RIWAYA: Black star

Naombeni sana msamaha kwa kuchelewesha kupost🤲🤲🤲🤲🤲 mwisho juma huu nimekuwa na kazi za kunibana rafiki zangu.
 
Black star 2: Astra 11
Na Tariq Haji
0624065911


Miezi minne baadae.

Ndani ya miezi hiyo Fahad alikuwa akimpa mafunzo makali sana Yuna. Ilifika wakati walifika mpaka wiki mbili bila kulala. Alimfanyisha mazoezi hayo yote akiwa amezifunga njia zake za meridian. Kwa Yuna ilikuwa kama kiama.

"Hongera" aliongea Fahad akimuangalia Yuna ambae alionekana kuchakaa kupita maelezo. Alikuwa ni kama mwanamke kinyanya aliekula chumvi nyingi sana wakati alikuwa na miaka kumi na tano tu.

"Nahisi kama huu mwili sio wangu vile" aliongea Yuna akijizoa zoa na kuinuka.

"Tutapumzika kwa siku mbili kisha tutaelekea kwa mzee Mash. Kabla sijaondoka nilimuomba anifanyie kitu" aliongea Fahad.

Baada ya siku mbili wakafunga safari na kuanza kurudi. Safari yao ilichukuwa takriban siku na nusu mpaka kuwasili nyumbani kwa mzee Mash.

"Karibu nyumbani Fahad" aliongea mzee huyo akitoka ndani baada Fahad kugonga mlango.

"Ahsante, natumai umzima wa hali" aliongea Fahad na kutabasamu.

"Mimi niko vyema, nimesikia habari kuwa unataka kupambana na shule ya upanga ya Hai Yu"

"Imekuwaje ikafika mpaka huku"

"Hahaha! Fahad ile shule ni miongoni mwa shule kubwa zaidi hapa Astra. Na pia inatambulika kwa kutofata sheria, wanafanya wanavyojisikia kwasababu tu mfalme ndio mkono wao wa pembeni"

"Ah! Haijalishi, kwasababu walishakuwa na bahati mbaya tokea walivyopita katika njia yangu"

"Natumai maneno yaki yana mfupa" aliongea mzee huyo na kuongoza njia kuelekea sehemu yake ya kazi. Wakiwa njiani wakaongea mawili matatu mpaka walipofika.

"Nimefanya kama ulivyonambia lakini sidhani kama kuna mtu ataweza kuvitumia" aliongea mzee huyo akimuangalia Yuna aliekuwa hana hili wa lile.

"Niamini, ndani mwezi mmoja tu ataweza kuvitumia vizuri na mpaka siku ya pambano atakuwa gwiji silaha hiyo" alijibu Fahad.

Mzee Mash akatoa kikapu na kumkabidhi Fahad, akakipokea na kuangalia ndani na kutabasamu.

"Mzee Mash nataka na wewe uwepo kipindi nikimpa mafunzo. Nataka uhisi furaha unapoona silaha ulioitengeneza kwa tabu ikitumika katika hali sahihi" aliongea na kutoka.

Mbali kidogo na eneo hilo kulikuwa na uwanja mkubwa, uwanja ambao ulitumia kama sehemu ya majaribio ya silaha kabla hazijapelekwa kwa wahusika.

"Yuna umekuwa ukiniuliza lini nitakufunza martial arts, sasa kuazia leo mpaka siku moja kabla ya pambano langu utakuwa fundi kisawasawa".

"Aina gani unakusudia kunifundisha"

"Nitakufundisha kitu ambacho hujawahi kukisikia katika maisha yako"

"Sidhani, mimi nimesoma sana vitabu vya kale. Kwa hiyo hakuna martial art nisiyoijuwa".

"Tenngeeku raikkoho"

"Ni kitu gani hicho" aliuliza Yuna.

"Ndio martial art nitakayokupa"

"Ten... nini"

"Tenngeeku raikkohoo au kwa maneno ya kawaida inajulikana kama aina ya martial art ya kuchomoza kwa jua jekundu" alifafanua.

"Sijawahi isikia, wewe umeijuaje?" Aliuliza.

"Kwasababu mimi ndie nilieitunga" alijibu na kumwaga vitu vilivyokuwa kwenye ile kapu. Vilikuwa visu kumi na mbili pamoja na pete kubwa tatu. Zilipishana kwa ukubwa kiasi kutoka kila moja wapo. Ni kama vile zilikuwa zimetengezwa kuongia ndani ya pete nyingine kila moja wapo.

Fahad akachukuwa pete kubwa kuliko zote akaiweka vizuri, kisha akachukuwa inayofuata na kuingiza ndani ya pete kubwa na mwisho kabisa akachukuwa pete ndogo na kuingiza ndani ya pete zile mbili.

Baada ya hapo akachukuwa vile visu na kuvipanga kuzunguka zile pete na kuvifanya vyote vionekana kama juwa lililokuwa linachonza asubuhi. Vile visu vilikuwa kama mionzi iliojichora vizuri.

