Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 9,972
- 8,275
Hawa waandishi wetu! Kusimamishwa na kufukuzwa ni vitu viwili tofauti. Ingawa hii biashara ya maamuzi ya jukwaani hainivutii inaelekea hapa palikuwa na jambo......
Saafi sana, what else do we need on the ishu? Wakuu kila ishu na time yake na mahali pake, kwenye hii ishu Pinda is right legally na hata politically, wananchi waliotoa michango yao wamemlalamikia waziri mkuu, ambaye haishi nao pale isipokuwa anapita tu kwenye ziara, anyehusika ameulizwa na akakubali mbele ya umma kuwa ni kweli hakutimiza wajibu wake,
wakuu mnaomshambulia Pinda, mlitaka afanye nini? Aunge kamati ya uchunguzi itumie hela zaidi ya zilizochangwa kwa ktiu ambacho ni clear na kipo wazi? wananchi waliachanga wapo, aliyepewa yupo, Waziri Mkuu yupo, mashahidi viongozi wengine wapo, sasa mlitaka Takukuru au bunge liingilie kati?
Kwenye hii ishu, Pinda was right 100%, na bravo kwa kuanza kusimamia uwajibikaji.
Sasa, on your view, unafikiri kwa kufanya alivyofanya Pinda ndiko kunatatua matatizo ya mfumo mbovu wa uongozi uliopo chini katika ngazi ya kata na vijiji?
Pamoja na matatizo ya makatibu kata wetu, ukweli ni kwamba wananchi wetu bado wana tatizo la kukubali kufuata taratibu na sheria za nchi, partly because sheria zenyewe ni mbovu na partly because kuna upendeleo katika utekelezaji wa hizo sheria. Sasa kwa wale waliokaa vijijini wanajua kwamba kiongozi yeyote anayejaribu kufuata sheria na kuzitekeleza huwa anageuka kuwa adui wa wananchi kwa sababu wananchi hawataki kioungozi anayefuata sheria, huwa anaitwa mnoko. Ndio maana basi ni uzembe na kujitafutia sifa za kijinga kwa kiongozi wa ngazi ya waziri mkuu kumsimamisha kazi katibu kata on the face value ya maoni ya wananchi.
Mi nilisema huyu mtu bogus tangu day one.Hofu yangu ni kwamba asije kuwa mtupu kuliko Sumaye.
Marshall na fundi inaonekana mnamtetea Pinda,thats fine na wala hakuna mtu ambaye hataki asifanye kazi yake,lakini wakuu tatizo hapo ni hiyo style ya ufanyaji kazi,hivi kweli ina maana kila atakayelalamikiwa na wananchi amekula pesa or whatever basi ni termination on the spot,kuna watendaji wilaya maelfu na maelfu sasa atafukuza wangapi kwa malalamiko ya wananchi...kumbukeni ile ni nchi huru and nobody above the law kwa hiyo taratibu lazima zifuatwe sio kufukuza tuu kwa sababu yeye ni PM,huo ndio mwanzo wa udikteta na kujenga nidhamu za woga katika jamii,namshauri arudi Dar akae na washauri wake wajue namna ya kudeal na wizi wa pesa wilayani na wajenge policy nzuri ambazo zitazuia wizi na kuwafanya waliopewa kazi wanafanya kazi kuliko kufukuza watu kazi majukwaani bila uhakika!

HAhahaha Pinda kweli kapinda kufukuza Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kabwe, ni kuonea wadogo, amfukuze basi kazi akina Hosea, Gray Mgonja, Ole Naiko, Mwanyika na wale wakuu wa mikoa wapo kwasababu ya kuwepo, James Nsekela, Kandoro, Gen Brig Kalembo wapo wengi tu untendaji wao wa hovyo
There is something to route for drastic measures in some instances.
Watanzania wakati mwingine tumeleema mno! Kazi tunafanya si kwa kujituma na wakati mwingine inakuwa kana kwamba tufanye tusifanye hakuna litakalobadilika.
Mimi nasema, it is about time tuwe na discipline ya kufanya kazi bila ya kusubiri kusukumwa; lakini ikibidi tusukumwe, basi tusianze kulialia kuwa tunaonewa.
2008-03-03 20:09:21
Na Mwandishi Wetu, Mpanda
Wale waliodhani Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Mizengo Pinda ni mtu laini laini, basi wameula wa chuya kwani mzee ni mchungu kuliko hata shubiri na tayari ameanza kufyatua makucha yake na kuwaonyesha watendaji wababaishaji kuwa, yeye ni kiboko na kamwe hawatapumua chini ya uongozi wake.
SOURCE: Alasiri
Ama kweli watanzania wasanii ninyi. Yaani Pinda kiboko kwa sababu ametoa mkwara kwa viongozi wa serikali za vijiji. Mbona huo mkwara mi naweza kuutoa hata bila kuwa na cheo cha usaidizi wa waziri!! Eti vigogo
Mie nilidhani eti Pinda kawaweka ndani EL, BM, ZM, OM, DB, na AK. Kumbe yale yale tu ya kila siku yanayoturudisha nyuma. Kila anayeteuliwa anaenda kuwapiga mkwara makatibu kata. Nchi inauzwa na akina Jetu
Kweli kabisa hayo unayosema. Hajafanya lolote kuhusiana na kashfa za BoT na Richmond. Bandarini kuna msongamano wa hali ya juu, pale tabata mamia ya wakazi wamevunjiwa nyumba zao hata kauli hajatoa kuhusiana na sakata hilo. Yeye bado yuko busy na kupongezwa kuukwaa uPM, halafu tunaambiwa kwamba huyu jamaa ni kiboko!