Prof Mbarawa: Serikali kutuma wataalamu kukagua ubora wa ndege mpya ya Dreamliner (B787)

Tulisema sisi humu kwamba huu ununuzi wa ndege kwa zaidi ya trilioni moja ($487 million) bila pesa hizo kuidhinishwa na Bunge na kufuata taratibu za manunuzi za Serikali umegubikwa na ufisadi. Sasa yamekuwa kweli! Yule mpiga madili maarufu nchini kishafanya yake! Eti unalipa cash kwanza halafu ubora wa bidhaa husika unaufanya miezi chungu nzima baadaye kwa kuwatumia watu ambao hawana uzoefu wowote wa kukagua ubora wa ndege!

Wameanza kukiri kuumbuka.
 
Sasa Laiti Tanzania hii tungekuwa na Wataalamu wa ndege wa ukweli si tungewahi kutengeneza hata ndege yetu ya demo?

Kauli ya Waziri ni ushahidi tosha kuwa Serikali haijui vizuri kuhusu ndege inazotaka kuzinunua, Otherwise sasa wataalamu wa Kuikagua wa nini tena, kama wanajiamini kuwa kila kitu kiko njema?

Serikali ilitwambia hapo awali kuwa tayari imeshalipia pesa yote na kilichobaki ni ndege kuja tu!, Sasa unajiuliza, Ina maana Wananunua Kitu kisha ubora wake wanakagua baadae? Hii ni ajabu sana.
 
Kama vile kuna mchanyato wa habari hapa terrible teens tuliambiwa ziko 20 zimedoda na baadhi zinapigwa na vumbi hangani "sio kadoda wa jF"

Na washawasha!
 
Sasa Tanzania tungekuwa na Wataalamu wa ndege si tungewahi kutengeneza hata ndege yetu ya demo?

Kauli ya Waziri ni ushahidi tosha kuwa Serikali haijui vizuri kuhusu ndege inazotaka kuzinunua, Otherwise sasa wataalamu wa Kuikagua wa nini tena, kama wanajiamini kuwa kila kitu kiko njema?
Kwa upande mwingine wako sahihi, hata mtu akitaka kununua gari mara nyingi anaambatana na fundi ama mjuzi zaidi kulikagua hilo gari kwa madhumuni kujiridhisha....huenda wangepuuza kelele zilizopigwa na baadhi ya watu na kusema kuwa wanajiamini na ndege ipo sawa, wapo wengine ambao wangewaponda na kusema serikali imetudharau haijatusikiliza....uongozi ni tabu you are damned if you do and damned if you don't:rolleyes:
 
SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni baada ya kuwapo taarifa mbalimbali zinazodai ndege hiyo haina viwango.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150 kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.
Namwamini Prof. Mbarawa na
naamini atawatetea WaTZ na watapata kilicho chema . Viva Prof.Ila natoa angalizo. Kwanza hao wataalam wana utaalam wa kukagua ndege? Pili, hawahongeki? Maana kampuni hizo kubwa kwa kuhonga noma.

Finally kuna jambo la kutatanisha hapa. Taarifa zilizopo ni kwamba hizo ndege zilishatengenezwa, ila zilihitaji marekebisho ambayo yangezifanya ziwe nzito, na hatimaye kuwa fuel inefficient and have reduced speed. Sasa taarifa hii anayotoa Waziri Mbarawa kwamba ndege hizi zinatengenezwa kwa order na kila hatua mteja ana-check ni ngeni. Could it be kwamba hiyo nayo ni katika mlolongo wa mambo yanayoashiria kwamba kuna udanganyifu? Kazi kwake Prof.
 
Vizur...
Tusubir kuckia hiyo list ya maprof na madocta... Ikitajwa na kuapishwa ikulu haraka iwezekanavyo.......
Labda na vijembe kidogo cku ya kuapisha
 
Hivi sio kuwa vimeshatengenezwa ni tunanunua tu? Kama hazijatngenezwa kwanini waendelee kutengeneza mbovu?
 
Juzi Zitto kasema kuhusu hiyo kuingizwa kichwa kichwa, ccm wakashinda hapa jukwaani kukebehi. Sasa ukweli hadharani ndio unasikia wanatuma wataalamu!! Kichekesho utasikia wataalamu ni wabunge na kabla ya kwenda kila mmoja anapewa mpunga kabisa kuja kutetea huo upigaji.
 
Nampenda huyu bwana ni msomi na msikivu. Atafika mbali kwenye shughuli zake. God bless!
 
Mtaalam kutoka Tanzania akakague ndege?

Kama sielewi hii imekaaje au watachukua watu kutoka huko ng'ambo coz hawajasema wataalamu hao watatoka wapi

Kama kuna mtu anawajua hawa wataalam please aje atuelezee hawa ni watu gani hasa kutoka bongo
Hii habari na mimi bado sijaiamini mpaka tupate list ya hao wataalam wanaotoka Tanzania
 
Hizo ni Terrible Teens Dreamliner yenye Serial No.19,anaenda kuganua nini sasa? Arudishe tu,Dola zetu 125m basi ndio tunachotaka.
 
Hakuna cha mtu kwenda kukagua chochote hapo. Zilitengenezwa 787 na namba zake zikawa 787-1, ndege ya kwanza 787-2, ya pili mpaka 787-19 .Hizo za kwanza zote zilikuwa mbovu tena hatari kabisa kuziendesha. Mashirika yote ya ndege yakazigomea. Baada ya kukataliwa hizo ndege watengenezaji wakapunguza bei toka $mil 224 mpaka $ mil 99. Kama namba za hizo ndege tulizouziwa sisi ni kati ya 787-1 mpaka 787-19 basi tumeliwa. Ziliitwa terrible teens kwa sababu ni the first 'terrible' 19 (teens- unaelewa teen ager? yaani someone under 20)
Hizi zilishatengenezwa na hazijauzika kwa miaka 9 sasa. Kama hizo tulizoagiza ni za namba za baadaye hakuna shida.
 
Wamelipa cash kabla ya kuangalia ubora wa ndege husika! Mafisadi katika ubora wao duh!

Na hawa "wataalamu wa Kitanzani" huu ujuzi wa kukagua ubora wa ndege walijifunzia wapi!? Na lini!?
Siyo Mara ya kwanza kupigwa, vipi meli ya Dar bagamoyo, ipo Siku marehemu watafufuka
 
Na mpigaji alikuwa huyu huyu mpiga madili maarufu nchini. CAG lazima akayaanike madudu yaliyofanywa na huyu mpiga madili makubwa makubwa.

Siyo Mara ya kwanza kupigwa, vipi meli ya Dar bagamoyo, ipo Siku marehemu watafufuka
 
Back
Top Bottom