Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,712
- 20,605
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwa Maisha ya Rais Samia hapa Duniani.ukifuatilia namna anavyoongoza Nchi,namna anavyo chapa kazi,namna anavyopambana kutatua kero na changamoto mbalimbali,namna anavyotekeleza miradi ya maendeleo,namna anavyohangaika huku na kule kuwasikiliza watanzania na kuwapatia majawabu.
Unaona wazi kabisa namna Mama huyu mwenye moyo wa huruma na upendo alivyojitoa na kujitolea Maisha yake kama Sadaka kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.inafika wakati unamuona sana huruma na unajiuliza anakaa saa ngapi na familia yake .maana muda wote na Mwingi unamuona yupo kazini akichapa kazi bila kuonyesha uchovu wala kuchoka.Ikumbukwe naye ni Mwanadamu mwenye moyo wa nyama na mwili kama binadamu wengine.
Kwa hakika itatuchukua miaka mingi sana kumpata Mama Samia Mwingine katika Taifa letu. Mwenye Moyo wa huruma ,upendo, uzalendo, uchapakazi, unyenyekevu na dhamira njema kwa Taifa letu.Najuwa wenye upofu wa akili na macho wanaweza wasielewe vyema maneno haya kwa sasa.
Najuwa wenye chuki binafsi na Mama wanaweza kuwa gizani bado na kupofushwa na mawazo ya kibaguzi kwa misingi ya ukabila ,Udini,ukanda na jinsia na wengine bila hata sababu ya msingi zaidi ya kufuata Mkumbo tu .
Lakini ipo siku baada ya kumaliza muhula wake wa pili 2030 tutamkumbuka sana huyu Mama,kuna watu watabubujikwa na machozi ya kujutia chuki zao kwa Mama huyu asiye na makuu wala majivuno wala kiburi wala dharau wala ubaguzi.Tutamkumbuka sana huyu Mama mwenye hofu ya Mungu ndani yake
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.