Rais Samia: Serikali Inaendelea na Ujenzi Barabara ya Amani - Muheza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,826
1,301

RAIS SAMIA: SERIKALI INAENDELEA NA UJENZI BARABARA YA AMANI - MUHEZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Amani - Muheza (km 40) kwa kiwango cha lami ambapo Serikali inaendelea kutafuta fedha kuhakikisha barabara hiyo inakamilika.

Rais Samia ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Muheza kwenye uwanja wa CCM - Jitegemee katika mkutano wa hadhara wilayani Muheza, Mkoani Tanga leo Februari 27, 2025 katika hafla ya kugawa mitungi ya gesi (LPG).

"Barabara hii tunaijua ni barabara ya kilometa 40 na tumeweza kujenga kilometa 14 na kilometa nyingine tatu zitajengwa mwaka huu”, amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utaendelea kujengwa kwa awamu mpaka itakapokamilka yote kwa kiwango cha lami.

Aidha, Rais Samia amefafanua kuwa barabara ya Muheza - Pangani bado haijafanyiwa usanifu ila itawekwa kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2025 -2030 kwa ajili ya utekelezaji wake.

Awali, Mbunge wa Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amemshukuru Rais, Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa fedha za kujengwa kwa barabara hiyo.
 

Attachments

  • SERIKALI INAENDELEA KUJENGA BARABARA YA AMANI - MUHEZA.MP4
    4.7 MB
  • WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.03.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.03.jpeg
    105.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.04.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.04.jpeg
    115.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.05.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.05.jpeg
    718.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.05 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.05 (1).jpeg
    409.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.06.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-27 at 15.08.06.jpeg
    765.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom