Rais Magufuli usipokaa vizuri na wateule wako wananchi tutakuchoka asubuhi na mapema sana

Serikali ililaumiwa sana kuhusu kuangalia kodi kwenye bia, soda na sigara tu. bigmind!!!
Tukilalamika awakusanyi kodi tunamanisha kwenye makampuni ya pombe km tbl, safari brewrse, kampuni za uwindaji, makampuni ya ujenzi, makapuni ya madini, mahotel makubwa, bandarini na viwanja vya ndege.
 
Ni kweli, wapo baadhi ya watanzania wanalipa kodi mara mbili-mbili, kazi ya kuendesha nchi ni ngumu.
Shida ni wasomi uchwara, shisa kubwa ya wasomi wa nchi hii ni kwamba wanatumia sana madesa, badala ya kuntransfer knowledge na skills walizopata vyuomi kwenye mazingira ya nchi yetu.
 
Kati ya wafanyakazi wote walimu ndo wanaisoma no vizur,ngoja waletewe na kod ya kupanga nyumba hahahahha,nacheka kwa dharaaau,hii serikali sijajua lengo lake mpaka sa ivi.
 
Sina nia mbaya ila napenda kuonya na kushauri jinsi ya uteuzi wa mh.rais hasa kwa mawaziri wenye dhamana zinazowagusa maisha ya kila siku ya wananchi.

Uteuzi wa waziri wa fedha ndugu Mpango unapwaya kitendo cha kushindwa kutafuta vyanzo halisi vya mapato ya fedha na kukimbilia kutoza VAT kwenye mihamala ya pesa pasipokuzingatia mzigo tuliojitwisha sisi wananchi ni udhaifukubwa.

Sisi wananchi tunapenda kulipa kodi ila si kwa namna hii fikiria mfanyakazi anakatwa kodi mshahara, anakatwa benki, anakatwa akinunua bidhaa dukani sasa hizi kodi tatu zote za nini? Bado km ana gari akatwe road License, akatwe bima, akatwe bima matibabu, hivi nini hiki?

Pia ujue tunataka majibu ya nini kinatokana na vitu vifuatavyo:-
Gesi
Madini
Utalii(uwindaji)
Misitu
Uvuvi
Bandari
Viwanja vya ndege
Treni.
Wananchi tutafurahi kuona mchangokubwa ukitoka kwenye rasilimali za nchi kuliko kutukaba mpaka tunashindwa kukohoa.

Simple minds produced by bigmind..
Pole sana kama ulitegemea mabadiliko yoyote kwenye utawala wa ccm , mara tu BAADA YA BAJETI kusomwa , nilikuwa wa kwanza kuuliza kama Dr Mpango aliwahi kufanya biashara yoyote , hata kama kuuza mapera .
 
Kati ya wafanyakazi wote walimu ndo wanaisoma no vizur,ngoja waletewe na kod ya kupanga nyumba hahahahha,nacheka kwa dharaaau,hii serikali sijajua lengo lake mpaka sa ivi.
Hujui lengo lake kivipi wakati mkuu alishasema kwamba anataka wale walioishi kama malaika waishi kama mashetani !
 
Pole sana kama ulitegemea mabadiliko yoyote kwenye utawala wa ccm , mara tu BAADA YA BAJETI kusomwa , nilikuwa wa kwanza kuuliza kama Dr Mpango aliwahi kufanya biashara yoyote , hata kama kuuza mapera .
Ndiyo maana nikasema tunahitaji viongozi wabunifu wanaoijua vyema nchi yetu, wabainishe rasimali za asili na kuziingiza kwenye vyanzo vya mapato ili kupunguza mzigo kwa raia maskini kwa miaka zaidi ya 50.
 
Sasa mbona ni sote ata tulioishi km mashetani tunaona moto mkubwa zaidi jamani..!

Hahahah labda alimaanisha sisi tunaoishi km mashetani tutaongezeka ushetani na wanaoishi kama malaika wataanza kuuonja onja ushetani, maana huku mitaani hali mbaya sana
 
Hahaha leo mnamkumbuka Saada?
cc FaizaFoxy ....
Unajua kwenye maisha kulinganisha vitu/watu kupo,,sasa uyu waziri wa fedha utendaji wake Haulidhishi ata kidogo,yaani ata yule mama saada mkuya alifanya vizuri sana ukimlinganisha na uyu.
 
Maelezo yako marefu umefanya utafiti kwa kulinganisha na nchi zingine au umeandika tuu, tupe walau mfano wa nchi iliyoendelea kama Africa kusini, Ethiopia na Kenya ili tuone cc tulipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom