Rais Magufuli alaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua Rubani Roger Gower

Rais kulaani jambo fulani si jambo la kawaida wala la kubeza. Baada ya kutolewa taarifa kuwa kuna mauwaji yamefanyika,ya Bwana Roger,yakiwahusisha majangili Rais ameguswa na kukasirishwa. Rais Magufuli na Serikali yake wapo katika vita vya ujangili,hasa wa tembo,nchini.

Kuuwawa kwa mshikadau wa vita ya ujangili ni jambo lililomgusa Mhe. Rais Magufuli. Rais ameagiza wahusika wasakwe na kuchukuliwa hatua. Agizo la Rais si la mchezo. Majangili wakae mkao wa maumivu makali. Kutamba kwao kunafikia mwisho tena kwa haraka.

Majangili wasisahau pia kuwa Katibu Mkuu,mtendaji mkuu wa Wizara,Wizara ya Maliasili na Utalii ni Meja Jenerali Millanzi. Naye wamembeep,wasubiri awapigie akilenga kulinda heshima na kuaminiwa kwake.
Petro naomba nirudie tena ushauri ambao nimekuwa nautoa mara kwa mara. Kwanza kukasirika kwa Rais pekee haitoshi kumaliza tatizo kama hakuna mikakati, atakasirika mzee wa watu hadi apasuke lakini huko field ni business as usual.
Nilishauri serikali ijitahidi kurudisha mahusiano mazuri kati ya askari wanyamapori na wananchi wanao ishi pembezeni mwa hifadhi zetu ili kuweza kupata taarifa za majangili. Askari wetu wanaona fahari kuwa nyanyasa wenyeji wa maeneo hayo kwa makosa hata ya kina mama wanaojikuta wamevuka mipaka na kuokota kuni za kutumia tuu. Wakina mama wanapigwa mpaka wanavuliwa nguo na kudhalilishwa na vijana wadogo kisa wanaokota kuni hifadhini.
Malalamiko hayo ndiyo yana wafanya watu wawachukie askari na kushindwa kuwapa ushirikiano pale waonapo mienendo ya majangili kama mwendelezo wa kukomoa. Huwezi kuwashirikisha watu kwenye ulinzi wakati unawafanyia vitendo visivyo vya kibinadamu, hiyo ni hulka ya watu waliokasirika.
 
Ngoja tusubiri
Majangili yanafichwa na wanakijiji
Ila mtandao au tuseme wanaoenda kuwauzia wapo dsm wanakula bata naskia wengine ni makatibu wakuu wa vyama
Kwa hio hapo inakuwa ishu kidogo
 
Umenena point kabisa mkuuu wakizingatia mkakati huo halkika ushirikiano utakuwa mkubwa mno
 
Hii vita na majangiri imetushinda. Mi naona ni bora serikali ibinafsishe hii kazi ya kulinda tembo
 
Ngoja tusubiri
Majangili yanafichwa na wanakijiji
Ila mtandao au tuseme wanaoenda kuwauzia wapo dsm wanakula bata naskia wengine ni makatibu wakuu wa vyama
Kwa hio hapo inakuwa ishu kidogo
ije operation tokomeza ingine
 
Nasikia majangili wana mahusiano ya karibu na magaidi,sitashangaa nikisikia kuna mtandao mkubwa wa wanasiasa na viongozi wa serikali wakihusika na ujangili.Ngoja Scotland Yard waanze kazi.
 
Petro naomba nirudie tena ushauri ambao nimekuwa nautoa mara kwa mara. Kwanza kukasirika kwa Rais pekee haitoshi kumaliza tatizo kama hakuna mikakati, atakasirika mzee wa watu hadi apasuke lakini huko field ni business as usual.
Nilishauri serikali ijitahidi kurudisha mahusiano mazuri kati ya askari wanyamapori na wananchi wanao ishi pembezeni mwa hifadhi zetu ili kuweza kupata taarifa za majangili. Askari wetu wanaona fahari kuwa nyanyasa wenyeji wa maeneo hayo kwa makosa hata ya kina mama wanaojikuta wamevuka mipaka na kuokota kuni za kutumia tuu. Wakina mama wanapigwa mpaka wanavuliwa nguo na kudhalilishwa na vijana wadogo kisa wanaokota kuni hifadhini.
Malalamiko hayo ndiyo yana wafanya watu wawachukie askari na kushindwa kuwapa ushirikiano pale waonapo mienendo ya majangili kama mwendelezo wa kukomoa. Huwezi kuwashirikisha watu kwenye ulinzi wakati unawafanyia vitendo visivyo vya kibinadamu, hiyo ni hulka ya watu waliokasirika.
Chakaza ushauri murwaa, hili ni jipu kwani askari pori hawana uhusiano mzur na wananchi jiran na hifadh hata kidogo
 
Hapana kwa kweli madhara waliyopata wananchi kwa ile ya kwanza yanatosha

Ujue hapo ni kazi ndogo tu
Ni ku deal na wale vigogo basi unakuwa umemaliza kazi serikali haina utayari
lakini wananchi nao wana matatizo kwann wana ficha wahalifu
 
Katika vita hii Kinana mbona anatajwa sana,,,ajiengue kwenye chama,,,awe huru.naona watu wanamsakama utafikiri hua wako wote kwenye hizo bness
 
Ni lazima Magufuli ahakikishe wananchi hawanyanyaswi kwenye maeneo ya hifadhi ili kupata taarifa toka kwa wananchi.
Atoe zawadi kwa watoa taarifa za majangali.

Pia anunue chopa za kijeshi sio kama ile iliyopigwa iko kama ya kufukuza ndege kwenye shamba la mpunga.
 
Nasikia majangili wana mahusiano ya karibu na magaidi,sitashangaa nikisikia kuna mtandao mkubwa wa wanasiasa na viongozi wa serikali wakihusika na ujangili.Ngoja Scotland Yard waanze kazi.

Ukiona tatizo halipati ufumbuzi miaka nenda miaka rudi kama madawa ya kulevya na ujangili ujue ni dhahiri kuwa viongozi wazito serikalini wanahusika. Ndipo utasikia mtu akisema "majina yao ninayo nawapa muda wajirekebishe".
 
Namtakia kila la kheri japo Jk naye alikua kwenye kiti hicho na alitangazia dunia anamfahamu kinara wa ujangili Arusha ,na alijisifu wale faru walioletwa kutoka south Africa watapewa ulinzi kuliko yeye ila matokeo yake ndio Kamweka George kwenye sportlight akala risasi za majangili na Pembe wakasepa nazo
 
Back
Top Bottom