QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Ila jamaa akipata muda huwa harembi, anashushaga mzigo wa kutosha. Hawezi kutuangusha, tumuamini. Nadhani saa bado yupo kwenye majukumu mengine ya kimaisha. Tuwe na subira.
 
kweli mkuu, akilazimishwa huwa anaharibu jumla, alichokifanya kwenye Peniela kilileta masikitiko. Tumuache alete kwa wakati atakaoona yeye unafaa. Tukimshurutisha tutajuta.
Mh. Ndio maana mi nazurula zurula tuu humu, nikikutana nayo inshalah

Siwezi mlazimisha asee

Alichonifanyia kwa Peniela sito msahau huyu kijana
 
kaeni mkao wa kula story nyingine toka kwa mtunzi yule yule aliyetunga peniela now kaja na kitu kiitwacho queen monica. kutana na kijana AUSTIN JANUARY mtanashati na jasusi hatari anafanya mambo makubwa sana.

ALBERTOS kundi hatari linalotaka kuitawala dunia limeingia pia tanzania
Duh, PATRICK CK namkubali sana, asije haribu mwishoni tu
 
SEHEM YA KWANZA

Kumepambazuka tena na habari
kubwa iliyotawala mitandao ya kijamii na
katika vyombo mbali mbali vya habari
Tanzania asubuhi hii ni habari
iliyochapishwa katika jarida la The Face
ambalo ni maarufu kwa habari za mitindo
na urembo duniani ,inayohusiana na
matokeo ya utafiti uliofanyika barani
afrika kuhusu masuala ya urembo.
Ukurasa wa mbele wa jarida hili
maarufu ulipambwa na picha kubwa ya
mwanamke wa kiafrika mwenye uzuri
uliotukuka akiwa ndani ya tabasamu
kubwa na huku kukiwa na maandishi
makubwa yaliyosomeka QUEEN OF
AFRICA.
Ukurasa wa nne wa jarida hili
kuliandikwa habari ndefu inayohusiana
na picha ile ya yule mwanamke
aliyeupamba ukurasa wa mbele.Habari
hiyo ilielezea kwa kina kuhusiana na
matokeo ya utafiti uliofanywa na jarida
hilo barani afrika matokeo yaliyoonyesha
kuwa msichana Monica Benedict
Mwamsole anayetokea Tanzania ambaye
picha yake iliwekwa katika ukurasa wa
mbele wa jarida lile ndiye mwanamke
mrembo zaidi barani afrika.
Habari hii ilisababisha kuwepo kwa
mijadala mingi katika mitandao ya kijamii
na katika vyombo mbali mbali vya habari
duniani.Watu walimjadili Monica na wengi
ambao hawakuwa wakimfahamu walitaka
kumfahamu ni nani huyu msichana hadi
atajwe kuwa ndiye mrembo zaidi kuliko
wote barani Afrika.
Monica Benedict Mwamsole ana
umri wa miaka 25 .Ni mtoto wa pili na wa
mwisho kwa mzee Benedict na bi Janet
Mwamsole.Monica anatokea katika familia
iliyobarikiwa utajiri mkubwa.Baba yake
mzee Benedict Mwamsole ni mmoja wa
mabilionea wakubwa wanaotambulika na
kuheshimika ndani na nje ya nchi .Kwa
uchache tu mzee Benard anamiliki
kampuni kubwa ya usafirishaji ,kiwanda
kikubwa cha kutengeneza mvinyo wenye
soko kubwa katika nchi za ulaya,anamiliki
pia biashara nyingine kubwa kubwa ndani
na nje ya nchi.
Monica mwenye urefu wa futi 5.9 ni
msichana mwenye ngozi nyororo na
weupe wa kung’aa.Ana nywele ndefu
ambazo huzitengeneza katika mtindo wa
kipekee ambao humfanya awe na uzuri
usioelezeka.Monica amebarikiwa mwili
mzuri mwembamba wastani ambao
huwafanya wengi waamini ameufanyia
upasuaji na kuufanya uonekane vile.
Kielimu Monica ni msomi mwenye
shahada katika mahusiano ya kimataifa
.Ukiacha sifa na uzuri wa nje Monica ana
sifa za kipekee za ndani.Ni msichana
mpenda watu asiye na makuu licha ya
kuogelea katika bahari ya utajiri mkubwa
wa familia yao.Pamoja na uzuri wake
uliopelekea apewe jina la Black Angel au
malaika mweusi,Monica hakuwa na
majivuno aliongea na kila mtu
,hakuchagua mtu wala tabaka Fulani la
watu kuwa nao karibu.Aliwasikiliza wote
waliomuendea na shida mbalimbali na
kuwasaidia kadiri alivyoweza.Alikuwa na
taasisi yake aliyoianzisha kwa ajili ya
kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali
lakini akilenga zaidi watoto na wazee
wasiojiweza.Kwa ujumla Monica alikuwa
ni mwanamke mwenye sifa lukuki na
kipenzi cha watu.Alipendwa na wakubwa
na wadogo.
Alipohitimu elimu yake ya
juu,Monica alichagua kufanya kile
ambacho alikuwa anakipenda kwa dhati
toka akiwa mtoto mdogo yaani
mitindo.Alipenda sana mambo ya mavazi
na urembo hivyo alianzisha kampuni yake
inayojishughulisha na masuala ya mitindo
kampuni ambayo imeliteka soko la afrika
mashariki kutokana na aina ya mitindo ya
mavazi wanayoibuni iliyotokea kupendwa
sana na watu wengi.
Kwa ufupi huyu ndiye Monica
Mwamsole ambaye jina lake maarufu
nchini Tanzania ni malaika mweusi jina
ambalo alipewa kutokana na uzuri wake
na matendo yake.Taarifa za yeye
kutangazwa na jarida la The Face kuwa
ndiye msichana mrembo zaidi barani
Afrika
hazikuwashangaza
wengi
waliomfahamu bali walikubaliana na
matokeo ya utafiti huo na kuwapongeza
watafiti ,Monica alistahili heshima hiyo ya
kuwa mrembo wa afrika.
 
SEHEM YA PILI

Sauti ya ndege mkubwa aliyekuwa
akilia karibu na dirisha ilimstua Monica
toka katika usingizi .Huku akionekana
kukerwa na sauti ile iliyomstua usingizini
akainuka na kukaa.
“ oh no ! Huyu ndege ameniharibia
ndoto yangu tamu..” akawaza
Monica,akainuka
kitandani
na
kujinyoosha halafu akatazama saa ndogo
yenye nakshi za dhahabu iliyoko mezani
“ Ni saa mbili na robo sasa,muda
umekwenda sana natakiwa niwahi ofisini
leo nina miadi ya kuonana na Daniel
ambaye alisema atamleta rafiki yake
anayehitaji kuchangia katika mbio
tunazoziandaa.Nashukuru wadau wengi
wanazidi kujitokeza na kuniunga mkono
katika mpango wangu wa kujenga shule ya
watoto wenye mahitaji maalum.Nina
hakika jambo hili litafanikiwa kwani
limepata mwitikio mzuri kwa watu wengi
matajiri kwa wasio na uwezo.” Akawaza
huku akivaa nguo zake za mazoezi na
kujiandaa kwa ajili ya kufanya zoezi la
asubuhi.Ni kawaida yake kila aamkapo
asubuhi kutembea kwa miguu kilometa
kadhaa kabla ya kwenda ofisini.Alipokuwa
tayari akatoka na kwenda kwanza
kuwasalimu watumishi wake wa ndani
waliokuwa katika harakati zao za kawaida
za asubuhi akaongea nao mawili matatu
na kutoa maelekezo kadhaa kisha akatoka
nje na kusalimiana na kijana mtunza
mazingira na mwisho akawajulia hali
walinzi wake wanaolinda nyumba yake
halafu akaanza zoezi lake la
kutembea.Haya ndiyo maisha ya kila siku
ya Monica,kila asubuhi kabla hajafanya
chochote lazima kwanza ahakikishe
amewasalimu watu wote anaoishi nao
nyumbani kwake na kujua hali zao na
ndipo huendelea na ratiba nyingine za
siku.
“ Sikufanya makosa kuamua
kuhamia huku.Ni kuzuri ,kuna hewa safi
na utulivu wa kutosha.Japokuwa ni mbali
na mji lakini hiyo hainipi taabu
ninachohitaji mimi ni kuishi sehemu
tulivu kama hii kusikokuwa na makelele
wala uchafuzi wa hewa.Huku ninapata
hewa safi toka baharini tofauti na mjini”
akawaza Monica wakati akipanda kilima
kidogo.
“ Hata hivyo eneo hili bado jipya na
lina changamoto nyingi,miundo mbinu
bado si mizuri,hakuna maji ya
uhakika,umeme barabara n.k.Natakiwa
kukutana na wakaazi wa eneo hili na kwa
pamoja tujadili namna ya kuzitafutia
ufumbuzi
changamoto
zinazowakabili.Wanahitaji huduma za
afya,shule n.k so I must help them.I want
to change this place.Kwa sasa
panaonekana ni kijijini lakini ndani ya
miaka michache ijayo patakimbiliwa na
kila mtu .Nina ndoto ya kulifanya eneo hili
kuwa mji mzuri sana na wa kupendeza”
akawaza Monica akiendelea na mazoezi
yake
Alirejea nyumbani na moja kwa moja
akaelekea chumbani kwake akaoga na
kujiandaa kwa ajili ya kuanza shughuli
zake za siku.Alipomaliza kujiremba
akajitazama katika kioo na kutabasamu
halafu akawasha simu zake.Jumbe nyingi
zikaingia mfululizo akakaa kitandani na
kuanza kuzipitia kwa haraka haraka na
mojawapo ya jumbe hizo ulitoka kwa baba
yake ambao ulikuwa na neno moja tu
“Congraturations
” Monica akatabasamu
“ Baba ananipongeza kwa jambo
gani? Kuna chochote nimekifanya
kinachostahili pongezi? Ngoja nimpigie
niongee naye anieleze sababu ya
kunipongeza” akawaza Monica na
kumpigia simu baba yake.
“ Hallow Monica” akasema mzee
Benedict Mwamsole baada ya kupokea
simu ya Monica
“ Goodmorning dady”

Good
morning
my
sweetie,umeamkaje?
“ Nimeamka salama dady,vipi nyie
huko wote wazima?
“ Sisi sote wazima wa afya,hofu
kwako “
“ Mimi pia mzima dady.Nimepata
ujumbe wako sasa hivi” akasema Monica
huku akitabasamu
“ Nimekutafuta sana jana usiku
lakini simu yako haikuwa ikipatikana
ndiyo maana nikakutumia ujumbe
ule.Bado hujaacha tabia yako ya kuzima
 
SEHEM YA TATU

simu usiku” akasema mzee Ben.Monica
akacheka kidogo na kusema
“ C’mon dady,you know me.Nina kazi
nyingi mchana kutwa kwa hiyo ikifika
usiku kichwa changu na mwili vyote
vinakuwa vimechoka mno that’s why
when I go to bed I switch off everything.By
the way you congraturated me,hongera
kwa jambo gani baba? Akauliza Monica
“ Ina maana bado hujapata habari?!!
Akauliza mzee Ben
“ Habari zipi baba? Kama
nilivyokwambia kwamba mimi huzima
kila kitu usiku na halafu mimi si mpenzi
sana wa kutazama taarifa za habari katika
luninga kwani taarifa nyingi zimejaa
mambo ya siasa na mimi kama
unavyonijua I hate politics.Kuna taarifa
gani kwani? Akauliza Monica kwa
wasiwasi kidogo
“ Monica unatakiwa uachane na huo
utaratibu wako wa kuzima simu usiku na
ujenge pia utamaduni wa kufuatilia
vyombo vya habari”
“ Kwani kuna nini baba? Akauliza
Monica
“ Too bad kama bado mpaka sasa
hujapata taarifa.Ni kwamba umetangazwa
na jarida la The face la Marekani katika
toleo lake la mwezi huu lililotoka jana
usiku kwa huku kwetu ambayo ni mchana
kwao kwamba wewe ndiye msichana
mrembo zaidi barani afrika.Hongera sana
Monica.You deserve it” akasema mzee Ben
“ What?? That cant be true..Me?
Monica akashangaa
“ kweli Monica.You are the most
beautifull woman in Africa.Your beauty is
amazing and I’m so proud of you” akasema
mzee Ben
Macho ya Monica yakaanza kuloa
machozi
“ Monica !! akaita mzee Ben
“ Naam baba” akaitika Monica huku
akifuta machozi
“ Ouh Monica you are crying again “
“ I’m sorry dady si unajua machozi
yangu yako karibu.Ninapokuwa na furaha
iliyopitiliza hujizuia kushindwa kutoa
machozi” akasema Monica
“ Sawa Monica basi endelea na
shughuli zako ila napenda tu kukutaarifu
kwamba tunaandaa sherehe ya
kukupongeza kama familia kwa jambo hili
kubwa” akasema Ben
“ Ahsanet Dady.See you later “
akasema Monica na kukata simu akavuta
pumzi ndefu na kuinua mikono yake
akatazama juu
“ Oh my God who am I to deserve all
these? Akasema Monica halafu akaiwasha
kompyuta yake na kuingia mtandaoni ili
kuthibitisha kile alichoambiwa na baba
yake. Katika akaunti yake ya barua pepe
kulikuwa na ujumbe toka kwa uongozi wa
jarida la The Face ambao walimtaarifu
kuwa kutokana na utafiti wao walioufanya
barani afrika kwa muda wa miezi kumi na
moja yeye ameonekana kuwa ndiye
mwanamke mrembo kuliko wote barani
afrika.Walimueleza kwa krefu kuhusiana
na namna walivyofanya utafiti wao na kwa
namna yeye Monica alivyoweza kuibuka
kuwa mrembo zaidi Afrika.Mwisho
walimtaarifu kuwa watatuma timu ya
wawakilishi wao waje kuonana na Monica
ikiwa ni pamoja na kumkabidhi zawadi
yake ya ushindi na kuzungumza naye
masuala kadhaa yanayohusiana na
mitindo afrika.Walimtumia pia nakala ya
tolea lililotoa matokeo hayo.Nje ya jarida
lile kulikuwa na picha kubwa ya Monica
akiwa katika tabasamu
“ oh my Gosh its true.....its true...”
akasema kwa furaha huku michirizi ya
machozi ikionekana mashavuni pake.
“ Dah ! siku yangu imeanza kwa
furaha namna hii.Sikutegemea kabisa
kama jambo hili lingetokea.Najifahamu
mimi ni mzuri lakini sikuwahi kuota kuwa
siku moja nitaweza kutangazwa kuwa
mrembo kuliko wote afrika.Nakumbuka
watu wa jarida la The Face waliwahi kuja
kuniona nikaongea nao nikawaeleza
shughuli zangu,wakanihoji mambo mengi
kuhusiana na maisha yangu na wakanipiga
picha nyingi za kutosha ila sikufahamu
kama walikuwa katika utafiti.Mimi
nilidhani walikuwa katika mojawapo ya
kazi zao za kila siku za kukusanya taarifa
za mitindo na urembo. Walitakiwa
waniweke wazi nini walichokuwa
wanakifanya kuliko kunistukiza namna hii
lakini hata hivyo I’m happy.Wamenifanya
nijulikane ghafla sana duniani.Oh my God I
real don’t know how to thank you for this
...” akawaza Monica na kurekebisha poda
usoni akatoka na kwenda moja kwa moja
katika chumba cha chakula ambako tayari
kulikwisha aandaliwa stafstahi.Alikunywa
chai haraka haraka na kisha akaagana na
watumishi wake akaondoka kwenda
kazini
 
SEHEM YA 4

ENDELEA.........
Mzee Benedict Mwamsole baada ya
kumaliza kuongea na mwanae Monica
simuni akamgeukia mke wake na wote
wawili wakatazamana na kutabasamu
“ Mbona unanitazama hivyo Ben?
Akauliza Bi Janet Mwamsole .Ben
akambusu mkewe na kusema
“ Monica amerithi uzuri wako .Yeye
ni mrembo afrika nzima lakini wewe ni
mrembo wa dunia nzima.Una uzuri wa
kipekee kabisa” akasema mzee Benedict
“ Thank you Ben” akasema mke
wake
“ Halafu kuna kitu kingine
umebarikiwa nacho ambacho wengi
hawana”
“ Kitu gani hicho Ben?
“ Huzeeki.Umri umesogea sana lakini
bado unaonekana ni kama vile una miaka
thelathini .Tazama mimi karibu kichwa
changu chote kitakuwa cheupe kwa mvi
lakini wewe bado unaonekana
mbichi.Unajua sana kujitunza na jambo
hili umemuambukiza hata mwanao
Monica anajua kujitunza na ndiyo maana
ameweza kuonekana mrembo zaidi ndani
ya mamilioni ya wasichana warembo
barani afrika.” Akasema mzee Ben na
kumbusu mke wake
“ Ben unajua sana namna ya
kunifanya nitabasamu.Maneno yako
huniingia taratibu na hujikuta nimehama
kifikra toka katika dunia hii na kujiiona
niko katika ulimwengu mwingine
kabisa.Umebarikiwa kinywa chenye
maneno matamu .Nadhani hata mwanao
Nathani amerithi hilo toka kwako na ndiyo
maana amekuwa anapapatikiwa na
wanawake kila kukicha.Ana maneno
matamu kuweza kumlainisha mwanamke
yeyote”
Mzee Ben akajikuta akiangua
kicheko kwa maneno yale ya mke wake
“ Unanifurahisha sana Janet.Hao
wanawake wanaompapatikia Nathani si
kwa sababu ya maneno yake matamu bali
kwa pesa zake.Nathani bado ni kijana na
anapenda sana starehe.Ukiwa na pesa
huhitaji kuwa na maneno matamu ili
kumpata mwanamke mrembo bali pesa
huongea yenyewe bila hata ya wewe
kufumbua mdomo wako utakipata kile
unachokihitaji.Hata hivyo nadhani ni
wakati muafaka sasa wa kukaa na
kumkanya Nathani kuhusiana na tabia
yake
ya
kuendekeza
starehe
kupindukia.Tukimuacha aendelee namna
hii mwisho wake hautakuwa mzuri hata
kidogo.Umri unakwenda na anatakiwa
atafute msichana mmoja mzuri atulie naye
kuliko kuruka ruka anakofanya sasa
hivi.Isitoshe sisi tumekwisha kuwa wazee
anatakiwa ajiandae kusimamia miradi
yetu kwani yey endoye mtoto mkunwa“
akasema mzee Ben
“ Hilo unalosema Ben ni la
kweli.Huyu mtoto tunatakiwa tumkanye
aachane kabisa na tabia yake hii mbovu
ya kubadilisha wanawake kama
nguo.Halafu vipi kuhusu huyu Monica?
“ Monica ana nini ? akauliza Ben .Bi
Janet akainuka na kukaa mzee Ben naye
akafanya hivyo
“ Monica ana miaka 25 hivi
sasa,tayari ana kila kitu katika maisha
yake
na
hakuna
kitu
anachokikosa.Kinachonipa wasi wasi ni
kwamba amekuwa mgumu sana kuweka
wazi masuala yake ya kimahusiano.Mpaka
leo hii mimi sifahamu mwanaume wake ni
yupi ,hatujui nini mipango yake kuhusu
jambo hili? Nafahamu sera yetu ni
kutokuingilia masuala binafsi ya watoto
hususan mahusiano lakini nimeanza
kuingiwa na woga kwa sasa baada ya
Monica
kupata
umaarufu
mkubwa.Wanaume watamsumbua sana na
wengi watakaomfuata ni watu wenye pesa
ambao hutumia nguvu yao ya pesa
kuwarubini wanawake na kuwapata
kimapenzi.Nina wasi wasi mwanangu
anaweza kushindwa kumpata mwanaume
mzuri wa ndoto zake .Ninahitaji Monica
ampate mwanaume mzuri mwenye
kumpenda kwa dhati na ambaye
atamfanya awe na furaha siku zote katika
maisha yake “ akasema Bi Janet Mzee Ben
akakuna kichwa kidogo na kusema
“ Hilo unalolisema ni la kweli
kabisa.Monica anatakiwa awe muangalifu
sana kwa sasa baada ya kupata umaarufu
mkubwa.Umaarufu ni kama ua lenye
harufu nzuri ambalo huwavutia nyuki
kulifuata na kuchukua asali na utamu
ukiisha huliacha ua likinyauka na
kupukutika mtini.Wanaume hasa wenye
pesa ni sawa na nyuki ambao huvutika na
uzuri na umaarufu wa msichana na
hutumia nguvu yao ya fedha kumpata na
wakisha fanikisha haja zao humuacha na
kwenda kutafuta wanawake wengine
kama nyuki wanavyoliacha ua lililoisha
utamu na kwenda kutafuta au
lingine.Monica anatakiwa awe makini
sana.Hata hivyo.....” akasema mzee Ben na
kunyamaza kidogo kana kwamba kuna
kitu anakikumbuka
“ Nini Ben ? akauliza mkewe
“ Kuna kitu nimekumbka.Monica ana
ukaribu sana na Yule Daniel mtoto wa
mzee Swai.Unamuonaje Yule kijana
anaweza kumfaa Monica? Ni kijana msomi
ana sura nzuri,ana adabu na familia yao ni
watu wa karibu sana na sisi isitoshe ni
watu matajiri .Nadhani Daniel ni kijana
mzuri kwa Monica.Unaonaje kuhusu hilo?
Bi Janet akaguna na kumtazama Ben
kwa macho makali
“ You don’t know anything about that
guy!!
“ Kwani Daniel ana tatizo gani?
Mbona mimi namuona ni kijana mzuri tu ?
 
SEHEM YA 5

“ Daniel is a snake.!! Hafai kabisa
Yule kijana kuwa hata na ukaribu na
Monica.Baada ya kugundua ukaribu wake
na Monica nilimfanyia uchunguzi
nikagundua kuwa ni kijana mshenzi
sana.Ana tabia chafu mno.Ana wanawake
karibu kila kona ya jiji.Anawabadilisha
wanawake kama nini sijui.Daniel hafai
hafai kabisa tena nina mpango wa
kumuonya Monica aache kabisa kuwa
karibu naye” akasema Bi Janet huku sura
yake ikionyesha wazi alikwisha anza
kukasirika
“ Dah ! sikuwa nikifahamu tabia zake
kama ni hizo.Anyway tuachane na hayo
mambo tutazungumza siku nyingine
nataka tujadili namna ya kuandaa sherehe
ya kumpongeza Monica kwa mafanikio
haya
makubwa
aliyoyapata.Hiki
walichokifanya The Face kumtaja kuwa
ndiye mwanamke mrembo zaidi afrika ni
suala kubwa hii ni bahati kubwa kwa
familia yetu kwa hiyo lazima tufanye
sherehe kubwa ya kumpongeza”
“ Sawa ben niachie mimi suala hilo
nitalishughulikia” akasema Bi Janet
*****************
Monica aliwasili katika jengo zilimo
ofisi zake.Ni jengo la ghorofa mbili
analolimiliki yeye mwenyewe.Kama ilivyo
kawaida yake akasalimiana na walinzi
wake baada ya kushuka garini pamoja na
baadhi ya wafanyakazi waliokuwa nje
kisha akaingia ndani.Mapokezi hakukuwa
na mtu akapanda moja kwa moja katika
ghorofa ya kwanza ambako kazi zote za
ubunifu hufanyikia hapo lakini hakukuwa
na mtu ila kompyuta karibu zote
zilikwisha washwa .Monica akashangazwa
kidogo kwa hali ile
“ Where is everyone? akajiuliza na
kuchukua simu akataka kupiga mara
akatokea Jesica mmoja wa wafanyakazi
aliyekuwa akihema kwa kasi..
“Madam ..!! akaita Jessica
“ Jessica kuna nini mbona hivyo?
“ Madam its Linah ..!! akasema
Jessica na kumstua Monica
“ Linah ?? amefanya nini? Akauliza
Monica kwa wasi wasi
“ Ameanguka ghafla .Twende
ukamuone..” akasema Jessica na kugeuka
akaanza kutembea haraka haraka Monica
akiwa nyuma yake
“ nini kimemtokea Linah? Akauliza
Monica lakini Jessica hakumjibu
kitu.Walipanda hadi katika ghorofa ya pili
kulikokuwa na ofisi ya Monica pamoja na
ukumbi mdogo wa mikutano.Jessica
akaufungua mlango wa ukumbi ule mdogo
wa mikutano kwa kasi akaingia
ndani,Monica naye aliyekuwa amkimfuata
nyuma akaingia kwa kasi na mara
akakutana na kitu ambacho hakuwa
amekitarajia..
“ Surprise !!!!... ikasikika sauti kubwa
toka kwa wafanyakazi waliokuwa
wamekaa katika mojawapo ya kona ya
ukumbi ule wakiwa na nyuso zenye furaha
.Linah msaidizi wa Monica alikuwa
amesimama mbeye yao akiwa na maua
huku akiwa na tabasamu zito
“ Oh my Gosh !!..akasema Monica
kwa mshangao ..Taratibu Linah
akamsogelea Monica na kumpa maua
“Congraturations queen of Africa”
akasema Linah .Kwa mara nyingine
Monica
akajikuta
akimwaga
machozi.Alikuwa
na
furaha
iliyopitiliza.Wafanyakazi
wake
walimpongeza kwa kutangazwa kwake
kuwa ndiye mrembo kuliko wote
afrika.Baada ya pongezi Monica akaomba
aongee machache
“ Thank you..!! akasema Monica na
kufuta machozi
“ Thank you so much for this
wonderfull surprise.Nimefurahi kupitiliza
na ndiyo maana mnaona machozi
yananitoka.Ahsanteni sana ndugu zangu”
akanyamaza akafuta machozi na
kuendelea
“ Hiki kilichotokea kwa mimi
kutangazwa kuwa mrembo kuliko wote
Afrika ni mafanikio ya juhudi
zenu.Nimeonekana mimi kwa sababu
ninyi ndio mlioniinua na kunifanya
nionekane kwa hiyo ushindi huu ni wa
kwenu ninyi.Mnatakiwa mjipongeze papo
hapo napenda kuwaasa kuwa tunatakiwa
kuongeza bidii ya kazi ili tufike mbali zaidi
ya hapa tulipofika.Tutakaa pamoja na
kujadili namna tutakavyoweza kuitumia
fursa hii iliyojitokeza lakini kwa sasa
tufungue shampeni na tugonganishe glasi
tutakieni heri na kupongezana kwa
mafanikio haya makubwa” akasema
Monica.Shampeni ikafunguliwa wote
wakashangilia halafu kila mmoja akaenda
kuendelea na kazi.Monica aliingia ofisini
kwake akajiegemeza kitini hakuwa na
hamu ya kufanya kazi yoyote.
“ Why me Lord? Katika wanawake
wote hawa wa afrika wenye uzuri
usioelezeka why me? Akajiuliza Monica
akainuka na kuanza kuzunguka zunguka
mle ofisini na mara siku ya mezani ikaita
akaunyanyua mkono wa simu
“ Hallow “ akasema
“ Madam kuna wageni wako hapa
mapokezi”
“ Ni akina nani?
“ Ni Mr Daniel na mwenzake”
“ Ok waruhusu waje moja kwa moja”
akasema Monica halafu kwa haraka
akaingia katika kijichumba kidogo
kilichomo ndani ya ofisi yake ambacho
hukitumia kujirembea akarekebisha poda
usoni na kutoka tayari kuwapokea wageni
wake.Baada ya dakika kama nne hivi
mlango ukagongwa akaruhusu mgongaji
 
SEHEM YA 6

aingie ndani na ndipo walipojitokeza
vjana wawili watanashati.Daniel Swai na
mwenzake..
“ Karibuni sana” Monica
akawakaribisha wageni wake katika sofa
nzuri zilizokuwamo mle katika ofisi
yake.Muhudumu akafika na kuwakirimu
wageni kwa vinywaji na maongezi
yakaanza.Daniel ndiye aliyeanzisha
maongezi
“ Monica huyu ni rafiki yangu
anaitwa Dr Marcelo Richard.Yeye kama
atakavyojieleza mwenyewe anayo taasisi
yake ya kuwahudumia wagonjwa wenye
matatizo ya saratani ya damu. Baada ya
kumueleza kuhusiana na jambo
unalokusudia kulifanya naye akajikuta
ameguswa na akaomba aje atoe mchango
wake..” akasema Daniel halafu
akamgeukia Dr Marcelo
“ Dr Marcelo huyu ni rafiki yangu
anaitwa Monica Mwamsole ambaye Jarida
la The Face limemtaja kuwa ndiye
mrembo kuliko wote barani Afrika.”
Akafanya utambulisho Daniel halafu
akainuka na kwenda kumpa mkono
Monica
“ Hongera sana Monica kwa
mafanikio haya makubwa.Unastahiili
kuvishwa taji hilo” akasema Daniel na
wote wakacheka.
“ Ahsante sana nashukuru.Nimeweza
kuonekana kutokana na uungwaji mkono
toka kwa wadau kama ninyi ambao kila
mara mmekuwa mstari wa mbele
kuniunga mkono kwa kila jambo”
Akasema Monica halafu akainuka na
kumfuata Dr Marcelo
“ Dr Marcelo nafurahi sana
kukufahamu.Karibu sana .Hapa ndipo
ofisini kwangu.Nina kampuni yangu
inayojishughulisha na masuala ya ubunifu
wa mitindo ya mavazi vile vile ninayo
taasisi inayojishughulisha na matatizo
mbali mbali yanayowahusu watoto
wadogo
na
wazee
wasiojiweza.Nitakutembeza uone namna
kazi zinavyofanyika hapa.Huyu mwenzio
Daniel yeye ni mwenyeji hapa anakuja
mara kwa mara,ni rafiki yangu wa siku
nyingi toka tukiwa wadogo “ akasema
Monica.Dr Marcelo akatabasamu na
kusema
“ Nashukuru sana Monica kwa
makaribisho mazuri.Daniel alinieleza
kuhusiana na jambo ulilokusuidia
kulifanya nikaguswa na nikaomba anilete
kwako ili niweze kufahamu kwa undani
zaidi juu ya jambo lenyewe na vile vile
mimi na taasisi yangu tuweze kutoa
mchango wetu kwa hiyo naomba katika
orodha yako ya wadau uniongeze na
mimi.” Akasema Dr Marcelo
“ Ahsante sana Dr Marcelo kwa kuwa
mmoja wa wadau wangu.Karibu
sana.Mchango wa wadau kama ninyi
unahitajika sana”
“ Usijali kuhusu hilo Monica tuko
pamoja..” akasema Dr Marcelo halafu
ukapita ukimya mfupi wa sekunde kadhaa
“ Taasisi yako inashughulika na
masuala gani? akauliza Monica
“ Taasisi yangu inajishughulisha na
kuwahudumia
wagonjwa
wanaosumbuliwa na saratani ya
damu.Tuna hospitali tunakowatibu
wagonjwa hawa ambayo ni kumbu
kumbgu ya baba yangu Dr Richard
aliyefariki kwa maradhi hayo ya saratani
ya damu”
“ Ouh I’m so sorry “ akasema
Monica.Baada ya sekunde kadhaa Dr
Marcelo akaendelea
“ Hospitali yetu ina wagonjwa zaidi
ya themanini tunaowahudumia kwa
sasa.Hatuna wafadhili wa nje bali ni
hospitali inayosimamiwa na familia
japokuwa tunapata msaada kidogo kutoka
serikalini lakini hilo si tatizo kwetu kwani
kama familia tumekwisha azimia
kulifanya hilo kumuenzi baba yetu
aliyefariki kwa maradhi hayo ya saratani
ya damu kwa hiyo tunatumia kila
tunachokipata kutoka katika miradi
kadhaa ya familia kuwahudumia
wagonjwa katika hospitali yetu.” Akasema
Dr Marcelo
“ Hongera sana Dr Marcelo kwa
namna wewe na familia yako mlivyojitolea
kuwahudumia wagonjwa hao wenye
mahitaji makubwa.Matibabu ya saratani ni
ghali sana lakini ninyi mnajinyima na
kuwahudumia
wagonjwa.Mungu
atawabariki kwa hilo mnalolifanya.Sisi
sote tuna malengo yanayofanana.Mimi na
taasisi yangu tunataka kujenga shule kwa
ajili ya watoto wenye mahitaji maalum
ambao wana ulemavu wa kutoona na
kutosikia.Tumegundua idadi ya watoto
wenye ulemavu wa aina hii imeongezeka
zaidi kwa hiyo tumeamua kujenga shule
maalum kwa ajili yao kwani changamoto
wanazozipata ni nyingi sana.Ili
kulifanikisha hilo tunahitaji kiasi kikubwa
cha pesa ndiyo maana tumekuwa tunapita
kwa wadau mbali mbali ili kuomba
misaada yao ya hali na mali.” Akasema
Monica na kwenda kufungua kabati kubwa
akatoa makaratasi manne makubwa yenye
picha za majengo ya shule wanayotazamia
kuijenga akamuonyesha Dr Marcelo .
“ Kwa hiyo Dr Marcelo majengo
tunayokusudia
kuyajenga
ndiyo
haya.Pamoja na kuzunguka kwa wadau
mbalimbali kuomba msaada lakini kuna
mambo kadhaa amabyo tumekusudia
kuyafanya ili kuweza kutunisha mfuko
wetu wa ujenzi.Kwanza tumeandaa mbio
za nusu marathoni ambazo zitakuwa ni
maalum kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa
shule hiyo.Wadau mbalimbali tayari
wamekwisha jitokeza kutuunga mkono na
kujiandikisha kushiriki katika mbio hizo.
Baada ya mbio hizo tutaandaa pia onyesho
 
SEHEM YA 7

la mavazi ambalo nalo lengo lake ni hilo
hilo kukusanya fedha kwa ajili ya shule
hiyo na mwisho kabisa tutaandaa chakula
cha usiku maalum kwa ajili ya lengo hilo
pia tutawaalika watu mbali mbali,viongozi
na makampuni, hata wewe na taasisi yako
mtaalikwa pia.Tuna imani kabisa baada ya
kukamilisha mipango hiyo tutakuwa
tumekusanya kiasi cha kutosha cha fedha
tayari kabisa kuanza ujenzi.Kwa hiyo
wewe na taasisi yako mtachagua mnataka
kushiriki katika tukio gani aidha
mbio,nyesho la mavazi , chakula cha usiku
au vyote” akasema Monica na wote
wakacheka.
“ Monica pamoja na kwamba tuna
mzigo mkubwa mimi na familia yangu
kuwahudumia agonjwa wa saratani kama
nilivyokueleza lakini kwa jambo kubwa
kama hili la kuchangia ujenzi wa shule
hiyo ya watoto wenye mahitaji maalum ni
jambo kubwa na la msingi sana ambalo
lazima tulichangie.Mimi na taasisi yangu
tutashirki katika matukio yote matatu
kuanzia mbio hadi chakula cha usiku.”
“ Nashukuru sana Dr Marcelo”
akasema Monica.
“ Katika hizi mbio mlizoziandaa
kwanza kabisa tutachangia kiasi cha
shilingi milioni themanini na vile vile
tutatoa msaada wa kitabibu kwa washiriki
wote watakapopata matatizo yoyote
wakati wa mbio hizo.Matibabu yote
tutayatoa bure kabisa.Katika onyesho la
mavazi pia tutatoa mchango wetu na
katika
chakula
tutachangia
pia.Tutashirikiana bega kwa bega
kuhakikisha jambo hili linafanikiwa.”
Akasema Dr Marcelo.Monica akainuka na
kumpa mkono Dr Marcelo.
“ Ahsante sana Dr Marcelo
.Nashukuru sana kwa msaada huo
mkubwa.Wadau kama ninyi mnahitajika
sana ili kuwasaidia watu wenye matatizo
mbali mbali” akasema Monica.Bila
kupoteza wakati Dr Marcelo akatoa kitabu
cha hundi katika mkoba wake na
kuandika hundi ya shilingi milioni
themanini akamkabidhi Monica.
Baada ya maongezi ya zaidi ya saa
moja Monica akawachukua Daniel na Dr
Marcelo akawatembeza sehemu mbali
mbali za jengo lile na kuwaonyesha kazi
wanazozifanya pamoja na hatua mbali
mbali za ubunifu wa mavazi.Baada ya
kuzungukia sehemu zote wakaagana
Daniel na Dr Marcelo wakaingia katika
gari lao na kondoka,Monica akarejea
ofisini kwake.
“ Ahsante Mungu kwa uungwaji
mkono mkubwa ninaoupata toka kwa
wadau mbali mbali.Najua jambo hili
litafanikiwa kwa nguvu zako.Endelea
kuwawezesha wadau mbali mbali wazidi
kujitokeza wajitolee michango yao ili
tuweze kukulifanikisha jambo hili la
kujenga shule ya watoto wenye mahitaji
maalum.” Monica akaomba na mara
akamkumbuka Dr Marcelo
“ Wengi wananiunga mkono lakini
Dr Marcelo na taasisi yake wametoa
mchango mkubwa kupita wote.Ningepata
wadau kumi kama hawa ningepiga hatua
kubwa sana katika jambo hili” akawaza
na kutabasamu
“ He’s so handsome.Ni mpole na ana
moyo wa huruma .Hata hivyo yeye na
familia yake wanaonekana ni watu wenye
kujiweza sana kifedha na ndiyo maana
wameweza kumudu kuwahudumia watu
wenye matatizo ya saratani ya
damu.Nimefurahi sana kukutana na mtu
mwenye malengo na mtazamo kama wa
kwangu.Sote tuna lengo moja la
kuwahudumia watu wenye matatizo mbali
mbali.” Akawaza Monica
 
SEHEM YA 8

Dr Marcelo umemuona Monica?
Akauliza Daniel wakiwa garini baada ya
kuondoka ofisini kwa Monica.Dr Marcelo
akatabasamu na kusema
“ Nimemuona.She’s hot.She’s an
angel.Anastahili kabisa kuwa mrembo
kuliko wote Afrika.” Akasema Dr Marcelo
na kumfanya Daniel aangue kicheko
“ Kwa kweli anastahili.Ni msichana
mwenye uzuri wa kipekee kabisa wa
ndani na nje.Waliomtaja kuwa mrembo wa
afrika hawakukosea.” Akasema Daniel na
kimya kifupi kikapita.Baada ya sekunde
kadhaa Daniel akasema
“ To be honest I love that woman so
much .Nimekutana na wanawake wengi
sana lakini kati ya hao wote hakuna kama
Monica.I’m a champion when it comes to
women lakini kwa Monica nadhani kuna
dalili za kugonga mwamba.Si mwanamke
rahisi kama nilivyodhani.Nimekuwa naye
karibu kwa muda mrefu nimejaribu
kutumia kila aina ya ufundi nilio nao
kumpata lakini sijafanikiwa ila sijakata
tamaa nitafanya kila linalowezekana hadi
Monica awe wangu.” Akasema Daniel.Dr
Marcelo hakusema kitu akabaki
kimya.Alionekana kuzama katika mawazo
ya ghafla.
“Daniel
ana
haki
ya
kuchanganyikiwa kwa uzuri wa Monica.
Kwa muda mrefu amekuwa akimsifia sana
Monica kuwa hajawahi kuona msichana
mrembo kama yeye leo nimeamini
maneno yake.Monica ni kifaa
hasa.Nilipomuona tu mwili wangu wote
ukanisisimka nikaingiwa na baridi ya
ghafla.Utadhani ninatazamana na malaika
kumbe ni mwanadamu mwenzangu.”
Akawaza Dr Marcelo
“ Baada ya kumuona Monica leo
naona
kama
akili
yangu
imechanganyikiwa kabisa na ninahisi
kumpenda ghafla. Nimesisimkwa mno na
sijui kama nitaweza kuendelea na
msimamo wangu wa kutojiingiza katika
mahusiano ya kimapenzi.Nahisi kuna
nguvu Fulani iliyonisukuma kutaka
kuonana na Monica.Yawezekana kuonana
kwetu ni kwa sababu maalum” akawaza na
kumtazama Daniel aliyekuwa akiongea na
simu na mmoja wa wanawake zake
“ Daniel anakiri kwamba anampenda
sana Monica na ameahidi kufanya kila
linalowezekana
hadi
ahakikishe
anampata.Namfahamu vizuri huyu jamaa
ni kijana mchafu sana wa tabia na siku
zote amekuwa akitumia utajiri wake
kuwapata na kuwachezea wanawake
wengi tu hapa mjini .Ni mtu mwenye
tamaa ya ajabu sana na akisha timiza haja
zake humuacha mwanamke na kwenda
kutafuta mwingine.Sintokubali afanye
hivyo kwa Monica.Hawezi kupeleka
uchafu wake kwa mwanamke malaika
Yule.Monica
hastahili
kabisa
kuchezewa.Daniel tayari amekwisha
watoa machozi wanawake wengi tu hapa
mjini na sintakubali hata kidogo amtoe
machozi Monica.Mwanamke kama Yule
anastahili mtu mwenye kumpenda kwa
dhati ambaye hatamtoa chozi.She
deserves someone like me ambaye
nitamtunza na kumlinda kama mboni ya
jicho langu lakini tatizo ni hii saratani...”
akanyong’onyea ghafla
“ Safari hii nitauvunja mwiko na
nitajiingiza katika mapenzi.Monica
ameustua sana moyo wangu.Potelea mbali
litakalotokea na litokee tu lakini lazima
niwe na Monica kwani nahisi ndiye
mwanamke wa maisha yangu.Kuhusu
Monica na Daniel lazima niuvuruge
uhusiano wao kwani sitaki kabisa huyu
jamaa aendelee kuwa karibu na
Monica.Najua kunaweza kutokea uadui
mkubwa kati yetu lakini sijali hilo ,kama
tukiwa maadui na iwe lakini nitafanya kila
niwezalo kwanza kumlinda Monica na pili
kuhakikisha ninampata na anakuwa
mpenzi wangu hata kama ni kwa kipindi
kifupi“ akawaza Dr Marcelo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom