Punguzo la PAYE: Kikwete alitabiri sifa atapata Rais anayemfuatia

Mkuu pamoja na mazuri mengi ya JK, lakini alipwaya vibaya kiutawala.
Hata panya wasiodhibitiwa walitetemesha pote walipopita, na kuneemeka kwa kula mali za wananchi.
Yeye alikuwa 50% ya muda wake yuko majuu akila bata.
Wengine tulionya hili , kuwa muda mwingi JK yuko majuu, kazi yake Ikulu nani anaifanya?
Ni kweli Kikwete alishindwa kuonesha nguvu za serikali. Mwalimu Nyerere akiwa raisi aliwahi kukiri kuwa serikali ina nguvu sana na akawashauri watu wasifanye mchezo na serikali. Alisema wazi kuwa serikali inatumia nguvu kwenye mambo yake na haibembelezi mtu. Kikwete alipenda mno dialogue kupita maelezo. Kama ni sheria zimevunja na wananchi kwa mfano kujenga kwenye hifadhi ya barabara huhitaji dialogue, kama serikali inahitaji eneo fulani kwa ajili ya uwekezaji huhitaji dialogue, ni utekelezaji kwa kufuata sheria
 
Rafiki yetu Mchambuzi ana kiwi ya macho. Zamani alikuwa na maono akiandika kurasa tatu za kuanzisha thread lakini baada ya kukengeuka hivi sasa anaandika vioja. Mchambuzi amejivika kitambaa cheusi machoni anasahau walioshadidia suala la ufisadi wa ENL. Sio CHADEMA tu bali hata CCM na wa CCM mkubwa alikuwa Sumaye!!

Wewe tulishakupoteza. Ni Bahati mbaya sana kwamba umegeuka kuwa mhanga wa siasa za nguvu ya giza ndani (CCM) pamoja na kuugulia maumivu baada ya wasaliti Zitto na Dr. Slaa kutotosha tena Chadema. Pamoja na kuondoka kwao na pamoja na kuunga mkono siasa za CCM za za nguvu ya giza, historia inaendelea kuandika kwamba nguvu ya Chadema ikaongezeka mara dufu. Fananisha kura za Dr. Slaa (2010 na Lowassa (2015), ni kielelezo tosha kwamba imani kwa chadema chini ya Lowassa miongoni mwa wananchi ni kubwa kuliko ya msalati Slaa ambae alihadaa wananchi kwamba anapambana na ufisadi na mwisho wake sasa anatunzwa na mafisadi nje ya nchi. Zitto nae survives kwa kutegemea mfumo huo huo.

Mimi nipo upande wa wananchi waliopigia UKAWA kura nyingi zaidi kuliko kipindi chochote cha historia ya uchaguzi wa vyama vingi. Wewe unasimamia wapi, 1% ya kura za ACT? au Upande wa CCM ulioiba kura? Sijui nini kilikupata kwa kweli.

Uchaguzi wa 2015, Upinzani ulipata kura nyingi kuliko katika kipindi kingine chochote cha historia ya uchaguzi wa vyama vingi. Lowassa alishinda kwa kupata Kura Milioni Kumi. Ziliibiwa. Nalisema hili bila hofu kwa sababu huo ndio ukweli. Lakini pamoja na wizi wote kupitia wataalam walioletwa na CCM kufanya kazi ya kudhulumu haki ya wananchi pale Mayfair plaza, Mlimani City Estate, Double Tree hotel, nk, bado kura zilishindikana kuibwa na CCM zikabakia kuwa ni nyingi tofauti na matarajio yenu na akina Zitto na Slaa ambao walidhania kwamba bila ya wao, Chadema kwisha. Kiongozi wako zitto hadi leo anaugulia maumivu na aibu ya kupata 1% tu ya kura za urais pamoja na mbwembwe zake nyingi. Tulisema awali kabisa kwamba Zitto habari yake imeisha. Hata huo ubunge bila ya kutumia udini na pia bila ya kubebwa na JK pale Kigoma (CCM), leo angekuwa analisikia bunge kwenye whatsap.

Kuhusu Ufisadi wa Lowassa kwanini msiende Mahakamani? Alishasema nani ni mhusika mkuu. Mna nafasi nzuri ya kumfungulia kesi kwani sasa hayupo tena kwenye mfumo wa kulindana. Agenda ya ufisadi mbona imekuwa kaa la moto ndani ya ccm? Unatumbua majipu huku bungeni mkimweka Chenge kuwa mwenyekiti? Please...

Ipo siku utarudi kwenye mstari na kubaini kwamba hakuna mabadiliko ya kweli nchi hii nje ya UKAWA iliyosafishwa kwa wasaliti Zitto na Dr. Slaa kutokomezwa. Ndugu yako Zitto anajua hilo. Pili, hakuna future ya CCM katika nchi hii zaidi ya nguvu ya dola na hila. Tulishasema, nguzo kuu ya CCM ni unafiki, dola na wizi wa kura. Nguzo nyingine zote alizoacha Mwalimu Nyerere zimeshapasuka, and its water under the bridge. Kinachoendelea Dodoma kuhusiana na suala la kukabidhiana kofia ya uenyekiti wa CCM taifa ni sehemu kubwa ya kielelezo hicho.

Ndugu, kwanza nikushurukuru kwa kuona kwamba nina maono. Najua ulikuwa unaniunga sana mkono, lakini kumbe itikuwa ni kwa sababu Zitto na Dr. Slaa, wasaliti wa mabadiliko ya kweli, walikuwa chadema. Nikufahamishe tu kwamba hayo 'maono' yapo pale pale na sijaacha kuandika thread za "kurasa tatu". Nimekuwa namsoma sana Rais Magufuli kama kweli ni Rais wa kuwaletea watanzania mabadiliko ya kweli, hasa kiuchumi; Kama kweli kwa Urais wake, CCM itabadilika kwa manufaa ya watanzania. Nimemaliza utafiti wangu. Muda sio mrefu nitakuja na uzi kujadili hili kwa kina na kwa takwimu kwanini Magufuli hawezi kuipeleka nchi hii popote kiuchumi - kuinua uchumi wa wananchi. Uzi utachambua uchumi wa Magufuli 2016-2021. Hata ndugu yako zitto ambae ndani ya roho yake ni pro - ccm kuliko pro - ukawa ameanza kuona ukweli upo wapi. But for him, its too late.
 
Back
Top Bottom