Rais Magufuli, msimamishe Makonda kazi kwa maslahi ya umma!

Kikubwa mnachokosea mnaomchongea Makonda kwa Magufuli ni the approach mnayotumia.

Nawashauri nguvu mnayotumia na watu mnaowatumia inaonesha kabisa kuwa nia yenu ni Makonda na hapo ndo magufuli anawaona wajinga na hamna. Leo mmetengeneza tukio la cctv eti makonda anaingia clouds media. Mlichokosea eti kuna mtu kavaa magwanda na bunduki kabisa.

Tangu lini nchi hii JW wakamlinda mkuu wa mkoa????? Tangu lini nchi hii askari wa JW akashika bunduki eti kumlinda mkuu wa mkoa alafu polisi hana silaha????? Hata raisi wa nchi halindwi na wavaa mabakabaka tena wakiwa na silaha wazi. Mnapotengeneza clip za namna iyo mtawadanyanya hao wasiofikiri wa wasioijua nchi hii na vyombo vyake.

Na kwa stahili iyo nawaambia mtazidi kumpandisha makonda na sio kumuangamiza kama mnavotaka.
 
Unaweza kuwa saww kama hukuunganisha kosa la uvamizi wa clauds . Uvamizi wa klauds huwezi utenganisha na tuhuma za vyeti fake.
 
CDF V. Mabeyo.


Nimeona vijana wakiwa na mitutu clouds na Rc makonda..

Ile nidhamu aliyoacha Gen. D. Mwamunyange iko wapi?


Kwanini Jeshi linatumika kisiasa?

Hivi ni viashiria vibaya sana..

Tafadhali ! Tunataka Jeshi safi.
Mkuu Hili Litafanyiwa Kazi Haraka Naamini Ndani Ya Muda Mfupi Ujao Utasikia Matokeo Yake Ile Ni Kwa Hao Askari Wenyewe Kujitoa Ufahamu
 
Mkulu we si unampenda ngoja siku utamkuta chumbani kwa jesca ndio utajua huyo mtoto sasa ametamalaki mpaka anaingia msikitini na viatu!
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa (DSM) huyo a.k.a amiri jeshi mkuu wa dar ndivyo kichwa kinavyomtuma kwamba majeshi yote mkoani yako chini yake so can do anything kama alivyofanya huko Clouds. Hongereni IPP Media kwa kupuuza habari za huyu jamaa. Mliona mbali sana. You're really Super Brand.

ila nna wasiwasi clouds ili waendelee kupendwa na baba... usistaajabu wakamsafisha bashite kwenye hili ili waendelee kupigiwa simu... jamaa wako kimaslahi zaidi sio kama ipp
 
kweli yule jamaa ana elimu na weledi mdogo sana yaan kila kukicha anaongeza tuhuma dhidi yake.
 
Inafika hatua wanajeshi wa JWTZ wanaacha lindo na kwenda kuvamia kituo cha utangazaji usiku wa manane kwa amri ya RC? Siku mukulu anatahamaki mara jamaa yupo mbele yake na full kikosi ndo atajua ile methali ya "anayeonja asali atachonga mzinga"
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa (DSM) huyo a.k.a amiri jeshi mkuu wa dar ndivyo kichwa kinavyomtuma kwamba majeshi yote mkoani yako chini yake so can do anything kama alivyofanya huko Clouds. Hongereni IPP Media kwa kupuuza habari za huyu jamaa. Mliona mbali sana. You're really Super Brand.
Pamoja na mapungufu ya Clouds lakini hili suala sio la kumwachia Kusaga peke yake. Kwangu mimi navishauri vyombo vyote vya habari kulipinga hili jambo kwa nguvu zote. Leo huyo kijana amevamia Clouds hivi atashindwa kwenda Mwananchi, Mtanzania, E-FM, Free media, au Mwanahalisi na kufanya kama hivi?
Na huyo aliyevaa hayo magwanda au kutumia sare za kijeshi ni vyema Jeshi letu likamtafuta na awaeleze ni kwa vipi alitumika katika kuvamia studio za Clouds.
 
864211cdcd67b87f9ecb680defece855.jpg


Si kwa sababu ya wabunge kumwita akakataa, la hasha!

Si kwa sababu ya kutumiwa na wauza madawa na kujifanya yupo kwenye vita dhidi ya dawa hizo huku akiifanya kazi hii kwa maelekezo ya wahusika wakuu ili kuua vita yenyewe kabla ya kufika kokote (akishirikiana na baadhi ya maafisa wa vyombo vya dola wasio na weledi wa kazi yao).

Si kwa sababu ya zile taarifa mfu alizokuwa akikupenyezea ili ang'are mbele zako na Taasisi nzima ya urais kuwa ni RC bora zaidi ya RC yeyote nchini.

Si kwa sababu ya tuhuma za kuwa na mali zenye mashaka mengi tangu akiwa DC na hata sasa ambazo vyanzo vyake idara nyeti zinajua na zimekudokeza mara kadhaa huenda hukujua athari zake.

Si kwa sababu ya yaliyotokea kupitia kijana huyu katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Jakaya Kikwete ambayo mengine kuyaandika ni aibu.

Si kwa sababu ya vyeti vyake vyenye utata, la hasha!

Ni kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka. Amelewa madaraka, ameota mapembe na sasa asipodhibitiwa Taasisi ya Urais (si wewe kama Magufuli) itaingia fedheha kubwa zaidi ya kinachoonekana sasa.

Haya unayoona ni mvua za rasharasha, mvua kamili itanyesha Aprili 2017 na hutoamini athari itakayoikabili Ikulu yako na kuchafua legacy yako.

Unao muda, chukua hatua mapema!
April 17 mbali sana hebu wekeni video na mapicha yote ya vitendo vyake ili sizonje aone aina ya Kijana anayemgroom
 
Ninaamini Mhe. Kitwanga hakuondolewa kwenye uwaziri kwa sababu ya ile "ulevi bungeni" hata kama alikunywa kweli! Ikumbukwe siku zile kashfa ya LUGUMI ilikuwa kwenye "burning hell", hivyo ni mtazamo wangu kuwa, ili kunusuru wengi, ilibidi Mhe. Kitwanga aondolewe kwa njia mbadala! "ulevi"!

Likewise, kashfa ya kughushi vyeti inayomkabili Makonda, endapo ikichukuliwa" seriously " ni wazi inaenda na wengi! Rais akimtumbua Makonda kwa kosa la vyeti bandia inabidi serikali yote ya mkoa wa Dar (hasa subordinates wa RC) ifumuliwe upya (ifahamike ma DC huapishwa na RC).

Hivyo, ili kuiepusha aibu hiyo dhidi ya MTEUZI na WANA USALAMA waliofanya "vetting" ya uteuzi, ni wazi sasa, aidha ni mbinu ya KITENGO au MTEUZI kumfanya MAKONDA afanye makosa mapya au kituko chochote ili aondolewe nayo, nje ya makosa ya vyeti!

Mfano:
1. kusafiri hovyo nje ya nchi,
2. kufanya jubilei ya gharama kutimiza mwaka kazini,
3. Kuvamia kituo cha redio usiku akiwa na "MAKUMANDOO" yenye silaha

Hayo ni baadhi ya matukio yanayolenga kumuondoa huyo jamaa bila kuhusisha kosa la vyeti bandia!

NB: nitamsifu Rais endapo Makonda atawajibishwa kwa suala la vyeti na si kosa lingine kwanza!

Nimewasilisha.

By the way, Wenye mapovu, leo weekend, mkafulie nguo zenu!

na alipoondolewa kesi ikaisha pale pale!! watanzania bana
 
Back
Top Bottom