THE SPIRIT THINKER
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 419
- 652
- Thread starter
- #121
Black star 2: Astra 21
"Karibu na samahani kwa usumbufu" aliongea Fang Shi akimuonesha Fahad kiti cha kukaa. Akakaa na kutulia bila kuongea kitu, uso wake tu ulionesha kuchukizwa na tukio lililotokea.
"Najua kijana wangu atakuwa amekuudhi lakini kwa niaba yake naomba msamaha" aliongea Fang Shi na kuinamisha kichwa. Fahad akashusha pumzi na kutabasamu, "achana nayo yashapita hayo" aliongea.
"Nashkuru kwa uwelewa wako, naomba nikufahamu jina lako" aliongea baada ya hali ya hewa kuwa nzuri.
"Mimi naitwa Fahad, na huyu ni mwanafunzi wangu Rahee. Sisi tumetokea Astra, tumeingia Sekai siku kadhaa tu" aliongea.
"Umesema umetoka Astra, lakini huu si msimu wa mlango kufunguliwa eti" alistaajabu.
"Kwani huwa kuna mlango maalum wa kuingilia huku"
"Ndio na utafunguka miezi miwili ijayo" alijibu.
"Basi sisi tulikiwa hatujui"
"Kwa hiyo mumefikaje?"
"Tumepita katika Koridoo ya muda"
"Ko ko...koridoo ya muda, wengi wanaopita huko hupotea kabisa au huchukuwa mpaka mwaka"
"Sasa mimi naomba hilo liwe siri kati yetu, sitaki macho mgongoni kwangu" aliongea Fahad na kukunja ndita.
"Sawa hakuna shida, mpaka umekuja hapa ni wazi kwamba una shida inayohitaji kutatuliwa"
"Ndio, nahitaji makazi".
"Kawaida huwa tuna maeneo ambayo wageni wetu hufikia hasa wale wanakatikaza kutoka ulimwengu mmoja kuingia mwingine. Lakini wewe umekuja mapema, hivyo wale waliokuwepo tokea mwanzo hawajaondoka na chama hakina makazi ya ziada".
"Si lazima yawe ya chama"
"Alaa, kuna makazi lakini yako mbali sana na hapa. Ni nyumba iliyojitenga, ipo mlimani na karibu yake hakuna nyumba nyingine. Ni nyuma ya aliekuwa mwenyewekiti aliepita kabla hajapata utakaso na kuelekea limwengu za juu zaidi".
"Hiyo hiyo itatosha, kwanza sipendi kukaa kwenye vurugu nyingi, tael ngapo kwa mwezi"
"Tatiza sio tael, kabla hajaondoka alisema mwenye sifa ndie atakaeweza kuishi pale lakini hakuzitaja sifa".
"Oh! Twende tukajaribu kama sifa ninazo" aliongea Fahad.
"Sawa subiri nieke mambo sawa, kisha tutaondoka" aliongea.
Fahad na Rahee wakatoka na kuelekea kwenye meza kwa ajili ya kusubiri. Ndani ya tawi hilo kulikuwa na mgahawa uliokuwa ukitoa huduma za chakula. "Master mimi nahisi njaa" aliongea Rahe akimeza funda kubwa la mate baada ya kunusa harufy ya chakula.
"Agiza chakula" aliongea Fahad, Rahee akainua mkono. Akafika mhudumu wa kike, "karibuni niwasaidie chakula gani" aliongea kwa sauti ya upole.
"Chakula namba moja mnachopika hapa" aliongea Rahee.
"Sawa" aliitika na kuondoka.
"Master lini utaanza kunipa mafunzo" aliongea Rahee kwa shauku akimuangalia Fahad usoni.
"Tukishapata makazi utaanza mafunzo" alijibu kwa kifupi tu na kuendelea kuzungusha macho yake kulia na kushoto. Alihisi kitu hakipo sawa, kazi zilikuwa nyingi katika ubao wa matangazo lakini hakuna mtu aliekuwa akishughulika nazo.
"Samahani kwa kuwasubirisha" alifika yule mhudumu akiwa na sinia kubwa iliokuwa na vyakula vya aina mbali mbali.
"Tael ya dhahabu moja" aliongea baada ya kuituwa mezani, Fahad akaingiza mkono mfukoni na kutoa tael hiyo. Akamkabidhi kisha akamuongeza tael nyingine ya shaba kisha akaongea "kama hutojali unaweza kunieleza jambo".
"Mbona ubao wa matangazo umejaa kazi lakini sioni mtu kushughulika?" Aliuliza Fahad.
"Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya wawindaji kuuwawa wanapokuwa kazini. Inasemekana huu ni msimu wa wanyama wakali sana wa kijini wanaotoka katika mapango yao kusini mwa mlima Zingi. Hivyo zoezi la wawindaji limesitishwa mpaka sherehe kuwinda zitakapowasili" alifafanua yule mhudumu.
