Rais wangu Magufuli trilioni 6 hizi hapa

Usisahau kodi ya kichwa. Kila MTU mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 alipie shs 1000 kwa mwezi kama ilivyokuwa Wakati wa ukoloni.

Wore tutakubali maendeleo kwa kasi yatapatikana.
Aaah huu sio uzalendo ni unyonyaji na kutaabishana....infact kijana wa miaka 18 bado hana ajira na ndo kwanza yupo zake form 3 au 4 anaitoa wapi hiyo buku kila mwisho wa mwezi? Usiwafikirie vijana wa dar na sehemu nyingine ambapo miji imekua ambapo hao vijana wa 18 yrs wanaeza kuafford kuipata hiyo buku ila fikiria wale wa vijijini ambao wazazi wao wenyewe wanaeza pitisha miezi miwili buku hawajaitia mkononi....
 
Ngoja niendelee kusoma kwanza ntapata kitu hakika siwezi toka kapa
 
Chamsingi tuboreshe miundombinu ya kutosha kwenye vivutio vyote vya utaliii, Wamarekani wametunyima Pesa sawa, ila hawata acha kuja kushangaa vyura wa kihansi
 
Sera ya kujitegemea lazima uwe na uchumi imara uwe umewekeza vizuri ktk ELIMU,KILIMO,HOSPITAL,VIWANDA,UMEME,JESHI NA MIUNDOMBINU.kama hivi vyote bado tunachechemia,basi bado tunahitaji wahisani wamaendeleo
 
Mawazo uliyotoa sio wewe uchangie kodi Bali unazungumzia wengine kutoa.

Laiti ungekuwa unakaa gongo La mboto ndani ndani ukapata adha ya usafiri ukadunduliza ukanunua kapasso kako halafu aje mtu kama wewe aseme uchangie 10,000 kuwa na gari, ninauhakika usingemwelewa.

Laiti ungesoma kidogo kugundua ni kwanini kodi haitoshi usingembana mwananchi wa kawaida. Awamu ya nne kodi kubwa ilikuwa inaenda kwenye matumizi ya kula na kunywa na sio maendeleo.

Kaulize au kasome mkataba uliyovuja wa kuchimba gesi kule mtwara. Ungetoa machozi. Hela ambazo zinatosha kabisa kuiinua hii nchi kuwa Geneva ya Africa.

Unajua kuna kodi anatozwa mwenye gari kwa sababu ya fire inspection fee elfu 20? Unajua mwenye gari ndiye hununua fire extinguisher na wala sio TRA. Hiyo hela ya zima moto mantiki yake ni nini?
 
Siyo kwamba naunga mkono ya Zanzibar, la hata kidogo ila sipendi kabisa nchi yangu na serikali yangu kuendelea kuishi kwa utegemezi.

Halafu serikali ianzishe kodi itakayojulikana lwa jina "Real Independence" kodi hii ikusanywe toka kwenye magari yote nchi nzima, na itengenezewe risiti yake, mfano kila gari ilipe Tsh.10000 kwa mwaka. Inamaana tukipata magari 1000000 yaani ni zaidi ya trioni 6, sasa hapo bado tutakuwa na haja ya MCC au mchina?

Katika kutafakari usiku na mchana ni nini serikali ifanye ili kuongeza mapato na kufidia na kuiepuka hela ya wanyonyaji kwa mgongo wa misaada. Huu huu ndo ushauri wangu.

Serikali ipitie upya idadi ya nyumba zote nchi nzima katika miji na majiji yote na kukusanya kodi toka kwa wenye nyumba. Nasema hivyo kwasababu wapanga wa vyumba vya kuishi wanalipa pesa nyingi mno ambayo haina makato ya TRA wala ushuru wa aina yeyote na hivyo kuifanya serikali kupata hasara ya matrion ya shilingi kila mwaka.
Mfano: siku hizi kila chumba katila miji mikuu ni Tsh.50,000 kila mwezi na unatakiwa kulipia walau kuanzia miezi 6=300, 000 inamaana kadri mtu anakuwa na vyumba vingi ndivyo atakavyolipia. Sasa mimi binafsi ni mzalendo kwelikweli na ninatamani sana nchi yetu iondokaena unyonyaji unaofanya naviongozi wezi wakishirikiana na wazungu na wachina.

