ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,812
- 69,495
My Take
Hongera sana Rais Samia Kwa kukuza Kiswahili na kufungua fursa Kwa Watanzania 👇👇
---
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inatarajia kufungua vituo 100 vya kufundisha lugha ya Kiswahili duniani, hivyo amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo kujiingizia kipato kama inavyofanyika katika nchi nyingine.
“Utamaduni una masuala mengi, maana inahusu jinsi tunavyoishi, kwetu sisi hatuwezi kuongelea utamaduni wetu bila kugusia lugha yetu pendwa ya Kiswahili, ndiyo lugha inayotuunganisha na kuwa na utamaduni mmoja. Lugha hii imefungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania.
“Kwa kutambua hili, wizara imenijulisha kwamba mwaka huu wamejipanga kufungua vituo 100 vya kufundisha Kiswahili duniani kote kwa kushirikiana na Watanzania waliko nje. Sasa niwatake Watanzania walioko nje kuchangamkia fursa hiyo,” amesema na kuongeza;
“…pamoja na jitihada hizi, vijana wengine wakiwamo vijana wabunifu kupitia mitandao mbalimbali wana fursa pia ya kueneza na kutangaza lugha ya Kiswahili na kujiingizia kipato… mitandao ile mnaweza mkafanya mambo tele, ukifungua mitandao mingine unawakuta watu wanafundisha Kiingereza mnaweza nanyi mkaingia mkafungua Kiswahili.”
Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Septemba 23, 2024 katika kilele cha tamasha la utamaduni lililofanyika katika Uwanja wa Majimaji Songea, mkoani Ruvuma.