Raia Mwema limewatambua wasiotaka kumkabidhi uenyekiti Magufuli

Huo mkutano hautarajii kufanyika karibuni maana hata ela za kuendesha huo mkutano bado hawajapata

Kuna change imebakia kama ile ya 12b kutoka NEC na kutoka sehemu zingine.

Hizi fedha zinafanyiwa mahesabu.

Maji ya kunywa na biscuits , vifuta jasho yaani "tissues", gharama za watumbuizaji na DJ unaweza ukaokoa fedha nyingi tu.

Wajumbe wa mkutano mkuu watajitegemea kwa chakula, malazi na nauli.
 
Ccm kuiongoza inakupasa uwe mtu mwenye kukubali uongo kwa maana ya kukubali kudanganya na kudanganywa.
Tofauti na hapo chama hakipo.
 
Kuna change imebakia kama ile ya 12b kutoka NEC na kutoka sehemu zingine.

Hizi fedha zinafanyiwa mahesabu.

Maji ya kunywa na biscuits , vifuta jasho yaani "tissues", gharama za watumbuizaji na DJ unaweza ukaokoa fedha nyingi tu.

Wajumbe wa mkutano mkuu watajitegemea kwa chakula, malazi na nauli.
Hiyo ingewezekana kirahisi kwenye utawala wa mswahili
 
Katiba ya CCM haimlazimishi JK kuachia Uenyekiti kwa sasa. Anao hiari kuachia au kusubiria muda wa kikatiba (miaka 5). Kwa maoni yangu JK aendelee ili Magu apate fursa ya kujifunza uimara na udhaifu wa chama chake, CCM.
 
tatizo la nchi zetu mtu akishakuwa rais kila aliyeko chini yake anamuogopa na kujenga unafiki. Hali inazidi akiwa rais na mwenyekiti wa chama.

Kwa sasa vyeo hivi vitenganishwe kuweka balance. Dhana ya chama kushika hatamu haiwezi kutimia ikiwa mkuu wake ndiye huyo huyo mkuu wa serikali na hili ni kosa ambalo ccm na vyama vingine vimefanya kwa muda mrefu.

Mtu aliyekulia ndani ya chama ni tofauti na yule ambaye hajatamadunika kwenye chama ingawa anafaa kuleta changamoto mpya.
 
Katiba ya CCM haimlazimishi JK kuachia Uenyekiti kwa sasa. Anao hiari kuachia au kusubiria muda wa kikatiba (miaka 5). Kwa maoni yangu JK aendelee ili Magu apate fursa ya kujifunza uimara na udhaifu wa chama chake, CCM.

Mwenyekiti wa sasa JK akiendelea na wadhifa huo rais Magufuli atashindwa kufanya kazi yake ipasavyo kichama na kiserikali.

Nadhani utanielewa kwa hoja hiyo.
 
Ni vigumu sana kuibomoa ccm Jk akiwa bado ni mwenyekiti. Ila akikabidhi kijiti kwa Magu, Nina imani ccm no longer to stand as u see
naoana mnamkubali sana mwana CCM nguli na jemedali wa vita Jakaya Mrisho Kiwete, safi sana wazungusha mikono naona mnaanza kupona
 
Yale ya Profesa Mwandosya yanatimia aliyosema..."mtu hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa tawi,unakuja kumpa uenyeketi wa ccm taifa?!" Naona Gwajima alitumwa na poti wake atishie marais wastaaf eti wakimnyima uenyekiti wa ccm na yeye anapeleka muswada bungeni marais wastaafu washtakiwe mahakamani kwa makosa waliyoyafanya wakati wakiwa madarakani,its okay...lakini akumbuke yaliyomkuta Chiluba...
 
Katiba ya CCM haimlazimishi JK kuachia Uenyekiti kwa sasa. Anao hiari kuachia au kusubiria muda wa kikatiba (miaka 5). Kwa maoni yangu JK aendelee ili Magu apate fursa ya kujifunza uimara na udhaifu wa chama chake, CCM.
There's no way JK anaweza kukubali kuendelea na Uenyekiti wa CCM though wenye chuki nae wanaamini (kwa chuki tu) kwamba eti ni yeye ndie anayeng'ang'ania Uenyekiti!

Pamoja na hizi porojo zinazoendelea, JPM atapewa Uenyekiti wa chama very soon. Hata hivyo, kuongoza CCM ni ngumu kuliko kuongoza nchi... hii ndiyo changamoto ambayo JPM anatakiwa kuifahamu!
 
Lkn wako sahihi si lazima mwenyekiti Wa chama awe rais, nakumbuka jaji ramadhan kunakipindi aliliongelea hili,
 
There's no way JK anaweza kukubali kuendelea na Uenyekiti wa CCM though wenye chuki nae wanaamini (kwa chuki tu) kwamba eti ni yeye ndie anayeng'ang'ania Uenyekiti!

Pamoja na hizi porojo zinazoendelea, JPM atapewa Uenyekiti wa chama very soon. Hata hivyo, kuongoza CCM ni ngumu kuliko kuongoza nchi... hii ndiyo changamoto ambayo JPM anatakiwa kuifahamu!

Mkuu,umesoma hiyo habari hapo juu mstari kwa mstari?
 
Mwisho wa CCM utakuja siku urais wa nchi na uenyekiti wa Chama vitakapotenganishwa!! Anayeota kutengamisha urais na uenyekiti, anaota ndoto ya kuiua CCM. Hiwezi kumvua uenyekiti wa Chama rais ukategemea kuwa Mwenyekiti asiyekuwa na madaraka ya dola atabaki na nguvu aliyonayo.

Mwenyekiti wa Chama asiyekuwa na nguvu ya Dola siku zote atakuwa ni subordinate kwa rais ambaye hana Chama Bali ana dola. Nyerere aliweza kuwa Mwenyekiti bila dola sababu yeye hata alipokuwa nje ya urais dola ilikuwa ikimtii. CCM wakijaribu hiyo kitu kwa mtu mwingine yeyote (much less Kikwete aliyezomewa na halmashauri kuu ya CCM aliyoiteua mwenyewe) utakuwa ndo mwisho wa CCM. Inaweza ikawa jambo jema kwa nchi though! Ingawa si automatic.
 
Back
Top Bottom