Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
4,049
13,866
Rais Samia akizindua Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe Machi 9, 2025


View: https://www.youtube.com/live/ZwUZMNQWlbc?si=stvFOddgPgJ_0AHW

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi w...jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kukamilika kwa Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe ni ukombozi kwa wananchi katika Wilaya za Same, Mwanga na Korogwe.

Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe. Rais Samia amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo alifika kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu kuweka jiwe la msingi la mradi huo.

Taswira ya eneo la mtambo wa kutibu maji (Water treatment Plant ) katika mradi wa Maji wa Same...jpg

Pia amesema mradi huo umeongeza uwezo wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Same-Mwanga kufikisha maji safi na salama kwa wananchi kutoka watu 50,615 hadi 300,000 kwenye vijiji 38 katika Wilaya za Same, Mwanga na Korogwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi w...jpg

Akizungumzia jitihada kubwa zilizofanyika kuukwamua mradi huo na kuhakikisha wananchi wanapata maji, Rais Samia amesema haamini katika kushindwa, na amewarai watumishi wa umma kuwa na moyo wa kupambana katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha awamu ya pili ya mradi huo inatekelezwa kwa ukamilifu ili kuimarisha upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Korogwe.

Taswira ya eneo la mtambo wa kutibu maji (Water treatment Plant ) katika mradi wa Maji wa Same...jpg

Vilevile, Rais Dkt. Samia amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa sekta ya maji, hususan katika kuhakikisha huduma ya naji safi na salama inakuwa endelevu katika maeneo ambako miundombinu ya maji imefika. Pia amewataka watumishi wa sekta ya maji kuwahudumia wananchi kwa weledi na kwa wakati na kulinda vyanzo vya maji ili kuwezesha Serikali kutimiza ahadi yake kwa wananchi.

Taswira ya eneo la mtambo wa kutibu maji (Water treatment Plant ) katika mradi wa Maji wa Same...jpg
 
π™ˆπ™§π™–π™™π™ž 𝙬𝙖 π™ˆπ™–π™Ÿπ™ž π™Žπ™–π™’π™š- π™ˆπ™¬π™–π™£π™œπ™–- 𝙆oπ™§π™€π™œπ™¬π™š 𝙏π™ͺπ™’π™šπ™£π™ͺπ™›π™–π™žπ™ π™– .

Maji ni Uhai ni sentensi yenye maana kubwa katika Maisha ya Binadamu kwamba uhai wetu na maisha yetu binadamu na viumbe hai wote ikijumuisha Wanyama na Mimea yametegemea maji katika ustawi wake lakini usemi huu una nguvu na maana kubwa zaidi kwa maeneo yenye ukosefu wa rasilimali hii .

Maji ni Uhai ilibeba maana kubwa zaidi kwa Maeneo ya Same,Mwanga na Korogwe kutokana na adha ya ukosefu au uadimikaji wa Rasilimaji Maji katika maeneo hayo kwa miaka mingi licha ya jitihada za Serikali na wadau .

Katika Ukuaji wetu haikuwa ajabu kuona Mama kutembea Kilometa nyingi kutafuta maji na akarudi na ndoo tupu isiyo na maji,haikuwa ajabu .

Katika Maeneo mengine tuliwatambua watu waliokesha nje usiku kama walinzi wa watu na mali lakini kwa Same ilikuwa tofauti kina mama na watoto walikesha bombani kulinda foleni ya maji ,na wala haikuwa ajabu Mtoto kukaa bombani siku mbili bila kurudi nyumbani .

Tumezoea kuona katika maeneo mengine Watu wakiwa na ratiba ya kupeleka Chakula maofisini na Hospitalini lakini kwa maeneo haya haikuwa ajabu kuwepo kwa zamu ya kupeleka Chakula kwa anaelinda foleni ya kuteka Maji bombani tena kwa rasilimali maji isiyo toshelezi na uhakika .

Wala haikushangaza kuona Wanafunzi wameshindwa kufika shuleni kupata elimu eti kwa kuwa wapo katika harakati za kutafuta maji kwa ajili ya familia na Maisha yao .

Wakati maeneo mengine wakiweka Bajeti ya Fedha na mambo mengine ,Same tuliweka Bajeti ya Matumizi ya Maji pamoja na vipaumbele vya matumizi ya Maji ikiwa ni kunywa na kupikia na matumizi mengine kadri hali itakavyoruhusu .

Wakati wa makuzi yetu Passport size ilikuwa ni sehemu ya maisha ,wakati passport size kwenu ikiwa chaguo kati ya mengi,sisi tulipiga passport size tukienda shule kwa sababu ndivyo hali ilivyoruhusu .

Maji ni Uhai ina maana kubwa kwa mtu aliyenunua Ndoo moja ya maji kwa shilingi Elfu 2 au 3 au 10 .Ina maana kubwa kwa mjasiriamali alieshindwa kutoa huduma ya Saloon kwa kuwa amekosa maji ya kuoshea wateja .

Wakati kwenu ngumi zilichapwa ulingoni kama michezo na mkafurahi ,huku ngumi zilichapwa Bombani au kisimani kwa kosa la kupita foleni ya mwengine ,wapo walioumia wapo walionyanyaswa kijinsia na kadhia kadha wa kadha .

Hivyo kwetu watu wa Same- Mwanga na Korogwe Maji ni Uhai ina maana kubwa sana na kukamilika kwa mradi huu kumeondoa kero kubwa sana ,tumenufaika na tumeboreka kwani sasa maji ni uhakika na toshelezi .

Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya kukamilika kwa Mradi huu na tunawaombea heri wote waliohusika katika ukamilifu wa kazi hii njema .Pongezi nyingi kwa Serikali chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa ya ukamilishaji wa mradi huu.Dhamira ni njema na matokeo tunayaona kila la kheri Mhe.Rais .

Amon Nguma
Same - Kilimanjaro .
IMG-20250309-WA0661(1).jpg
IMG-20250309-WA0662(1).jpg
 
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe, Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 09 Machi, 2025.
 

Attachments

  • VID-20250310-WA0001.mp4
    24.4 MB
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Machi 09, 2025 anatarajiwa kuwa Mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na mengine, anatarajiwa kuwa Nyumba ya Mungu, Wilayani Same kuzindua mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe.

Mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ulisanifiwa mwaka 2008 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Arab Bank for Economic Development in Afrika na wadau wengineo walilenga kujenga mradi mkubwa wa maji kwaajili ya kuhudumia wakazi wa Miji ya Same na Mwanga na Vijiji 38 vya Wilaya ya Korogwe ili kuondokana na changamoto iliyokuwepo awali.

Mradi huu umetumia takribani Bilioni 300 kwa awamu ya kwanza na kwasasa kazi zinazoendelea ni pamoja na kuendeleza mtandao wa mabomba na kufanya maunganisho ya maji kwa wananchi, kukarabati na kuboresha miundombinu ya maji chakavu ikiwa ni pamoja na kubadilisha mabomva makubwa kulinganisha na mahitaji, kazi ambazo kufikia April 2025 huduma ya maji inatarajiwa kuwa imewafikia wananchi walengwa kwa asilimia 95.

Kukamilika kwa mradi huo wa Maji Same-Mwanga-Korogwe kunatajwa na serikali kuwa kutapelekea uwepo wa maji ya kutosha Mjini Same na Mwanga hivyo kutoa fursa kwa wawekezaji kuchangia kukuza uchumi wa maeneo hayo na Kilimanjaro kaa ujumla kwani upatikanaji wa maji utakuwa ni wa uhakika kwa saa 24 kutoka saa sita kwa siku zilizokuwepo awali.
 

Attachments

  • IMG-20250309-WA0018.jpg
    IMG-20250309-WA0018.jpg
    130.5 KB · Views: 1
  • IMG-20250309-WA0021.jpg
    IMG-20250309-WA0021.jpg
    66.6 KB · Views: 1
  • IMG-20250309-WA0024.jpg
    IMG-20250309-WA0024.jpg
    78 KB · Views: 3
Back
Top Bottom