"Anhaa, Ahsante sana" aliongea Fahad na kutabasamu, yule mhudumu akainamisha kichwa na kuondoka.
"Master wewe hutaki kula" aliongea Rahee akiwa nusu sahani, "kama ungetaka nile ungenikaribisha mwanzo kabla hujaanza kula. Hata hivyo chakula hakitutoshi watu wawili, mimi ili nihisi nimekula nikashiba basi angalau nile nusu nyati" aliongea Fahad.
"Nani mwengine zaidi ya Master wangu mwenye uwezo kama huwo" alisifia akiendelea kula. Jambo moja ambalo Rahee alikuwa vizuri ukiachia martial arts basi ilikuwa ni kula. Kwao alitambulika kama mfalme wa chakula asiepingika.
Wakati wakiwa hapo, Fang Shi akafika. "Samahani kwa kukuweka sana" aliongea.
"Usijali, kwanza huyo jamaa hata hajamaliza kula" alijibu Fahad. Rahee hakuongea jambo aliendelea kufakamia kama sinia ikawa nyeupe. "Mffffuuu!" Akaegemea kitu huku akipigapiga tumbo lake lililoonekana kujaa.
***********
"Huu ndio mlango wa kuingilia katika eneo la nyumba hii lakini hakuna hata mmoja alieweza kuufungua" aliongea akiwa amesimama mbele ya mlango mkubwa wa chuma. Fahad akauangalia mlango huwo kwa makini na kushusha pumzi.
"Umesema hakuna alieweza kuufungua huu mlango" aliuliza.
"Ndio, tumejaribu sana lakini imeshindikana kabisa"
"Lakini mbona naona kabisa kama hauna shida huu mlango" aliongea na kuusukuma kidogo tu. Mlango ukatikisika na kutoa vumbi kabla ya kufunguka. Macho yakamtoka Fang Shi. Mlango ambao umewashinda watu wengi, Fahad ameusukuma kama si kitu vile.
"Umewezaje kuufungua kirahisi hivi" ikabidi aulize maana alihisi shauku lingemtia roho.
"Ah, huu mlango ili ufunguke ulikuwa unahitaji mtu asafirishe Neigong kutoka mwili mwake na kuingiza katika chuma hichi" aliongea mvukr wenye rangu ya ajabu ukatika mwilini mwake na kuingia kwenye chuma.
"Neigong ndio nini" aliuliza kwa sintofahamu.
"Neigong ni nguvu ya akili, wengie wenu hamujifunzi kuitumia kwasababu ya mumewekeza sana katika matumizi ya Qi" alijibu na kuendelea "ukitaka kujuwa zaidi kuhusu neigong na nguvu nyingine za asili zinazopatikana katika mwili wa binadamu inabidi uandae siku maalum nikueleze".
"Nitafanya hivyo, kwa leo mi naomba niishie hapa nikuache upumzike".
"Tutakuwa katika mafunzo kwa miezi mitatu, nitakutafuta nikitoka" aliongea Fahad na kuagana na Fang Shi kabla ya kuufunga mlango huwo mkubwa.
"Master na mimi nataka nijifunze Neigonga kama wewe" aliongea Rahee.
"Wewe hutaweza kujifunza, leo tupumzike. Kesho nitakueleza kwanini huwezi kujifunza neigong" aliongea Fahad na kumuangalia Rahee machoni. Aliiona kabisa huzuni katika macho yake lakini hakukuwa na njia nyingine.
Waliikagua nyumba hiyo nzima na mazingira yote yanayozunguka eneo hilo. Walipojiridhusha kila mmoja akachagua chumba cha kulala na kupumzika.
Fahad akiwa chumbani, "inaonekana watu wengi huku wanajifunzia kutumia Qi peke yake. Hii inaeleza kwanini misingi yao ni mibovu sana" alikuwa akijisemea mwenyewe.
Akasimama katikati ya chumba na kufunga macho, "hatua ya kwanza, Neigong katika akili" aliongea kufunga macho. Mvuke wenye rangi ya maruni ukaanza kutoka mwilini mwake. Macho yake yakabadilika na kuwa mekundu, kila kitu katika chumba kilikuwa kama kimeganda. Akili yake ilikuwa inafanya kazi mara kumi zaidi ya akili ya binadamu wa kawaida.
Hadi wadudu warukao alikuwa akiwaona wakiruka taratibu kabisa. Akatoa sindano kadhaa na kuzirusha kwa kasi, kila moja ilivyochoma ukutani ilikuwa na imedunga mdudu. Akashusha pumzi na kuangalia dirishani, mwezi ulishafika katikati.
"Usiku umekwenda sana" alijisemea na kupanda kitandani. Badala ya kulala akakaa kitako na kukunja miguu, akalala kwa mfumo huwo.