"Mzer Mash, inaonekanaje"

"Sijawahi kutengeneza silaha inayopendeza machoni kama hiyo" aliongea huku macho yake yakijaa maji maji.

"Huu ni mwanzo tu, ngoja uone pale atakapokuwa ameweza kuitumia" aliongea Fahad kwa majigambo.

"Naibebaje, maana sioni sehemu ya kushikia" aliongea Yuna.

"Kweli kabisa Fahad, itakuwa ni upotevu wa muda na nguvu tu ikiwa haibebekie" aliongezea Mzee Mash.

"Msiwe na pupa, kwani mi nilikwambia ni lazima silaha iwe na sehemu ya kushika. Yuna yale mazoezo yote niliyokuwa nakupa yalikuwa ni kwa ajili ya silaha hii. Kuanzia leo na kwa mwezi mzima unatakiwa uwe unaingiza Qi yako kwenye hiyo silaha. Inatakiwa kuwa kama sehemu ya mwili wako, isikupe shida pale unapoitumia. Isiwe tofauti na mikono au miguu yako"

"Nitawezaje kufanya hivyo?"

"Nimekwambia fikiria kama hiyo silaha ni miguu au mikono yako. Kwani unapata shida yeyote kupeleka Qi kwenye mikono yako" aliongea Fahad na kusimama pembeni.

Yuna akakaa kitako mbele yake ilikuwepo silaha aliyoambiwa aingize Qi yake. Akafumba macho na kutuliza akili yake, haikuwa rahisi kama alivyoadhani. Alilifanya zoezi hilo kila siku bila kukata tamaa. Fahad aliendelea kumsimamia pasi na kumueleza kitu. Alitaka agundue jambo hilo kwa akili yake mwenyewe.

Mwezi mmoja ulikatika kama mchezo, kwa Yuna aliona hakuna mabadiliko yeyote yale.

"Yuna imetosha sasa, umefanya nilichokwambia kwa mwezi mzima pasi na kuuliza jambo. Najua unahisi kama hakuna mabadiliko lakini sivyo" aliongea Fahad na kumgusa bega Yuna aliekuwa amefumba macho.

"Funguwa macho yako" alitoa amri, Yuna akafunguwa. Mbele yake kulikuwa na visu kadhaa vikielea.

"Unahisi uzito wowote" aliuliza Fahad.

"Hapana, sihisi kitu"

"Vizuri, simama", Yuna akasimama na kushusha mikono yake. Ghafla visu vyote pamoja zile pete tatu zikaanza kuelea.

"Binadamu unaposimama, kila kitu kinasimama na wewe. Mwili mzima unanyooka, sawa na hiyo silaha. Kwasababu unadhani ni sehemu ya mwili wako ndio maana na zenyewe zimeinuka na wewe" alifafanua Fahad.

Japo vilikuwa vinaelekea lakini havikuwa katika mpangilio maalum. Vilizunguka huko na kule na laiti kama kungekuwa na mtu karibu basi vingemuuzi.

"Usifikirie kama hizo ni silaha tofauti bali ni moja tu. Na kitu kimoja hukaa sehemu moja. Vikusanye nyuma ya mgongo wako. Hiyo ndio itakuwa sehemu yake ya kukaa" aliongea Fahad.

Yuna akafanya hivyo, mwanzo ilikuwa ngumu lakini taratibi vitu hivyo vikaanza kuhamia mgongoni kwake.

"Leo utapumzika, kesho tutaanza mazoezi ya kutumia silaha yako mpya. Nitatumia mwezi kasoro kidogo kukufundisha. Jitihada zako ndio zitakazofanya uitumie ipasavyo.

************
Watu walikuwa wamekusanyika katika uwanja mkubwa wa shule Hai Yu kushuhudia pambano lilipigwa mnada kwa muda mrefu sana.

"Wote sujuduni, paladin la mfalme linapita" aliongea mtu mmoja kwa nguvu. Paladin ni kama chombo ambacho kinatumiaka kumbeba mfalme. Chombo hicho kimebebwa mabegani na baadhi ya watu waliokuwa hawana nguo za juu.

Watu wote walokuwa eneo hilo wakasujudu, wakatulia hivyo paladin ilipofikishwa eneo la kushuka mfalme. Akashuka na kuelekea sehemu ya juu zaidi na kuketi kwenye kiti chake. "Inukeni" ikatoka amri nyingine, watu wote wakainuka.

"Karibu mfalme wangu" aliongea Master Dan kwa u imani.

"Wako wapi wahusika" hakujibu bali akatupa swali.

"Labda wameogopa, mpaka sasa hawajafika" alipomaliza kuongea tu. Geti kubwa likafunguliwa, aliepita alikuwa Fahad nyuma yake akifuatiwa na Yuna, Master Lu pamoja na Master Jerome. Nyuma yao na kikundi kidogo cha watu kutoka chama cha wawindaji.
 
Black star 2: Astra 13

"Shameless bastard, unadiriki kuuza maisha ili uthibitishe kwamba sikuwezi" aliongea Fahad. Alionekana kutotikiswa kabisa na mabadiliko ya Gahena. Kama mwenda wazimu Gahena akamvamia Fahad na kuanza kufanya mashambulizi ya kasi.

"Ngoja nikusaidie" alionge Fahad, akakwepa shambulizi moja kisha akazunguka kwa kasi na kumchapa ile fimbo ya mgongo. Hakuishia hapo, akamzunguka na kumchapa tena na tena. Na kadri alivyozunguka ndivyo kasi na ukali wa mashambulizi yake ulivyoongezeka.

Shambulizi lake la mwisho aliinuwa fimbo yake juu kwa kuilaza kidogo na kuishusha kwa kasi. Ila kabla haijafika, Rahee akatua mbele ya Gahena.

"Imetosha usiendelee kumuadhibu kakaangu" akaongea machozi yakimtoka. Fahad akamwangalia kwa macho makali sana lakini akaamua kumsiliza.

Wakati wakiwa katika hali hiyo Gahena akaona hiyo ndio nafasi ya kummaliza adui. Kwa kutumia uwezo wake wote akamchoma Rahee panga la mgongoni na kulizamisha kwa nguvu. Likatokea upande wa pili, hakuishia hapo akazidi kulisukuma mpaka likamfikia Fahad.

"Gahena kwanini lakini" aliongea Rahee kwa tabu kidogo.

"Hahaha, katika familia yetu hatuhitaji kuwa na warithi wawili. Na nikwambie kitu, mimi sikuwahi kukuona kama mdogo wangu. Wewe utabakia kuwa mwanaharamu tu" aliongea na kutaka kulichomoa panga.

Fahad akalishika kwenye makali, akazunguka kwa kasi na kufyatua teke kali sana lilitua kifuani mwa Gahena na kumrush mpaka ukutani. "Samahni Fahad lakini (kof kof)" alitaka kuongea lakini akashindwa na kukohoa damu. Akambeba na kumepeleka walipo Yuna na wengine.

"Master Jerome, nataka uwe unamsaidia huyu kijana kwa kuingiza Qi katika mwili wake. Ukichoka utapishana na mtu mwengine lakini zoezi hilo liendelee mpaka nitakapomaliza kazi hapa" aliongea mishipa ya kichwa ikiwa imevimba. Ilikuwa ikitweta kama mapigo ya moyo.

Akarudi ulingoni na kuinuwa mikono juu, "Yuna" akaita kwa nguvu. Yuna akarusha visu viwili vilivyokwenda kugonga katika zile bangili alizokuwa nazo mikononi. Bangili hizo zikaanguka na kusababisha nyufa katika baraza hiyo.

"Baba na wengine kaeni nyuma yangu, kitakachokwenda kutokea sasa si pambano tena bali ni mauaji ya halaiki. Kama mkubwa amevurugwa" aliongea na ile silaha iliyokuwa mgongoni ikahamia mbele na kuanza kuzunguka kwa kasi mpaka ikatengeza ngao ya Qi.

Wakati huwo Gahena alikuwa akijizoa zoa, "nilikwambia kuwa ni takataka zilizooza, sasa ngoja nikuoneshe sehemu yako ni wapi" alisikia sauti hiyo ikitokea pembeni. Ikafuatiwa na kofi kali kali sana lilituwa shavu la kulia. Akarushwa juu huku akizunguka mara kadhaa, kabla hajatua akatahamaki kofi jingine.

Makofi yaliendelea, mwisho yalikuwa yakisikika kama mabomu. Kila lilipotua ulitoka moshi, kofi moja likatua kifuani na kumpaisha Gahena juu. Fahad akavuta pumzi nyingi, wakati anatua akafyatua mkono wake na kiganja kikatua kwenye kitovu. Gahena alifyetuka kwenye mkono huwo kama jiwe kwenye manati yenye mipira mahiri kabisa. Akabamiza ukutani na kucheua damu, alikuwa hatambuliki. Kila mfupa kwenye mwili wake ulikuwa umevunjika.

"Umemtia ulemavu mwanafunzi wangu" aliongea Master Dan akitua na kumuangalia Gahena ambae alikuwa hajitambui.

"Sio ulemavu tu, nimevunja dantian zake zote tatu. Kuanzia leo mpaka mwisho wa maisha yake hataweza kucheza martial art tena. Si hilo tu, atakuwa kichaa maisha yale yote. Tena hapo nimemuonea huruma" alijibu Fahad.

"Wanafunzi wote pamoja shule zote zilizokubaliana kutusaidia hakikisheni huyu mshenzi anakufa" aliongea kwa nguvu. Watu wengi wakaruka na kuingia ulingoni.

"Na mimi nasema hivi, kama hutaki shule yako itoweke ondoka uwanjani. Vinginevyo siku ya kesho haitakuwepo, nitaua walimu wote walioruhusu vijana wadogo kuja kaburini kwao" aliongea kwa nguvu.

