Rais Samia kuwa kama Hayati Magufuli, achana na maridhiano na wasiotaka, watakupotezea muda

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,930
19,085
Nadhani tunahitaji kujadili siasa za nchi yetu kwa uhalisia zaidi kuliko kwa kujipa moyo au kwa wishful thinking

Uhalisia upo hivi, Rais Samia Suluhu ndio Rais ambaye amejaribu kuwa fair zaidi kwa Chadema kuliko Rais yeyote, na sidhani kama atatokea Rais mwingine akawa fair kwao kama Samia.

Chadema kwa miaka zaidi ya 5 walikuwa treated kama 'kikundi cha waasi ama wahalifu, na haki zao nyingi kuporwa na hakuna walichoweza kufanya zaidi ya kukimbia nchi na kuomba msaada kwa wazungu.

Walimtishia sana Rais Magufuli kwa maandamano na migomo, Magufuli akawatilia ngumu mwanzo mpaka mwisho, walipoona huyu mtu hatishiki wakaona waombe kukutana naye, hata hivyo Magufuli akawapuuza na kuwaweka ndani, na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu wote mnajua kilichofanyika.

Chadema pamoja na vitisho vyote hawakuweza kufanya kitu zaidi ya kukimbilia nje ya nchi, Rais Samia alipoingia kitu cha kwanza kufanya ni waliomba wakutane naye, Rais Samia kwa ubinadamu wake akawakubalia kwa sababu ni watanzania wenzetu, waliokimbilia nje akawaruhusu warudi nyumbani na kuwahakikishia usalama.

Pia akawaruhusu kufanya mikutano waliyokuwa wamezuiwa kuifanya kwa miaka mitano, sasa katika CCM, kama vyama vingi duniani, kuna makundi mawili, kuna kundi la hardliners na kundi lingine la moderates

Hili kundi la moderates, ni lile kundi linaloamini kuwa CCM ni chama ambacho kinafaa kukosolewa na vyama vya upinzani, na vyama vya upinzani vinatakiwa kupewa nafasi ya kuikosoa CCM na kupewa nafasi katika uwanja wa kisiasa

Hili kundi la Hardliners ni lile kundi linaloamini CCM ni chama kinachotakiwa kutumia nguvu zozote kukandamiza upinzani, na upinzani hawapaswi kupewa upenyo kabisa wa kuitikisa CCM.

Hili kundi ndio kubwa ndani ya CCM na ndio lililokuwa linashika hatamu katika awamu ya 5

Samia alipokutana na Wapinzani na hata kuwapa nafasi ya kufanya mikutano, alikutana na upinzani mwingi kutoka katika kundi hili, lakini kwa kuwa anaamini wapinzani wana mchango pia katika siasa za nchi hii, alienda against nao na kuwapa upinzani haki nyingi ambazo walikuwa hawana kabla ya Samia kuingia.

Sasa wanachokifanya Chadema, kutumia lugha ambazo ni very provocative kwenye mikutano yao, kususia vikao vyenye kujenga utaifa, nao wanakua ni hardliners, au misimamo mikali, na wanawa prove right au kuwa 'vindicate' lile kundi la hardliners ndani ya CCM ambalo lilikuwa linamtahadharisha Samia kuwa asiwape upenyo wapinzani maana atakuja kujutia.

Sasa kitakachoweza kutokea ni either Samia ataendelea kuwa mvumilivu au atawasikiliza hardliners wa CCM

Akiwasikiliza hardiliners ni kuwa tunarudi kwenye Magufulism 2.0

Je, Chadema wataweza kukabiliana na wahafidhina wa CCM?
 
Nadhani tunahitaji kujadili siasa za nchi yetu kwa uhalisia zaidi kuliko kwa kujipa moyo au kwa wishful thinking

Uhalisia upo hivi, Rais Samia Suluhu ndio Rais ambaye amejaribu kuwa fair zaidi kwa Chadema kuliko Rais yeyote, na sidhani kama atatokea Rais mwingine akawa fair kwao kama Samia

Chadema kwa miaka zaidi ya 5 walikuwa treated kama 'kikundi cha waasi ama wahalifu, na haki zao nyingi kuporwa na hakuna walichoweza kufanya zaidi ya kukimbia nchi na kuomba msaada kwa wazungu

Walimtishia sana Rais Magufuli kwa maandamano na migomo, Magufuli akawatilia ngumu mwanzo mpaka mwisho, walipoona huyu mtu hatishiki wakaona waombe kukutana naye, hata hivyo Magufuli akawapuuza na kuwaweka ndani, na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu wote mnajua kilichofanyika

Chadema pamoja na vitisho vyote hawakuweza kufanya kitu zaidi ya kukimbilia nje ya nchi,
Rais Samia alipoingia kitu cha kwanza kufanya ni waliomba wakutane naye, Rais Samia kwa ubinadamu wake akawakubalia kwa sababu ni watanzania wenzetu, waliokimbilia nje akawaruhusu warudi nyumbani na kuwahakikishia usalama

Pia akawaruhusu kufanya mikutano waliyokuwa wamezuiwa kuifanya kwa miaka mitano,

Sasa katika CCM, kama vyama vingi duniani, kuna makundi mawili, kuna kundi la hardliners na kundi lingine la moderates

Hili kundi la moderates, ni lile kundi linaloamini kuwa CCM ni chama ambacho kinafaa kukosolewa na vyama vya upinzani, na vyama vya upinzani vinatakiwa kupewa nafasi ya kuikosoa CCM na kupewa nafasi katika uwanja wa kisiasa

Hili kundi la Hardliners ni lile kundi linaloamini CCM ni chama kinachotakiwa kutumia nguvu zozote kukandamiza upinzani, na upinzani hawapaswi kupewa upenyo kabisa wa kuitikisa CCM

Hili kundi ndio kubwa ndani ya CCM na ndio lililokuwa linashika hatamu katika awamu ya 5

Samia alipokutana na Wapinzani na hata kuwapa nafasi ya kufanya mikutano, alikutana na upinzani mwingi kutoka katika kundi hili, lakini kwa kuwa anaamini wapinzani wana mchango pia katika siasa za nchi hii, alienda against nao na kuwapa upinzani haki nyingi ambazo walikuwa hawana kabla ya Samia kuingia


Sasa wanachokifanya Chadema, kutumia lugha ambazo ni very provocative kwenye mikutano yao, kususia vikao vyenye kujenga utaifa, nao wanakua ni hardliners, au misimamo mikali, na wanawa prove right au kuwa 'vindicate' lile kundi la hardliners ndani ya CCM ambalo lilikuwa linamtahadharisha Samia kuwa asiwape upenyo wapinzani maana atakuja kujutia

Sasa kitakachoweza kutokea ni either Samia ataendelea kuwa mvumilivu au atawasikiliza hardliners wa CCM

Akiwasikiliza hardiliners ni kuwa tunarudi kwenye Magufulism 2.0

Je Chadema wataweza kukabiliana na wahafidhina wa CCM?
Hii mikutano ya kisiasa hivi kila rais akiingia hutoa favor au hili likoje? Maan naona wengi wanazungumzia mikutano kama vile wapinzani hupewa zawad tu ili wafanye mikutano yao!! NB: CCM hawako tayar kbs ku deal na vyama vingi au upinzani ni vile bas tu ni msukumo wa MABEBERU!!
 
Hii mikutano ya kisiasa hivi kila rais akiingia hutoa favor au hili likoje? Maan naona wengi wanazungumzia mikutano kama vile wapinzani hupewa zawad tu ili wafanye mikutano yao!! NB: CCM hawako tayar kbs ku deal na vyama vingi au upinzani ni vile bas tu ni msukumo wa MABEBERU!!
Tanzania ni nchi huru, hakuna cha beberu wala nani atakayetutishia kwenye maamuzi yetu...Kama mikutano imejaa matusi na uchochezi inafungiwa tu, tunachapa kazi... Hatutaki kuwa kama DRC nyingine
 
Mimi ni katika MODERATES....

Ninaamini katika siasa za kiasi....kukosoa na KUKOSOANA kwa STAHA......

Kinyume na siasa za staha siamini kutumia njia za STAHA kuwaendea wasiotaka STAHA.....

Post hii ina MADINI ADHIMU kabisa

Kudos mtoa hoja

#SiempreJMT

#Punda Afe JMT Ibaki Tulivu Na Salama amen

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Isije ikawa HARDLINERS wa CCM wameingia UBIA na "hasimu wao" TL et al kumsumbua sana mh.Rais SSH na utawala wake.....

Hapa panahitaji tafakuri pana na majibu kutoka kwa MIZIMU yetu inayolilinda taifa hili

Oooh Tanzania ya Ngorongoro nakupenda kuliko nafsi yangu

#SiempreJMT

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mabilioni anayopokea huko Kwa mabeberu yanamlazimu awe kigeu geu plus hulka yake ya u pwani. Hamna kitu hapo
Acha bigotry masta kiraka....hata nafsi yako inahitaji ifurahie chakula cha mapenzi na utu na yasiyo ya ubaguzi wowote ule

Back to the table.....

Mh.Tundu Lissu yuko mapumzikoni Ulaya na Marekani....amepokea mäbilioni kutoka Singida ?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom