Rais Samia apokea Ndege mpya ya Mizigo Boeing B767-300F Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Juni 3, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,715
13,467
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ndege mpya ya mizigo aina ya BOEING B767-300F katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam - Terminal One.



- Rais Samia ameshawasili Uwanjani tayari wa ajili ya zoezi la kupokea ndege ya mizigo

- Katibu Mkuu wa kamati ya Uchukuzi akitambulisha Wageni waliohudhuria upokeaji.

- Ndege mpya ya mizigo ya Tanzania (Boeing 767-300F) imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

1685800051916.png

Ndege mpya ya mizigo ya Tanzania (Boeing 767-300F)

- Zoezi la kuimwagiandege maji (Water Salute) linaendelea.

- Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila apewa nafasi ya kutoa salaam zake

1685799873904.png

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila

Akitoa salamu hizo mbele ya Rais Samia Chalamila amesema "Sisi Wakazi wa Dar es Salaam tumefarijika sana kwa kazi kubwa ambayo umeendelea kuitenda kwenye mkoa wetu. Natoa taarifa kwamba mkoa wa Dar es Salaam upo salama sana na tumeahidi mimi na ndugu zangu Wananchi hawa kwamba Dar es Salaam haitakuwa uwanja wa fujo za kisiasa hata siku moja."

Tumejipanga mimi na Madiwani na Wananchi wote kwamba tunaondoka na safari ya Mwendokasi ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia hapa kuna ndege watu wote unaowaona hapa ni kwa ushirikiano mkubwa sana ambao wametupatia Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wabunge na Madiwani wote.

Lakini nitatumia nafasi hii kueleza changamoto za wakazi wa Dar es Salaam. Hii mvua unayoiona hii watu wanalia kila kona lakini wewe Rais Samia miezi michache iliyopita umeidhinisha bilioni 217 ziweze kuchakata mtambo wa maji taka hapaBunguruni lakini umeidhinisha pia bilioni 153 ziweze kuweka mtambo mkubwa wa kuchakata maji taka pale Mbezi Beach.

Lakini pia ulipoingia hapa Dar es Salaam kumekuwa na tatizo kubwa la foleni huko barabarani, wewe umeleta mradi wa BRT na kuuendeleza.

Hapa Dar es salaam kwa wiki ijayo nitakuwa na kikao na viongozi wa dini, ajenda kubwa ni tokomeza adui ili Rais Samia apenye bila kupingwa

Lakini pia Rais Samia ndege hii iliyokuja unahitaji Marubani, miezi michache iliyopita umeidhinisha bilioni 4 zinunue ndege mbili ambazo zitatumika kufundishia Wanafunzi wanaosomea Urubani Chuo cha NIT.
---

- Marubani wa ndege wanatambulishwa

1685796525218.png

Picha: Rubani Neema Swai

Marubani mbalimbali wanatambulishwa wakiongozwa na Neema Swai ambaye anatajwa kuwa Rubani wa kwanza wa Tanzania kuongoza ndege kubwa kiasi hicho.

- Rais Samia na Viongozi wengine wakipiga pichambalimbali.

Taarifa ya Ndege ya Mzigo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Air Tanzania Mhandisi Ladislaus Matindi

1685798048022.png

Mkurugenzi Mtendaji wa Air Tanzania Mhandisi Ladislaus Matindi
Mpango wa ununuzi wa ndege za mizigo umelenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka na kuingia Tanzania na hivyo kuongeza thamani ya bidhaa zetu. Aidha ujio wa ndege hii utasaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa bidhaa za kitanzania, uhakika wa bidhaa na bidhaa zinazotumika katika uzaishaji.

Kwa kuiwezesha atcl upande wa usafirishaji wa mizigo kunifanya nchi yetu ifaidike kwa fursa nyingi za hapa nchini zinazohusiana na usafirishaji mizigo kwenda nje ya nchi. Mizigo hiyo ni pamoja na minofu ya samaki kutoka kanda ya ziwa, dagaa na samaki wa mapambo kutoka ziwa Tanganyika, nyama kutoka Kanda ya Ziwa, Mikoa ya Kaskazini, maua matunda na mbogamboga kutoka kaskazini mwa nchi na Nyanda za Juu Kusini, Mazao ya baharini kutoka Zanzibar na maeneo mengine ya Ukanda wa Bahari ya Hindi hapa nchini.

Mazao haya ni rahisi kuharibika hivyo, kufanya usafirishaji kwa njia ya anga kuwa sahihi zaidi na kuhifadhi ubora wake yanapofika sokoni. Usafirishaji wa bidhaa hizi kupitia nchi za jirani unapunguza thamani.

Upokezi wa ndege hii kunaifanya ATCL kuwa na ndege 13 huku 3 zikienelea kuundwa. Hadi mwaka 2026/27 ATCL inatakiwa iwe na ndege 20 zikiwemo ndege za masafa mafupi nane, za masafa ya kati nane, za masafi marefu tatu na ndege moja kubwa ya mizigo. Hata hivyo, kutokana na uhitaji wa soko la usafirishaji wa mizigo ni vyema ndege za mizigo zikawa mbili. Hivyo tunaleta ombi letu kwako.

Ndege hii ina uwezo wa kubeba tani 54 za mzigo (sawa malori matano na nusu ya tani kumikumi), ina uwezo wa kusafiri kilometa 11,070 za angani bila kutua kuongeza mafuta (sawa na kusafiri muda wa saa 10 bila kutua).

Matanki yake ya mafuta yana uwezo kubeba lita 90,770, mabawa yake yana urefu wa meta 47.6, pia inaweza kwenda mwendokasi wa kilometa 850 kwa saa na ina urefu wa meta 54.9.

Ndege hii itaanza na kusafirisha mizigo sehemu mbalibali nadani na nje ya bara la Afrika baadhi ya maeneo hayo ni Nairobi, Harare, Kishansha Mumbai na nchi za kiarabu.

Rias Samia azungumza, Awashukuru Wananchi kuendelea kuipa Serikali nguvu ya kufanya maendelep
- Waheshimiwa Wananchi tunawashukuru sana kwa kutuombea na kutupa nguvu kuweza kufanya mambo haya ya Maendeleo ndani ya nchi yetu tunawaomba muendelee kuwa pamoja nasi, mtuombee mtupe nguvu tufanye kazi tupate mapato tuweze kuendelea na mambo kadhaa.

Tumeombwa ndege nyingine hapa ya mizigo ahadi yetu kwenu Wananchi tutalifanyia kazi.

Tunawashukuru sana karibuni sana.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ndege mpya ya mizigo aina ya BOEING B767-300F katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam - Terminal One.

tanzania nchi yangu dah
 
Watanzania Wanahitaji maji huku vijijini .. hiyo midege hawaitaki.
 
Back
Top Bottom