Wakajifanya kama hawajasikia na kuanza mashambulizi, Fahad hakutaka kucheza nao. Kila shambulio alilofanya liliwaondoa kadhaa na kuwafanya washindwe kuendelea. Vilikuwa ni vilio tu uwanjani hapo na baada ya nusu saa wote walikuwa chini. Fahad ndie aliekuwa amesimama, mwili wake ulikuwa ukitoka kitu kama mvuke.

"Haiwezekani, hakuna binadamu anaeweza kupambana na watu wote wale. Hasa wakiwa daraja la jin dan na kutoka pasi na kuwa na hata mkwaruzo" alijisemea Master Dan.

"Walimu wote naomba muingie ulingoni" aliongea kwa nguvu na walimu hao wakafanya hivyo lakini hakukuwa na tofauti. Haukuwa mpambano tena bali ni kipigo kwa upande mmoja. Fahad hakuonesha huruma hata kidogo, aliwasulubu kama watoto wadogo ambao wamejuwa kutembea karibuni.

"Huu ndio uwezo wenu wote" aliuliza akimuangalia Master Dan ambae tayari kijasho kilishaacha kumtoka.

"Master Dan, huna haja ya kuingia ulingoni. Niachie mimi huyo mpuuzi" hatimae mfalme aliongea na kutuwa ulingoni kwa kishindo na kusababisha tetemeko dogo la ardhi.

"Nafasi ya yule kijana kushinda haipo tena, mfalme wa ngome hii ndie anajulikana mtu mwenye nguvu kuliko yeyote".

"Masikini kijana wa watu, laiti kama asingechokoza angeishi miaka mia kadhaa lakini ni bahati mbaya sana kwake"

Watu walikuwa wakinong'ona pembeni, Fahad alisikia minong'ono hiyo lakini wala haikumshutuwa sana.

"Unaonaje kijana ukasalimu amri, mimi kama mfalme nitakupa adhabu ndogo sana. Nitaivunja dantian yako ya tumboni pamoja na kukukata miguu na mikono yote kisha nitakuacha uishi. Hakika ya mimi ni mfalme mwenye busara sana" alijigamba mfalme huyo.

"Acha upumbavu, unaonaje ukawaambia watu ukweli pamoja na kuwatajia daraja lako halisi. Tong san ni daraja la maonesho tu kwako, eti mfalme wa majini" aliongea Fahad.

"Mfalme wa majini?"

"Ndio nani huyo?"

"Huyu kijana kweli anataka kufa, mpaka kumsingizia mfalme jambo baya kama hilo" watu waliongea.

"Mumeona nimewaambia kuwa huyu ni mwana martial art anaejufunza aina za kijini lakini mkaona si kweli. Sasa anamsingizia mfalme kuwa ni mfalme wa majini" Master Dan alitumia nafasi hiyo kuwasha moto wa chuki katika mioyo ya watu.

"We mfalme juha, ukiwa hutapambana na mimi kwa uwezo wako wote nasi jihesabu kama umekufa. Huwezi ujasiri na mimi ukiwa unatumia mbinu za daraja la tong san, kama unadhani kuficha uwezo wako na kudanganya watu ni vyema basi nasikitika sana" aliongea Fahad.

"Hahaha, kijana inabidi uchague kati ya maisha yako ama ya mzee huyu" aliongea mfalme na kuinuwa mkono juu. Wakafika walinzi wawili wakiwa na mzee Mash, alionekana kupigwa kiasi.


"Fahad usimisikilize, anajua kabisa kutoka katika kina cha wake kuwa hawezi kukupiga. Anapanga mbinu chafu ili usalimu amri" aliongea mzee Mash. "Nyamaza maluuni mmoja wee" alichezea kibao kutoka kwa mmoja kati ya walinzi.

Moyo wa Fahad ukauma sana, akahisi kama anachanwa kwa kitu kikali sana.

"Nini maamuzi yako Fahad, tunafahamu kuwa huyu mzee nae anajifunza martial art za majini ndio maana nikamkamata. Nina imani una huruma sana na wazee, kubali na usalimu amri" aliongea mfalme bila hata chembe ya aibu.

"Fahad kumbuka kilichokuleta huku, na pia kumbuka sio kila kinachoonekana kwa macho basi ndivyo kilivyo kiuhalisia" aliongea mzee Mash. Mlinzi mmoja kwa hasira akamkita kisu cha shingo, mzee Mash akaanguka chini taratibu damu zikimtoka. anamuangalia Fahad kwa macho nakavu na tabasamu kisha akanena maneno kadhaa kabla pumzi haijaacha mwili wake.

Bila mategemeo machozi yakaanza kumtoka, akadondokea magoti na kujiinamia. "Laiti ungekubali mapema tusingefika huku" aliongea mfalme akijifanya kusikitishwa na jambo lililotokea.

"Si mulikuwa mnataka vita, sasa nimeipata" aliongea na kuonua uso wake. Macho yake yalikuwa yamebadilika kiabisa. Viini vyake vilikuwa na alama.ya yin na yang, akazigonga zile bangili zilizokuwepo miguu na kuzivunja.

"Master Jerome, baba na wengine hakikisheni mnapeleka Qi nyingi kichwani. Kaka mkubwa amekasirika kweli kweli, aliwahi kunambia ikiwa atatuyumia theluthi moja ya uwezo wake basi hakuna anaeweza kusimama nae sawa katika ulimwengu wa Astra. Na kwasasa amefunguwa meridian moja, mnachokwenda kukiona sasa Fahad mwengine. kabisa" aliongea Yuna kukaa kitako.
 
Black star 2: Astra 14


Akaanza kuzungusha Qi yake kwa kasi sana huku nyingi ikienda kichwani. Wengine nao wakakaa chini na kuanza kufanya hivyo. Fahad akaangalia walipo kisha akatabasamu na kusimama.

Kwa sekunde kadhaa kila kitu kikawa kimya, taratibu mawingu yakaanza kujikusanya na kuanza kuzunguka. Mfalme pamoja na master Dan wakaangaliana huku kila mmoja akijaribu kutafakari juu ya manadiliko hayo.

"Ni nini hiki master Dan" aliuliza mfalme.

"Siamini ninachoshuhudia, mtu ambae amefika daraja la chakra tu ndie anaweza kusababisha mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa. Nahofia kwamba huyu Fahad si mtu wa kawaida hata kidogo. Mfalme wangu tusipotumia uwezo wetu wote kuna hatari ya kupoteza maisha" aliongea Master Dan.

"Ila si unajua tukiamua kutumia uwezo wetu wote tutaharibu mipango ya muda mrefu".

"Unadhani kwanini leo nimekusanya watu wengi, ni kwasababu ya huyu mpuuzi au. Sivyo, siku kadhaa nyuma nilipata maono kuwa kuna hatari ya mpango wetu kukamilika kutokana na ujio wa kiumbe ambae sikufanikiwa kumtambuwa. Hivyo nikaona kwasababu kazi yetu ilishakaribia kukamilika, niitumie nafasi ya kutangaza pambano na huyu jamaa".

"Nilikuwa na uhakika kuwa uwanja ungefurika watu na miongoni mwa watu hao wasingekosa wanawake bikira"

"Master Dan una akili sana, hata mimi sikuwaza hilo"

"Huh usinisifie sana, hii ni sehemu ya uzalendo wangu kwa mabwana zangu tisa waliolala kuzimu".

"Kwa kuniambia hivyo nina imani umeshamaliza kazi kabisa"

"Ndio, muda si mrefu nimemtoa kafara mwanamke wa elfu tisa mia tisa na tisini na tisa. Namba hiyo inafanana na roho anazohitaji mtukufu Hezoromo ili kuja katika ulimwengu huu"

"Vizuri sana, basi mimi nitapambana na huyu kijana wakati wewe unakamilisha maandalizi ya kumuamsha. Unahitaji muda gani hasa"

"Nahitaji dakika zisizopunguwa thalathini" alijibu Master Dan na kutoweka mbele ya macho ya watu.

"Kwanza nikusifi sana kijana, sijui umeishi miaka mingapi mpaka kugundua kuwa mimi si binadamu kwa urahisi hivyo. Lakini hilo halitasaidia, tumekuwa tukifanya maandalizi kwa miaka mingi sana takriban mia moja na namba zake huko. Siku ya leo ulimwengu wa Astra utashuhudia jambo zuri sana na baada ya hapo wote mtakufa kupoza hasira za kufingiwa kwa bwana wetu" aliongea mfalme.

Macho yakaanza kubadilika, nguo alizovaa zikaanza kuchanika kutokana na mwili wake kutanuka. Mbawa kubwa zenye mfanano na zile za popo zikatokea mgongoni kwake. Zikifuatiwa na mkia mkubwa uliokuwa na manundu. Mikono yake ilibadilika na kutoka makucha, alitisha sana.

"Jini", "jini". Watu wakaanza kukimbia hovyo, kila mmoja alikuwa akijaribu kuokoa maisha yake. Katika ulimwengu wa martial art hakuna jambo lililokuwa likiogopeka kama majini na viumbe vya ajabu. Hilo lilitokana na uwezo wa viumbe hao kuwa mkubwa kuliko binadamu wengi. Na pia iliaminika kadri jini alivyoishi miaka mingi ndivyo uwezo wake wa kuishi na binadamu ulivyokuwa mzuri.

"Unajua nina miaka mingapi" aliongea mfalme ambae wakati huu alikuwa ni kiumbe cha ajabu.

"Kutokana na ukubwa wa pembe zako naweza sema, upo katika miaka elfu moja na elfu tano. Lakini miaka yako isikutie kiburi kwasababu umekutana na mimi" alijibu Fahad.

