Rais Magufuli: Kazi ya Serikali sio kulisha watu, sitatoa chakula cha bure kwa wataokumbwa na njaa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,430
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaagiza Watanzania kutumia mvua zinazonyesha kipindi hiki kulima mazao ya chakula na biashara ili kuepukana na janga la njaa, na endapo eneo lolote litakumbwa na njaa serikali haitokuwa tayari kupeleka chakula.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa Wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati akielekea jijini humo akitokea Tabora, amesema kuwa maeneo ambayo hayatafanya kazi kwa uzembe wao hatovumilia viongozi wa maeneo husika.

“Sitatoa chakula kwenye Wilaya yoyote, hakuna chakula cha bure kama mlivyozoea huko nyuma, usipofanya kazi usile na usipokula kufa, lazima tuambiane ukweli, Watu wafanye kazi, walime, na asiyefanya kazi asile”, amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa, “Wilaya itakayopata njaa DC ataondoka na Viongozi wengine wanaostahili kuhamasisha Wananchi kufanya kazi wataondoka, tunataka pesa tunayopata ifanye kazi nyingine, tunatoa Elimu bure, tunajenga SGR ndio kazi za Serikali, sio kukulisha".
 
Sitatoa Chakula? Yeye ana hekari ngapi, au analima wapi?

Hata watu wakilima kuna chakula cha bure? au wanatoa pesa zao kununua hivyo vyakula na wakati mwingine bei juu mvua inyeshe au isinyeshe? (refer sukari, mafuta n.k.)

Siasa bana kazi kweli kweli...., nadhani tunahitaji kukaa na kuona vipi tunaweza tukakuza production sio kwa vitisho au kuambiana so called ukweli bali kupeana mbinu za kisasa.

Si vibaya serikali ikiweka shamba darasa huko kwa so called wavivu ili wawe wanafanya kitu practical ( na huku kukosa ajira sidhani kama watakosa wadau / nguvu kazi) ingawa kwa sasa ukulima manual nadhani umepitwa na wakati.
 
Sijuti kuto mpa kura mtu wa namna hii Hakika sikushiriki kweny hii dhambi
Sijutii kumpa kura Magufuli,!

Hata tetemeko la kagera mlimtukana kwamba mbona hizo hela hawapi watu wanunulie ndizi na mahindi ili wale yeye akasem tz hii haina shida na chakula, sasa umeona kituzimefanya zile hela? Je kuna mtu alikufa sababu kakosa hela ya kununulia mahindi na ndizi?
 
Back
Top Bottom