Rais Magufuli, Ruhusu usafiri (Mabasi) yasafiri usiku

Mabasi yaruhusiwe kufanya biashara 24/7 halafu wapange wao hata gari ziwe zinaanza safari saa tatu usiku.

Kuna haja ya binadamu kujitofautisha na wanyama wengine tutumie muda visiting muda ni rasilimali muhimu mno.

Watanzania wanahitaji huduma hiyo ndio maana unakuta wengine wanasafiria magari ya magazeti au mizigo kwa kuwa na haraka.

Muda wote unahitaji kua na usalama movement zetu haziwezi kuzuiliwa kwa sababu za kiiusalama si kweli hata kidogo serikali haishindwi kuwahakikishia usalama huko wanakoteka abiria.

Kwenye viwanda huwa uzalishaji huendelea 24/7 nategemwa hata kwenye sekta hii inawezekana.

Ni kuhakikisha kwa kuwakagua madereva hao muda wa kuanza safari.
 
Boss hayo yote ni makosa kisheria kama serikal inavopigana na wakwepa kodi wapambane na majambazi madereva walevi na magari yanayoenda spid zaid ya kiwango kuna mamlaka zifanye kazi zifanye kaz excuse hizo ni uzembe serikal ingalie sana Watanzania tuamke fursa ni nyingi ndugu tukianzia hapo tu.
 
Tanzania ndio nchi pekee Afrika Mashariki marufuku mabasi kusafiri usiku. Marufuku hii inatugharimu kiuchumi na usumbufu mkubwa kwa wasafiri. Usafiri wa usiku ungewezesha mfano mkazi wa mbeya kuwahi shughuli zake Dar siku ya pili na kurudi mbeya siku hiyo hiyo. Kwa hali ilivyo baadhi yetu inabidi kudandia mfano magari ya magazeti ili kuwahi shughuli siku ya pili. Uchumi wa 24/7 bila usafiri usiku ni ndoto za mchana. Serikali ifute marufuku hii angalau kwa baadhi ya routes ambazo usalama siyo issue.
 
Naungana na wewe,,kitendo cha kulazwa morogoro saa tano usiku sikukipenda asilan,,,saa tano moro aisee nilikereka sana
 
Mimi naona iendelee tu maana mabasi yakianza kusafiri mpaka usiku uvamizi utazidi kama ukiwa na haraka zaidi unapanda ndege tu
 
Kweli kabisa kwani kama ni kuogopa ujambazi Kenya na Uganda haupo au wenyewe wanatuzidi ulinzi.
Yaanze kwa hawamu kutokana na umbali.
Bukoba .MUSOMA.Uganda.Mbeya. Rukwa. Yote yanayotoka nchi nyingine nk.

Mwisho tusije tukaogopa kutembeza treni ya mwendo kasi usiku.
 
Nadhani hoja ya kuzuia mabasi ucku, haikuwa ujambazi. Nakumbuka aliyepiga marufuku safari za mabasi ucku, alikuwa John Malecela wakati huo akiwa ni waziri mkuu. Alifanya hvyo kwa hoja kupunguza ajali.
 
Tatizo hujui chanzo cha marufuku hii.Hii marufuku ilitolewa miaka ya tisini baada ya ajali kutokea sana mida ya usiku.Nakumbuka kuna ajali ilitokea dodoma/ihumwa ilitokea ajali iliyoua watu zaidi ya thelathini chanzo kikiwa kusinzia kwa madereva.
 
Tatizo ni speed limit tu, zaman wakati hajuna speed limit Dar-mby-Tunduma ni masaa 10 tu, wakati barabara mbovu na Dar songea masaa 12 tu
Sasa barabara nzuri kdogo lakini speed limit ni janga, kila kona toch wakati magari yameboreshewa technologia/automated. Ni vyema madereva wetu wapewe elimu na mafunzo stahiki kuendana na wakati.
Haiwezekani gari ina max speed 220 alafu mtu anakutaka utembee 50, 70, 80 .
 
Nadhani hoja ya kuzuia mabasi ucku, haikuwa ujambazi. Nakumbuka aliyepiga marufuku safari za mabasi ucku, alikuwa John Malecela wakati huo akiwa ni waziri mkuu. Alifanya hvyo kwa hoja kupunguza ajali.


Sio Lyatonga Mrema kweli?
 
Mimi naona iendelee tu maana mabasi yakianza kusafiri mpaka usiku uvamizi utazidi kama ukiwa na haraka zaidi unapanda ndege tu
askari kazi yao nini?...kila mwaka tunaingiza askari wapya wanaota vitambi uzembe wao ndio walitakiwa wakae barabarani na road patrol 24/7 kama wenzetu kenya .pindi anapotokea jambazi ni shot to kill tuone kama kutakuwa naupuuzi kama huo wa kuteka teka ovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…