Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,430
- 118,836
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo ziko kwenye magazeti mawili, Gazeti la Nipashe la kila Jumapili na gazeti la Mwananchi la kila Jumatano, pia kuna kipindi cha TV cha KMT, kila Jumapili saa 3:00 usiku na marudio Jumatano saa 9:30 alasiri on Channel Ten, nikiangazia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi makubwa kwa taifa.
Jana niliangalia tukio la uapisho wa wateule wapya, Ikulu Dar es Salaam, kwanza nilifarijika sana kuona miongoni mwa waalikwa wa tukio lile, ni Mzee wa Ngomeni, Musa Richard Mwasha kwa jina maarufu la Kuhani Musa, nimefarijika kwasababu mwaliko huu wa Kuhani Musa ni kuonyesha kuwa Kuhani Musa anatambulika na serikali. Huko nyuma niliwahi kushauri Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea
Pili nimefarijika sana kumuona Rais Samia akitoa sababu za kumteua kila aliyemteua na kumpa majukumu kwa uwazi kabisa. Katika uteuzi niliwahi kuandika Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!
Enzi za Kikwete, Tanzania tulisaini ule mkakati wa Open Government Partnership, OGP, na kuwa nchi ya pili barani Afrika kusaini baada ya Africa Kusini. Mpango huo uliokuwa unasisitiza ushirikishwa wa umma kwa ukweli na uwazi, truth and transparency, katika kila kitu serikali inachokifanya.
JPM alipoingia, aliufuta mpango mkakati huo, na Tanzania, ikajitoa, hata Bunge live likafutwa, mikutano ya vyama vya siasa ikapigwa marufuku na hata mikutano ya ndani kuzuiwa.
Rais Samia alipoingia, na falsafa yake ya 4R, akafanya mabadiliko mengi makubwa ikiwemo kufungulia mikutano ya siasa.
Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT, Rais wa JMT anaweza kushauriwa na wasaidizi wake, lakini kwenye kufikia maamuzi, rais anafikia uamuzi yeye kama yeye, na halazimiki kufuata ushauri wa yeyote, na hawajibiki kutoa sababu yoyote ya maamuzi yake kwa yeyote.
Powers za rais kuteua na kutengua ni discretional powers, kwa rais kuteua, kutengua au kutumbua at her pleasure bila kutaa sababu yoyote kwa yeyote, na teuzi hizi hazihojiwi na mamlaka yoyote.
Hivyo kitendo cha Rais Samia kuwa open and transparent kwa kueleza sababu za kumtea fulani mahala fulani na kumpa majukumu kwa uwazi, hii ni hisani kubwa na nzuri kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.
Anachokifanya rais Samia kuwa muwazi, open and transparent sababu za kuwateua wateule wake, ni hisani tuu, tena hata uapisho live mubashara kisha kutolewa hotuba, kumeanza na JPM, zamani hatukuwahi kuwa na hotuba kwenye uapisho, ni kuapa tuu and that was it.
Kitu kizuri zaidi, sio tuu Rais Samia anakuambia kwanini amekuteua, bali anaelekeza uende ukafanye nini!. Mfano RC Makonda amepewa special task Arusha, jiji la kitalii, hivyo anapaswa kwenye kukuza Utalii, ila pia kuna maelekezo mengine ya kuyashughulikia na kuwashughulikia ikiwemo issues za wale machalii wa RChuga na 'cha Arusha'.
Yule RC wa Mara ambaye ni mjeshi, kaelekezwa kwenda kushughulikia kijeshi jeshi kile kilimo cha lile zao, (hakulitaja) ambalo Mara ni maarufu na kulivusha mpakani na nchi jirani.
Hiki anachofanya Ras Samia ni sawa na ile Open Government Initiative, kwa mteuliwa kupewa changamoto openly and transparently, akishindwa ku deliver
The public yote itajua hivyo hiki ni kitu kizuri kwa uwajibikaji.
Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, au kupata taarifa, the right to information act, hivyo wananchi kuelezwa kila kinachowahusu ni haki yao na sio hisani.
Kwa vile Rais Samia ameisha onyesha njia kwa kutuhisania, tuwe watu wa shukrani kwanza kwa kumshukuru kwa hiyo hisani tuu kwanza, kisa sasa tumuombe atupe na haki ya kupata taarifa, asiishie kwenye kutupatia taarifa za uteuzi tuu, tupatiwe na taarifa za sababu za utenguzi kwasababu maofisa hao ni watumishi wa umma, wanaolipwa na fedha za umma, hivyo umma una haki zote za kujua kuhusu utendaji wa wateule hao, na sababu za kutenguliwa kwao na kutumbuliwa.
Mfano Paul Makonda, baada ya kuteuliwa Mwenezi wa CCM, amefanya wonders katika kipindi kifupi na kurejesha imani ya wananchi kwa CCM, kwa kuwakimbiza viongozi mchaka mchaka, wengi wakitaraji mchaka mchaka huo ungeendelea hadi 2025, katika uchaguzi ujao Makonda aingie Bungeni, na kupewa Wizara nyeti, lakini mara ghafla Makonda kama Mwenezi, akatumbuliwa!.
Mtu yoyote mwenye cheo kikubwa, akaondolewa na kuteuliwa cheo kidogo ni kutumbuliwa tuu!, hivyo Makonda ametumbuliwa uenezi na kupoozwa na u RC, Dr. Bashiru Ali Kakurwa alitumbuliwa uenezi na kupoozwa na ubunge wa kuteuliwa. DGIS wametumbuliwa mara kadhaa na kupoozwa na ubalozi, wengine wakitumbuliwa wanasugua bench, kama Balozi Liberata Mulamula, Prof. Kabudi, William Lukuvi na wengine wengi, the public has the right to know sababu, na sio kusubiria kuhisaniwa.
Kama ilivyo sifa njema kuteuliwa, mtumishi wa umma akiboronga, the public ielezwe kama nilivyo shauri hapa - Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
Tena kwa maoni yangu, nafasi za juu zote wakiwemo wakuu wa mihimili, Jaji Mkuu, Spika na wakuu wa zile independent organs zote, nafasi zinapokuwa wazi, zitangazwe, Watanzania wenye sifa waombe, washindanishwe kwa uwazi, tupate the best ndipo rais apelekewe kuteua, na sio huu utaratibu wa sasa wa watu kuokotana, kuteuana na baada ya siku mbili kutenguliwa, haileti picha nzuri sana kwa awamu hii ya Rais Samia.
Nchi nyingi wakiwemo jirani zetu Kenya, Jaji Mkuu, anaomba kazi, wanashindanishwa, wanasailiwa, the best anachaguliwa, ndipo rais anapelekewa kuteua.
Nimalizie kwa kumpongeza tena Rais Samia kwa kutuhisania openness and transparency kwenye teuzi zake, openness hii na transparency hii tuifanye ni haki na sio hisani.
Wasalaam
Paskali

Tanzania imejitoa rasmi katika Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership-OGP) hatua ambayo inazua wasiwasi kuhusu utekelezaji wa sera ya uwazi na uwajibikaji iliyoasisiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Hatua hiyo ya kujitoa kwa Tanzania imetangazwa na Kamati ya Uongozi ya mpango huo iliyokutana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.
Hii ina maana kwamba kuanzia sasa mipango yote ya serikali itakuwa ikiendeshwa kwa usiri mkubwa (itafanyika gizani). Hakutakuwa na uwazi tena.
Moja ya athari za uamuzi huo ni pamoja mikataba mbalimbali inayohusu rasilimali za taifa kusainiwa kwa siri bila umma kushirikishwa. Pia nyaraka zinazohusu maamuzi nyeti ya nchi zitafichwa, na iwapo mwananchi atakutwa nazo atakuwa ametenda jinai na anaweza kushtakiwa (disclose of classified information), chini ya sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1971.
Bado haijaeleweka kwanini Tanzania imeamua kujitoa katika mpango huo na kuamua kuendesha mambo yake gizani, lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiksnda, Dr.Aziz Mlima amesema “Ni kweli tumejiondoa. Lengo ni kuutathmini mpango huo kama unaendana na masilahi ya Taifa. Kama tutaona una maslahi kwa taifa tutajiunga tena”
Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2011 na kuwa nchi ya pili barani Afrika ikitanguliwa na Afrika Kusini. Kwa sasa nchi zaidi ya 40 za Afrika zimesaini mpango huo wa kuendesha mambo kwa uwazi. Pia zaidi ya 75% ya nchi zote duniani zinatekeleza mpango huo.
malisag