Ninaamini Mhe. Kitwanga hakuondolewa kwenye uwaziri kwa sababu ya ile "ulevi bungeni" hata kama alikunywa kweli! Ikumbukwe siku zile kashfa ya LUGUMI ilikuwa kwenye "burning hell", hivyo ni mtazamo wangu kuwa, ili kunusuru wengi, ilibidi Mhe. Kitwanga aondolewe kwa njia mbadala! "ulevi"!
Likewise, kashfa ya kughushi vyeti inayomkabili Makonda, endapo ikichukuliwa" seriously " ni wazi inaenda na wengi! Rais akimtumbua Makonda kwa kosa la vyeti bandia inabidi serikali yote ya mkoa wa Dar (hasa subordinates wa RC) ifumuliwe upya (ifahamike ma DC huapishwa na RC).
Hivyo, ili kuiepusha aibu hiyo dhidi ya MTEUZI na WANA USALAMA waliofanya "vetting" ya uteuzi, ni wazi sasa, aidha ni mbinu ya KITENGO au MTEUZI kumfanya MAKONDA afanye makosa mapya au kituko chochote ili aondolewe nayo, nje ya makosa ya vyeti!
Mfano:
1. kusafiri hovyo nje ya nchi,
2. kufanya jubilei ya gharama kutimiza mwaka kazini,
3. Kuvamia kituo cha redio usiku akiwa na "MAKUMANDOO" yenye silaha
Hayo ni baadhi ya matukio yanayolenga kumuondoa huyo jamaa bila kuhusisha kosa la vyeti bandia!
NB: nitamsifu Rais endapo Makonda atawajibishwa kwa suala la vyeti na si kosa lingine kwanza!
Nimewasilisha.
By the way, Wenye mapovu, leo weekend, mkafulie nguo zenu!