu. Wewe endelea na mambo yako" aliongea Edward akimuangalia binti huyo aliekuwa anatembea kwa mwendo wa madaha.

Shida nyingine iliyozuka baada ya binadamu kugundua uwepo wa itherion ni matabaka. Japo mwanzo yalikuwepo lakini baada ya miaka kadhaa kupita yakaongezeka na kuwa makubwa zaidi. Baada ya miaka miambili wakaanza kuzaliwa watoto ambao moja kwa moja walizaliwa na uwezo wa kunyonya itherion kutoka kwenye hewa.

Hawa waliitwa kizazi cha nne na hilo likapelekea kutokea kwa familia ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya itherion kwa wingi mno hivyo kuwafanya kuwa na nguvu kuliko wengine wa tabaka hilo na pia kuwa na uwezo zadi kuliko raia wa kawaida.

Yakatengezwa madaraja ambayo yaliwawakilisha watu wenye uwezo wa kutumia itherion. Yalianza na F ambayo iliwakilisha wale wenye uwezo wa chini zaidi ambao hawa walikuwa ni raia wa kawaida.

E iliwawakilisha wale wenye wa juu kidogo kuliko F lakini hawakuwa na uwezo wa kuingia vitani. Hawa wao walikuwa ni kundi lilihusika na marekebisho ya maroboti ya kivita.

D iliwawakilisha wale ambao walikuwa na uwezo wa karibia na kati. Kundi hili lilikuwa la watu waliongia vitani lakini kwa ajili ya kutoa msaada tu.

C iliwawakilisha kundi la wanajeshi wa kawaida, walihusika na kupanda na viumbe wenye uwezo wa chini.

B iliwawakilisha kundi la majenerali, hawa walipambana na viumbe wenye uwezo wa kati.

A iliwawakilisha kundi la makomanda, hawa walikuwa wachache na walikuwa na uwezo wa kupambana na viumbe wenye uwezo wa juu.

S iliwakilisha kundi la asilimia moja tu la binadamu wote, hawa walikuwa na uwezo wa hali ya juu sana na waliweza kupambana na viumbe waliokuwa na uwezo zaidi.

SS, kundi hili lilichangia asilimia sifuri nukta tano ya watu wote duniani, na waliotambulika kuwa katika hili hawakuzidi hata kumi. Ni kundi la watu maalum ambalo halikuwa na mfano wake mpaka wavamizi walikuwa wakiliogopa kundi hili.

Kwa kesi ya Baston, yeye hakuingia katika kundi lolote kati ya hayo nane. Alizaliwa na kutokuwa na uwezo wa kunyonya itherion kabisa. Hivyo kundi la watu kama yeye lilipewa jina la walemavu na uwepo wao haukuwa na tofauti na takataka.

Edward na Shanequeen walikuwa ni daraja A huku Shanequeen akiwa juu kidogo kiuwezo kuliko Edward.

"Ahsante" Baston aliongea na kuvita kitoroli chake nyuma, akapita pembeni na kuelekea ilipo henga namba tano ambako ndipo alipopangiwa kufanya usafi. Katika henga hiyo kulikuwa roboti moja tu ambalo lilikuwa kongwe mno. Pamoja na kutelekezwa huko Baston alihakikisha kila siku analisafisha.

"Fuata upepo, utasafiri katika gharika" ndio maneno yaliokuwa yameandikwa kwenye kifuoa chanroboti huyo. Baada ya usafi, Baston akakaa pembeni ya roboti hilo na kuongea "thamani yako inakuwepo pale unapokuwa na jambo la kuwapa tu" aliongea na kuliangalia.

"Sijui nani alikuwa rubani wako lakini naamini kabisa kipindi chako ulikuwa bingwa" aliendelea na kugusa mkono wa roboti hilo.

"Mpaka sasa nahisi hamu yako ya kuingia vitani", Baston alikuwa akiongea mwenyewe na kufanya kama vile chuma hicho chakavu kilikuwa kinamsikia. "Hata mimi nilikuwa na ndoto ya siku moja kusimama vitani kupigania nchi yangu lakini wachache wakaamua kuwa siwezi kufanya hivyo kutokana na mwili wangu kushindwa kunyonya itherion kutoka katika hewa".

Ghafla kigora kikasikika na taa nyekundu za henga hiyo zikaanza kuwaka, "vikosi vyote katika henga zenu na mjiandae na vita, tunasoma mawimbi ya itherion ya wavamizi" sauti ilisikika kutoka katika speaker maalum ndani ya henga hiyo.

"Wale ambao siyo wanajeshi mnatakiwa kuwa watulivu"

"Vikosi vyote katika henga zenu na mjiandae na vita" kauli hiyo.

"Nichukue vitani, nataka kusimama kwa mara ya mwisho", Baston akasikia sauti lakini eneo hilo alikuwa yeye peke yake na roboti huyo.

"Upweke wangu naona sasa unanifanya kusikia sauti" alijisemea.

"Nichukue vitani, nataka kwenda zangu kama shuja na siyo chuma chakavu" alisikia tena sautu. Alipogeuza uso kuangalia akakutana na macho ya roboti huyo yaakiwa yanawaka taa nyekundu.

_ca2b3fe1-00e3-411e-9792-65c33b1d8d82.jpeg
 
TO THE END (MPAKA MWISHO) Ni riwaya inayo fuata baada ya Black Star.

KIONJO KWA UFUPI.............



TO THE END (mpaka mwisho)

KITABU CHA KWANZA





Na Tariq Haji



0624065911



Kalenda ya stela mwaka mia nne na tisini na tisa tokea dunia ilivyobadilisha kalenda yake. Kalenda hiyo imebadilika baada ya dunia kupata wageni kutoka anga za mbali, wageni hao hawakuwa na nia njema na dunia hata kidogo. Hivyo vita kubwa ikazuka na baada ya binadamu kugundua hakuna uwezekano wa kushinda, wachache wakaamua kuungana na wavamizi ili kunusuru maisha yao.



Ni katika nyakati hizo ngumu binadamu wakafanikiwa kupiga hatua moja mbele kiteknolojia. Silaha ya kwanza yenye uwezo wa kuwaumiza wavamizi ikaundwa. Ilikuwa ni robot ambalo liliebdeshwa na binadamu, ilikuwa imebeba silaha nzito ambazo zilikuwa na uwezo wa kusababisha madhara kwa wavamizi.



Hata hivyo halikudumu sana kutokana na marekebisho yake kuwa magumu na yenye kuchukuwa muda. Hata hivyo taratibu binadamu wakaanza kuendelea kiakili na kimwili. Na ni katika huwo binadamu wakagundua uwepo wa chembechembe maalum katika hewa aina 'itharion'.



Chembechembe ambazo ziliwapa uwezo wa ajabu katika kupambana na wavamizi wao. Kwa kupitia majribio mengo hatimae binadamu wakafanikiwa kuunda seli maalum ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya itharion kutoka katika hewa na kuzisambaza katika mwili wa binadamu.



Hilo likapelekea kuzaliwa kwa kizazi cha kwanza binadamu wapya ambao walitumika kama wanajeshi katika vita dhidi ya wavamizi. Miaka baadae binadamu wakapiga hatua nyingine na kusababisha mageuzi makubwa ya kiteknolojia.



Kwa kutumia vyuma vilivyong'oka kutoka katika mashine za wavamizi walifanikiwa kutengeneza maroboti yenye uwezo wa hali na ustadi mkubwa. Na kutokea hapo vita ikawa nyepesi na pia binadamu wakafungua kurasa mpya katika maisha yao. Kalenda ikabadilishwa na kuitwa kalenda ya stela ikiwa na maana mwaka ambao dunia ilishuhudia uvamizi na pia milango mipya ikafunguka.



**********



Republic of Iron City (mji wa chuma).



Taratibu na maandalizi ya kushherekea siku ya uhuru mwaka mia nne na tisini na tisa ziliendelea. Kila mti alionekana kuzama katika maandalizi hayo.



"Mlemavu anapita" minong'ono ilisikika kila alipokuwa akipita, kijana mwenye nywele nyeusi kuliko na macho ya rangi hazel. Alikuwa akiburuza kitoroli ambacho kilikuwa na maji ya sabuni ndani kwa ajili kufanyia usafi.



"Oooow! Kama sio Baston" kija mmoja mwenye nywele za kijani kibichi akasimama mbele ya kitoroli hicho na kumfanya Baston ashindwe kuendelea na safari yake. "Edward, unataka nini" aliuliza Baston akimuangalia usoni kijana huyo aliesimama mbele yake.



"Inaonekana kipigo cha nyuma hakijakutosha, nilikwambia unaponiona mimi huruhusiwi kuniangalia usoni" aliongea Edward na kuwapa ishara vibwengo wake.



"Inatosha" sauti laini ya mtoto wa kike ikasikika ikitokea mbali kidogo na wakipokuwa wamesimama. Ikafuatiwa na harua za taratibu kabisa ambazo kila zilipokanyaga ardhi zilitoa tafsiri ya mtu huyo aliekuwa anakuja.



"Shanequeen, hilo halikuhusu. Wewe endelea na mambo yako" aliongea Edward akimuangalia binti huyo aliekuwa anatembea kwa mwendo wa madaha.



Shida nyingine iliyozuka baada ya binadamu kugundua uwepo wa itherion ni matabaka. Japo mwanzo yalikuwepo lakini baada ya miaka kadhaa kupita yakaongezeka na kuwa makubwa zaidi. Baada ya miaka miambili wakaanza kuzaliwa watoto ambao moja kwa moja walizaliwa na uwezo wa kunyonya itherion kutoka kwenye hewa.



Hawa waliitwa kizazi cha nne na hilo likapelekea kutokea kwa familia ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya itherion kwa wingi mno hivyo kuwafanya kuwa na nguvu kuliko wengine wa tabaka hilo na pia kuwa na uwezo zadi kuliko raia wa kawaida.



Yakatengezwa madaraja ambayo yaliwawakilisha watu wenye uwezo wa kutumia itherion. Yalianza na F ambayo iliwakilisha wale wenye uwezo wa chini zaidi ambao hawa walikuwa ni raia wa kawaida.



E iliwawakilisha wale wenye wa juu kidogo kuliko F lakini hawakuwa na uwezo wa kuingia vitani. Hawa wao walikuwa ni kundi lilihusika na marekebisho ya maroboti ya kivita.



D iliwawakilisha wale ambao walikuwa na uwezo wa karibia na kati. Kundi hili lilikuwa la watu waliongia vitani lakini kwa ajili ya kutoa msaada tu.



C iliwawakilisha kundi la wanajeshi wa kawaida, walihusika na kupanda na viumbe wenye uwezo wa chini.



B iliwawakilisha kundi la majenerali, hawa walipambana na viumbe wenye uwezo wa kati.



A iliwawakilisha kundi la makomanda, hawa walikuwa wachache na walikuwa na uwezo wa kupambana na viumbe wenye uwezo wa juu.



S iliwakilisha kundi la asilimia moja tu la binadamu wote, hawa walikuwa na uwezo wa hali ya juu sana na waliweza kupambana na viumbe waliokuwa na uwezo zaidi.



SS, kundi hili lilichangia asilimia sifuri nukta tano ya watu wote duniani, na waliotambulika kuwa katika hili hawakuzidi hata kumi. Ni kundi la watu maalum ambalo halikuwa na mfano wake mpaka wavamizi walikuwa wakiliogopa kundi hili.



Kwa kesi ya Baston, yeye hakuingia katika kundi lolote kati ya hayo nane. Alizaliwa na kutokuwa na uwezo wa kunyonya itherion kabisa. Hivyo kundi la watu kama yeye lilipewa jina la walemavu na uwepo wao haukuwa na tofauti na takataka.



Edward na Shanequeen walikuwa ni daraja A huku Shanequeen akiwa juu kidogo kiuwezo kuliko Edward.



"Ahsante" Baston aliongea na kuvita kitoroli chake nyuma, akapita pembeni na kuelekea ilipo henga namba tano ambako ndipo alipopangiwa kufanya usafi. Katika henga hiyo kulikuwa roboti moja tu ambalo lilikuwa kongwe mno. Pamoja na kutelekezwa huko Baston alihakikisha kila siku analisafisha.



"Fuata upepo, utasafiri katika gharika" ndio maneno yaliokuwa yameandikwa kwenye kifuoa chanroboti huyo. Baada ya usafi, Baston akakaa pembeni ya roboti hilo na kuongea "thamani yako inakuwepo pale unapokuwa na jambo la kuwapa tu" aliongea na kuliangalia.



"Sijui nani alikuwa rubani wako lakini naamini kabisa kipindi chako ulikuwa bingwa" aliendelea na kugusa mkono wa roboti hilo.



"Mpaka sasa nahisi hamu yako ya kuingia vitani", Baston alikuwa akiongea mwenyewe na kufanya kama vile chuma hicho chakavu kilikuwa kinamsikia. "Hata mimi nilikuwa na ndoto ya siku moja kusimama vitani kupigania nchi yangu lakini wachache wakaamua kuwa siwezi kufanya hivyo kutokana na mwili wangu kushindwa kunyonya itherion kutoka katika hewa".



Ghafla kigora kikasikika na taa nyekundu za henga hiyo zikaanza kuwaka, "vikosi vyote katika henga zenu na mjiandae na vita, tunasoma mawimbi ya itherion ya wavamizi" sauti ilisikika kutoka katika speaker maalum ndani ya henga hiyo.



"Wale ambao siyo wanajeshi mnatakiwa kuwa watulivu"



"Vikosi vyote katika henga zenu na mjiandae na vita" kauli hiyo.



"Nichukue vitani, nataka kusimama kwa mara ya mwisho", Baston akasikia sauti lakini eneo hilo alikuwa yeye peke yake na roboti huyo.



"Upweke wangu naona sasa unanifanya kusikia sauti" alijisemea.



"Nichukue vitani, nataka kwenda zangu kama shuja na siyo chuma chakavu" alisikia tena sautu. Alipogeuza uso kuangalia akakutana na macho ya roboti huyo yaakiwa yanawaka taa nyekundu.










View attachment 2848504
Vitu vyako mkuu sio vya nchi hii, nakubali sana kazi za mikono yako na Mungu akubariki sana uendelee kutuburudisha kama hivi na zaidi.
 
Vitu vyako mkuu sio vya nchi hii, nakubali sana kazi za mikono yako na Mungu akubariki sana uendelee kutuburudisha kama hivi na zaidi.
tuombe uzima tu. maana hapa JF kuna kurasa wenye nazo wapo chini ya dunia wamefunikwa na mchanga. Kalam zao hazitumiki tena
 
Black Star 30

Tariq Haji

0624065911

Usikae chini ya huwo mti, inasemekana mtu alokufa hapo aliwauzi miungu aliongea mpita njia
mmoja. Alikuwa amevaa kofia kubwa iliyosukwa kwa ukili na mgongoni alikuwa na kikapu kilichokuwa na mawe. Samahani kama hutojali naomba nikuulize, mimi hapa siyo mwenyeji aliongea na kusimama. Uliza tu hakuna shida alijibu yule mpita njia.

Nimesafiri kutoka mji wa mbali sana, na sasa nimechoka. Nilikuwa natafauta sehemu ya kulala
aliongea. Kuna kijiji kipo umbali siku moja kutoka hapa, na mimi naelekea huko. Unaweza kuuungana na mimi kwasababu usiku unakaribia na kusafiri peke yako usiku ni hatari alijibu na kutabsamu.

Ahsante ipo siku nitakulipa wema wako alijibu na kuungana na mzee huyo. Wakaanza safari
kuelekea chini ya mlima. Baada ya mwendo mrefu mzee huyo alionekana kuishiwa pumzi, naomba nikusaidie mzee wangu aliongea.

Hapana kijana, huu mzigo nauweza vizuri. Tukipata mapumziko kidogo nitaubeba bila shida alijibu mzee huyu na kutabasamu. Tabasamu hilo lilificha maumivu makali sana aliokuwa akiyapata mzee huyo.

Basi tupumzike hapa kabla ya kuendelea na safari aliongea nakumsaidia mzee huyo kutuwa mzigo.

Ahsante mwanagu alishukuru na kukaa kitako, mgongo wake ulikuwa umerowa damu kutokana na
kubeba mzigo huwo mzito kwa muda mrefu. Tunatembea pamoja lakini bado hatujuani majina, mimi naitwa Karakantha aliongea na kujitambulisha.

Mimi naitwa Pinyai alijibu yule mzee na kutabasamu. Mdomo wake ulikuwa umepunguwa meno kadhaa lakini alionekana kufurrahia uwepo wa Karakantha.

“Mzee wangu naomba nikuulize kama hutojali

“Hakuna shida kijana

Umri wako unaonekana mkubwa lakini unaenda mbali na mzigo mzito peke yako, kwani nyumbani
hakuna kijana wa kufanya kazi hii.

Nafahamu kama wewe ni mgeni hili hivyo hufahamu nini kinaendelea katika eneo hili. Kwa miezi
mitatu sasa tumekumbwa na ugonjwa mbaya sana. Tumeutibu kwa dawa zote lakini hakuna hata moja iliosaidia. Nimesikia kuwa katika kijiji cha chini ya huu mlima kuna mtu ana dawa ambayo ina uwezo wa kutibu ugonjwa huu. Akakohoa kidogo na kutema damu nyeusi, Karakantha akamuangalia kwa makini.

Huwo si ugonjwa bali na madhara ya kuvuta hewa chafu kwa muda mrefu. Hakuna dawa inayoweza
kuutibu huwo ugonjwa ila sio kama hautibiki aliongea Karakantha.

Kijana wewe ni daktari au vipi aliuliza mzee huyo.

Ndio mimi ni daktari alijibu.

Mwanangu mimi sina cha kukupa ila kama unaweza turudi nyumbani kwangu, ukamponye
mwanangu tu. Yeye ndio mwanangu wa pekee, hapa nilikuwa napeleka haya mawe katika hicho kijiji ili kubadilisha kwa dawa. Mawe yote haya ni muhimu sana katika familia yangu aliongea na kupiga magoti.

Kwanza kabla ya kurudi huko nyumbani kwako, ngoja nikuponye wewe kwanza. Sihitaji unilipe
chochote zaidi ya kunipatia sehemu ya kulala tu

Kweli mwanangu ubarikiwe na Mungu yeyote yule alienikutanisha na wewe, kusikia hivyo
Karakantha akatabasamu. Alifahamu kama kuna watu walikuwa hawaamini katika hao miungo wa uongo. Vua nguo yako ya juu, nitakachokifanya ni kurekebisha mzunguko wako wa Qi ambao ndio ulioathirka zaidi. Utahisi maumivu makali sana lakini yakupasa uvumilie alimpa maelekezo.

Kama maumivu nishapata ya kutosha, hakuna kipya alijibu yule mzee na kuvua nguo yake ya juu.

Akakaa kitako na kumpa mgongo Karakantha, Karakantha akamuwekea mkono wa mgongo na
kuanza kusafirisha Qi yake kueleka katika mwili wa mzee huyo. Mzee Pinyai akaanza kukohoa damu nyingi, ilikuwa nyeusi na yenye harufu.

Alipata maumivu makali sana mpaka machozi yakaanza kumtoka lakini hakufunguwa mdomo kupiga kelele. Baada ya dakika tano zoezi likawa limekamilika, mzee Pinyai akaanguka na kupoteza fahamu.

Karakantha akamsogeza pembeni kumfunika kwa nguo, yeye akavua nguo na yake ya juu na kuanza
kufanya mazoezi pamoja na kurudisha Qi aliopoteza wakati wa kumtibu mzee Pinyai. Aliendelea kufanya mazoezi mpaka kulipokucha.

Mzee Pinyai akaamka na kujinyoosha, unajisikiaje aliuliza Karakantha. Sijawahi kujisikia na afya
kiasi hiki kwa muda mrefu sana. Ni kama ujana wangu umerudi tenaaliongea na kusimama. Akaanza kujinyoosha, ahsante mwanagu, ipo siku nitakulipa aliongea na kuinamisha kichwa. Bila kuchelewa tunaweza kuondoka, hali ya hewa inaoneka si nzuri aliongea Karakantha.

Mzee Pinyai akanyanyua kikapu chake na kukipachika mgongoni, twende, kutokana na hali ya mwili
wangu, tunaweza fika nyumbani wakati jua linapinduka aliongea Mzee huyo. Alionekana kujaa maisha, alitembea kwa mwendo wa haraka. Kama alivyosema, jua lilivyoanza kupinduka tayari walishakiona kijiji. Kilikuwa katika ardhi iliokauka, haikuonesha kuwa uhai hata kidog.

Mbona umerudi mapema alifika mtu mmoja na kuongea, nimeshushiwa baraka mimi, njiani
nimekutana na daktari. Amenitibu kabisa shida yangu, na amesema atamtibu kila mtu bure. Anataka sehemu ya kukaa tu aliongea bila kuficha furaha yake. Kweli unaweza kututibu aliuliza mtu huyo, kama alivyosema mzee Pinyai alisema.

Wanakijiji hao walimpokea kwa furaha sana, kwao alikuwa kama masia wa mungu aliekuja
kuwatatulia tatizo lao. Karakantha alitumia siku saba mpaka kumaliza kuwapa tiba wana kijiji wote.

Ahsante sana, sijui hata tukupe nini aliongea kiongozi wa kijiji hicho. Kama hamutojali naweza
kuongea na wazee wa kijiji, kuna jambo la muhimu nataka kuwaambia aliongea. Wazee wakakubali na kuamua kukutana nae siku ya pili.

Enhe kijana wetu, tunasubiri ulichotaka kutueleza aliongea kiongozi wa kijiji, wazee wangu mimi
naomba niishi hapa, hapa ndio yawe makazi yangu. Nimefurahi sana kuona watu wa kijiji hichi walivyokuwa na upendo. Nataka niwasaidie kurudisha hali nzuri katika kijiji hichi, vitabu vya historia vimeanidika kuwa kijiji hichi kilikuwa na uoto mzuri sana wa asili. Kurudisha uoto huwo itachukuwa muda mrefu lakini mukikubali niishi hapa hamtaishi na njaa tena katika maisha yenu aliongea kwa kujiamini.

Utawezaje kufanya hivyo, kijiji hiki kiko mbali sana na vijiji vingine. Hata kufanya nao biashara ni
ngumu aliuliza Mzee Pinyai.

Wala usijali, hakuna mtu atakaetoa mguu wake katika kijiji hiki. Watu wa vijiji vingine ndio
watakaokuja hapa alijibu na kuendelea mnachotakiwa kufanya ni kusambaza tu taarifa kuwa ule ugonjwa sugu unaowasumbuwa unatibika. Baada ya hapo niachieni mimi alikuwa akijiamini sana.

Na kweli vijana walipewa kazi ya kusambaza taarifia hizo kadri walivyoweza, baada ya wiki moja
watu wakaanza kumiminika katika kijiji hicho kwa ajiliya kupata tiba. Wapo ambao walisubiri majibu ya wenginie waliokwenda. Baada ya mwezi mmoja, mpaka watu wa kubwa wa ngome mbali mbali walifika kwa ajili ya kupata tiba katika kijiji hicho.


Tiba aliyotoa haikuwa na kiwango maalum cha malipo. Masikini walitoa hata mbegu za miti, ila matajiri walimwaga tael nyingi sana (tael ni vipande vya shaba, silver na dhahabu ambavyo vinatumika kama pesa katika ulimwengu wa Dao). Watu wa kijiji hicho walifurahi sana, maisha yao yalibadilika kabisa.

Jioni ya siku hiyo kulikuwa na kikao kingine cha wazee mapoja na Karakantha. "Leo kuna jambo jingine nataka niwaambie" alianza kuongea, wazee wote wakainuwa masikio ili kumsikiliza.

"Kijiji chetu sasa kinatajirika, lakini hakina mipaka wala ulinzi wa kutosha. Hawa hawa tunaowapa tiba, huenda wakatugeuka na kutaka kutupora mali yote tulikusanya. Hivyo basi napendekeza tuanze kujenga kuta amabazo zitafanya kazi kama mstari wa kwanza wa ulinzi ili kuhakikisha maisha yetu yanakuwa salama" aliongea.

"Lakini kijiji hiki kina watu wa chache sana, itatuchukuwa muda mpaka kuukamilisha ukuta huwo" aliongea Mzee Pinyai.

"Kuhusu nguvu kazi watu usijali, vijana wapo wa kutosha na wana uwezo wa kuujenga bila shida yeyote ile. Ila ukuta huu tutaujenga kwa siri. Tutaudhihirisha pale utakapo kamilika tu" aliongea. Wazee wakaguna, hawakuelewa ukuta mkubwa utajengwaje kwa siri kiasi cha watu kutoushuhudia.

"Na tutajengaje" aliuliza kiongozi wa kijiji. "Hapa kijijini tutaendelea kama kawaida, ila umbali wa safari ya siku moja ndipo tutakapoujenga ukuta huwo. Baada ya kukamilika tutajenga na nyumba kisha watu watahama kutoka hapa na kuelekea katika kijiji hicho kipya. Na yote hayo yatafanyika nyakati za usiku.

Wazee wa kijiji walisikiliza mipango ya Karakantha kwa makini zaidi. Mwisho wakakubaliana nae. Usiku huwo huwo wakaitisha mkutano na wanakijiji wengi. Walipohakikisha hakuna mgeni kati yao. Wakatoa taarifa hiyo. Muitikio ukawa mkubwa sana. Si vijana tu, mpaka waschana na wakina mama wenye umri wa kati wakajitolea kushiriki.

Kikao kiliisha na kila mtu akaelekea kupumzika. "Hatuwa ya kwanza imekamilika, sasa hatuwa ya pili" alijesemea Karakantha akiwa nyumbani kwake. Akatoa karatasi kubwa na kuanza kuchora ramani ya ukuta huwo. Kwa wanakijiji ulikuwa ni ukuta tu ila kwa Karakantha alikuwa anajenga ngome, amabayo itasimama miaka na miaka.

Siku ya pili wanakijiji wakiendelea na maisha yao kama kawaida. Jioni Karakantha na wazee wachache wakatoka kijijini na kuelekea huko wanapotegemea kujenga ukuta. Walipofika walitalii eneo hilo vizuri. Karakantha akaweka mipaka na kuwapa maelekezo wazee. Baada ya zoezi hilo wakarudi kijijini na kupumzika.

Siku mzee Pinyai na mtoto wake wakaelekea sokoni kwa ajili ya kununuwa vitendea kazi. Walirudi baada ya siku tatu wakiwa na mzigo wa kutosha. Baada ya hapo kazi ikaanza, usiku watu walifanya kazi mchana walilala. Kazi hiyo ilifanyika kwa usiri wa hali ya juu.

Kijijini Karakantha aliendelea kutoa tiba kama kawaida. Sasa alitumia miti shamba kutengeza dawa aina mbali mbali. Jina lake likakuwa na kusafiriki kusini na kaskazini. Magharibi na mashariki.

**********
 
BLACK STAR. 31
Na
TARIQ HAJJ

Katika milima ya Range.

"Mkuu, nimesikia taarifa kuwa kuna kijiji cha hovyo kina mali nyingi sana" alifika mtu mmoja na kutoa taarifa. "Ongea" alijibu kiongozi huyo, "inasemekana kuwa kuna daktari ana uwezo wa kutibu ugonjwa wowote ule" alifafanua.

"Tukimkamata akatufanyia kazi sisi, tutajijirka" aliongea kiongozi huyo na kutabasamu. Kisha akaendelea kuongea "waambie vijana wajiandae, tutakivamia katika usiku wa mbala mwezi, mwezi ukipinduka" alitoa maelekezo.

Hicho kilikuwa kikundi cha wezi machachari, walishashindikana kila eneo. Na kila walipokaa walifukuzwa kutokana na kusababisha majanga. Katika milima hiyo ya Range ndio palikuwa nyumbani kwao kwa sasa. Shida kubwa waliokuwa nayo hapo ni chakula, kilikuwa cha tabu sana.

Kikundi hicho kilikuwa na watu zaidi ya miambili. Wengi wao walikuwa watafutwa sugu na wengine walikuwa ni watu waliofanya matukio na kukimbia mkono wa sheria.

Siku ya mbala mwezi.

Siku hiyo Karakantha alibaki kijijini usiku kwa ajili ya kumshuhulikia mama mja mzito. Alikuwa akikaribia kujifunguwa, "kuna nzi wanazunguka katika mipaka ya kijiji changu" alijisemea na kumalizia kuzalisha. Akawaachia wakunga wengine wamalizie, yeye akatoka nje. Kitendo cha kukanyaga tu kizingiti, akapotea.

Alisimama sehemu moja nje ya kijiji, "nyinyi ni kina nani na mumefata nini kijijini kwangu" aliuliza kwa sauti. "We mzee huna la kufanya, kijiji chako chote tumekizunguka" alijibu mtu mmoja. "Nawapa nafasi moja tu, ondokeni kama munayapenda maisha yenu".

Wakati anaongea akasikia hatuwa nyuma yake, "usijaribu, kabla hiyo panga yako haijanifika kichwa chako kitakuwa chini" aliongea.

"Samahani mkuu, tumekosea kuvamia kijiji chako. Tunaondoka" aliongea kiongozi wa kundi hilo. "Mkuu unafanya nini, tumesafiri muda mrefu sana. Tunakaribia kutimiza lengo letu unasema tunaondoka" aliongea mmoja wao. "Nyamaza wewe mpumbavu, unataka tufe hapa. Mimi sijakimbia huko nilipo ili nije kufa sehemu ambayo haijulikani" aliongea kiongozi huyo.

Alifahamu kabisa kuwa vijana wake, hawakuhisi alichokihisi yeye. Lakini hapo alipo alikuwa akipata tabu sana kupumuwa. Alihisi hewa ni nzito, ukiachia usiku huwo kuwa na baridi lakini alikuwa akivuja jasho kama mtu aliekimbia kwa muda mrefu katika jua kali sana.

"Samahani mkuu lakini hatuwezi kufanya hivyo" alisikia sauti hiyo ikitokea pembeni yake na kuhisi kitu chenye ncha kali sana kikizama chini ya mbavu. "Kuna tajiri ameahidi, tukimpelekea huyo daktari atatukaribisha nyumbani kwake na kutupa vyeo" aliongea mtu huyo ambae alikuwa ni yule aliepeleka taarifa.

"Watu kuanzia sasa mimi ndio kiongozi wenu na hii ni amri yangu ya kwanza. Muueni huyo mpuuzi na tumtafute huyo daktari" aliongea kwa nguvu. Ghafla akapigwa kikumbo na kutupwa mbali kidogo. "Nisikilizeni mimi, hamumuwezi huyo mtu. Mkimsikiliza huyu mjinga mtakufa nyote. Huyu anaonekana ni master kabisa" aliongea yule kiongozi aliyechomwa kisu.

Kikundi cha watu kama watatu hivi wakapita mbele na kumnyanyua. "Sisi tunamuamini huyu, hajawahi kutupeleka katika kifo chetu" walimnyanyua na kuanza kuondoka. Watu zaidi ya hamsini wakakubaliana na hilo na kuanza kuondoka.

"Hao waliyoondoka ni wasaliti, kwanza tunaanza na huyu mjinga kisha tuna.." hakumaliza kichwa chake kikaanguka chini. "Kijana umekosa hekima" aliongea Karakantha akikumuta mkono wake uliokuwa na damu.

"Umeona, amemkata kichwa kwa mkono"

"Hapana mbona mimi nimeona kama alikuwaa na kisu".

"Acha ujinga wewe, ametumia mkono bila silaha yeyote ile".

"Naomba uwaache waondoka kama unataka kuwauwa, najitolea mimi. Waache watu wangu waende zao" aliongea yule kiongozi alokuwa na jeraha. "Hapana, sina mpango wa kuwauwa na pia sina mpango wa kuwaachia. Ngoja niokoe maisha yako kisha tutaongea vizuri".

*************************************
 
BLACK STAR. 32
NA
TARIQ HAJJ

Akawaamuru watu wawili wamsaidie, wakampeleka mpaka nyumbani kwa Karakantha. Walipomlaza akawaamuru wote watoke na kuwaonye wasije wakafanya chochote. Mpaka wakati huo hawakuhitaji onyo lolote lile walishajuwa kabisa kama maisha yao mbele ya mtu huyo hayana thamani yeyote.

Wakiwa nje wanasubiri walisikia ukwenzi mkali sana. Walitamani waingie ili kujuwa nini kinaendelea lakani haikuwezekana. Wote waliogopa hata kugonga mlango. Baada ya masaa mawili, Karakantha akatoka na kuwaruhusu waende kumuona. Alikuwa kapitiwa na usingizi kabisa.

"Mnaweza kubaki hapa mpaka atakapoamka" aliwaambia na yeye akaondoka. Alitoka mpaka nje ya kijiji na kuanza kufanya mazoezi, alioga katika mwanga wa mwezi. Alfajiri ikamkuta akiwa nje ya kijiji, mwili wake ulikuwa umetota kwa jasho. "Vizuri sana, nimefanikiwa kufika daraja la Qin" alijisemea akiwa anarudi nyumbani kwake.

"Anaendeleaje" akwauliza alowakuta nje, "ndio kwanza ameamka" alijibu mmoja. Karakantha akaingia ndani na kumkuta akiwa amekaa. Yule kiongozi alipomuona tu alipiga magoti. "Ahsante kwa msaada wako, sijui nitakulipa nini" aliongea na kutaka kusujudu. Karakantha akamazuia, na kumpa ishara amfuate nje.

Pamoja na watu wake wakatembea mpaka nje ya kijiji. "Unaweza kubadilisha maisha yako, hujachelewa bado" aliongea Karakantha akilishangaa jua. "Kwa mambo ambayo nimeyafanya, sidhani hata hao miungu watananisamehe" alijibu akiwa kajiinamia.

"Mimi naitwa Karakantha, sijui wewe" alijitambulisha. "Mimi naitwa Ge Rhong" alijibu yule kiongozi. "Ge, ungana na mimi. Nina ndoto kubwa sana" aliongea na kumuangalia. Hapo walikuwa wawili tu, wengine wote walikuwa mbali.

"Mtu kama mimi sina nafasi katika ndoto, nitaichafuwa tu. Nimefanya makosa mengi sana" aliongea. "Kwanza nikuambie kitu, hao unaowafikiria ni miungu ni waongo tu. Hawana lolote, ni binadamu kama sisi tu isipokuwa wanaa uwezo zaidi kuliko sisi" aliongea na kuonesha chuki ya dhati.

"Baada ya hao sifahamu kama kuna miungu mingine. Nimekuwa nikiwa nawaabudu hao" alijitetea Ge Rhong. "Itakuwaje nikikwambia yupo ambae ana cheo hicho na yeye ndie aliewazadia uwezo baadae wakamsaliti".

"Kwasasa siwezi kuyaamini au kuyakataa mawazo yako lakini kwasababu umenisaidia na mimi nitakulipa kwa kukufuata" aliongea Ge Rhong.

"Kwasasa hilo linatosha, nashukuru" alijibu Karakantha. Baada ya makubaliano hayo waliongea mambo mengine mengi sana. Ge Rhong akafikisha taarifa kwa watu wake. Kuna baadhi mwanzo walikataa lakini alipowaambia kuwa kula na malazi hayatakuwa shida tena kwao. Wote walikubali.

Kazi za kufuata mizigo aliziacha kwa Ge Rhong, yeye akashuhulika zaidi ujenzi wa ukuta ambao baada ya miezi saba ulikua unakaribia kukamilika. Baadhi ya watu wa Ge Rhong walihusika na ulinzi pamoja na uchunguzi. Pale walipohisi kuna kikundi chochote kilichotaka kuvamia. Walimalizana nacho huko huko. Walipeleka taarifa baadae.

Hatimae baada ya miezi tisa, ukuta ukakamilika. Ulikuwa mkubwa na mnene, wanakijiji wote walifurahi sana.

Katika kikao.

"Nawashukuru wazee kwa kufanikisha jambo hili kwa hali na mali. Haya ni matunda ya umoja wetu, ila kuna taarifa ambayo si nzuri nimeipokea. Kuna mfalme mmoja wa ngome ya karibu ana mpango wa kuvamia kijiji chetu. Hivyo basi itatulazimu tukihame mapema kuliko nilivyopanga. Kwasababu saa hivi hatuna uwezo wa kupambana nae" aliongea Karakantha.

Taarifa hizo ziliwashtuwa wazee wengi lakini mpaka wakati tayari maji yalishamwagika. Walifahamu kabisa kuwa siku kama hiyo ingefika tu, hakukuwa na namna. Taarifa zikafikishwa kwa wanakijiji wengine na kupewa amri ya kujiandaa. Usiku wa siku hiyo hiyo wakaanza kuhama.

"Kamanda, tuna tatizo" alifika mtu mmoja na kutoa taarifa kwa Ge Rhong. "Tulia kwanza, vuta pumzi. Haya niambie sasa" aliongea Ge Rhong.

"Kuna jeshi kubwa la mfalme Tayi wa ngome ya maji, wanakuja hivi sasa" aliongea mtu huyo.

Ge Rhong akazifikisha taarifa hizo kwa Karakantha. "Chaguwa vijana hamsini kati ya vijana wako, hao watabaki na sisi hapa. Walobaki wahakikisha wanaohama wanafika salama. Wakishaingia tu ndani ya ukuta, watakuwa salama" alitoa amri.

Ge Rhong akafanya kama alivyoelekezwa, vijana hamsini walibaki na wengine walikwenda na msafara. "Kama una mpango wowote ni vyema ukanambia sasa hivi" aliongea Ge Rhong.

"Tulia, hilo jeshi halitaweza kupita hapa. Nimeamuwa kubaki na watu wachache kwasababu. Sitaki wengi wajue kitakachotokea hapa" aliongea na kuvua nguo yake ya juu. Mgongoni alikuwa amevaa mkanda uliobeba lile shoka. Akalichomoa na kuliachia, lilipogusa ardhi tu. Ukaisikika mtetemeko mdogo.

"Sijanyoosha viungo muda mrefu sana, niahidi utakachoshuhudia leo hakitabadlisha kitu kati yetu" aliongea akimuangalia Ge Rhong. Ge Rhong akameza funda kubwa la mate.

Wakiwa eneo hilo, wakaanza kuhisi miguu ya watu na farasi ikija. Baada ya dakika kumi, mita kadhaa kutoka waliposimama. Kulikuwa na kundi kubwa la wanajeshi. Akafika mtu mmoja akiwa na waraka mkononi.

"Nani kiongozi wenu" aliuliza, Karakantha akasogea mbele kidogo. Yule askari aliefika, akufunguwa ule waraka na kuanza kuusoma.

"Kwa kiongozi, mimi Mfalme Tayi ni mkarimu sana. Hivyo nataka mjisalimishe muwe chini yangu, nitawalinda kwa malipo kidogo tu. Na pia mnipe mali zenu zote kwasababu mfalme pekee ndie anaetakiwa kuwa na mali. La muhimu zaidi namtaka daktari wenu awe ananisimamia mimi tu. Ikiwa mtakataa, musinilaumu kwa kutumia nguvu"

Alimaliza kusoma na kumuangalia, "wewe maskini umesikia ukarimu wa mfalme, haya fanya haraka ukasujudu" aliongea akimuangalia Karakantha kwa jicho la jeuri.

***********
Farasi wa yule aliekwenda na ujumbe wa mfalme alirudi, mgongoni alikuwa amebeba mzoga wa mjumbe. Katika mgongo wa mzoga huwo kulikuwa na barua ilioandikwa kwa maandishi mekundi. Damu ndio iliyotumika kama wino wa kuandikia barua hiyo.

"Kwako mfalme wa Tayi, ahsante kwa ukarimu wako. Ila hichi kijiji sio mali yako, hivyo nakuonya. Kusanya mifugo yako na urudi nyumbani ukalale na mkeo. La si hivyo hutaliona jua, Karakantha" ulisomeka hivyo.

Mfalme Tayi akacheka sana, akamuita mmoja katiya makamanda wake. "Ifanye inyeshe" alitoa amri. Yule kamanda akageuk na kuongea, "kikundi cha mishare, inyeshe". Kikundi hicho kikaachia mishare mingi sana.

"Kamanda, kuna mishare inakuja" aliongea mtu. "Wote simameni nyuma yangu" aliongea Karakantha nao wakatii.

Akatanuwa mikono yake, akairudisha kati ikakutana na kupiga kofi. Upepo mkali sana ukavuma, mishale yote ilionekana kugonga kitu kama ukuta. Ikaanguka chini, "Ge Rhong mi natangulia. Nyinyi mtamshuhulikia yeyote ambae atanipita japo sidhani kama itawezekana" aliongea na kuondoka kwa kasi kiasi cha kutoonekana kwa jicho. Alikuwa kama mtu mwingine, kiu yake ya damu ilikuwa juu kiasi cha kutoa harufu kali sana.

"Mfalme kuna kitu kina kuja kwa kasi sana" aliongea mtu mmoja. "Kikosi cha ngao, weka ngao" alitoa amri kamanda wa kikosi cha ngao. Kikosi hicho kikashusha ngao na kuzichomeka chini lakini hazikuzaa matunda. Ndani ya dakika chache, mejenerali wote wakawa wamepoteza maisha. "Mfalm.." alitaka kutoa lakini alipomuangalia mfalme, hakuwa na kichwa.

**********************************************
 
TARIQ HAJJ
Black Star 34

Fahad anafumbuwa macho, mashine zikaanza kupiga kelele. Wakafika wauguzi wawili na kumuangalia. Baada ya sekunde kadhaa kadhaa akafika daktari na kutoa tochi. Akaiwasha na kummulika machoni, "unajisikiaje" akauliza daktari. "Vizuri" alijibu.

"Toeni mashine, mpatieni maji anywe kidogo" alitoa maelekezo na kutoka. Wale wauguzi wakafanya kama walivyoambiwa. Baada. Dakika tano yule daktari alirudi akiwa kaongozana na Don Pizallo. "Unajisikiaje" aliuliza alipofika.

"Mbona niko vyema, kwani kuna nini" alijibu akionesha kutoelewa nini kinaendelea. "Ni kweli kabisa fahamu nini kimetokea, ila umekuwa katika usingizi mzito wa miezi miwili" aliongea Don Pizallo. "Ati nini, miezi miwili?"

"Ndio, uliingia katika coma usiku ule ule ulotoka katika pambano. Maisha yakawa hatarini, jambo zuri ni kwamba nilikuwa nimeshampigia simu daktari hivyo akafanikiwa kuokoa maisha yako" alifafanuwa Don Pizallo.

Fahad akajilaza kitandani na kufunga macho, "Eunice, uhali gani mke wangu" alijisemea moyoni mwake.

Don Pizallo akaondoka ili kumpa nafasi ya kucheka alichomwambia. Baada nusu Fahad akatoka chumbani na kumkuta Don akiwa sebleni. "Kuna taarifa nyingine yeyote natakiwa kuijuwa. Nina mpango wa kurudi kwa master Ge kwa ajili ya kuendelea na mafunzo" aliongea Fahad.

"Ndiyo ipo ni nzuri mno, baada ya pambano lako na Francois Chaka umepanda daraja mpaka Super league daraja la tatu. Ligi hiyo itafanyika miezi ishirini na nne kutoka sasa. Hivyo unaweza kuenda utakapo wala usiwe na shaka" aliongea Don Pizallo.

"Nafurahi kusikia hivyo, kesho nitaondoka kuelekea China. Mimi na wewe tutaonana baada ya miezi ishirini na tatu. Nitarudi mwezi mmoja kabla ya pambano. Fungu langu nusu niwekee kwenye akaunti yangu na nusu nipelekee kwa mzee wangu. Ziende pesa, sitaki ionekana kama kuna uhusiano wowote kati yao na sisi" aliongea Fahad. Don akakubali kufanya hivyo.

Siku iliyofuata asubuhi Fahad akaondoka kuelekea China. Baada ya masaa tisa ndege ikakanyaga ardhi ya uchina, hapo hapo akachukuwa ndege nyingine mpaka mji wa mawe, Baoshan. Kutoka hapo akatembea kwa miguu mpaka ilipo nyumba ya Master Ge. Akaweka mizigo yake na kubadili nguo.

Alipofunguwa mlango kwa ajili ya kutoka, akajikuta tayari yupo katika ulimwengu wa Dao. Akapiga mruzi mkubwa, baada ya dakika kama moja hivi zikasikika kwato za farasi zikija. Alikuwa ni yule Farasi wake, "ulikuwa ukinisubiri" aliongea na kupanda.

Safari ya kuelelekea ngomeni kwake ikaanza. Jambo lilimshangaza ni uwezo wa farasi huyo, japo alikimbia masafa marefu lakini hakuonesha dalili yeyote ya kuchoka. Baada ya safari ya siku sita, akawa amekaribia kabisa ngome.

Eunice akiwa chumbani kwake, akashuhudia shoka ikianza kutikisika. "Amerudi" alijisemea na kusimama, akatoka nje. "Malkia umetoka kumuangalia Prince au" aliuliza mwanamke mmoja aliekuwa nje. "Mleteni hapa akiwa kashavaa vasi lake la utawala" alitoa amri. Mwanamke huyo akaondoka na kwenda sehemu aliokuwa mwana wa mfalme. Akamchukuwa na kwenda kumbadilisha.

Akiwa hapo akafika master Ge, "malkia na wewe pia umehisi" aliuliza. "Ndio, mfalme amerejea" alijibu Eunice. "Na amerudi akiwa na uwezo kuliko alivyoondoka" alionesha furaha yake wazi kabisa.

"Mama kuna nini, mi nilikuwa nacheza" aliletwa mwanae. "Nenda ndani kaichukue shoka ya babaako" aliongea Eunice. Kitoto hicho kikaingia chumbani na kutoka na shoka mkononi. Eunice akambeba na kuanza kuelekea getini.

Getini.

Fahad alikuwa kasimama chini geti hilo kubwa, "tafadhali jitambulishe" aliongea mlinzi. Sehemu ya kushuto ya geti hilo kulikuwa na mlango mdogo ambao ndio ulitumika kwa watu, wanyama na mizigo kupita. Fahad akashuka kutoka kwenye mgongo wa farasi. Akaweka mikono yake katika geti kubwa na kuanza kulisukuma.

Mishipa yote ya damu ukatuna na misuli ikajaa. Geti hilo likatikisika na kuanza kufunguka, lilifunguka mpaka likawa na njia ya kutosha mtu kupita. Alikaribishwa na sura nzuri ya mkewe aliekuwa ametabasamu. Mkononi alikuwa amebeba mtoto mdogo, akatembea na kusimama mbele ya Eunice. "Shoka" akaongea kwa mshangao.

"Mama huyu nani, mbona anashangaa" aliongea yule mtoto. "Nyamaza! Huyo ni mfalme", "lakini umenambia mimi ndio mfalme" aliongea mtoto.

"Karibu nyumbani mfalme Fey" aliongea master Ge na kuinamisha kichwa. "Nafurahi kuwaona muwazima wa hali" alijibu nae akainamishwa kichwa. Alipoinuwa kichwa macho yake yakagongana na mwanae. "Unaitwa nani?" alimuuliza. "Mama kanambia nisiwe naongea na wageni".

"Wewe.." Eunice akataka kuongea kitu ila Fahad akaweka kidole mdomoni. "Amekufundisha pia kuwa kuchezea viti vya watu si vizuri" aliongea na kuinuwa mkono wake juu. Shoka ikatoka mkononi mwa mwanae kutua katika mkono wake. "Mshushe, halafu nyie tangulieni" alitoa amri.

Eunice akamshusha mtoto, wakaaga na kuondoka. "Mama ako hajakwambia kitu kingine" aliuliza Fahad. "Kanambie baba ndio mti pekee mwenye uwezo wa kubeba hiyo shoka" alijibu kwa sauti ya chini kisha akainamisha kichwa. Fahad akainama na kumbeba kisha akaanza kutembea nae.

"Unaitwa nani?"

"Sijapewa jina, nimeambiwa jina utanipa wewe ukirudi"

"Hahaha! Una akili sana kuliko hata mimi babaako" aliongea Fahad akichekea. Kisha akaendelea "Minhe, ndio litakuwa jina lako".

"Nimelipenda hilo" alijibu na kujitikisa ikiwa ni ishara ya kutaka kushushwa. Fahad akamshusha, akakimbilia kwa mama ake aliekuwa mbele. "Mama, baba kanipa jina" aliongea kwa nguvu kiasi cha watu wote waliokaribu kusikia.

"Amekupa jina gani"

"Minhe, na nimelipenda"

Alivyotaja tu jina hilo watu wote waliokaribu isipokuwa Eunice wakapiga magoto na kusema, "ubarikiwe na maisha marefu mwana mfalme Minhe. Ahsante mfalme kwa kumpatia jina damu yako. Tunaahidi kumthamini kama tunavyokuthamini wewe na tutampa heshima na ushirikiano wetu wote".

Fahad akatabasamu na kuwafanyia ishara ya kusimama. Akawaruhusu waende kuendelea na mambo yao. Akambeba Minhe na kuongea, "Baba twende ofisini". Master Ge akainamisha kichwa na kuongoza njia, Eunice nae akaungana nao.

Ofisini.

"Mambo yanaendaje tokea nilipoondoka" aliuliza.

"Hali ya amani ni nzuri, wananchi wetu waliokuwa wametawanyika maeneo mbali wamerudi wengi" aliongea Master Ge.

"Hakuna mtu alieleta tabu yeyote"

"Mambo hayo yapo kwenye ngome yeyote ile, ila usiwe na shaka. Wote wamefanyiwa na kazi na kupata adhabu stahili"

"Vipi mafunzo"

"Yanaendelea vizuri, watu wengi wamejifunza njia mbali mbali za kutumia Qi. Na njia ya kilimo uliyotufundisha imetusaidia sana"

"Vipi wale watu nilokwambia waungane Fu Shu".

"Tokea siku waliongia katika msiti hatujaonana nao tena ila hakuna hata mmoja alierudi mpaka sasa".

"Kuna jambo lolote nahitaji kulijuwa"

"Ndio, unatakiwa umtawadhe Mwana mfalme Minhe kuwa mrithi wako"

"Sawa, hilo nitalifanya miezi mitatu kutoka sasa. Leo nitapumzika, kesho nitafunguwa geti kwenda kuwaangalia watu wangu waliokuwa msituni".

Walimaliza kuongea, Fahad akaondoka na Eunice na Minhe na kwenda zake nyumbani kwake.

Duniani.

Ommy akiwa nyumbani kwake, simu yake ikaita. "Hello" aliipokea, "naongea na Omary Mzee" upande wa pili uliongea. "Ndio, unaongea nae, wewe ni nani na nikusaidie nini" aliongea. "Usiongee kwa hasira, mimi na wewe tuna adui mmoja. Japo Ni adui mmoja lakini mimi wangu ni mtoto wako ni baba" uliongea upande wa pili.

"Fafanuwa sijakufahamu"

"Tuonane ukitaka tuongee vizuri tukutane usiku, eneo la kukutana nita kuandikia katika ujumbe" simu ikakatwa. Sekunde chache ukaingia ujumbe ukiwa na eneo kuonana.

Jioni ya siku hiyo Ommy akatoka mapema ili kuepuka foleni. Saa moja na nusu akawasili katika hoteli alioambiwa afike. Simu yake ukaita, "kuna muhudumu amevaa shati nyeupe yenye ukila mweusu. Mfate huyo" ikakatwa akaangalia na kumuona mhudumu huyo akiwa anajuangalia. Akashusha pumzi na kumfata, wakapandisha ngazi mpaka ghorofa ya pili. Akapelekwa mpaka chumba cha wageni muhimu (VIP), "karibu" alifunguwa mlango na kumkaribisha.

Yule muhudumu akaondoka, Ommy akaingia na kufunga mlango. "Karibu Mr Omary" alisikia sauti nzito. Akaenda mpaka yalipo makochi akakaa. "Ahsante naomba kukufahamu kwanza kabla hatujaendelea na chcochote" aliongea akikaa. "Kama nilivyotegemea, una akili ya kufanya kazi na mimi" alijibu mtu huyo na kuvua kofia.

"Mimi niko hapa kwa niaba ya bosi wangu, naitwa Chiketo. Bosi anapendelea kukaa kizani hivyo amesema nisimyambulishe" aliongea. "Kujutambulisha wewe tu inatosha" aliongea Ommy.

"Sawa, basi tusipoteze muda. Kama nilivyokwambia kwenye simu kuwa mimi na wewe tuna adui mmoja isipokuwa tu wa kwangu mimi ni mtoto wako wewe ni baba au niseme kaka ako" aliongea Chiketo. "Unakusudia Abedi" aliuliza Ommy.

"Ndio, ila mimi adui yangu ni mtoto wake wa kwanza Fahad"

Ommy akatabasamu na kukaa vizuri, "umelikamata sikio langu" aliongea.

"Vizuri, shida yangu mimi ji Fahad awe chini yangu ila siwezi kufanya hivyo kwasababu sina cha kumfanya afanye hivyo. Hivyo basi nitashirikiana na wewe katika kudili na kaka ako. Halafu tutaitumia familia yake kuhakikisha anakuwa chini yangu. Baada ya hapo, mimi nitabaki na baba ake na wewe utaichukuwa familia yake na mali yote. Unasemaje?"

"Ni wazo zuri japo sifahamu kwanini unamtaka Fahad. Yule mpumbavu wa nje ya ndoa hana faida hata moja. Yeye na kinyesi bora kinyesi" Ommy alionesha wazi chuki dhidi ya Fahad.

"Suala la kuwa au kutokuwa na faida wewe halikuhusu. Uko tayari kushirikiana na mimi au la. Nipe jibu maana leo natakiwa nirudishe jibu kwa bosi wangu" aliongea Chiketo.

"Hakuna shida, muda wowote" aliongea Ommy na kutoa mkono. Chiketo akaupokea, "patna".

"Kama sehemu ya kudumisha umoja wetu, kwenye hiyo briefcase kuna kiasi kidogo cha fedha kama zawadi kutoka kwa bosi wangu. Nina imani kitakutosha kutumia kwa siku mbili tatu. Nina uhakika bosi atakupatia fedha nyingine akisikia umekubali" aliongea na kumsogezea briefcase. Akainuka na kuondoka, Ommy hakutaka kulifunguwa. Akalibeba na kuondoka.

Ofisini kwa Victor Smith.

"Mkuu kuna taarifa hapa" alifika Mapunda na kuongea, "nipe".

"Inaonekana, Ommy ameenda kukutana na mtu. Sijajuwa ni nani lakini alipotoka alikuwa na beiefcase. Kwa muonekano tu linafanana na yale yanayotumika vikosi vya kimafya" aliongea.

"Anaweza kuwa anapanga shambulio kubwa, sawa nimekuelewa. Endelea kumfatilia". Victor akatoa simu yake na kupiga, "Victor, habari ya saa hizi" mzee Abedi aliipokea na kuongea. "Nzuro, unaweza kufika hapa ofisini mara moja. Kuna jambo muhimu nataka kukuambia" alionge Victor.

"Sawa, nitakuwa hapo ndani ya dakika arobaini na tano zijazo" mzee Abedi aliongea na kukata simu. Akamuaga mkewe na kutoka, aliendesha gari kasi na kwasababu usiku ulikuwa umeshaenda tayari hakukuwa na foleni barabarani. Baada dakika ishirini akaingia katika jengo kubwa na kuegesha gari. Akkashuka kuelekea ndani ya jengo hilo.

"Hizi ndio arobaini na tano" aliongea Victor alipomuoan mzee Abedu akiingia ndani ya ofisi yake. "Sina muda mrefu wa kukaa hapa, niambie ulichooniitia" aliongea.

Victor akamueleza kila kitu bila kuacha hata kimoja. "Omary nakuapia kwa Mungu safaro nitakuuwa" aliongea mzee Abedi. "Endeleeni kufatilia, na pia Paul yuko wapi?".

"Paul yuko Bangkok tokea mwezi ulopita, kuna dili anakamilisha" alijibu Victor.

"Mwambie namuhitahi kesho, hata kama atapaa kutoka huko. Usiku nimkute hapa" aliongea mzee Abedi na kuondoka. Alikuwa kafura kama mbogo, akaingia kwenye gari ya kuondoka kwa kasi sehemu hiyo. Alipofika karibu na nyumba yake akazima taa za gari yake na kuendesha taratibu. Akasimama mita kadhaa kutoka getini.

Akazima gari na kufunguwa sehemu kwenye kiti cha mbele. Akatoa bastola na kuofunga kiwambo cha kuzuia sauti. Akashuka na kuichomeka nyuma kwenye suruali yake. Karibu na geti la nyumba kulikuwa na gari. Gari hiyo alishaiona zaidi ya mara moja ikisimama hapo.

Akafika mpaka kwenye mlango wa dereva, akagongo kioo. Dereva alipofunguwa tu mlango, kwa kasi mzee Abedi akatoa bastola na kutengeneza matobo mawili katika paji la uso la dereva huyo.

Kisha akatoa simu na kumpigia victor, "njoo uchukue mzoga huku, gari myaofanya mnavyotaka" akakata simu na kuorudisha mfukoni. Akarudi kwenye gaei yake na kupanda, akasogea mpaka getini. Akabonyeza rimoti, geti likafubguka. Akaingia ndani na kushuka, akamkabidhi mlinzi funguo yeye akaelekea ndani.
************
 
BLACK STAR 35
TARIQ HAJJ

"Tumepoteza mawasiliano na Simon" aliingia mtu mmoja ofisini kwa Chiketo na kutoa taarifa. "Inaonekana hapa hatudili na mtu wa kawaida. Ila tushajuwa jinsinya kumuingia" aliongea Chiketo na kumruhusu alieleta tarifa aondoke.

"Abedi Mzee, bila shaka wewe ni Mwamba kweli. Pamoja na siku nyingi kupita bado hujapoteza makali yako" alijisemea na kutoa simu. Akaingiza tarakimu kadhaa kisha akapiga.

"Bosi, kila kitu kinakwenda kama ulivyopanga. Na yale mashaka yako ulokuwa nayo yaondoe kabisa. Abedi Mzee ndie Mwamba, yule yule tuliekumbana nae Mexico miaka ishirini iliyopita" aliongea Chiketo. "Sawa, kwasasa endelea kumuangalia tu, hakikisha hakikupiti kitu. Mtumie vizuri huyo mjinga mwengine mpaka pale utakapohisi hana tena faidia muue" simu ikakatwa.

Chiketo akaweka simu chini na kushika jicho lake la kushoto. "Mwamba, kila nikilikumbuka hili jina jicho langu linauma japo halipo tena" alijisemea na kuingiza vidole katika jicho hilo. Akalotoa na kuliingiza katika maji maalumu. Lilikuwa jicho la bandia. "Ila nina imani tutaonana muda si mrefu, nitalipa tu. Jicho kwa jicho"

Bangkok, Thailand.

Paul alipokea simu, "oya Mwamba anasema kukutwa mjengoni kesho usiku. Maliza unachofanya urudi, anaonekana kavurugea vibaya sana" aliongea Victor. "Sawa, kesho jioni jitaingia nyumbani" alijibu Paul na kukata simu. Mkono wake mmoja ulikuwa umeshika bastola iliyokuwa mdomoni mwa mtu. Akabonyeza kitufe cha kufyetulia risasi na kumpasua kichwa. "Nina imani nimekamilisha kazi yako" aliongea na kuondoka.
*******************************************

Asubuhi mapema aliamka na kufanya mazoezi kisha akajisafisha na kuvaa joho lake la kifalme. Mfalme Fey, baada ya kupata kifunguwa kinywa. Akatoka na kutembea maeneo mbali mbali katika ngome yake ili kuwajuliwa hali watu wake. Alipokea pia baadhi ya malalamiko na kuahidi kuyafanyia kazi akirudi.

Juwa lilipofika kati akarudi nyumbani kwake na kupata chakula cha mchana. Kisha akabadili na kuvaa mavazi mengine. Akatoka na kuongozana na baadhi ya viongozi wake mpaka katika geti. "Baba, nakuachia tena ngome kwa siku kama nne mpaka wiki mbili. Sidhani kama itakuwa rahisi kuwapata kwa muda mfupi. Pia naomba mtu yeyote asije akapiga hatuwa hata moja nitakapofunguwa geti.
Harufu ya damu ninayoinusa sidhani kama kuna mti kati yenu ana uwezo wa kuvumilia".

Akaweka mikono yake getini na kulisukuma kwa nguvu. Pua zake zikakaribisbwa na harufu kali sana ya damu. "Ni matumaini yangu bado mtakuwa na hamjapoteza uyu wenu" alijisemea na kuaga. Akalifunga geti na kusimama kwa dakika kadhaa kabla ya kuanza safari.

Msitu huwo haukonekana kuwa na dalili zozote za uhai. Baada ya mwendo wa dakika kama kumi hivi akakutana na kibao. "Kama unayathamini maisha yako rudi ulipotoka" kilisomeka hivyo. Akatabasamu na kukipuuza, baada ya kutembea kidogo akakutana na kibao kingine. "Hili ni onyo la mwisho, usije ukasema hatujakuonya".

Akakipuuza pia na kuendelea kutembea, ghafla akainama. Mshale ukapita kwa kasi kupenya katika mti na kutoka upande wa pili. Akainuka mara akalaza kichwa upande wa kushoto, ukapita mshale mwingine na kuzama katika mti. Safari hii mti ukakatika na kuanguka, "munaweza kujificha lakini hamuwezi kuficha kiu yenu ya damu. Njooni wote, nitawachukuwa" aliongea.

Ndani ya sekunde chache akawa amezungukwa na watu kumi na moja. Walikuwa na silaha tofauti, mmoja wao akapita mbele na kuongea "jitambulishe na utambulishe biashara yako huku". "Nitajitambulisha ikiwa tu utaniletea kiongozi wako tu.

Siwezi kuongea na sisimizi mimi" alijibu makusudi ili kuwatia hasira. "Kwa uwezo gani ulokuwa nao, unadhani bosi wetu ni mtu wa kuonana na kila mtu. Amesema tumuite endapo tu, mwalimu wake atakaporudi" alaijibu akionekana kutokuwa na pupa.

"Ina maana nikiwachakaza nyinyi anaweza kuja" aliongea. "Huna huwo uwezo na chunga kauli yako" aliongea kiongozi huyo. "Unaonaje tukapimana uwezo", "nyote nyinyi njooni kwa wakati mmoja. Sina muda wa kupoteza"

Yule kiongozia akarudi nyuma na kuwapa ishara washambulie, ila kabla hajafanya hivyo wachache wakajikuta wakianguka chini na kupoteza fahamu. Sheria ya kwanza ya vita katika kitabu cha Asura, shambulia wakati anadui anajiandaa kushambulia aliongea maneno hayo akiwa nyuma ya yule kiongozi.

Umefika saa ngapi nyuma yangu aliongea yule kiongozi na kuruka pembeni akigeuka upande wa Fahad. Sheria ya pili ya vita katika kitabu cha Asura, usitoe macho yako kwa adui yako. Kufanya hivyo kuna hatarisha maisha yako na walionyuma yako aliongea tena Fahad akiwa nyuma ya kiongozi wao.

Ila akarudi nyuma kwa kasi kabla ya kufanya mashambulizi, una macho makali sana akasikia sauti nzito ikitokea mita chache kutoka aliposimama. Kamanda Fu, kwanini umetoka katika kiti chako aliuliz yule kiongozi. Sheria ya tatu ya vita katika kitabu cha Asura, mchezeshe adui yako ngoma uipigayo aliongea na kuukita mkuki wake chini. Akapiga goti moja chini na kukutanisha mikono yake juu, umerudi mfalme wangu aliongea.

Naona umefika katika daraja la mbingu na ardhi, Fu kwa tabasamu alijibu na kumuinuwa Fu Shu, heshima kwa mfalme ikasikika sauti ikitokea kutoka juu ya mti. Wakashuka watu kama matone ya mvua na kutuwa ardhini, hakukuwa na kishindo nyuma.

Wote wakapiga magoti na kukutanisha mikono yao na kuongea karibu nyumbani mtukufu mfalme. Simama alitoa amri na wote wakasimama. Mtukufu mfalme, nimeshindwa kukutambuwa. Nastahili kifo au hata kama kuna adhabu nyingine kali kuliko kifo, nipo tayari kuipokea aliongea na kupiga magoti.

Hapa zaidi ya Fu, hakuna mwengine yeyote ambae angenifahamu hivyo huna kosa lolote aliongea Fahad na kumshika yule kiongozi begani. Hapana, ingekuwaje kama ningeichuna ngozi yako takatifu, sitasimama mpaka uniadhibu. Sawa, adhabu yako ni hii.

Ndani ya wiki mbili nataka uwezo wako ufike daraja la mbingu na ardhi aliongea Fahad. Umetukuka mfalme, nitahakikisha kuwa ndani ya muda huwo nitafika katika daraja ulilosema. Akasimama na kurudi kwa wenzake, Wanajeshi aliongea Fahad kwa nguvu, tupo katika mikono yako waliitika kwa pamoja na kuinuwa silaha zao juu.

Ndani ya miezi mitatu ijayo nitakuwa namtawadha mwanangu kuwa mrithi wa kiti changu, mpaka kufika wakati huwo nataka wale wote waliochini ya daraja la mbingu na ardhi wawe wamefika katika daraja hilo. Wale waliokuwepo katika daraja la mbingu na ardhi wawe katika la juu zaidi, daraja la transidient.

Na hili la sasa ni maalum kwa kamanda Fu, wewe nataka uwe katika daraja la ulimwengu, mtafikaje huko msijali nitawapa mafunzo mimi mwenyewe. Fungeni vibwebwe maana damu itawatoka na nyongo itatapikwa aliongea na kusababisha baridi itembee katika miili ya watu hao.
****************
 
BLACK STAR 36.
TARIQ HAJJ

Miezi mitatu baadae.

Geti likafunguliwa, Fahad akiwa mbele akiongoza msafara wa wanajeshi. Nyuma yake akafuata Kamanda wa kwanza, Kamanda Fu. Nyuma ya Fu wakafuata makamanda wasaidiz kumi na wawili, watu hao kumi na mbili walikuwa wamejifunga vitambaa katika macho yao.

Nyuma ya watu hao kumi na mbili likafuata kundi zima la wanajeshi, walijitahidi sana kulazimisha tabasamu. Walishapoteza uwezo, miezi mitatu hiyo hakuna hata mmoja alietamana kuikumbuka. Ilikuwa ni kiama kwao, kuna wakati walikwenda kwa mfalme na kupiga magoti wakiomba kifo.

Master Ge akafika na kuwapokea, karibu tena nyumbani, myukufu mfalme aliongea na kuinamisha kichwa. Ahsante baba alijibu, mke wangu yuko wapi aliuliza. Anakusubiri nyumbani kwako alijibu Master Ge na kusogea pembeni akimaanisha aende kumuona.

Dalili hiyo ikapiga mshale wa hatari kichwani mwa Fahad. Kamanda Fu, nakukabidhi kwa Master Ge. Atawapeleka katika eneo husika, mimi nitawakuta huko aliongea na kuondoka. Alitembea taratibu ili asiwatie wasiwasi, alipofika nyumbani kwake akakaribishwa na Qi ya baridi sana.

Akaingia ndani na kumkuta Eunice akiwa amekaa chini. Alikuwa amekunja miguu, jasho lililikuwa likimtoka. Alionekana kupambana na kitu, inatosha mke wangu aliongea Fahad na kukaa pembeni yake. Mtoto wako wa pili pia si kiumbe wa kawaida. Mwili wake unatoa Qi ya baridi mno na kila siku inaongezeka, usijali kuanzia sasa hatofanya hivyo aliongea na kuweka mkono wake katika tumbo la mkewe.

Siku ya pili mapema maandalizi ya sherehe yalinza ngome nizma ikawa na mshike mshike, Minhe, unajuwa nini maana ya kuwa mrithi wa kiti cha mfalme, ikitokea siku nikaondoka wewe ndie utakae kuwa na amri katika ngome hii. Baada ya kukutawadha tu, nitahakikisha unakuwa mtu mwenye nguvu zaidi katika ngome hii baada yangu aliongea Fahad akiwa anamvika mwanae joho la kifalme.

Mfalme, maandalizi yamekamilika alifika mtu mmoja na kutoa taarifa, sawa alijibu na kumuangalia mwanae. Wakasimama na kuanza kutoka nje, walipokelewa na kikosi kikubwa cha ulinzi na kupelekwa mpaka katika hekalu la wazee. Taratibu za kumtawadha zikaanza na baada takribana saa tatu zikawa zimeisha. Fahad akasimama na kutoa amri watu wamsikilize, amri hiyo ikarudiwa tena na kamanda Fu.

Kwa sasa tupo katika kipindi cha amani, nafahamu kila mtu anatamani amani hii ibaki milele na mile lakini ni jambo ambalo haliwezekani. Hivi sasa sisi kuwa hivi kuna watu tunawauzdhi, na amini kwamba. Pindi miaka ishirini itakapoisha, basi tutapokea wageni wengi sana katika kizingiti chetu. Katika utawala wangu natangaza rasmi mambo yafuatayo.

Moja hakutakuwa na matabaka, watu wote katika ngome yangu watakuwa sawa. Mbili kila mtu atalazimika kulipa kodi ili kuhakisha huduma muhimu zina patikana. Mgawanyo wa kodi utatangazwa na waziri husika. Tatu watoto wote watahudhuria mafunzo ya shule mpaka watakapofikisha miaka kumi na mbili, baada ya hapo kila mtoto atachaguwa kitu anachotaka kufanya

Nne, ili kujenga jamii yenye haki na usawa. Nitaanzisha mahaka ambayo itakuwa inahukumu kutokana na sheria zitakazoandaliwa. Kila mtu atapata haki yake, kwa kusema hivyo naamanisha hakuna anaeruhusiwa kuchukuwa sheria mikononi mwake.

Tano, nitaanzisha kitengo cha askari pamoja na magereza. Sita, wafanya biashara wote lazima wasajiliwe ili kuendelea na biashara zao, kwa kufanya hivyo mutapata ruhusa ya kukodi walinzi watakaowasindikiza katika safari zenu
**********************************************
Nasisitiza kuwa yeyote yule atakae vunja sheria, ataadhibiwa bila kujali hali yake katika ngome hii. Na mwisho kabisa, ndano ya siku mbili hizi kutatoka nafasi za kujiunga na vyombo vya usalama vya ngome hii. Kila mtu, mwanamke kwa mwanaume aruhusiwa kuomba alimaliza kuongea na kurudi kwenye kiti chake.

Master Ge akasimama na kuanza kuongea mfalme wetu ni mtu mwenye busara sana, nafahamu kuwa kuna kundi la watu litaathirika zaidi kutokana na maamuzi ya mfalme lakini niwaonye kabisa, musiifananishe busara na upole. Mfalme Fey, ni mfalme mwenye busara lakini ni mfalme mwenye kusimamia kile anachokiamini alimaliza na kurudi kwenye kiti chake.

Uishi maisha marefu mtataktifu mfalme kundi kubwa la watu likaongea kwa sauti kubwa na kupiga goti moja chini kuonesha maridhia yao katika maamuzi yake. Hafla hiyoikaisha huku watu wakiruhusiwa kula na kunywa mpaka waridhike. Fahad akaondoka na familia yake na kurudi nyumbani kwake.

Unadhani watakaa kimya aliuliza Eunice, Fahad akashusha pumzi na kutabasamu. Hawatakaa kimya, ila hii ni hatuwa muhimu ya kutengeneza ngome yenye umiyhili wa chuma. Ngome ambayo haitaanguka kwa usaliti wa ndani wala kwa uvamizi wa nje. Yajayo yanafurahisha alijibu na kumbusu mkewe katika paji la uso. Akatoka nje na kuelekea katika ofisi yake, Mtukufu mfalme, karibu aliongea kamanda Fu aliekuwa mlangoni.

Nipe taarifa aliongea Fahad akikaa kwenye kiti chake, inaonekana ulichokuwa unakifikiria kilikuwa sahihi kabisa. Kuna watu ambao si watu ngome hii na wapo hapa kwa ajili ya kukusanya taarifa na pia kupika usaliti.

Watu hao wengi na wafanya biashara na wamejiunga na familia kubwa za ngome hii ili kuhakikisha usalama wao. Kutokana na sheria za awali ilikuwa ni vigumu kuwagusa lakini sheria mpya ulizozitangaza leo zimewaondolea kinga hiyo. Sasa tunasubiri amri yako tu, tuwafanye nini aliongea kamanda Fu.

Hakuna haja ya kuchafua mikono yetu kwa damu, tunaendelea na mipango yetu kama tulivyopanga. Kesho bandikeni matangazo ya wote wanaotaka kujiunga vikosi vya usalama, baada ya hapo wote watafanya majaribio.

Sio kila mtu ana uwezo wa kuwa mlinda amani, nina uhakika kuwa miongoni mwa watakaoomba nafasi hizo watakuwa ni watu ambao watakuwa na uwezo katika maeneo mingine. Tukikamilisha hilo nitawaambia sehemu ya pili ya mpango wangu. Kamanda Fu akaitika na kutoka, sijui huko upande wa pili mnaendeleaje alijisemea na kuendelea na kazi zake nyingine.

Katika ngome ya Masyo, kikao kilikuwa kikiendelea na ajenda kubwa ilikuwa ni kwa namna wataweza kuvamia ngome ya Asura. Mlezi wetu amesema atabariki maamuzi yeyote yale tutakayofikia aliongea mfalme Damesh, Lakini si amepewa miaka ishirini ya amani na waliongazi za juu. Acha ujinga Soyyer, unadhani baada ya miaka ishirini itakuwani rahisi kuvamia.

Mimi nakwamba hujakutana uso kwa uso na mfalme Fey. Yule mpumbavu ana roho mbaya kuliko ubaya wenyewe, hivi sasa naweza kusema kuwa uwezo wake uko sawa na mlezi wetu au kama hajamzidi. Sio mtu wa mchezo mchezo kabisa, ni kama vile anataembea na maisha ya mtu mkononi aliongea Damesh.

Hapo mi naungana na Damesh, wazee wakale wanasema ni vyema ukangowa mti angali mchanga. Ukishakomaa tu itakuwa ni vigumu kuunyofoa ardhini aliongea Kesen. Tuache kupoteza muda, tuamuwe kinafanyika kitu gani ili kumziba mdomo aliongea Felshi mwanamke pekee katika kikao hicho. “Mimi nina wazo na vijana wangu wako tayari kulitekeleza aliongea Damesh na kuchezea ndevu zake nyingi nyeupe. Wote wakainuwa masikio na kuyategesha ili kutaka kujuwa hilo wazo.

Kwanza inabidi tumkate nguvu, tunamkataje hizo nguvu. Hivi karibuni nimefanikiwa kupata sumu inayouwa taratibu. Tunachotakiwa kufanya ni kuichanganya dawa hiyo katika vyanzo vya maji vya adui yetu. Kisha tutakaa siku tatu kabla ya kuanza safari kuelekea huko kwa ajili ya kufanya mashambulizi.

Na hiyo sumu tutaifikishaje huko aliuliza Felshi.

Kuna vijana wangu wamefanikiwa kuingia katika ngome ile na wanafanya kazi chini ya kivuli cha familia kubwa na za enzi katika ngome hiyo. Si hilo tu, kazi yetu itakuwa rahisi kwasababu siku tatu nyuma mfalme wao alitangaza kuwa watu wote katika ngome yake watakuwa sawa chini ya sheria.

Hilo limeonekana kuwakera sana wale wenye hadhi ya juu ambao tokea zamani walikuwa na mamlaka ya juu kuliko wengine. Hivyo kwa kushirkiana na hao kazi itakuwa nyepesi sana kwa sababu nusu na robo wapiganaji wa ngome nzima wanamilikiwa na familia hizo. Alifafanuwa.

Kama kawaida yako nyoka, niliona ajabu wewe kukaa kimya baada kudhalilishwa kiasi kile na mtoto mdogo sana aliongea Kesen na kutabasamu. Kwa kuongea hayo ni wazi kwamba mjadala huu umekwisha, leo nitawaagiza vijana wangu watie sumu na sisi tutakutana keshokutwa usiku kwa ajili ya kuanza safari kuelekea ngome ya Asura.

Tutaua kila kiumbe hai isipokuwa wanawake na watoto wadogo wa kiume. Hao wanatosha kuwa watumwa na makahaba kwa ajili ya madanguro yetu aliongea Damesh na kuinuwa gilasi ya mvinyo juu. Wengine nao wakainuwa na wote wakanywa.
**********************************
 
BLACK STAR 36.
TARIQ HAJJ

Miezi mitatu baadae.

Geti likafunguliwa, Fahad akiwa mbele akiongoza msafara wa wanajeshi. Nyuma yake akafuata Kamanda wa kwanza, Kamanda Fu. Nyuma ya Fu wakafuata makamanda wasaidiz kumi na wawili, watu hao kumi na mbili walikuwa wamejifunga vitambaa katika macho yao. Nyuma ya watu hao kumi na mbili likafuata kundi zima la wanajeshi, walijitahidi sana kulazimisha tabasamu. Walishapoteza uwezo, miezi mitatu hiyo hakuna hata mmoja alietamana kuikumbuka. Ilikuwa ni kiama kwao, kuna wakati walikwenda kwa mfalme na kupiga magoti wakiomba kifo.

Master Ge akafika na kuwapokea, karibu tena nyumbani, myukufu mfalme aliongea na kuinamisha kichwa. Ahsante baba alijibu, mke wangu yuko wapi aliuliza. Anakusubiri nyumbani kwako alijibu Master Ge na kusogea pembeni akimaanisha aende kumuona. Dalili hiyo ikapiga mshale wa hatari kichwani mwa Fahad. Kamanda Fu, nakukabidhi kwa Master Ge. Atawapeleka katika eneo husika, mimi nitawakuta huko aliongea na kuondoka. Alitembea taratibu ili asiwatie wasiwasi, alipofika nyumbani kwake akakaribishwa na Qi ya baridi sana. Akaingia ndani na kumkuta Eunice akiwa amekaa chini. Alikuwa amekunja miguu, jasho lililikuwa likimtoka. Alionekana kupambana na kitu, inatosha mke wangu aliongea Fahad na kukaa pembeni yake. Mtoto wako wa pili pia si kiumbe wa kawaida. Mwili wake unatoa Qi ya baridi mno na kila siku inaongezeka, usijali kuanzia sasa hatofanya hivyo aliongea na kuweka mkono wake katika tumbo la mkewe.

Siku ya pili mapema maandalizi ya sherehe yalinza ngome nizma ikawa na mshike mshike, Minhe, unajuwa nini maana ya kuwa mrithi wa kiti cha mfalme, ikitokea siku nikaondoka wewe ndie utakae kuwa na amri katika ngome hii. Baada ya kukutawadha tu, nitahakikisha unakuwa mtu mwenye nguvu zaidi katika ngome hii baada yangu aliongea Fahad akiwa anamvika mwanae joho la kifalme.

Mfalme, maandalizi yamekamilika alifika mtu mmoja na kutoa taarifa, sawa alijibu na kumuangalia mwanae. Wakasimama na kuanza kutoka nje, walipokelewa na kikosi kikubwa cha ulinzi na kupelekwa mpaka katika hekalu la wazee. Taratibu za kumtawadha zikaanza na baada takribana saa tatu zikawa zimeisha. Fahad akasimama na kutoa amri watu wamsikilize, amri hiyo ikarudiwa tena na kamanda Fu.

Kwa sasa tupo katika kipindi cha amani, nafahamu kila mtu anatamani amani hii ibaki milele na mile lakini ni jambo ambalo haliwezekani. Hivi sasa sisi kuwa hivi kuna watu tunawauzdhi, na amini kwamba. Pindi miaka ishirini itakapoisha, basi tutapokea wageni wengi sana katika kizingiti chetu. Katika utawala wangu natangaza rasmi mambo yafuatayo. Moja hakutakuwa na matabaka, watu wote katika ngome yangu watakuwa sawa. Mbili kila mtu atalazimika kulipa kodi ili kuhakisha huduma muhimu zina patikana. Mgawanyo wa kodi utatangazwa na waziri husika. Tatu watoto wote watahudhuria mafunzo ya shule mpaka watakapofikisha miaka kumi na mbili, baada ya hapo kila mtoto atachaguwa kitu anachotaka kufanya

Nne, ili kujenga jamii yenye haki na usawa. Nitaanzisha mahaka ambayo itakuwa inahukumu kutokana na sheria zitakazoandaliwa. Kila mtu atapata haki yake, kwa kusema hivyo naamanisha hakuna anaeruhusiwa kuchukuwa sheria mikononi mwake. Tano, nitaanzisha kitengo cha askari pamoja na magereza. Sita, wafanya biashara wote lazima wasajiliwe ili kuendelea na biashara zao, kwa kufanya hivyo mutapata ruhusa ya kukodi walinzi watakaowasindikiza katika safari zenu


**********************************************

Nasisitiza kuwa yeyote yule atakae vunja sheria, ataadhibiwa bila kujali hali yake katika ngome hii. Na mwisho kabisa, ndano ya siku mbili hizi kutatoka nafasi za kujiunga na vyombo vya usalama vya ngome hii. Kila mtu, mwanamke kwa mwanaume aruhusiwa kuomba alimaliza kuongea na kurudi kwenye kiti chake.

Master Ge akasimama na kuanza kuongea mfalme wetu ni mtu mwenye busara sana, nafahamu kuwa kuna kundi la watu litaathirika zaidi kutokana na maamuzi ya mfalme lakini niwaonye kabisa, musiifananishe busara na upole. Mfalme Fey, ni mfalme mwenye busara lakini ni mfalme mwenye kusimamia kile anachokiamini alimaliza na kurudi kwenye kiti chake.

Uishi maisha marefu mtataktifu mfalme kundi kubwa la watu likaongea kwa sauti kubwa na kupiga goti moja chini kuonesha maridhia yao katika maamuzi yake. Hafla hiyoikaisha huku watu wakiruhusiwa kula na kunywa mpaka waridhike. Fahad akaondoka na familia yake na kurudi nyumbani kwake.

Unadhani watakaa kimya aliuliza Eunice, Fahad akashusha pumzi na kutabasamu. Hawatakaa kimya, ila hii ni hatuwa muhimu ya kutengeneza ngome yenye umiyhili wa chuma. Ngome ambayo haitaanguka kwa usaliti wa ndani wala kwa uvamizi wa nje. Yajayo yanafurahisha alijibu na kumbusu mkewe katika paji la uso. Akatoka nje na kuelekea katika ofisi yake, Mtukufu mfalme, karibu aliongea kamanda Fu aliekuwa mlangoni.

Nipe taarifa aliongea Fahad akikaa kwenye kiti chake, inaonekana ulichokuwa unakifikiria kilikuwa sahihi kabisa. Kuna watu ambao si watu ngome hii na wapo hapa kwa ajili ya kukusanya taarifa na pia kupika usaliti. Watu hao wengi na wafanya biashara na wamejiunga na familia kubwa za ngome hii ili kuhakikisha usalama wao. Kutokana na sheria za awali ilikuwa ni vigumu kuwagusa lakini sheria mpya ulizozitangaza leo zimewaondolea kinga hiyo. Sasa tunasubiri amri yako tu, tuwafanye nini aliongea kamanda Fu.

Hakuna haja ya kuchafua mikono yetu kwa damu, tunaendelea na mipango yetu kama tulivyopanga. Kesho bandikeni matangazo ya wote wanaotaka kujiunga vikosi vya usalama, baada ya hapo wote watafanya majaribio. Sio kila mtu ana uwezo wa kuwa mlinda amani, nina uhakika kuwa miongoni mwa watakaoomba nafasi hizo watakuwa ni watu ambao watakuwa na uwezo katika maeneo mingine. Tukikamilisha hilo nitawaambia sehemu ya pili ya mpango wangu. Kamanda Fu akaitika na kutoka, sijui huko upande wa pili mnaendeleaje alijisemea na kuendelea na kazi zake nyingine.

Katika ngome ya Masyo, kikao kilikuwa kikiendelea na ajenda kubwa ilikuwa ni kwa namna wataweza kuvamia ngome ya Asura. Mlezi wetu amesema atabariki maamuzi yeyote yale tutakayofikia aliongea mfalme Damesh, Lakini si amepewa miaka ishirini ya amani na waliongazi za juu. Acha ujinga Soyyer, unadhani baada ya miaka ishirini itakuwani rahisi kuvamia. Mimi nakwamba hujakutana uso kwa uso na mfalme Fey. Yule mpumbavu ana roho mbaya kuliko ubaya wenyewe, hivi sasa naweza kusema kuwa uwezo wake uko sawa na mlezi wetu au kama hajamzidi. Sio mtu wa mchezo mchezo kabisa, ni kama vile anataembea na maisha ya mtu mkononi aliongea Damesh.

Hapo mi naungana na Damesh, wazee wakale wanasema ni vyema ukangowa mti angali mchanga. Ukishakomaa tu itakuwa ni vigumu kuunyofoa ardhini aliongea Kesen. Tuache kupoteza muda, tuamuwe kinafanyika kitu gani ili kumziba mdomo aliongea Felshi mwanamke pekee katika kikao hicho. “Mimi nina wazo na vijana wangu wako tayari kulitekeleza aliongea Damesh na kuchezea ndevu zake nyingi nyeupe. Wote wakainuwa masikio na kuyategesha ili kutaka kujuwa hilo wazo.

Kwanza inabidi tumkate nguvu, tunamkataje hizo nguvu. Hivi karibuni nimefanikiwa kupata sumu inayouwa taratibu. Tunachotakiwa kufanya ni kuichanganya dawa hiyo katika vyanzo vya maji vya adui yetu. Kisha tutakaa siku tatu kabla ya kuanza safari kuelekea huko kwa ajili ya kufanya mashambulizi.

Na hiyo sumu tutaifikishaje huko aliuliza Felshi.

Kuna vijana wangu wamefanikiwa kuingia katika ngome ile na wanafanya kazi chini ya kivuli cha familia kubwa na za enzi katika ngome hiyo. Si hilo tu, kazi yetu itakuwa rahisi kwasababu siku tatu nyuma mfalme wao alitangaza kuwa watu wote katika ngome yake watakuwa sawa chini ya sheria. Hilo limeonekana kuwakera sana wale wenye hadhi ya juu ambao tokea zamani walikuwa na mamlaka ya juu kuliko wengine. Hivyo kwa kushirkiana na hao kazi itakuwa nyepesi sana kwa sababu nusu na robo wapiganaji wa ngome nzima wanamilikiwa na familia hizo. Alifafanuwa.

Kama kawaida yako nyoka, niliona ajabu wewe kukaa kimya baada kudhalilishwa kiasi kile na mtoto mdogo sana aliongea Kesen na kutabasamu. Kwa kuongea hayo ni wazi kwamba mjadala huu umekwisha, leo nitawaagiza vijana wangu watie sumu na sisi tutakutana keshokutwa usiku kwa ajili ya kuanza safari kuelekea ngome ya Asura. Tutaua kila kiumbe hai isipokuwa wanawake na watoto wadogo wa kiume. Hao wanatosha kuwa watumwa na makahaba kwa ajili ya madanguro yetu aliongea Damesh na kuinuwa gilasi ya mvinyo juu. Wengine nao wakainuwa na wote wakanywa.

**********************************
 
KARIBU KWA MAONI JUU YA RIWAYA HII. ILI NIPATE KUFAHAMIANA NANYI KWENYE JUKWAA HILI.

NIMETIMIZA SEHEMU YANGU KWENYE JUKWAA SASA FARASI KAFIKA SALAMA MWISHO WA SAFARI.

NASUBIRIA MWITIKIO WAKO ILI NIONE KAMA KITABU CHA PILI HADI CHA NNE KAMA MTAKIPOKEA.
MKIWA KIMYA NAMI NAKAA KIMYA. ITAKUWA HAMJANIELEWA KWENYE KITABU CHA KWANZA HIVYO CHA PILI HAMTONIELEWA KABISA.
 
Huyu farasi mkuu nimemuelewa sana,kuna mambo umeandika humu nitaenda kufanyia kazi nione,kwa sababu nawasikia tu hawa wachungaji na manabii,twende mlimani,wengine msituni. Kumbe kuna nguvu ipo kwenye mazingira haya haya tu.

Kuhusu uandishi wako, huko poa makosa madogo ya spelling tu. Ila kwanini Indra anaonekana kumuogopa sana Fey,au ndio mtoto wake nini huyu fahad. Duniani Fahad anajulikana kama mtoto wa nje? Asante sana kwa hii zawadi,kweli wewe ni THE SPIRIT THINKER hakika,hadithi ipo Dao kwa sana.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Asante
Huyu farasi mkuu nimemuelewa sana,kuna mambo umeandika humu nitaenda kufanyia kazi nione,kwa sababu nawasikia tu hawa wachungaji na manabii,twende mlimani,wengine msituni. Kumbe kuna nguvu ipo kwenye mazingira haya haya tu.

Kuhusu uandishi wako, huko poa makosa madogo ya spelling tu. Ila kwanini Indra anaonekana kumuogopa sana Fey,au ndio mtoto wake nini huyu fahad. Duniani Fahad anajulikana kama mtoto wa nje? Asante sana kwa hii zawadi,kweli wewe ni THE SPIRIT THINKER hakika,hadithi ipo Dao kwa sana.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Asante kwa Mrejesho wako
 
KARIBU KWA MAONI JUU YA RIWAYA HII. ILI NIPATE KUFAHAMIANA NANYI KWENYE JUKWAA HILI.

NIMETIMIZA SEHEMU YANGU KWENYE JUKWAA SASA FARASI KAFIKA SALAMA MWISHO WA SAFARI.

NASUBIRIA MWITIKIO WAKO ILI NIONE KAMA KITABU CHA PILI HADI CHA NNE KAMA MTAKIPOKEA.
MKIWA KIMYA NAMI NAKAA KIMYA. ITAKUWA HAMJANIELEWA KWENYE KITABU CHA KWANZA HIVYO CHA PILI HAMTONIELEWA KABISA.
Ni miongoni mwa farasi wa kifalme aghalabu sana kuwaona. Kazi iko poa kupita maelezo hongera sana mkuu na tunashukuru kwa madini yako.
 
Back
Top Bottom