Napekeza hivi, serikali ikusanye 10% toka kwenye nyumba zote ambazo wapangaji wake wanalipia 50,000 kila mwezi. Kwa maana hiyo serikali ifanye sensa ya nyumba zote kwenye miji na majiji, ikipata hata nyumba 1,000,000 tu halafu ukachukua 5000 kwa kila chumba ni pesa myingi kuliko hata hiyo ya mcc. Hebu tufanye hii hesabu

5000x1000000=5000000000 hapo inamaana serikali itapata hicho kiasi kwa kila mwezi. inamaana kwa mwaka serikali itapata kiasi kisichopungua trion 6. yaani huu utakuwa ni mwanzo mzuri kabisa, na wananchi naamini wako tayari kwa hili kuwa Raisi aliyeko madaraka kwakweli kaonyesha ananiya ya kweli kuifanya Tz ijitegemee. Nadhani Wahusika watapata taarifa hii

Naomba kuwasilisha kwenu wakuu kwa mjadala, kama mathematics haijakaa sawa ilekebishwe tu maana hamna namna, ila ni katika kutafuta ufumbuzi wa nini kifanyike ili siku moja nasisi watz tuone fahari na kuheshimika duniani.

Mkuu hesabu vipi????10,000*1,000,000=10,000,000,000 hii ndo zaidi ya trillion sita au...au labda trilioni ina sifuri ngapi kwa uelewa wako???
 
Siku zote changamoto ndizo hukufanya mtu kutafuta mbinu za kujikwamua; sasa ni wakati muafaka kwa Tanganyika kuachana na utegemezi. Aidha kodi ya mapato ni 30%; wenye nyumba wasiwe tofauti, serikali itavuna feza ya kutosha kabisa kufidia mapungufu ya misaada ya nje. Wazo jema.

Sawa kabisa twaweza kuongeza mapato ya shilingi, lakini kumbuka tunahitaji mapato ya fedha za kigeni pia. Je hizi zitaongezwaje kwa kipindi kifupi? Tunaweza kuishia shilingi yetu kuporomoka sana dhidi ya fedha za kigeni. Kuziba pengo la fedha za kigeni ni ngumu ukitilia maanani kuwa malighafi nyingi za viwanda vyetu na mashine zote zinaagizwa kwa fedha za kigeni.
 
mwaka 2013 EATV kipindi cha uswazi kuna jamaa aliwahi kutoa wazo kwa serikari kuwathamini wa machinga(wafanya biashara) wanaweza wakatoa mchango kwa bajeti ya taifa kwa kulipa ushuru wa tsh.500 kwa siku na akakadiria kwa nchi nzima wawe 1000000 hivyo kwa siku serikali itapata 500000000 ambayo kwa mwezi ni 15bilioni na kwa mwaka ni 180bilion.nadhani tujaribu kuangalia na hapa
 
Sawa kabisa twaweza kuongeza mapato ya shilingi, lakini kumbuka tunahitaji mapato ya fedha za kigeni pia. Je hizi zitaongezwaje kwa kipindi kifupi? Tunaweza kuishia shilingi yetu kuporomoka sana dhidi ya fedha za kigeni. Kuziba pengo la fedha za kigeni ni ngumu ukitilia maanani kuwa malighafi nyingi za viwanda vyetu na mashine zote zinaagizwa kwa fedha za kigeni.

Jawabu ni kufufua n kuanzisha viwanda vipya ili kuongeza thamani ya bidhaa zetu na kuzitafutia masoko ya nje; kuimarisha kilimo cha kibiashara; kusimamia raslimali zetu vizuri; madini, gesi, "mafuta" mifugo, misitu;
utalii nk, ili kuinua kipato cha fedha za kigeni, kimsingi raslimali hizi zimekuwa zinawanufaisha wajanja wachache; imagine; Tanza"nite" ni gem kutoka tanganyika tu lakini eti wazalishaji wakuu ni India na Kenya! Utashindwa kushangaa?! Umasikini wetu tumeuzalisha wenyewe kutokana na udhaifu na umimi wa watawala wetu! Yees! Mimi nakubaliana na JPM, tanganyika tuna uwezo wa middle income country ndani ya kipindi cha muongo mmoja kama tutaachana na pepo la umimi, wizi, rushwa na ufisadi.
 
Tungekuwa tunasimamia rasilimali vzuri za madini gesi huu mzigo usingemwangua mwananchi maskini mana kila kitu ghali na nyumba kwa Dar ni expensive hafu mzigo utakuwa kwa mpangaji. Kodi muhimu ila kukurupuka tu na kuacha utegemezi ngumu thou ni muhimu kujitegemea
Wazo lake sio baya ila kwanini tusikabane penye vyanzo rasmi hizi khabari za vyanzo mbadala vitakuja baadae pana nchi kama Ethiopia wana Shirika lao la ndege na wana mifugo mbona wanasonga?kuna pesa nyingi zinaishia mfukoni mwa wajanja.
 
Watu wanafikri trillion 1 ni mchezo! Ona jamaa yetu huyu wa vyumba yeye kafikri vyumba 1,000,000 vitatengeneza trillion 6 kumbe ni billion 60 tu kwa mwaka ambacho ni sawa na tone la maji kwenye bahari! Tukubali tu kwamba mcc imeacha pengo ambalo kuliziba lazima tushikane ubaya!
Hapo sasa!!

Watu hawajui kuwa hizo Trillion 1 tugigawia kila Mtanzania atapata zaidi ya Tshs 20,000 na change inabaki!!
 
Utakuwa na damu mbichi kichwan badala ya ubongo... Mtanzania atazid kurundiiwa kodi mpaka lini... Hivi tunsshindwa kufikiria nje ya boksi hususan kuifanyia marekebisho mikataba ya kinyonyaji ambayo nchi iliingia na mabepar...

Fikra zako ni maji taka yaliyotuama..

Samahan lakin kwa kuingilia uhuru wako wa kutopoka
 
pesa zinazopatikana katika madini ,utalii na mafuta zinafanya kazi gani.Watakaoumia ni wapangaji sio wenye nyumba .
Utakuwa na damu mbichi kichwan badala ya ubongo... Mtanzania atazid kurundiiwa kodi mpaka lini... Hivi tunsshindwa kufikiria nje ya boksi hususan kuifanyia marekebisho mikataba ya kinyonyaji ambayo nchi iliingia na mabepar...

Fikra zako ni maji taka yaliyotuama..

Samahan lakin kwa kuingilia uhuru wako wa kuropoka
 
Obsaver, hayo magari 1,000,000 nchi yako wapi? Ukichukua magari yote ya serikali na binafsi jumla haifiki hiyo 1,000,000! Pili macho yote ya serikali yako kwenye kodi za magari, ziko juu mno kuanzia importation hadi road license ambapo kwa gari dogo tu kama Suzuki Escudo, kodi yake ni 200,000 kwa mwaka!

Hilo la kodi za nyumba ni sawa lkn kumbuka kuwa sio miji yote nchini kodi ya chumba inafika 50,000. Hata hivyo Serikali ina tatizo kubwa upande wa kuvumbua vyanzo vipya vya kodi, ni ajabu sana Serikali inashindwa kukusanya hata kodi za Ardhi! Naamini kama Watanzania wataona maboresho katika huduma za jamii, wengi watakuwa tayari kulipa kodi ipasavyo.

Ikiwa siasa zitawekwa pembeni na kuanza kutoza road license kwenye bodaboda hata 10,000 kwa mwaka TRA haitakosa 1bn lkn kwa sababu za kisiasa, bodaboda ziliondolewa kulipia road license!

Vv
 
nashauri ngoma za vigodoro nazo zitozwe kodi haswa wale watazamaji pia ile kodi ya kichwa irudishwe tena mgambo hapo watapata ajira,baiskeli na baiskeli za vilema nazo zitozwe kodi...tusisahau pia mahotelini na mama ntilie watozwe kodi kwa kila sahani wanayouza,mathalani sahani ya buku itozwe sh 50 hapo tutaongeza mapato mengi saaaaana. Asanteni wazalendo kwa kunielewa
 
Hesabu ulipata ngapi vile hebu usijiaibishe trill 6 unaijua haya mambo mtuachie tuliosoma egm

huyu nae sijui ana nini.. jamaa si kasema kabisa ka kuna mathematics ambayo haiko sawa irekebishwe?
 
Siyo kwamba naunga mkono ya Zanzibar, la hata kidogo ila sipendi kabisa nchi yangu na serikali yangu kuendelea kuishi kwa utegemezi.

Halafu serikali ianzishe kodi itakayojulikana lwa jina "Real Independence" kodi hii ikusanywe toka kwenye magari yote nchi nzima, na itengenezewe risiti yake, mfano kila gari ilipe Tsh.10000 kwa mwaka. Inamaana tukipata magari 1000000 yaani ni zaidi ya trioni 6, sasa hapo bado tutakuwa na haja ya MCC au mchina?

Katika kutafakari usiku na mchana ni nini serikali ifanye ili kuongeza mapato na kufidia na kuiepuka hela ya wanyonyaji kwa mgongo wa misaada. Huu huu ndo ushauri wangu.

Serikali ipitie upya idadi ya nyumba zote nchi nzima katika miji na majiji yote na kukusanya kodi toka kwa wenye nyumba. Nasema hivyo kwasababu wapanga wa vyumba vya kuishi wanalipa pesa nyingi mno ambayo haina makato ya TRA wala ushuru wa aina yeyote na hivyo kuifanya serikali kupata hasara ya matrion ya shilingi kila mwaka.
Mfano: siku hizi kila chumba katila miji mikuu ni Tsh.50,000 kila mwezi na unatakiwa kulipia walau kuanzia miezi 6=300, 000 inamaana kadri mtu anakuwa na vyumba vingi ndivyo atakavyolipia. Sasa mimi binafsi ni mzalendo kwelikweli na ninatamani sana nchi yetu iondokaena unyonyaji unaofanya naviongozi wezi wakishirikiana na wazungu na wachina.

Napekeza hivi, serikali ikusanye 10% toka kwenye nyumba zote ambazo wapangaji wake wanalipia 50,000 kila mwezi. Kwa maana hiyo serikali ifanye sensa ya nyumba zote kwenye miji na majiji, ikipata hata nyumba 1,000,000 tu halafu ukachukua 5000 kwa kila chumba ni pesa myingi kuliko hata hiyo ya mcc. Hebu tufanye hii hesabu

5000x1000000=5000000000 hapo inamaana serikali itapata hicho kiasi kwa kila mwezi. inamaana kwa mwaka serikali itapata kiasi kisichopungua trion 6. yaani huu utakuwa ni mwanzo mzuri kabisa, na wananchi naamini wako tayari kwa hili kuwa Raisi aliyeko madaraka kwakweli kaonyesha ananiya ya kweli kuifanya Tz ijitegemee. Nadhani Wahusika watapata taarifa hii

Naomba kuwasilisha kwenu wakuu kwa mjadala, kama mathematics haijakaa sawa ilekebishwe tu maana hamna namna, ila ni katika kutafuta ufumbuzi wa nini kifanyike ili siku moja nasisi watz tuone fahari na kuheshimika duniani.

Mzee mimi kama wewe, sifurahishwi kabisa na migogoro ya sisi kwa sisi kama Zanzibar na hata kuanza kubaguana kwa lugha za uarabu, uCUF nk. Lakini pia si mhanga kabisa wa utegemezi tulio ujenga na kuwafanya watu wetu kuamini kuwa hatuwezi hadi tusaidiwe. Lakini kila nitembeapo, kila tatizo tulilo nalo niliangaliapo, naliona ni fursa ya wazi kabisa na moja tayari umesha lielezea vizuri tu hata kama umekosea hesabu (sina uhakika, ila kuna mtu kashauri urudi darasana). Mimi kwangu suala ni wazo lililo zuri, ambalo kwa hakika kabla hata ya mgogoro huu, nilisha liona sana na kulifikilia kama njia mwafaka ya kimapato. Sasa naongezea yafuatayo ili uone na kuhakikisha hatuhitaji misaada.

1. Kuna haja kurasimisha (formalize) sekta zote zisizo rasmi (informal) na kuziingiza katima mfumo wa kuchangia kodi hata kama ni kidogo kiasi gani (haba na haba ndio hujaza kibaba, na hizi ni kauli za wahenga wetu hawakuzitunga bure, tuzitumie). Katika kufanya hivyo, nashauri yafuatayo.

a) Ushuru wa magari: Nimeishi Ulaya kwa muda na kila sekta au sekta ndogo (sub sekta) zina mchango. Miji yetu (Dar es Salaam, Arusha, Mwanza nk) yana magari mengi sana na katika hayo yapo yanayo paki nje kwenye public spaces. Kuwepo na kibali kitakachotolewa na Halmashauri za majiji/miji kwakulipia say Tsh 20,000 kwa mwaka. Hii ni kwa ajili ya matumizi ya public space ambapo ukipita kila mahali magari yamejazana. Itatolewa sticker maalum na ambaye ata egesha bila kuwa nayo faini iwe kali sana. Pesa hizi ni za halmashauri husika lakini zitachangia sana kutoa huduma za jamii.

b) Kodi ya msongamano wa magari mijini: Hii inawezekana kabisa na itasaidia sana magari machache ndio yafike mjini na wengine kutumia public buses ambazo karibu zitaanza. Kuna namna mbili, kwanza kuwapo kwa geti la kielectronik kama la daraja la kigamboni, ambapo zitawekwa scan bila kusimamisha magari zinaweza kumulika na kujua kama gari imelipia au la. Mwenye gari anaweza nunua ticket yake kwa simu au kama vocha katika maduka. Hii pia itaongezea mzunguko wa uchumi kama ilivyo kwa M Pesa na vocha hivi sasa. Namna ya pili ni QUARTER SYSTEM, ambapo itakadiliwa magari mangapi yakiingia mjini msongamano utakuwa wa kawaida na hivyo kutumia statistics hizo kuruhusu idadi ya magari yawezayo ingia mjini kati kwa siku ipi na gharama ipi. Hili ni baada ya upembuzi na kujua ni kiasi gani hasa yanatakiwa yachangie na ndio itakuwa gharama halisia ya kuingia mkini. Hili litafanikiwa zaidi kama halmashauri (kwa kuanzia ya Dar es Salaam, ambayo ipo tayari), kutenga maeneo ya kupaki magari kwa usalama mkubwa (Part & Rides).

2. Kuna haja ya kutumia majeshi yetu kuongoza na kusimamia uzalishaji mali. Vijana wetu wengi ambao hawana kazi wanaweza jitolea au hata wale ambao wanakamatwa wanacheza pool asubuhi wawekwe kwenye makambi chini ya usimamizi wa majeshi yetu (JWTZ, JKT, Magereza etc), sio kwa maana ya kifungo, bali Jeshi la Uzalishaji Mali (JEUMA) au Jeshi la Mapinduzi ya Uzalishaji Mali (JEMAUMA). Kabla hawajaanza uzalishaji, wapewe mafunzo kama tuliyo pata JKT (depo) ya miezi hata 3 na kufundishwa stadi (skills) mbali mbali za kazi na uzalishaji kulingana na watakavyo onyesha vipendeleo vyao (interest) na uwezo pia chini ya uangalizi wa discipline ya hali ya juu kabisa na ndio sababu ya kushauri iwe chini ya majeshi. Iwe ni sifa kubwa kwa kijana kupitia hatua hii na heshima stahiki ziwepo kwa muda utakao kubalika. Ulaya wanaita "Community Service" lakinii iwe ni "community service" kwa namna yetu wenyewe. Chini wa uongozi wa majeshi haya, ambayo tayari yana rekodi ya utendaji mzuri (mfano magereza na JKT, huwa naona katika maonyesho ya sabasaba), wazalishe bidhaa za kilimo na viwanda vidogo vidogo zenye ubora wa hali ya juu kabisa, ikiwa ni pamoja na finishing, packing nk. Wataalam wa marketing watajikita pia katika kuhakikisha soko linapatikana ndani na nje ikiwa ni pamoja na kuhimiza watu kutumia bidhaa hizi za ndani na ikibidi hata sheria ya kuhimiza au kuzipa kipa umbele.

Sehemu ya mapato yatakayo kusanywa kwenye kodi za nyumba/magari nk vinaweza kuwa vyanzo vya kwanza mwafaka kabisa ya operation hii na nashauri ipewe jina la OPERATION JITEGEMEE.

Wakati tunafanya haya, sisi kama watanzania lazima tfauti zetu zote za kiitikadi tuzimalize. Kama suala ni katiba, na tafadhali tuipitie na kuirekebisha kwa ukweli na uwazi kabisa, tujenge umoja kama wa zamani kama watanzania na wazungu wabaki wanashangaa na kuona tofauti zetu hazitutenganishi bali kutukomaza. Tanzania ni moja na itaendelea kuwa moja regardless ya tofauti zetu za kiitikadi. Hatuwezi na haingii akilini tukisutana na kuwasifia wazungu.

Yapo mengi tu ambayo ni vema tuyabuni na kuyaweka katika mazingira ya kikwetu zaidi. Kwa leo niishie hapa lakini ni bora tufunguwe forum ambayo wataalam ha hata wasio wataalam wanaweza toa mawazo na yachambuliwe kila mwisho wa siku (PUBLIC THINK TANK-PTT) na hakika tunawezamake.
 
Hata zile nyumba za shirika la nyumba (NHC) wanazojenga walipie kodi.
 
Wazo lake sio baya ila kwanini tusikabane penye vyanzo rasmi hizi khabari za vyanzo mbadala vitakuja baadae pana nchi kama Ethiopia wana Shirika lao la ndege na wana mifugo mbona wanasonga?kuna pesa nyingi zinaishia mfukoni mwa wajanja.
Na huko mifukoni kwa wajanja ndo tatizo lilipo hapo hata ukusanye vipi kutokudhibiti mianya kaz itakuwa bure. Wakianzisha kodi wapangaji watakuwa na mzigo mana dar kuna poor housing hafu kod ni kubwa hapo itakua kuongeza umaskini
 
Mzee mimi kama wewe, sifurahishwi kabisa na migogoro ya sisi kwa sisi kama Zanzibar na hata kuanza kubaguana kwa lugha za uarabu, uCUF nk. Lakini pia si mhanga kabisa wa utegemezi tulio ujenga na kuwafanya watu wetu kuamini kuwa hatuwezi hadi tusaidiwe. Lakini kila nitembeapo, kila tatizo tulilo nalo niliangaliapo, naliona ni fursa ya wazi kabisa na moja tayari umesha lielezea vizuri tu hata kama umekosea hesabu (sina uhakika, ila kuna mtu kashauri urudi darasana). Mimi kwangu suala ni wazo lililo zuri, ambalo kwa hakika kabla hata ya mgogoro huu, nilisha liona sana na kulifikilia kama njia mwafaka ya kimapato. Sasa naongezea yafuatayo ili uone na kuhakikisha hatuhitaji misaada.

.
Labda kuna kitu hamjui kabisa. Tatizo kubwa kabisa la ukusanyaji wa kodi ni matumizi. Vyanzo vya kodi vipo vingi na hivi ulivyoorodhesha mbana vinatozwa? Tatizo liko kwenye wale wanaokusanya. Ni wezi kupindukia. Hii ina-create virtuous circle ya watu kukata tamaa ya kulipa.
 
Back
Top Bottom