Prof Mbarawa: Serikali kutuma wataalamu kukagua ubora wa ndege mpya ya Dreamliner (B787)

Hakuna cha ukaguzi hapo.. Halafu mbona hamjiulizi je wenzenu wanafanya hivyo katika manunuzi..!?

Yale makubaliano waliosaini au receipt/ purchasing order waliopewa baada ya kulipa cash cash cash inaruhusu kukagua bidhaa?
 
Jamani watanzania, tuwekeni akiba ya maneno, ndege tuliyonunua Siyo mojawapo ya Hizo terrible teens, tulieni, msiwe na wasiwasi ingawa ni haki yenu kuhoji maana maisha kwa sasa ni magumu mnoo, sasa kwa hali hii ya maisha ya sasa afu uambiwe kuwa ndege tuliyonunua ni "terrible teens" afu tumepigwa ni lazima mtu uongee na kilaza sauti.

Sasa, tafuteni Website genuine ya Boeing ndio mchunguze mtabaini ukweli wa hili,

andika: www.Boeing.com ingia hapo ndo utajua kuwa tumepigwa au lah...

Taarifa zote zipo hapo, hadi orders/ delivery za mwezi wa tatu zipo hapo, za mwaka huu zipo hapo, na walio-order ndege na aina ya ndege zipo hapo.

nimegundua, kuna website fake za Boeing mtandaoni.
mkuu there is no way isiwe Terrible Teen,ile namba ndo inawamaliza,19 hawana ujanja wa kufuta hiyo namba,hiyo namba maana yake ile ni ndege ya 19 kutengenezwa.
5H- Air Tanzania LN19 - Was moved out of 45-12.

5H- Air Tanzania Boeing 787-8 Dreamliner - C/N 35508 / LN 19
 
SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni baada ya kuwapo taarifa mbalimbali zinazodai ndege hiyo haina viwango.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150 kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.
Acha Leo nitumie msemo wa kike ACHA NICHEKE MIE naona huyo waziri kapata fursa ya kutafuna hela za kwenda nje ya nchi hao wataalamu anaosema atawatuma kukagua ubora wa ndege zinazo undwa na mainjinia ulaya si kichekesho Tanzania kichwa cha mwendawazimu tutaweza kukagua ndege na mapungufu bora tutumie taharifa zilizo Fanya kama hizo ndege zimekataliwa masoko ya nchi kubwa tuachane nazo
 
TZ hakuna wataaalamu wa kukagua ubora wa ndege maana hakuna kiwanda cha kutengeneza hizo ndge. Wanaenda kutmbea tu. Hao ni sawa na wale wanaoenda Japani kukagua mashangingi wakati hadi baiskeli tunaagiza kwao.
Huo ndo ukweli wanakwenda kunywa kahawa na kushangaashangaa mashine tu
 
TZ hakuna wataaalamu wa kukagua ubora wa ndege maana hakuna kiwanda cha kutengeneza hizo ndge. Wanaenda kutmbea tu. Hao ni sawa na wale wanaoenda Japani kukagua mashangingi wakati hadi baiskeli tunaagiza kwao.
Wanadhani kupewa riport na kudoma ndiyo kukagua
 
TZ hakuna wataaalamu wa kukagua ubora wa ndege maana hakuna kiwanda cha kutengeneza hizo ndge. Wanaenda kutmbea tu. Hao ni sawa na wale wanaoenda Japani kukagua mashangingi wakati hadi baiskeli tunaagiza kwao.
Yani wewe umeniwahi

Hivi unawezaje kukagua usichokijua
 
Kinachoendelea ni kwa wapandaji wa hizo ndege za Magufuli kupungua kwa kasi ya USAIN bolt
 
Kuna wataalam wa kukagua ubora wa ndege kutoka Tanzania?

Au mnataka kupeleka watu wa kulipana posho za safari tu?
 
Tatizo sio ubora,tatizo bei ya ndege inaonekana kuna deal imechezwa hapa,
hiyo ndege ni ya 19 kutengezwa kati ya dreamliner karibu 1000 ambazo zimetengenezwa,
hiyo ndege ilikuwepo parking kwa zaidi ya miaka 5,
wakati zile prototype zikiwa parking walizitoa ingine,
na sasa ndo wanafanya reworking ambayo kufikia mwezi dicember itakuwa tayari,
ndege si mpya ilikuwepo na inafanyiwa reffiting tu ya vitu,anaposema eti inaundwa hatumwelewi,wabongo wa leo hawadanganyiki kirahisi kiasi hicho
Hii ni kama issue ya radar l, kuna wakubwa wanahisiwa ku-double bei ili wale cha juu
 
Tulisema sisi humu kwamba huu ununuzi wa ndege kwa zaidi ya trilioni moja ($487 million) bila pesa hizo kuidhinishwa na Bunge na kufuata taratibu za manunuzi za Serikali umegubikwa na ufisadi. Sasa yamekuwa kweli! Yule mpiga madili maarufu nchini kishafanya yake! Eti unalipa cash kwanza halafu ubora wa bidhaa husika unaufanya miezi chungu nzima baadaye kwa kuwatumia watu ambao hawana uzoefu wowote wa kukagua ubora wa ndege!
Mbona kajieleza vizuri na huu utaratibu Mbona kwenye bombadia ndio ulitumika
 
TZ hakuna wataaalamu wa kukagua ubora wa ndege maana hakuna kiwanda cha kutengeneza hizo ndge. Wanaenda kutmbea tu. Hao ni sawa na wale wanaoenda Japani kukagua mashangingi wakati hadi baiskeli tunaagiza kwao.
Well said mkuu. You have really hit the bull.
 
Mv Dar

es salaam nyingine
Mwishowe itaishia jeshini kubeba vifaru
 
Wataalamu kutoka Tanzania kwenda kukagua Boeing 787 Dreamliner.! Hii hatari sana, kutengeneza pikipiki tu huwezi unakaguaje ndege ..!?
Wanaropoka tu! Dreamliner ikaguliwe na nai Tanzania, they must be joking! Kwani hii mitumba ya magari mingine kama hujaambiwa huwezi jua ni makapi/mitumba. Sasa wale wanakuwa na delibarate move msiweze kugundua, mtaweza kweli.
 
mkuu there is no way isiwe Terrible Teen,ile namba ndo inawamaliza,19 hawana ujanja wa kufuta hiyo namba,hiyo namba maana yake ile ni ndege ya 19 kutengenezwa.
5H- Air Tanzania LN19 - Was moved out of 45-12.

5H- Air Tanzania Boeing 787-8 Dreamliner - C/N 35508 / LN 19
Shida hawa wakulima wanadhani dunia ya sasa unaweza kufanya upigaji wa kishamba shamba.

kubalini yaishe, hizo dola milioni 125 zirudisheni tafuteni dili jengine.
 
TZ hakuna wataaalamu wa kukagua ubora wa ndege maana hakuna kiwanda cha kutengeneza hizo ndge. Wanaenda kutmbea tu. Hao ni sawa na wale wanaoenda Japani kukagua mashangingi wakati hadi baiskeli tunaagiza kwao.
Wataangaria masofa kama yananesa tu.
 
Wamelipa cash kabla ya kuangalia ubora wa ndege husika! Mafisadi katika ubora wao duh!

Na hawa "wataalamu wa Kitanzani" huu ujuzi wa kukagua ubora wa ndege walijifunzia wapi!? Na lini!?
NIT .
 
Back
Top Bottom