KERO  PSSSF Dodoma tofautisheni msaada na Haki ya Mtu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,668
3,751
Wanajukwaa habari za muda huu.

Ninalazimika kupanda jukwaani kutokana na usumbufu mkubwa sana uliopo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF .

Hawa watu wanakuwa na vipengele vingi vya kufuatilia na hata ukishakamilisha wanafanya malipo wanavyotaka.

Hivi inakuwaje mtu anajaza taarifa zinachukua zaidi ya siku 30?
Kunakuwa na uswahili, ubabe, ukorofi na roho mbaya.

Mambo hayo yanakuwa kero kubwa kwa wanufaika wa mfuko.

Ninavyoiona PSSSF hawafai kuwa kimbilio kwani ni wasumbufu sana.

Nimewaza kama yanatengenezwa mazingira ya rushwa ila nikasema hapana bali ni roho mbaya tu mlizonazo watumishi wa mfuko hapo Dodoma.

Acheni usumbufu lipeni hela haraka huo sio msaada ni haki za watumishi.

Badilikeni.

Majibu ya PSSSF soma hapa ~ PSSSF yampa pole Mdau aliyelalamikia huduma yao, yatoa ufafanuzi na kusisitiza inazingatia Maadili, Uaminifu, Weledi na Uwazi
 
Kama walivokua wanakata hela za watumishi kwa wakati wangekua wanalipa kwa wakati ingekua Raha sana.

Ila huyo mkurugenzi hamna mtu pale maana amesumbua sana ndugu zetu akiwa bodi ya mikopo pale Leo kahamishiwa ofisi nyingine

Kwanini hii nchi watu wanaojielewa,wenye huruma,uwajibikaji na wanaozingatia sheria hawapewi nafasi hizo NYETI. Kama kuna mahali mama anatakiwa afanye mabadiliko nikwahuyu mkurugenzi. Sio mweledi kabisa na hana maana asaidiwe
 
Kwa wanaotarijia kustaafu niwatahadharishe mjiwekee pesa akiba ya angalau mishahara ya mwaka mmoja au miwili kabla ya kustaafu.

Najua ni ngumu lakini inawezekana.

ps
Hakikisha una nyaraka zote. Kama hujaambatanisha nyaraka zote 7 zinazotakiwa, kusoteshwa miezi 6 au 12 kabla ya kupata mafao yako ni kawaida kwa hao wababe wa psssf.
 
Mkurugenzi wao kazi imemshinda. Hamna mtu pale
Unakaaje na hela za watu muda wote hujali. Anajua wenzake wanaishije?
Anafikiri tunapewa gari nyumba na vinywaji vya ofa kama wao. Toa hela za watu mzee