Polepole: CCM tunaendelea kuwa chama bora kwa kuwa tunajitahidi kusahihisha makosa yetu

Watu wamuwawa mwaka.mzima mpka wamefika 30+ halafu.leo.ndio.anasikitishwa
 
Kila tukisema kitu tunaitwa NYUMBU............. SAA NYINGINE WAPUUZI.

Je sisi ambao sio wamoja wao haturuhusiwi kusema kitu??????
 
Huyu jamaa alikuwa very critical mind. Baada tu ya kujiunga na hilo bandwagon amegeuka na kuwa feeble mind! That is the difference...
 
Hicho chama huwa hakibadiliki. Lakini chenyewe kina tabia ya kubadilisha wanachama wake kuwa waongo waongo na wenye uchungu na chama zaidi ya nchi yao.
 
Kuwaita wanaohoji kuwa ni wapuuzi sio lugha bora ya mwanasiasa, ni lugha ya kijinga inayoweza kutolewa na mjinga tu. Kama CCM inajisahihisha why imewapa wezi waliotufikisha hapa madaraka makubwa hadi kwenye bunge letu? Kama CCM inajisahihisha kwa nini mpaka sasa hawajamtaka rais afufue mchakato wa katiba ya Warioba ambao hakuna asiejua kuwa ndio salama pekee ya Taifa? Kama CCM inajisahihisha kwa nini isiwafukuze uanachama wale wote waliosababisha wizi huu?
CCM anayoisema Polepole iliondoka na Mwalimu Nyerere!
Lugha sahihi hapa ni kusema Mheshimiwa Rais ndiye anayejaribu kujisahihisha kwani haya yote aliyajua kwa zaidi ya miaka 20 lkn alikuwa kimya! Ni yeye anayejisahihisha na sio CCM!
Polepole why hujazungumzia suala la rambirambi kwenda kukarabati hospital? Au huko CCM haihusiki?
Siku nitakaposikia Magufuli anatanganza kamati ya kuangalia uwezekano wa kurejesha nyumba za umma walizojibinafisisha yeye akiwa ndiye mratibu wa ubinafisahaji ndipo nitakapoamini kuwa Mheshimiwa Rais ndiye anayejaribu kujisahihisha, na nitatafuta tawi la CCM liliokaribu nami nichukue kadi ya kijani!
 
CCM hawana ubora wowote na haiwezi kuendelea kuwa bora kwa kuwa hawajawahi kuwa bora hata siku moja,makosa wanayodai kusahihisha yanatokana na CCM yenyewe,wakisahihisha kosa moja wanafanya kosa baya zaidi nafuu na kosa la jana.
 
Jana mh Slow Slow alitanabahisha kuwa kuna watu walijitokeza kumuhonga baba Jeska pesa zenye thamani ya bilioni mia tatu za Kitanzania ili apotezee ishu ya mchanga wa madini, akawachomolea!
Ikumbukwe, pesa hiyo ni sawa na nusu ya utajiri wa Bhakresa...
 
Jana mh Slow Slow akitanabahisha kuwa kuna watu walijitokeza kumuhonga baba Jeska pesa zenye thamani ya bilioni mia tatu za Kitanzania ili apotezee ishu ya mchanga wa madini, akawachomolea!
Ikumbukwe, pesa hiyo ni sawa na nusu ya utajiri wa Bhakresa...

Uongo mtupu kama aliweza kupokea vijisent akiwa Mbunge ili apitishe miswada bomu atakataa hiyo??

Kama Bilion nane zilipigwa zikaleta kivuko kibavu halafu ati bilion 300,duh Huyo jamaa aache kutudanganya labda adanganye Lumumba FC
 
Uongo mtupu kama aliweza kupokea vijisent akiwa Mbunge ili apitishe miswada bomu atakataa hiyo??

Kama Bilion nane zilipigwa zikaleta kivuko kibavu halafu ati bilion 300,duh Huyo jamaa aache kutudanganya labda adanganye Lumumba FC
Hongera kwa vile unajua kusoma na kuandika!
 
Hongera kwa vile unajua kusoma na kuandika!

Hahahahhahahahah ukweli unauma,kama alipiga Bilion 8 tu ataacha bilioni 300?Kwanini adanganye umma??SIpendi uongo na hili linamfanya huyo Slowslowa kudharaulika
 
anachofanya baba jesca ni kutiimiza wajibu wake kama raisi wa tanzania,mbona waliopita waliruhusu vitu vya ovyo na bado mkasema ni chama bora?
 
Tunasikitika kuwa katika hili tumeachwa wenyewe, vyama vya siasa tulipaswa kushikamana, ukimya wa wenzetu umetusikitisha.
Mh polepole kumbuka mpinzani ndani ya sasa za sasa zinazosimamiwa na ccm anatakiwa awe makini kila taarifa yao nyinyi mnaijibu kwa kejeli na dharau mkiamini nchi ni yenu peke yenu.MF hivi sasa mnatumia uvccm kujibu kila kitu cha ushauri bays zaidi mko kimipasho zaidi kuliko hoja.
Jiulize wapinzani muda wote wa kupitisha au kuhoji mambo makubwa ya taifa MF mikataba ya madini huonekana wachochezi sasa hivi mh rai kusimamia mlemle inaonekana ajenda mpya.
Mauaji msisikitike wapinzani kukaa kimyaa toeni muongozo wafuate maana nyie kwenu ndo mnataka hivyo mawazo mbadala hamtaki Leo hili kiongozi wa upinzani akithubutu kutembelea huko ili kuwafariji wananchi jua jela inamuhusu.
 
CCM kwa hili jambo wanataka vyama vingine vya kisiasa washirikiane na wakati hivyo vyama haviruhusiwi hata kuongea?
 
Mnara Babeli ulishayumba siku nyingi huo ubora mtaupata wapi ktk karne ya watu wenye uelewa labda huko mlikotoka sio sasa. Rusuni mikutano ya hadhara ili mwangalie mlipwaya
 
Kwahiyo mnajifunza kuongoza Nchi kwa miaka 60 na,

Mnajisasahihisha, Mkikosea mtajisahihisha tena, yaani Waalimu ni Nyinyi na wanafunzi ni Nyinyi hahahahahaaaa kweli hiki chama ni kibiko.
 
Back
Top Bottom