. . Majira ya saa moja usiku, Asia na Lucas walikuwa katika mazungumzo mazito. Mazungumzo juu ya namna ambavyo watakuwa wakifundishana. Wakafikia makubaliano, Asia akabadili mada. Mara aseme hiki mara kile.
Hatimaye akaamua kuirusha karata yake.
Akayakumbuka maneno ya yule bwana aliyempatia ile dawa.
. . “Huko Bukoba wanayo SHUNTAMA….huku sisi tunaiita hii Daiko…..akichomoka hapo basi mwanaume.”
. . Asia akachomoa pipi akabugia moja kisha akawahi kuomba samahani kwa kula peke yake.
Akatoa nyingine akampatia.
Maongezi kadha wa kadha yakaendelea kisha wakaagana.
. . Asia akayangoja majibu. Na hakika usiku huo haukupita, mara ukaingia ujumbe Lucas alihitaji kumpigia simu.
. . Asia akakubaliana naye.
Lucas alivyopiga simu akakosa la kuzungumza badala yake akawa anabwabwaja kama tahira.
Asia akawa anamuunga mkono.
. . Hatimaye wakakubaliana kesho waonane mida ya usiku.
Hicho kitu Asia alikuwa anakisubiria ili amalize mchezo.
Akili ya Lucas na usomi wake alikuwa amekamatwa kimadawa, hakuwa akijielewa.
Lakini ni bora hali ile ingeishia pale lakini akafanya kosa kujiruhusu kuonana na Asia faragha.
. . Ulikuwa usiku wa namna yake.
. . Asia akakolezea mapenzi. Akazidi kujikita katika mapenzi ya kijanja janja, nia yake ikiwa kumkamata vyema Lucas.
. . Ile hali ya kuelezwa kuwa Lucas si mcha Mungu sana ilimpa nafasi Asia ya kuamini kuwa hata kinga yake kijana huyu itakuwa ndogo na hakika ilikuwa hivi.
Iwapo unaifahamu shuntama na madhara yake basi Daiko huwa ni mara mbili yake.
. . KWA WASIOJUA: Shuntama, hii dawa maarufu kabisa mkoani Kagera, ukifanyiwa hii na mwanamke utarukaruka wee huko unapojua lakini kila atakalosema utamsikiliza. Unakuwa kama umeshikiwa akili vile, na iwapo akikutishia kukuacha unaweza kufa kwa presha.
. . Usiku huu Asia alivyoipata nafasi ya kukutana kimwili na Lucas asiyejielewa, akamwongezea pigo jingine.
. . Sasa hii ilikuwa ni aina ya ‘GENDA UGERUKE’…hii nayo ni ya aina yake, ukimpenda mtu ambaye yupo Mwanza, akikufanyia hii, hauutamani mji mwingine zaidi ya Mwanza. Yaani kila mara unatamani kuwa katika mji ambao mpenzi yupo. Hii hutumiwa sana na wale wapenzi wenye wasiwasi wa kuwa mbali na wapenzi wao.
. . Asia akajipakaa vyema kabla ya kumkabili Lucas.
Lucas alikuwa amekolea kumbe mwenzake ni king’amuzi anang’amua chaneli mpya mpya za burudani na michezo.
****
SEHEMU YA PILI
. . Baada ya siku nne Asia alikuwa na wale wanawake waliompa dili hilo la kumkamata yule mwanaume hadi amsahau mkewe na familia kwa ujumla.
. . “Tutaaminije kama kweli umefanikiwa?” mwanamke alimuuliza.
. . “Mnataka nimfanyie nini kwa sasa.” Aliuliza Asia, kwa mujibu wa saa zao ilikuwa saa tatu usiku.
. . “Mwambie aje sasa hivi.” Mmoja wao alijibu.
. . Asia bila kusema neno alichukua simu yake, akabofya jina la Lucas. Akaweka sauti ya juu simu ikaanza kuita wote wakisikia.
Ikapokelewa.
. . “Samahani mpenzi wangu kwa kuchelewa kupokea simu.” Alianza kujitetea Lucas.
. . “Nataka kukuona Luka.” Aliamrisha Asia kwa nyodo.
. . “Lakini….”
. . “Luka unakuja hauji?”
. . “Upo wapi sasa hivi..nakuja.”
. . “Sinza kwa Remmy.” Alijibu Asia kisha akakata simu.
Wale wanawake walitazamana, kisha wakajikuta wakiwa midomo wazi bila kujua kama wapo katika hali ile.
Kazi imefanyika namna ile kwa nini wasifanye malipo?
. . “Sasa tunataka kumuumiza yule mkewe.”
. . “Msijali nawapa mwezi mmoja wanaachana naye.”
. . Malipo yakafanyika.
Baada ya mwezi mmoja wakakutana kupongezana juu ya kutalikiana kwa Lukas na mkewe wa ndoa.
. . . . . . ASIA AUNDA FUMANIZI.
. . Kitendo cha kumkamata akili Lucas na kumpelekesha anavyotaka kilimfanya ajijengee heshima kwa waliomfahamu. Asia akaonekana ni kiboko ya viboko.
Wanawake na mikasa yao ya kimapenzi hawakuisha kumfikiria iwapo anaweza kuwasaidia.
. . Fundi mitambo wa kikundi chao ambaye alikuwa na cheo cha waziri wa mipango, Husna Messi alikuwa anazurura huku na kule kujaribu kusaka dili lolote linaloweza kuwapatia pesa.
Husna alikuwa mzungumzaji sana na pia alikuwa msikilizaji mzuri sana.
. . Neno linalomtoka mtu kwake lilikuwa biashara.
Alichokuwa anafanya Husna ni kutembelea saluni za kike kadha wa kadha, ni huku alipoweza kupata siri kadhaa.
. . Wanawake wasiokuwa na staha waliyataja mapungufu ya wapenzi wao huku wengine wakitumia nafasi hizo hata kusema siri zao za ndani.
Husna akapata jipya huku.
. . Alipomaliza kusukwa nywele zake akateta kidogo na yule mwanamke.
. . Alimweleza kuwa dawa ya kilio chake ipo na huyo mtoaji dawa hakuna kinachoshindikana kwake.
. . “Wewe shida yako ni kumkomoa tu…”
. . “Ndio hiyo tu kumkomoa maana yaani sijui hata nisemeje. Yaani mimi ni wa kuchezewa na kuachwa kijinga jinga vile. Amenikuta nina mpenzi wangu, nimemuacha nikijua kuwa jamaa atanioa kumbe laghai. Tapeli mkubwa…Malaya mzoefu.” Mwanamama alijieleza kwa uchungu, uchungu mkubwa.