"Hahahahaha! Wewe huonekani hata kufika miaka mia moja, unadhani una uwezo wa kunishinda mimi"

"Ukiwa unaongea uwe unamuangalia unaeongea nae" alisikia sauti ikitokea upande wake kulia. Ikafuatiwa na ngumi kali sana iliyomrusha mita kadhaa kutoka aliposimama.

"Amefikaje pembeni yangu bila mimi kufahamu" alijiongelea mwenye akiinuka.

"Unazubaa nini, utakufa" alisikia tena, na kujikuta akibamiza ukutani. Fahad alikuwa akifanya mashambulizi ya kasi, mfalme akawa na wakati mgumu sana.

Akapiga mkia wake chini kwa nguvu na kusababisha ardhi, jambo hilo likakata mnyororo wa mashambulizi wa Fahad. Baada akamvamia na kuanza mashambulizi. Fahad akajitahidi kukwepa mashambulizi hayo ya kasi. Mfalme akanguruma kisha akanena maneno fulani katika ulimi ambao Fahad hakuuelewa kabisa.

Kwenye makucha ya kiumbe huyo kukaanza kuwaka moto mweusi. Akazungusha mikono yake kwa nguvu, moto ule ukazidi kuwa mkubwa na baada ya akafanya kama anarusha. Fahad akakwepa kurudi nyuma, "sijui kwanini ila nina hisia huu moto ukinipata itakuwa kwisha habari yangu" alijisemea huku akichezesha macho yake kwa kasi.

Alikuwa akitafuta upenyo wa kufanya shambulizi moja kali sana ili limpe nafasi ya kujipanga vizuri. Mfalme akazidi kufanya mashambulizi bila kumpa Fahad nafasi ya kufikiria cha kufanya isipokuwa kukwepa mashambulizi hayo.

Kwa mfalme hilo lilikuwa ni muelekeo wa ushindi, kidogo asichojuwa ni kwamba alikuwa akicheza katika mikono ya Fahad. Fahad alielewa kadri yalivyokuwa makali ndivyo alivyoweza kuyaona vizuri. Akili yake ilikuwa ikifanya kazi mara dufu kutengeza kila aina ya tukio litakalotokea. Ilikuwa ikisoma na kutengeneza kumbukumbu za aina ya mashambulizi anayoyafanya adui yake.

Duara nyembamba zilijichora kuzunguka viini vyake, pete hizo zilikuwa zinang'ara. Mwanzo alionekana kupumua kwa shida lakini baada ya kama dakika tano za mashambulizi pumzi yake ikatulia. Ni kama alijua ni eneo gani adui yake atashambulia. Hivyo alikwepa kwa wepesi bila kuhofia kugusa na mashambulizi hayo.

Wakati anafanya hayo alimuangalia adui yake kwa makini na kugundua kila baada ya mashambulizi matatu alivuta pumzi. Fahad akaitegea nafasi hiyo, mfalme alipofika kuvuta pumzi Fahad akakunja ngumi na kuikaza kisawa. Akapiga hatua moja kuingia ndani kisha akaachia sumbwi kali vibaya sana. Sumbwi hili likamkuta mfalme pasi na mategemeo yake. Alitupwa na kujigonga ukutani, ukuta ukavunjika.

Fahad akaburuza mguu na kuurudisha nyuma, akabonyea kidogo na kuanza kuchezesha misuli yake. Taratibu ikaanza kujaa, damu nyingi iliyosafiri katika misuli ilithibitishwa na mishipa midogo iliotuna kwa juu.

"Ngoja nikuvujishie siri, mimi sio mtumiaji wa silaha aina yoyote ile. Mwili wangu ndio silaha yangu, natumia silaha tu uwezo wangu mkubwa" aliongea Fahad. Mfalme akachomoka alipo na kutaka kumvaa lakini Fahad akakwepa na bila kutulia akazunguka na kuachia teke kali lililoingia mbavuni. Alihis kabisa amevunja mbavu kadhaa na kiumbe hiyo.

"Aggghhh!" Mfalme aligugumia kwa maumivu akishika upande wa mbavu uliyopata jeraha. Ngumi kali ikatuwa utosini mwa mfalme, ililia kama chuma kilichogonga chuma kingine. Mfalme akapigiza uso chini na kupasuwa sakafu.

"Damn! Una kichwa kigumu, lakini leo nitakiponda" aliongea Fahad na kutabasamu. hapo mfalme akajua kabisa kuwa Mpaka wa kushinda ulikuwa mdogo sana. Akapiga kelele na kunguruma kwa nguvu, ardhi ikaanza kutetemeka.

"Fahad kwa leo tunaishia hapa, ikiwa utapona kutoka katika wimbi la viumbe wangu basi tutakutana siku nyingine" aliongea na kutabasamu.

"Mimi na wewe hatuna siku nyingine" maneno hayo yaliambatana sahihi kabisa na ngumi kali iliyotua kifuani upande wa moyo. Fahad akaachia wimbi kubwa la Qi iliopenya mpaka ndani na moyo wa mfalme na darasa upasuke. Mfalme akaanguka chini na kupoteza maisha.

Fahad hakuoana haja ya kukaa eneo hilo, alihitaji kuwa na ulinzi kama wengine wako salama. Akatoka nje ya ulingo na kumkuta Yuna na wengine wakisubiri. "Kwasasa tuonomdokeni hapa, ninapata hisia kwamba kiumbe kinachokuja si cha kawaida. Tunahitaji kujipanga ili kupata nacho" aliongea.​
 
Black star 2: Astra 15

Wakaondoka eneo hilo na kuelekea nyumbani kwa Master Lu. Wakati huwo hali ya hewa ya Astra ilishaanza kubadilika. Kwa watu wa kawaida au kwa wale ambae kiwango chao cha martial art ni kidogo waliona mabadiliko hayo si ya kutisha sana lakini kwa kikundi cha Fahad walihisi kabisa hali ya hatari.


Walifika nyumbani kwa master Lu na kuingia katika ukumbi mdogo wa vikao vya dharura. "Najua mimi huku si mwenyeji lakini kuanzia hapa kama kuna mtu anatamani kuishi basi afuate maelekezo yangu" aliongea Fahad baada ya kutulia tu.


"Ukiwa master wa daraja lako hakuna sehemu ambayo watu wataacha kukusikiliza, tufungue macho" aliongea Master Lu na kuinamisha kichwa.


"Najua mumesoma vitabu au mumewahi kusikia kuhusu wafalme tisa wa kuzimu. Hezoromo ni mmoja kati yao, huyu ni mfalme wa kuzimu mwenye uwezo mdogo zaidi kuliko nane wengine lakini huwo uwezo wake si mdogo kama mnavyofikiria" aliongea.

"Hezoromo ameishi miaka mingi sana na mara ya mwisho alivyopigwa na kufungiwa kuzimu ilikuwa ni zaidi ya miaka elfu mingi iliyopita. Wakati huwo alikuwa kati na uwezo ambao kwa binadamu tunaweza sema ni sawa na ule wa master alie katika daraja la Mage. Na sasa sijui atakuwa katika daraja gani, hivyo kati yenu hakuna hata mmoja ambae anaweza kusimama nae".

"Tumeelewa sasa tuambie nini kinagitajika kufanyika" aliongea Master Lu.

"Kwanza nakadiria ndani ya dakika kumi atawasiki Astra, ninachohitaji ni nyinyi mniazime dakika kumi nyingine baada ya kuamka kwake ili nifanye maandalizi. Ili kushinda nahitaji kutumia uwezo wangu wote".

"Lakini umesema kati yetu hakuna mwenye uwezo wa kusimama nae" alidakika Master Jerome.

"Ndio, ila pindi anapowasili huwa hana nguvu sana. Ninachohitaji ni nyinyi kumpumbaza. Ukitimia muda niliowaambia, mtatafuta sehemu ya kujificha. Mimi nitashughulika nae kuanzia hapo" alifafanua.

"Anhsa sawa, kama kuna jambo jingine naomba utuambie kabisa" aliongea Master Lu.

"Yuna, pindi nitakapoanza kujiandaa. Qi yangu iliyokuwepo mwilini mwako huenda ikashindwa kuidhibiti, hivyo wewe nahitaji ukae kule bustani na ujitahidi kadri ya uwezo wako kuituliza. Baada ya hapo kutokana na sheria za kimazingira, mimi na wewe tutapitia utakaso wa radi. Najua unaelewa maana ya jambo hilo".

"Ndio naelewa kaka mkubwa" alijibu Yuna.

"Sawa wote mkafanye nilichowaambia mimi nitabaki hapa kujiandaa" aliongea na kusimama. Kila mtu akatoka na kuelekea alipoambiwa aende. Fahad kasogea katikati ya ukumbi huwo na kukaa kitako.

"Baada ya kufungua meridian zangu zote, nitakuwa na muda usiopunguwa nusu saa kumalizana na Hezoromo. Aidha nimuue au aniue lakini sitamrudisha tena kuzimu" alijisemea na kuanza kujibonyeza katika baadhi ya maeneo ya mwili wale.

"Kumi na mbili tayari" alijisemea na kuvuta pumzi nyingi. Qi nyingi ikaanza kusafiri kutoka kwenye dantian zake, macho yakabadilika kabisa viini vyake vikawa vyekundu na kuzungukwa na pete mbili za rangi ya dhahabu.

Kofia aliokuwa amevaa kichwani mwake ikaanza kuelea ma kushuka mgongoni. "Alambara, piga ngoma ya vita nahitaji kufungua meridian nane za dragon" aliongea na kujifonga kwa kasi katika shingo mara mbili, kifua mara mbili na pembeni mbavu zote mbiili mara mbili. Ngoma ya kivita ya alambara ikaanza kulia.

Fahad akakutanisha viganja vyake na kufumba macho, mvuke wenye rangi ya damu ya mzee ukaanza kumtoka na kadri muda ulivyokwenda rangi hiyo ilikoza na taratibu ikaanza kubadilika na kuwa nyeusi.
**********
Master Lu akabamizwa katika miti, "master Lu unajisikiaje" Master jerome alifika na kumsaidia.

"Katwambia akifika hatakuwa na nguvu lakini sijui kamaanisha nini" aliongea Master Lu na kutema mate.

"Nina uhakika kamaanisha alichosema, sema hili dudu lina nguvu sana" aliongea Master Jerome.

"Tusiwaweke wengine, turudi tukaendelee kupambana, zimebakia dakika kumi tu" aliongea na kupaa kwa kasi.

"Mungu wangu wa Nirvana, tulinde ndani ya dakika hizi kumi" aliongea Master Jerome na kupiga mruzi. Akafuka chui mkubwa mitihili ya nyati. Akapanda mgongoni na kuelekea walipo wengine.

"Binadamu ndani ya kipindi ambacho tumefungiwa mumekuwa na kiburi sana" aliongea Hezoroma na kungurima. Pembe zake kubwa nyeusi zilizokuwa zikiwaka moto katika ncha zake zilitisha sana. Mpaka wakati wana martiao art wengi walishapoteza maisha na waliobaki walikaribia kukata tamaa.

"Bwana wangu hao wote wanakupotezea muda, kuna mtu wanamsubiri" aliongea Master Dan.

"Hahahaha, pumbavu sana. Nani katika ulimwengu huu anaweza kupambana na mungu" aliongea Hezoromo. Mwili wake ukaanza kutoa moshi na kimo chake kikaanza kupungua na baada ya dakika kama tatu hivi akawa na urefu sawa na binadamu wa kawaida. Uwezo wake ulikuwa unakamilika rasmi.

"Muda wa kucheza umekwisha binadamu, nimerudi katika mimi wa zamani. Bahati mliokuwa nayo haipo tena" aliongea na kuinuwa mkono wake wa kushoto juu, angaa ikaanza kupasuka na mapande ya mawe yawakayo moto yakaanza kushuka kwa kasi.

"Master Lu nahisi huu ndio mwisho wa maisha yetu" aliongea Master Jerome akijifuta damu iliyokuwa ikimchuruzika katika paji lake la uso na kufunga macho. Hakuwa na uwezo hata wa kusimama, alishatumia nguvu zake zote kupambana.

"Mumefanya vyema, nendeni mkapumzike" walisikia sauti ikifuatiwa na umbile la mtu akitua mbele yao. Hawakusikia hata kishindo ni kama vile aliekuwa anaelewa milimita chache kutoka ardhini.

"Fahad ni wewe au" aliuliza Master Lu kwa sintofahamu.

"Ndio"

"Umetukuka mutukufu Asura" maneno hayo yalitoka kinywani mwa Master Lu na kupiga magoti. "Mchukue bwana Jerome na muondoke hapa" aliongea Fahad. Akabonyea kidogo na kurudisha mkono nyuma, akakunja ngumi na kupiga hewani. Ikafuatiwa na upepo mkali sana wa moto uliosababisha yale mapana ya mawe yenye moto kuzimika na kusambaratika kabisa.

"Wewe ni nani?" Aliuliza Hezoromo.

"Umemsahau aliekupiga mpaka ukapiga magoti na kuomba uachie maisha yako" alijibu Fahad.

"Asura, hehehe. Grrree! Hakuna siku mtumishi bila mimi kuwaza jinsi gani nitakavyokuuwa" alijibu Hezoromo na kumrukia Fahad. Fahad akarudisha mguu wa kulia nyuma na kuzunguka, akafyetua teke kali sana lilimkuta Hezoromo sawia usoni.

Hezoromo akatupwa kwa kasi na kubamiza katika nyumba kadhaa na kuvunjika. Wakati anajikusanya akatahamaki akichezea msumari mkali sana wa kifua. Akapaishwa mpaka nje ya ukuta mkubwa wa ngome hiyo.

"Inakuwaje unaweza kuniumiza kiasi hiki" aliongea Hezoromo na kukohoa damu.

"Mimi sie niliyekufunga, mimi ni mwanafunzi wa aliekufunga" aliongea Fahad na kukita mguu chini. Ardhi ikapasuka, "usijali mimi sita kuzimu, nitakuua kabisa. Sina huruma kama mwalimu wangu" aliendelea kuongea.

"Unadhani kwanini hakuniuwa, unadhani alipenda kufanya hivyo. Laa! Ni kwasababu hakuwa na uwezo wa kifanya hivyo" alijitamba Hezoromo. "Endelea kujitamba lakini leo utakufa, maana wewe ni wa kwanza tu, nane waliobaki watafuata" aliongea Fahad na kubonyea. Misuli yake mikubwa ikaanza kutetemeka, Qi nyeusi iliyotoka mwili mwake ilisababisha mpaka miti iliyokuwa karibu nae kunyauka.
 
Back
Top Bottom