Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,176
1642076439999.png

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri wasiwe na ugomvi na Manaibu Waziri kwa kuwa kila mmoja ameteuliwa kwa vigezo tofauti. Ametaka kila mtu ajue nafasi yake.

Amesema mara nyingi watu hugombana kwa sababu ya safari na maslahi ambayo mara nyingine huwa ni maslahi ya wananchi.

Rais amesema amewahi kuwa Waziri na hakuwahi kuwa na ugomvi na Naibu wake kwa kuwa alikuwa anajua nafasi yake.
 
Ndio maana siku hizi mtu kupewa uwaziri au unaibu waziri anapewa pongezi toka kila upande, hizi kazi sasa zimeshageuzwa fursa tu kama zilivyo fursa nyingine.

Zile pongezi toka kwa ndugu na marafiki humaanisha wanafurahi kwa jamaa yao "kutoboa", wanajua wamepata upenyo wa kuombea misaada. Wengi wao hujipendekeza mitandaoni kwa malengo maalum, wala sio kuwatumikia watanzania.
 
Wanagombania kugawana vitalu vya uwindaji. Sasa hao ni wenye mishahara mikubwa na posho, halafu Mimi wa laki 5 naambiwa niwe mzalendo
 
VP yeye mbona hampi safari makamu wakati enzi za mwenda yeye alimegewa masafari ya kumwaga?

Alafu utaskia Mimi nilishatembea Manchu kibao saivi natafuta michongo!!! Kumbe posho za safari, tuna mabalozi msiendeende nje!!
 
Ajira ngumu,kila mtu anataka kupiga pesa kwa njia halali au haramu,lazima washikane uchawi
 
VP yeye mbona hampi safari makamu wakati enzi za mwenda yeye alimegewa masafari ya kumwaga?

Alafu utaskia Mimi nilishatembea Manchu kibao saivi natafuta michongo!!! Kumbe posho za safari, tuna mabalozi msiendeende nje!!
VP si yupo Malawi hata sasa hivi
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri wasiwe na ugomvi na Manaibu Waziri kwa kuwa kila mmoja ameteuliwa kwa vigezo ytofauti. Ametaka kila mtu ajue nafasi yake

Amesema mara nyingi watu hugombana kwa sababu ya safari na maslahi ambayo mara nyingine huwa ni maslahi ya wananchi

Rais amesema amewahi kuwa Waziri na hakuwahi kuwa na ugomvi na Naibu wake kwa kuwa alikuwa anajua nafasi yake
Hakuna anayetaka kutumikia wananchi zaidi ya maslahi binafsi
 
Daah nazidi kumkubali Prof Assad, alilizungumzia hili hivi majuzi tuu kwamba anashangaa mawaziri kukimbizana huko field/ mawilayani wakati siyo jukumu Lao... Akamalizia labda kama issue ni per diem...
Unakuta Waziri anaanza Safari Dodoma-Tabora-Katavi-Rukwa-Songwe-Mbeya-Iringa-Morogoro-Pwani-Dar then anarejea Dodoma baada ya wiki 3 za Per diems
 
Back
Top Bottom