. . Husna akainusa harufu ya pombe. Bila shaka mama yule alikuwa anajihusisha katika ulevi ilimradi tu kuondoa ama kupunguza msongo wa mawazo ambao ulikuwa unamkabili.
. . Husna akafurahia kimoyomoyo alipogundua kuwa yule mama alikuwa anamiliki usafiri wake mwenyewe. Bila shaka alikuwa na pesa ya kutosha.
. . Biashara njema kabisa.
. . Mwisho wa maongezi wakabadilishana namba za simu.
. . “Yaani mimi muda wowote nipigie usijali…nahitaji sana kumwonyesha mimi ni nani huyo mjinga….” Alisema kwa hasira yule mama ambaye kwa makadirio alikuwa na miaka isiyopungua arobaini.
. . Husna alifika nyumbani kwa Asia baada ya kuwa amempigia simu na kupewa maelekezo kuwa mwanadada alikuwa yu nyumbani.
. . Asia alikuwa amejikita katika kutazama filamu za kiingereza hasahasa za mapenzi. Huku alijifunza mengi sana yaliyomuwezesha kufanya utapeli wake ipasavyo.
. . Asia alisimamisha ile filamu baada ya Husna kuingia.
. . “Shoga hadi sa’hivi umejikalisha tu nyumbani.”
. . “Niende wapi sasa wakati hujanipa dili mtaalamu wangu…si unajua tena madili hayajileti mpaka yasetiwe.” Alijibu kichovuchovu Asia huku akijinyoosha.
. . Mapaja yake yalikuwa nje na wala hakujishughulisha katika kuyasitiri.
. . “Nd’o nimekuja mwenzangu….mguu wangu kama ilivyo kawaida ni mguu wa pesa…sema siwezi kuzichukua bila akili yako mpenzi.” . . . . Husna akazungumza haya huku akijiweka sawa katika kochi.
Asia akafanya mfano wa tabasamu hafifu. Tabasamu la ujivuni.
Alifurahia namna ambavyo alikuwa anakubalika kwa wenzake.
. . Husna Messi hakutaka kupoteza muda, akaanza kupepeta mdomo wake juu ya mwanamama anayetaka kumkomesha mwanaume ambaye alimtenda.
. . Asia akasikiliza kwa makini kabisa. Ni kama alikuwa ana shahada ya jambo alilokuwa anashrikishwa. Akalitafakari kwa kina kisha akanyanyua kinywa chake.
. . “Ana bei gani? Maana mambo ya kugandana kama alivyoniganda huyo Lucas sitaki sahivi.” Alilalama Asia.
. . Husna akamtazama kisha bila kusema neno akachukua simu yake akabofya kisha akaipeleka sikioni.
. . “Mambo shosti za mida….nipigie.” alizungumza upesi upesi akakata simu. Husna alikuwa na tabia ya ubahili.
Baada ya dakika moja, simu ikaita.
. . “Huyu hapa…” akajisemea Husna. Kisha akapokea simu.
Sasa hakuwa akizungumza harakaharaka tena.
. . “Nipo naye hapa yule mtaalamu….ongea naye basi nimemweleza nia yako.” Alibwabwaja Husna kisha akampatia simu Asia.
Baada ya salamu na kufahamiana majina, ikazungumzwa bei.
. . “Jamani dada nifanyie kitu kimoja basi chukua milioni moja na nusu halafu hiyo laki tano nitakumalizia baada ya kumkomoa…..” alibembeleza yule mama akiwa amewekwa katika ‘loud speaker’.
. . Asia akafanya tabasamu kisha akamkubalia mteja wake.
Wakapanga siku na mahali pa kukutana ili waweze kupeana maelekezo kadha wa kadha.
. . Husna akamwachia rasmi jemedari Asia kazi.
Yeye akabaki kusubiri majibu.
Husna alikiri kuwa Asia alikuwa mwanadada wa maajabu sana.
. . . . . . . . . . ****
. . GARI aina ya Toyota Rav4 liliegeshwa katika ukumbi maarufu wa burudani, ukumbi mkongwe kabisa unaoenda kwa jina la Lango la jiji.
Ukumbi uliopo maeneo ya Magomeni mikumi.
. . Baada ya kuegeshwa gari ile ilidumu kwa muda mrefu bila mmiliki kutelemka chini. Hakuna aliyejali, kila mmoja alikuwa na mambo yake.
. . Waliokuwa na kampani walijikita katika kampani hizo na waliokuwa peke yao peke yao walibaki na upweke wao huo ambao aidha uliwapendeza ama kuwapoozesha.
Baada ya nusu saa gari nyingine iliingia. Nayo ikaegeshwa kwa fujo.
Baada ya gari hii kufika kelele za hapa na pale zilizuka, huenda mwenye gari hilo alikuwa anafahamika.
Kitendo cha gari hili kuwasili kilienda sambamba na milango ya Toyota Rav4 kufunguliwa.
. . Marashi ya aina yake yalitawala baada ya mlango ule kufunguliwa, kisha ndani ya lile gari akatelemka mwanadada, alikuwa amevaa nguo nyekundu na alipendeza kumtazama masikioni kwa jinsi hereni zake zilivyorandana na gauni lake.
Gauni lake lilikuwa katika mfumo wa kichokozi, lilikuwa fupi na liliacha mapaja yake kwa kiasi kikubwa yakitalii kwa nje.
Kwa jinsi alivyopendeza aliamini kuwa kila jicho lilikuwa likimtazama japo kwa wizi wizi na alijua ni kiasi gani alikuwa akiwaumiza wasichana wengine roho, huku wale ambao waume zao walikuwa dhaifu wakianza kuingia wasiwasi.
. . Mwanadada huyu hakuwa na shida ya kianalojia ya kumfikia kila mtu ilimradi anayo luninga na kiantena, shida yake ilikuwa kidigitali na alitaka kama ingewezekana jicho la mwanaume mmoja tu nd’o limuone.
. . Na alijua kuwa lazima atatizamwa.
. . Mwanadada akaifunga vyema milango ya gari lake.
. . Kisha akageuka. Hatua kwa hatua hadi akaufikia mlango wa kuingilia.
. . Walinzi wakampisha, siku hiyo ilikuwa ni ladies free.
. . Akaingia kwa pozi na viatu vyake vya mchuchumio lakini ambavyo havikumsumbua katika kutembea.
. . Akatazama huku na kule akajichukulia nafasi.
. . Akaanza kunywa vinywaji vya bei ghali sana, vinywaji ambavyo viliwababaisha wanaume wengi na kuhofia kuweza walau kumkaribia.
. . Jicho lake lililofichwa nyuma ya miwani lilikuwa makini sana kumhesabia muhusika wake muda wa kumshambulia.
. . Bahati nzuri muhusika mwenyewe tamaa alizionyesha mapema sana.
. . Kama alivyotegemea yule mwanadada. Mara akiwa ameketi akijikita katika kutumia simu aina ya iPhone5 ambayo waliichota katika tukio la kumhamishia Deniss digitali, mara akakaribiwa na mwanaume ambaye kwa sifa moja unaweza kumweka katika kundi la watanashati.
. . Bila kusema lolote akamwekea mbele yake chupa ya kinywaji alichokuwa anatumia.
. . “For what?” mwanadada akauliza.
Yule mwanaume akajiumauma kujieleza lakini mwanadada hakukubali ofa ile.
Jaribio la muhusika wake likawa limeshindikana.
. . Majira ya saa sita usiku, taarabu ikanoga.
. . Taarabu nd’o asili ya lango la jiji, kila ambaye hutembelea pale hufuata taarabu.
Asia akasimama, mkoba wake kwapani, akajiunga katika kucheza taarabu ile iliyokuwa imenoga.
. . Alicheza kwa uwezo huku akiruhusu mara kwa mara kiuno chake kucheza faulo na kuonesha mali kadha wa kadha katika kiuno chake.
Jwa kila ambaye angemtazama angekiri kuwa mwanadada yule alifuata taarabu pekee katika ukumbi huo.
. . Yule mwanaume ambaye alikuwa amemtamani Asia tangu alipomuona wakiwa nje alitumia nafasi hii kujipenyeza na kujikuta akituliza mikono yake katika kiuno cha yule dada.
Mwanadada akakatika vyema sana, kijana naye akazidi kukamatilia.
Asia alitambua nini kinaendelea lakini akajifanya hajui lolote.
. . Wakati wakicheza muziki huo wa mwambao yule bwana akajitambulisha.
. . “Naitwa Branco……”
. . “Mimi Fatuma…” alidanganya Asia kama kawaida yake.
Branco lilikuwa jina lake halisi. Kijana ambaye alimtesa mwanamke ambaye sasa alikuwa amemlipa Asia kwa shughuli moja tu…kumkomesha Branco ikiwezekana kumfanya aukimbie mji.
. . Asia alikuwa amejipanga vyema, sasa alikuwa katika utendaji.
Hatua ya kwanza ilikuwa kumtambua vyema Branco, mwanzoni alipewa picha yake na kisha kuelezwa kuwa kijana huyo huwa hakosekani katika taarabu, ni tabia yake kuhudhuria sehemu hizo ili akwapue watoto wa kike wanaojua nini maana ya kitanda.
. . Branco aliamini kuwa wacheza mduara mara nyingi ni watundu kitandani.
Sasa Asia yupo na Branco walikuwa wakianza kufahamiana.
Baada ya muda Asia akarejea katika kiti chake na Branco akiendelea na mambo yake.
Asia wa kidigitali alikuwa anaungojea ule muda ambao alikuwa ameuseti kidigitali. Muda ambao ungeamua hatma ya Branco na tabia zake za kubadili wanawake hovyo.
. . Msema chochote (MC) alisimama mbele ya jukwaa baada ya mziki kusitishwa kwa muda.
Kila mmoja alikuwa na hamu ya kusikia washindi wa siku hiyo ni nani na nani.
Mashindano ya binti na bwana waliotoka vyema kimavazi..kisha washindi wa kuucheza mduara.
Asia alikuwa anatabasamu peke yake alipokuwa anawatazama wadau wengine wakifanya ubashiri wa nani kuibuka kimwana wa usiku huo.
. . Asia alikuwa na haja ya kutabasamu, kwani kabla ya mkesha huo wa taarabu, tayari alikuwa amepitia mlango wa nyuma na alikuwa ametoa rushwa kwa MC…hivyo kwa namna yoyote ile ni jina lake lingependekezwa kuwa kimwana wa taarabu aliyependeza usiku huo.
Asia hakuwa mpumbavu ajiweke yeye peke yake, alilipia pia jina la mwanaume ambaye anataka atajwe usiku huo.
. . Pesa ikazungumza.
. . Wakati ulipowadia MC akawaamsha vitini.
. . “Huyu mwanadada ni mgeni…sijamjua jina lakini nimetuma vyombo vyangu vya usalama vimemtambua jina……FATUMAAAAAA…..” akapayuka MC, Asia akazuga kushtuka, akasimama kama asiyeamini kabisa alichokisikia.
. . Hakika alikuwa muigizaji mzuri.
Akajikongoja kuelekea mbele. Mate yakawajaa midomoni wanaume wenye tamaa……lakini binti huyu alionekana kuwa matawi mengine kabisa.
Wakati shangwe zikizagaa wakati Asia akipiga hatua kwa madaha kuelekea jukwaani, msema chochote akamtaja mwanaume matata wa siku hiyo.
Hapa napo Asia alipangoja kwa hamu maana alikuwa amepapika na ilikuwa lazima papikike.
. . “Papaaaaa Brancooooooo” akatajwa Branco. Kijana huyu machachari akaruka juu, hakutegemea kabisa iwapo ataitwa.
Mbio mbio akakimbia mbele na kumkumbatia Asia.
. . Hili nalo Asia alilitegemea.
. . Baada ya kukutana katika jukwaa lile wakiwa wawili huu ukawa mwanzo wa kufahamiana vizuri.
Papaa Branco akatumia ukaribu ule kumchombeza Asia.
. . Mwisho wa siku majira ya saa tisa usiku, Asia akiwa na gari yake na Branco katika gari yake walikuwa wanaelekea nyumbani kwa Branco.
Majira ya saa kumi walikuwa katika chumba cha Branco. Asia akakiri kuwa yule mama aliyempa biashara hiyo alikuwa amesema ukweli tupu.
. . “Branco ana tabia ya kuingiza hovyo wanawake chumbani kwake.”
Hakika ilikuwa hivi, Asia naye alikuwa ameingia katika chumba cha Branco.
Papara za hapa na pale kitandani, tayari walikuwa wapenzi kufikia dakika hiyo.
Branco alimgalagaza Asia huku na kule, Asia alitamani kucheka lakini akasita. Branco alikuwa ni mlafi sana, na pia mwenye haraka kupitiliza.
Mara alambe huku mara ashike kule.
Hisia za Asia zilikuwa zimesafiri mbali kabisa na hakujiruhusu kudanganyika.
Baadaye ikafuata zamu ya Asia kumfanya Branco mtumwa.
Lakini Asia hakuwa mlafi na mwenye papara.
. . “Kaoge bwana….” Alimsihi Branco.
Branco akamtaka waende wote Asia akakataa akidai kuwa anahitaji faragha ya kike, kujisafisha. Baranco akamwachia Asia chumba.
Hili lilikuwa kosa la jinai alilofanya Branco.
Asia alipoachiwa chumba, akiwa amebakiwa na chupi pekee mwilini aliparamia mkoba wake akatoka na kimfuko kidogo.
. . Bila kutetemeka akafunua kitanda cha Branco na kuweka kisha akarejesha godoro katika hali ya kawaida.
. . Branco alivyorejea Asia naye akaingia kuoga.
. . Akiwa bafuni akamuita Branco ambaye alikuwa amelegea macho kutokana na hamu kubwa ya kufanya ngono.
Mbio mbio Branco akamfuata bafuni akiwa bado yu uchi.
. . “Nisugue mgongo baby…” Asia alilalamika.
Branco akachukua cha kusugulia.
. . “Noo honey kitaniumiza hicho…mi nataka unisugue kwa mikono.” Asia alifanya kudeka. Branco akaanza kumpapasa.
. . Asia wa digitali akaanza kuhema juu juu. Branco akazidi kupapasa, sasa vidole vyake vikahama kutoka mgongoni vikaingia kunako katikati ya mapaja ya Asia. Hapa Asia akapiga yowe kuu la hamu.
. . Kisha akajiweka katika pozi ambalo Branco akiwa kama mzoefu wa mambo hayo alijua ni kipi anamaanisha.
. . Wakaanza kuvurugana kuanzia bafuni, mchezo wao ukaja kuishia sakafuni.
Wakasinzia waliposhtuka tena walimalizia sebuleni.
. . Asia akajifanya kuwa amechoka sana. Lakini haikuwa hivyo.
Aliondoka akiwa na tabasamu usoni, Branco alidhani kuwa Asia anatabasamu kwa kuwa ameahidiwa ahadi hewa ya kuolewa.
. . Branco akajiona kuwa mjanja kuliko Asia.
Katika orodha yake akamuhesabia kuwa msichana wa arobaini na tano tangu ajitambue kuwa yeye ni mwanaume.
. . Laiti kama Branco angejua ni kwanini Asia anatabasamu kamwe asingemdhihaki na kumweka katika orodha ya wasichana wake.
Huenda alikuwa sawa kumweka katika orodha ya wanawake aliowapitia kama kawaida lakini tatizo lilikuwa moja tu.
Asia hakuwa katika mfumo wa analojia kama wanawake waliotangulia.
Kumtumia Asia lazima ulipie.
. . FARIDA alikuwa katika sebule yake kubwa, alikuwa akicheza cheza na mtoto wake wa mwisho.
Lakini hakuwa na furaha hata kidogo. Hali hii ilitokana na kujishtukia kuwa ameingizwa mjini kwa namna ya kipekee huku akiulaumu ujinga wake na visasi vya kipuuzi.
Farida aliamini kuwa Asia hakuwa na harakati zozote za kuweza kumkomoa Branco, mwanaume ambaye alimdhulumu furaha yake kwa kumtenda kimapenzi.
. . Farida alijutia pesa ambayo aliitoa na kumpatia Asia baada ya kuaminishwa na Husna kuwa pale ni mwisho wa matatizo.
Farida alijisonya mara kwa mara huku akibanwa na hasira. Wazo la kuwa Asia amekolea kwa Branco lilimuumiza kichwa sana, akajiona mpumbavu namba moja ambaye hajawahi kutokea duniani.
. . Pesa nimempa na bwana nimempa……aliwaza Farida.
Akainama kwa uchungu mkubwa, chozi likadondoka.
Kikataka kufuata kilio cha kwikwi lakini mlio wa ukasikika ukamkatisha.
. . Simu yake iliita, akaitazama…..hasira zikamzidi baada ya kugundua kuwa mpigaji ni Asia.
Aliamini kuwa zilikuwa ni longolongo tu. Alitamani kumtukana lakini nafsi ikamsihi ajishushe.
. . “Najishusha kwa mara ya mwisho….” Aliapa Farida kisha akapokea simu.
. . “Nipigiee sasa hivi…” Asia alisema kisha akakata simu.
Farida akajikuta anatokwa na tusi zito la nguoni. Yaani ampigie tena….
. . “Huyu Malaya huyu hanijui eeh hata kama tuliandikishana atazitema pesa zangu…yaani milionii…” alisema kwa sauti ya juu akiwa amehamakinika.
Akabofya namba akampigia Asia huku akijaribu kuidhibi hasira yake.
. . “Nambie shoga..” Asia alianza.
. . “Poa tu nipe ripoti..”
. . “Branco ulisema ana pesa nzuri eeh….”
. . “Ndio anazo kwani vipi…tuzungumze yetu aisee..” alisema kwa jazba.
. . “Sikia sasa nishamaliza yangu….lakini nataka kukusaidia jambo moja.”
. . “Jambo gani? Na umemfanyaje hadi unasema umemaliza yako..”
. . “Taarifa utazipata muda si mrefu….ninachotaka kukusaidia ni kurejesha pesa zako na ziada kama inabidi. Ukwapi sahivi….” Aliongea kwa furaha kubwa Asia.
Farida akajieleza mahali alipo. Bahati nzuri Asia alikuwa hayupo mbali sana.
. . “Nakuja muda si mrefu…”
. . Farida alipokata simu ambayo alikuwa amempigia Asia, hapohapo ikaingia simu kutoka kwa rafiki yake mwingine.
Akapokea upesi kumsikiliza. Hata kabla hajasema neno lolote. Mpigaji alianza kuzungumza.
. . “Mwenzangu Mungu ametulipia…..yaani huku mbona kitimtimu…”
. . “Nini mbona sikuelewi…”
. . “Branco shosti…”
. . “Amefanyaje Branco…”
. . “Amenatiana huku mbona kazi ipo huku….”
. . “Amenatiana kivipi?”
. . “Mwenzangu yaani hata mimi sijui…halafu ilivyo aibu yupo na mke wa mtu….ni aibu huku…”
. . Farida alikuwa katika fumbo hakujua nini kinaendelea, alishikwa na mshawasha, akataka kutimua mbio achukue usafiri kwenda kwa Branco lakini akakumbuka alikuwa na ahadi ya kuonana na Asia baada ya muda mfupi.
. . Hakika baada ya dakika kadhaa simu ya Asia iliingia, tayari alikuwa amefika eneo ambalo Farida alikuwa amemueleza.
. . Farida akatoka nje wakaonana.
. . Asia akamsimulia Farida juu ya tego la kisu na ala yake alilomuwekea.
. . Farida hakuelewa chochote. Maneno ya Asia pekee yalikuwa hayajitoshelezi. Wakaongozana kuelekea sehemu ya tukio.
. . Mwanzoni palikuwa na watu wachache lakini baada ya taarifa kusambaa hapakuwa hata na upenyo wa kuweza kuchungulia nini kinaendelea.
Farida alimtazama Asia kwa jicho la wizi wizi. Alishngaa sana aibu hii kuwa kubwa kiasi hicho.
. . Katu hakuwahi kutegemea kuwa ingekuwa namna ile.
. . “Huyu binti ni kiboko…” alikiri katika nafsi yake.
Baada ya muda kila mtu alikuwa macho juu juu kutazama nini kinatolewa katika nyumba ile.
Alikuwa ni Branco akiwa amenatiana na mke wa mtu.
Aibu ya karne. Farida hakuamini kabisa. Lakini kilichoonekana ndo hicho kilikuwa mbele yake.
. . Asia alimsogelea Farida kisha akamnong’oneza “ Nimalizie changu…”
Farida akatabasamu. Alikuwa amemkubali Asia kwa kila namna.
Akamkonyeza kidogo ishara ya kuwa hakuna kitakachoharibika.
. . . . . . . . . . ****
. . Asia alijitia kuwa jasiri sana mbele ya Farida lakini kwa hali halisi alikuwa ameshangazwa sana na utaalamu ule wa TEGO…..hakujua kama kuna imani kali kama zile zinaweza kufanya kazi katika maisha halisi.
Kile kisu ambacho alikiweka chini ya godoro kikiwa katika ala yake kilikuwa kimezua haya.
. . Asia anakumbuka kuwa sharti la kuwanasua wawili hawa ilikuwa ni kukichomoa kisu kutoka katika ala yake.
. . Hapa ghafla wazo la kibiashara likamuingia.
Nani wa kukichomoa kisu?
. . Farida alionekana kuridhika sana na aibu ambayo Branco alikuwa ameipata lakini hakukumbuka kuwa Asia alimweleza kuwa anaweza kujipatia pesa baada ya tego lile.
. . Asia akapiga akili ya upesi upesi. Akagundua kuwa ipo njia ya kumwingizia pesa nyingi zaidi tena bila jasho.
. . Ndege wawili kwa jiwe moja. Asia alijipa kichwa.
. . Akachukua simu akabofya namba fulani.
. . “Kamanda nataka kukuuzia ugomvi…”
. . “Shilingi ngapi msaghane.” Sauti ya mwanadada wa kikurya, Janeth ilijibu.
. . “MIlioni mbili, yako moja na yangu moja…aahh hapana milioni nne, yako mbili na yangu mbili” Asia alimjibu kwa uchangamfu huku akitweta.
. . “Wewe Asia acha zako…wewe…ugomvi gani huo.”
. . “Ugomvi wa amani…sikia tukutane posta nikupange tule pesa.”
. . “Poa.” Janeth alijibu.
. . . . . . . . . . ****
. . Janeth alijiandaa upesi, akaona kuchukua daladala ama taksi ni kupoteza wakati. Akachukua pikipiki.
. . Kona hapa na pale hatimaye wakafika posta.
. . Asia naye alikuwa amefika tayari.
Akamsimulia Janeth juu ya lile janga la kumwekea tego Branco, tego lililonasa baada ya Branco kuingiza mke wa mtu chumbani kwake kisha kutumia kitanda kilichowekewa tego…..
. . Tego likanasa, nao wakanatana.
. . “Wewe jifanye ndo mwenye lile tego, tafuta nafasi ya kusema na Branco kisha mtajie dau akiingia laini unaenda nyumbani kwake, cha kufanya ni kuchomoa kile kisu kutoka katika ala yake.
. . Mwisho wa mchezo.
. . Mwanadada wa kikurya akaingia kazini.
Siku hiyohiyo baada ya hospitali kushindwa kuwasaidia Janeth akafanikiwa kuteta na Branco.
Kwa aibu kubwa Branco akakubaliana na Janeth. Akampa maelekezo rafiki yake. Akamsindikiza nyumbani kwa Branco.
. . Akapewa pesa yake, kisha akafanya kama alivyoelekezwa na Asia.
Amakweli digitali haina mfanowe.
Palepale kisu kilipotoka katika ala, jogoo wa Branco naye akatoka katika mwili wa mke wa mtu.
Maajabu.
. . Milioni nne kibindoni. Biashara ikaishia hapo.
Branco akatoweka mjini na hakujulikana ni wapi alipopotelea hata marafiki zake hawakujua ni wapi amekwenda.
. . Hayo hayakumuhusu Asia digitali maana yeye tayari alishamaliza yake.
. . . . . . . . . . ****
. . . . . . *********ASIA MATATANI.**********
. . HASSAN TEMBO, kijana machachali mzaramo wa asili. Mkazi wa jiji la Dar es salaam wilaya ya Temeke.
. . Jina lake lilikuwa midomoni mwa watu wengi sana, wakubwa kwa wadogo, wazee kwa vijana.
. . Sio utajiri wake wa ghafla tu uliomstaajabisha mshangaaji bali pia umri mdogo na umbo dogo la Hassan.
. . Hakuwa muumini safi wa dini ya kiislamu lakini kila ijumaa hakuwahi kukosa msikitini.
Utajiri wake ulikuja kama utani, kwanza alikuwa mvuvi. Mvuvi mdogo kupita wote.
Maisha yake yalikuwa ya kulala na kuamkia majini.
. . Hakuwa na mahali pa kujihifadhi. Baadaye akapata kazi ya kuwa anauza samaki za bwana mkubwa mwingine. Bwana huyu alimpatia mahali pa kulala.
. . Hassan akaacha rasmi maisha ya kuishi majini, lakini aliendelea kuwa na undugu na maji.
Hassan alikuwa anakutana na wadau wengi sana katika biashara ya kuuza samaki.
. . Kuna mteja ambaye kila siku alikuwa akitembelea bishara ya Hassan Tembo, cha ajabu hakuwa akinunua mkitu zaidi ya kupiga soga na Tembo, kwa jinsi siku zilivyozidi kwenda ndivyo walivyoonekana kuwa marafiki wakaribu zaidi. Hakuna aliyehoji ukaribu wao.
Kuna kipindi alipotea ghafla kwa majuma mawili. Alitoweka bila kumuaga bosi wake, na alikuwa hajakabidhi mahesabu ya siku hiyo. Hali hii ilizua sintofahamu, hakuna aliyekuwa anajua Tembo amepotelea wapi.
. . Bosi akaanza kumsaka bila mafanikio. Siku ambayo Hassan anaonekana tena pale feri yule bosi wa kihindi alipewa taarifa na wapambe wake akafika upesi akiwa na kikosi cha polisi watatu wakamtia Tembo nguvuni.
. . “Hii mwiji ondoka na pesa mingi sana..” muhindi akiwa amebadilika rangi ya uso na kuwa nyekundu alitoa karipio huku akitaka kumpiga Hassan kibao usoni. Polisi wakawahi kuepusha.
. . “Dogo pesa ya jamaa iko wapi?” polisi walimjuuliza Tembo Hassan.
. . “Muulizeni ni shilingi ngapi?” Tembo bila hofu aliwauliza wale askari ambao walikuwa wamemshika shati na suruali yake.
. . Umati wa watu ulikuwa unashuhudia tukio hilo. Wengi wao walikuwa wakimuhurumia Hassan Tembo kutokana na ucheshi wake aliokuwanao pia umri wake mdogo kuingia katika misukosuko hiyo lilikuwa jambo baya sana.
. . Walisikitika lakini nani wa kuweza kutoa walau shilingi yake kumuepusha na mkasa huo?
Hakuwepo…..
. . Muhindi akaanza kuhesabu vidole ili amuangushie mahesabu makubwa Hassan.
. . “Laki mbili na efu shirini..” muhindi akatoa mahesabu yake. Kila mkazi wa pale feri aliguna.
. . Mzigo aliokuwa anapewa Hassan Tembo kuuza haukuwa na thamani walau ya shilingi laki moja.
. . Miguno yao ilikuwa haina maana, polisi walingoja jibu la Hassankama anayo hiyo pesa alipe ama hatua ya kwenda mbele zaidi ichukuliwe.
. . “Amesema laki mbili na nusu?” Hassan alisema kwa sauti tulivu sana. Kila aliyeujua umasikini na maisha magumui anayoyapitia Hassan alishangaa.
. . Polisi walimkamata vyema asiweze kukimbia.
. . “Ngoja nimpe pesa yake.” Hassan aliwaomba askari, nao bila hiana wakalegeza mikono yao.
. . Akapata upenyo wa kuzama mifukoni, akachomoka na kibahasha kidogo.
Akafungua akatoka na pesa za kitanzania mpya zilizofungwa katika mpangilio mzuri.
. . Akahesabu noti moja baada ya nyingine.
Akawakabidhi wake askari, nao wakahesabu.
. . “Ni laki tatu hii..” askari mmoja alidhani Tembo amekosea kuhesabu alimkumbusha. Wakati huu hawakuwa wamemshikiria. Pesa ililainisha mikono yao.
. . “Hiyo hamsini ya kwenu msijali.” Tembo aliwaambia, huku akitoweka.
Muhindi, askari na umati wote ulibaki ukistaajabu.
. . Mbwembwe za Tembo hazikuishia hapo. Akaendelea na kufuru pale feri. Akanunua meza kubwa ya kuuzia samaki, akaajiri watu.
. . Matumizi yake yalikuwa makubwa sana. Kila mtu aliyekuwanaye karibu alimfaidi.
Wapo waliosema kuwa alipata dhahabu kubwa tumboni mwa samaki, wapo waliosema kuwa alikuwa akimuibia sana yule muhindi.
Lakini aliwanyamazisha wote kwa pesa. Tembo atake nini akikose?
Rafiki yake na dereva wake kwa kipindi hicho, Nyamang’asa akampachika jina.
. . “Munyama mkubwa kamba fedha”
. . Jina likamkaa.
. . Akafupishwa na kuwa anaitwa Mnyama.
. . Jina lake la kuzaliwa likasahaulika.
. . Mnyama akawa mnyama kweli.
. . Kuhusu alipata wapi utajiri…alijua mwenyewe.
. . . . . . . . . . *****
. . SIFA kemkem kuhusu tabia njema ya Hassan kujitolea katika msikiti ambao huwa anasali mara kwa mara, zilipenya huku na kule na hatimaye zikamfikia kimwana machachali Husna. . . . . Akapeleleza huku na kule akapata nafasi ya kumuona kijana yule.
. . Huyu naye kama kawaida yake hakuweza kuzifanyia kazi bila uwepo wa Asia mdigitali.
Husna akazifikisha salamu zile kwa shoga yake.
. . Asia akazipokea katika namna ya kipekee. Lilikuwa ni dili jingine ambalo lingeendelea kuwapatia pesa ya kununua mafuta ya kuweka kwenye gari kila siku.
Kama ilivyo kawaida ya Asia, hakumwambia lolote Husna juu ya mipango ambayo ataitumia kumuingiza mkenge kijana yule.
. . Asia akapanga kuingia kazini ijumaa ya juma hilo.
. . Jua lilikuwa kali, kilammoja alifanya jitihada za kupambana na joto la jijini Dar es salaam.
Hekaheka za hapa na pale Kariakoo ziliufanya mji kuonekana mdogo sana.
Kanzu nyeupe na mabaibui meusi yalitapakaa huku na kule ishara ya sala ya ijumaa.
. . Asia naye alikuwemo katika hekaheka za siku hiyo.
. . Muda wa sala ulipowadia kila mtu alikuwa mahala pake akiswali.
. . Asia naye alikuwa mmoja kati ya waliojumuika kuswali katika msikiti ambao hajawahi kuswali hapo kabla.
. . Asia aliswali huku mahesabu yake yakienda sawa kabisa juu ya mipango yake madhubuti kichwani.
. . Muda wa swala ulipomalizika Asia alitoka nje ya msikiti.
. . Akaangaza macho huku na kule.
. . Aliyategea mawindo yake yaweze kunasa.
. . Hatua kwa hatua Asia alijitembeza, kwa kasi huku akipigia mahesabu makali ya tukio ambalo litatokea.
. . Asia alikuwa akimtazama mwanaume mfupi mweusi ambaye huenda alikuwa amependeza kuliko wote ndani ya kanzu yake yenye thamani ya juu.
Asia alimtazama jinsi alivyokuwa amejikita katika kutumia simu yake. Asia akatumia upenyo ule.
. . Akajipitisha mbele yake, bwana yule pasipokumwona Asia akajikuta amemkanyaga. Asia akajilegeza akatua chini.
. . Aliyemgonga alikuwa ni Hassan Tembo, Munyama mukubwa kamba fedha.
Hassan alikuwa anajulikana sana, asingeweza kumkimbia Asia ama kumpuuzia, aliheshimika kutokana na moyo wake wa kujitolea.
. . Tukio la Asia akalitumia kama nafasi nyingine ya kuthibitisha kuwa ana pesa.
Akaamuru apelekwe katika gari lake binti yule.
Wafuasi wakambeba Asia hadi ndani ya gari la Tembo.
. . Akisindikizwa na wanaume wawili Hassan alimchukua Asia hadi katika hospitali ya watu binafsi maeneo ya mnazi mmoja.
Hapa sasa hakuwahitaji wale watu tena, akabaki peke yake.
. . Hassan baada ya kuelezwa kuwa binti yule hakuwa amepata majeraha makubwa sana aliamua kuondoka naye aweze kumrejesha nyumbani.
Wakiwa ndani ya gari Hassan Tembo akakumbuka kuwa siku hiyo hakuwa ametimiza kile ambacho alikuwa akikitumikia.
. . Dini ya shetani.
Hassan alitakiwa kumwongezea wafuasi shetani. Na wafuasi waliokuwa wakihitajika ni wasichana.
. . Hassan alitakiwa kuwa anawaingiza wasichana katika utumwa ambao utawaweka dhambini.
Tayari alikuwa amewavuruga wasichana wapatao sita. Wasichana hawa sita kadri walivyokuwa nao wanaunda cheni kubwa zaidi ndivyo Tembo alivyozidi kutajirika.
Hii iliitwa biashara ya mtandao ambayo Tembo alijiunga ili aweze kujikwamua kutoka katika umasikini.
. . Mitindo yake ya kizaramo, ujanja katika mapenzi ulimuwezesha kuwakamata wasichana wengi sana.
. . Sasa aliona hata Asia alikuwa msichana sahihi sana kwake.
. . “Binti..unaishi wapi kwani?” Tembo alivunja ukimya.
. . “Mbagala rangi tatu..” Asia alidanganya.
. . “Ok..naomba tupite mahali nimesahau kifaa changu halafu nikupeleke nyumbani.” Tembo akaingiza ujanja.
. . Asia hakupinga, kwani hata yeye alikuwa anataka Tembo ajilengeshe aweze kumtapeli kidigitali.
. . Tembo aliendesha gari hadi akaifikia hoteli maarufu na ghali mitaa ya Kinondoni.
Akamuacha Asia garini, upesi upesi Tembo akachukua chumba.
. . Akamwendea Asia garini.
. . Akamsihi wapate chakula kabisa. Asia hakupinga akakubali.
Moyoni kila mmoja alikuwa akifurahia kuwa na mwenzake zaidi na
zaidi.
. . Kila mmoja alikuwa akiwaza la kwake lakini lililofanana na la mwenzake. Asia alikuwa akiwaza namna ambavyo atamuingiza mkenge Hassan Tembo na kisha kujipatia pesa za bwelele, Hassan Tembo naye alikuwa akiwaza na kuwazua namna ambavyo atamtumia Asia kupata pesa nyingi zaidi.
. . Kila mmoja alikuwa kidigitali zaidi. Pagumu hapo…
. . Tembo hakuwa na wasiwasi kuhusu kufanikiwa kwake kwani alikuwa anaamini kuwa yupo ambaye alikuwa akifanya kazi badala yake.
. . Asia alilazimika kutumia akili zaidi.
. . Baada ya kupata chakula Tembo nd’o alizuga kukumbuka kitu ambacho alikuwa amekisahau katika chumba kimojawapo katika hoteli hiyo.
. . “Vipi nikusindikize?” Asia aliingiza ujanja wake. Tembo akafurahia ombi lile.
Asia digitali na Hassan Tembo wakaongozana hadi chumbani.
Kama ilivyokawaida ya Asia akazuga hapa na pale mara ajikalishe vibaya.
Tembo akatabasamu kisha akafanya kitendo cha ghafla ambacho Asia hakukiona lakini taratibu hali ikabadilika.
. . Matiti ya Asia yakaanza kumwasha taratibu, akayakuna kidogo. Mara yakaendelea kumwasha tena.
. . Hali hii ikamshangaza kidogo, muwasho huu ulikuwa wa aina yake. Haukuwa katika namna ya kukera lakini ulikuwa wa kusisimua.
. . Asia anasisimka? Maajabu.
Matiti yakaendelea kuwasha kwa fujo.
. . Asia sasa alikuwa anamuhitaji mkunaji.
. . Nani zaidi ya Tembo?
. . Tembo alielewa ni nini kinaendelea. Alimsikitikia sana Asia kwani alikuwa anaenda kuingizwa katika mtiririko wa aina yake ambao unamaana moja tu. Kumtumikia shetani.
Ni kweli Asia alikuwa amemtumikia shetani kwa kipindi kirefu, lakini hii ya sasa ilikuwa ni utumikiaji wa kilazima.
. . Tembo alikuwa anamuingiza katika ajira mbaya.
Asia akiwa pale kitandani jicho limemlegea hakuelewa ni nini kinaendelea lakini hakika alikuwa anahitaji huduma kutoka kwa Tembo.
Hassan Tembo akajawa na huruma akamvagaa Asia pale kitandani.
. . Kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa Asia alikuwa akifurahia penzi. Hisia zilikuwa juu mno na alionyesha ushirikiano wa hali ya juu.
Wazo la kutumia upenyo ule kumwibia Tembo lilipotea, Asia alikuwa katika dunia nyingine.
. . Laiti kama Asia angekuwa anamtambua Tembo vizuri, asingethubutu kujiingiza katika jaribio la kumdhulumu.
. . Tembo alikuwa mwanaume kama wanaume wengine kwa sababu anavaa suruali kama wengine lakini Tembo hakuwa mwanaume wa kawaida.
Alikuwa anasambaza ajira ya kutoka kuzimu. Ajira ya kumtumikia shetani.
. . Baada ya tendo Asia alikuwa amechangamka sana. Alikuwa amepata faraja ya mwili wake.
Asia akaijiwa na wazo la kuzungumza zaidi na Tembo ikiwezekana wawe wapenzi.
Akapanga kusema haya kwa Tembo baadate wakiachana.
. . Tembo kama alivyoahidi alimwendesha Asia hadi Mbagala akamwacha kituo kikuu. Wakapeana namba na kuagana. Asia akiwa anashangaa Tembo ni mwanaume wa aina gani hadi ameweza kumpagawisha namna ile.
. . Siku iliyofuata kizungumkuti kikaanza.
. . Asia akiwa peke yake chumbani, alianza kupatwa na hisia za maajabu.
Zile hisia za kuwashwa matiti na kupata hamu ya kufanya ngono.
. . Asia alizipuuzia lakini mara zikaendelea kumnyanyasa.Asia alihitaji kukunwa, lakini mkunaji angetoka wapi?
. . Mkusanya uchafu alisikika akiugonga mlamgo wa Asia.Kinyume na siku zote Asia alimkaribisha ndani. Mkusanya uchafu akaingia, Asia akafika hadi sebuleni akiwa na kanga moja.
. . Mkusanya uchafu akashangaa lakini hakuweza kufumba macho.
. . Asia alikuwa katika mateso makubwa.
. . Mkusanya uchafu naye mwanaume anajua mwanamke akiwa katika uhitaji anakuwaje.
. . Mkusanya uchafu akaona hii ilikuwa nafasi ya kipekee ya kutuliza hamu zake. Akamvamia Asia akaitupa kanga mbali naye.
. . Kilichofuata Asia hawezi kukisimulia zilikuwa ni raha za kipekee.
Baada ya tendo Asia akakimbia chumbani kwa aibu kubwa. Mkusanya uchafu akaondoka zake huku akistaajabu nini kimetokea.
. . Hali hii ya utumwa iliendelea tena siku nyingine.
Siku hii mwili wa Asia ukawa mali ya ‘Mr. kucha’…….
. . Hii nayo ikapita. Asia hakuwa kibiashara tena bali alikuwa analiwa bure tena alikuwa akipata faraja ya hali ya juu.
. . Asia yule wa digitali akajikuta amaewingizwa mkenge. Sasa akawa mfuasi wa mapenzi.
Hakujua kama mapenzi hayo alipachikwa na Hassan Tembo ili amsaidie kuongeza idadi ya waumini katika kontena lake la kishetani.
Kila muumini mpya mmoja, pesa ya Tembo ilikuwa inaongezeka.
Asia hadi kufikia wakati huo alikuwa amevuta wateja wapya sita na alikuwa anaendelea kuvuta wengine.
. . Fedheha na aibu zikamtawala na kumpelekesha Asia, akajikuta katika maamuzi mabaya sana.
Maamuzi ya kukataa kurejea alipotoka.
. . Asia alikuwa mfuasi wa mapenzi hapo zamani, alikuwa akipenda amependa kweli lakini baadaye akayageuza mapenzi hayo kuwa biashara. Akapata pesa nzuri. Lakini tangu akutane na Hassan Tembo basi mambo yakabadilika, hazikuwa zikipita siku tatu, Asia alikuwa anahitaji mwanaume wa kukidhi haja zake.
. . Alikuwa anawashwa sana matiti yake, ni mwanaume pekee alihitajika kwa ajili ya kumkuna.
Kila alivyokunwa akajikuta akitoa na utupu wake.
Hii kwake ilikuwa dharau isiyostahimilika.
. . Asia akaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Hawa nao wakamtaka kimapenzi.
Akawapa huduma bila mafanikio.
. . Baadhi ya waganga wakampa maelekezo kuwa kila anapowashwa awe anawatembelea wampe tiba. Huu akaona ni upuuzi.
. . Waganga wa jadi hawakumsaidia chochote.
. . Hospitali napo walisema lugha zao ngumu ambazo Asia hakuzielewa, wakampatia vidonge lakini bado hali ikawa tete. Hamu kwa Asia ikadumu. Na alipoipata haikupoa hadi pale alipopata wa kumpooza. Leo akipoozwa na huyu kesho anapoozwa na yule.
. . Wanaume wakahadithiana na sasa wakawa wanamlia ‘taiming’ akiwashwa wamkune.
Hali hii ikamdhoofisha Asia. Na kumweka katika hali ya kukata tamaa.
Hakuwa mchakarikaji tena. Hakuwa kidigitali tena.
Asia hakungoja ukurasa ujifunge wenyewe akaamua kuufunga kwa nguvu.
. . Ilikuwa siku kama siku nyingine, wanaume kadhaa walikuwa wakiranda randa jirani na nyumba ya Asia wakingoja akumbwe na muwasho.
Walingoja sana kwa siku hiyo lakini hapakujiri chochote. Hali ambayo iliwakera sana, kwani waliufanya mwili ule kama mali yao halali.
. . Wengine waliendelea kuvuta subira hadi usiku lakini cha kustaajabisha Asia hakusikika walau kujishughulisha katika chumba chake.
Ajabu na kweli.
. . Siku nzima bila kutoka kitandani.
. . Wanaume wenye uchu wakaamua kuingia ndani, kutazama kulikoni.
. . Wakatumia tochi zilizo katika simu zao.
. . Wakapekua huku na kule, hawakuona mtu.
Mwisho wakalifikia jiko.
Ni huku walipoukuta mwili wa Asia ukiwa unaning’inia juu.
Ulimi nje.
Asia hakuwa hai tena. Alikuwa ameamua kujiua
. . Alizaliwa kianalojia akaishi kidigitali na hatimaye anakufa kianalojia akiwa na upande wa kanga shingoni kwake, ulimi nje. Miguu ikining’inia.
. . Wale waliokuwa marafiki zake walikana kumjua. Wale walioshiriki naye kuzitumia pesa alizochuma kidigitali wote wakajiweka mbali na mwili ule.
Serikali ikachukua maamuzi baada ya kutangaza na ndugu kukosekana.
Asia akazikwa na serikali.
Huu ukawa mwisho wa simulizi yake ya maisha.
USIKOSE SIMULIZI YA ‘AJIRA KUTOKA KUZIMU’….sio simulizi ya kutisha lakini inamuelezea kiundani Hassan Tembo, kijana ambaye alipewa ajira kutoka kuzimu bila kujielewa, na mwisho akaanza kuisambaza zaidi na zaidi…….ni simulizi mahusuasi kwa vijana….inakanya kuhusu kuwa na tamaa za mali nyingi pasipo kutoa jasho…
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.