mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,628
Magufuli aliweza kufanya vile kwa sababu Wananchi walimwelewa kwa jinsi alivyokuwa akiwashughulikia hata wenzie ndani ya Ccm na ndani ya Serikali !!Nadhani tunahitaji kujadili siasa za nchi yetu kwa uhalisia zaidi kuliko kwa kujipa moyo au kwa wishful thinking
Uhalisia upo hivi, Rais Samia Suluhu ndio Rais ambaye amejaribu kuwa fair zaidi kwa Chadema kuliko Rais yeyote, na sidhani kama atatokea Rais mwingine akawa fair kwao kama Samia.
Chadema kwa miaka zaidi ya 5 walikuwa treated kama 'kikundi cha waasi ama wahalifu, na haki zao nyingi kuporwa na hakuna walichoweza kufanya zaidi ya kukimbia nchi na kuomba msaada kwa wazungu.
Walimtishia sana Rais Magufuli kwa maandamano na migomo, Magufuli akawatilia ngumu mwanzo mpaka mwisho, walipoona huyu mtu hatishiki wakaona waombe kukutana naye, hata hivyo Magufuli akawapuuza na kuwaweka ndani, na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu wote mnajua kilichofanyika.
Chadema pamoja na vitisho vyote hawakuweza kufanya kitu zaidi ya kukimbilia nje ya nchi, Rais Samia alipoingia kitu cha kwanza kufanya ni waliomba wakutane naye, Rais Samia kwa ubinadamu wake akawakubalia kwa sababu ni watanzania wenzetu, waliokimbilia nje akawaruhusu warudi nyumbani na kuwahakikishia usalama.
Pia akawaruhusu kufanya mikutano waliyokuwa wamezuiwa kuifanya kwa miaka mitano, sasa katika CCM, kama vyama vingi duniani, kuna makundi mawili, kuna kundi la hardliners na kundi lingine la moderates
Hili kundi la moderates, ni lile kundi linaloamini kuwa CCM ni chama ambacho kinafaa kukosolewa na vyama vya upinzani, na vyama vya upinzani vinatakiwa kupewa nafasi ya kuikosoa CCM na kupewa nafasi katika uwanja wa kisiasa
Hili kundi la Hardliners ni lile kundi linaloamini CCM ni chama kinachotakiwa kutumia nguvu zozote kukandamiza upinzani, na upinzani hawapaswi kupewa upenyo kabisa wa kuitikisa CCM.
Hili kundi ndio kubwa ndani ya CCM na ndio lililokuwa linashika hatamu katika awamu ya 5
Samia alipokutana na Wapinzani na hata kuwapa nafasi ya kufanya mikutano, alikutana na upinzani mwingi kutoka katika kundi hili, lakini kwa kuwa anaamini wapinzani wana mchango pia katika siasa za nchi hii, alienda against nao na kuwapa upinzani haki nyingi ambazo walikuwa hawana kabla ya Samia kuingia.
Sasa wanachokifanya Chadema, kutumia lugha ambazo ni very provocative kwenye mikutano yao, kususia vikao vyenye kujenga utaifa, nao wanakua ni hardliners, au misimamo mikali, na wanawa prove right au kuwa 'vindicate' lile kundi la hardliners ndani ya CCM ambalo lilikuwa linamtahadharisha Samia kuwa asiwape upenyo wapinzani maana atakuja kujutia.
Sasa kitakachoweza kutokea ni either Samia ataendelea kuwa mvumilivu au atawasikiliza hardliners wa CCM
Akiwasikiliza hardiliners ni kuwa tunarudi kwenye Magufulism 2.0
Je, Chadema wataweza kukabiliana na wahafidhina wa CCM?
Hata sasa akija hardliner mwingine akafanya vile vile mpaka watu wakubwa wakanywea hakik Wananchi watamwelewa sana !!
Je mnataka muanze kutumbuliwa hata mikutanoni ??!!
Naona labda majipu yameshaiva 😅😅😅🙏🙏🙏🔥