Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,771
- 121,828
- Thread starter
- #561
Naendelea,Mkuu Pasco au mshana au yeyote, kwa kweli leo mmenifumbulia kitu nilichokuwa najiuliza mimi nimeumbwaje. Tatizo langu kubwa ni kwamba karibu watu wengi ninaokaa nao jirani hasa wanawake na baadhi ya wanaume wananiogopa sana kiasi kwamba nikiwa nyumbani wanarudia nje ya geti wakati mimi ni mcheshi na napenda sana kuzungumza na watu pia karibu zaidi ya 90 % ya wanawake ninaowataka lazima niwapate siku hiyohiyo na wengine hunianza wenyewe kwa mfano mwanamke wa kwanza kuduu naye alinianza mwenyewe kwa kutuma mtu na mimi nikaogopa kumkatalia, Pili kwa kadri ya maisha yangu sijawahi kugombea nafasi yoyote ya uongozi nikaikosa, tangu nikiwa mdogo mpaka sasa , pia wale wote niliowajazia fomu za ugombea wote wanafanikiwa. Tatizo linalilonisumbua ambalo ilibidi niombe Mungu anisaidie na nikafaulu ilikuwa ni kuota mambo na nikimwambia mke wangu anabisha lakini yanakuja kutokea vilevile hata kama itachukuwa mda mrefu kutokea kwa hiyo kila nilipokuwa jambo furani la kutisha nilikuwa Napata hofu sana. hii ilinianza baada ya baba kufariki dunia na alikuwa ananitokea mara kwa mara na kunileleza mambo mbalimbali ambayo yatatokea na yanatokea kweli. Kwa mfano kulikuwa na kazi nimeombwa niifanye na taasisi Fulani bila mimi sikutuma maombi ya kazi hiyo, baba alinitokea akasema mawajiri wako wa sasa atakuambia usubili mwezi mmoja lakini baadae hutaifanya kazi hiyo utakuja kuifanya badae, na ndivyo ilivyokuwa kwa MWAJIRI WANGU kukataa kuniruhusu, lakini nilikuja kuajiriwa tena kazi hioyhiyo baada ya miaka ya miaka 7 tangu nilipokuwa nimeombwa kwa mara ya kwanza na pia nilifanya kuteuliwa tu wala sikufanya intavyuu yoyote. Kwa sasa mara kwa mara naota naruka hewani na hata leo nimeota naruka hewani, je hii ni ishara gani?
Niliishia kwenye ulimwengu wa roho, yaani, spiritual world, huko ndiko kwenye pepo, yaani spirits, maeneo haya yanatajwa kama mbinguni, peponi, ahera, motoni , kuzimuni, toharani etc, huko kwenye ulimwengu wa roho, kuna good spirits, bad spirits na evil spirits!.
Good spirits ni zile powers za kutenda mema kama kupandisha Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, kuwa na kipawa cha kuponya, kukemea, kufanya miujiza, matumizi yoyote ya hizi inner power kutenda mema ndiko kuliko dhamiriwa na Mungu wakati akituumba.
Bad spirits ni zile power za kutenda maovu, kama ghosts , mizimu elekezi kwa yasiyo mema, claivoyance, mediums, pepo wachafu kama pepo la ngono, pepo la wivu wa kupindukia, pepo la tamaa, wagaga wa kienyeji wasiotumia alternative medicines , majini faida, na vitendo vingine vyovyote vinavyokwenda kinyume.
Na evil spirits zikiongozwa na the devil, mashetani, majini, wachawi na matumizi ya hizi power kufanya maangamizi.
Hilo la kupaa, inaweza kuwa ni ndoto tuu au astra travel.
Pasco