Picha: Siku ambayo Rais Magufuli alipata PHD yake akiwa waziri

Sasa kama ni hivyo kwanini hiyo teknolojia haitumiki kuzuia kutu maana nyumba nyingi na magari mengi vyote vinaharibiwa na kutu. Hilo andiko liko wapi tulitumie jamani!
 
Sijui ni mawazo yangu au ni generalization inaonekana jamaa anampenda mama kuliko wife...
Weweee mwacheni mama hakuna kama mama upendo wa mama wapita vyote chukulia mfano umeoa bahati mbaya ukafariki mke anao uwezo wa kuolewa na mwingine,
Lakini mama alichukua alikubeba miezi tisa kwa shida na karaha zote alizopitia akajifungua kwa uchungu amekulea akakunyonyesha ukilia anakubembeleza, ukiumwa mama hana raha hata ukiwa mkubwa ukawa mtukutu bado mama atazidi kukupenda na mapungufu uliyo nayo kwa kweli mwacheni mama kama alivyo.
 
Hivi wewe mwana UKAWA mke na Mama nani bora kwako? Mbona mnahoji mambo ya KIPUMBAVU hivi? Kweli nimeamini kwenye UKAWA wawili wote ni Vichaa.
 
View attachment 454464 View attachment 454465 View attachment 454464 View attachment 454465 Mh. John Pombe Magufuli akitunukiwa shahada yake ya uzamivu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Balozi Fulgence Kazaura baada ya kukamilisha nondo zake katika fani ya sayansi ya kemia . Du hapo nakubali.

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye fani ya kemia katika mahafali ya 39 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kufanya utafiti kuandika na kufanikiwa kuitetea tasnifu (thesis) inayohusu matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu. Tasnifu hiyo inahusu uwezo wa tabaka jembamba linalojipanga lenyewe la aside ya anakadi itokanayo na kioevu cha maganda ya kokwa za korosho kama njia ya mpako wa kuzuia kutu.

Mh. Magufuli alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Fulgence Kazaura akiwa mmoja wa wanafunzi 19 wa shahada hiyo. Mbali na hao katika mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo wanafunzi wengine 4,331 walitunukiwa vyeti, stashahada na shahada mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza akitambuliwa kama Dr. Magufuli alisema kuwa baada ya kufanya utafiti huo, maganda ya korosho badala ya kutupwa kama zamani kwa kuonekana kama takataka sasa yatatumika katika kuzuia kutu. Alisema kuwa kutu ni tatizo linalokumba dunia na kuongeza kuwa nchi ya Marekani huingia gharama za dola milioni 100 kwa ajili ya kuzuia kutu. Eeh kweli penye nia pana njia , hongera Dr.PJM.(habari/picha -Daily News)

Chanzo
MIRINDIMO: November 2009
Hizo alishusha kwa kutumia lugha ipi ki TZ au ki UK tujuze mkuu
 
PhD hewa
 
Sifahamu Mkuu, naomba elimu kidogo.

Defence ya PhD inakuwa oral, not recorded, wahudhuriaji mara nyingi ni internal and external examiners na supervisors wako tu, incase unaingia inapaswa uwe na invitation na iwe imekuwa processed na restricted
 
Asante "kilichochako"
Kumbe university zinatofautiana. University nyingine examiners wanauliza uliyoandika na ni public presentation.
 
Sijui ni mawazo yangu au ni generalization inaonekana jamaa anampenda mama kuliko wife...
Siyo mke tu mkuu,kama mama alitimiza majukumu yake kwa mwanae accordingly hakuna mtu yeyote atakayekuwa bora kwa mtoto huyo kuliko mama,kama wewe ni mwanaume halafu unatuambia eti mke wako ni bora kulikp mamaako inawezekana mama hakutimiza wajibu wake kwako,au inawezekana umeamua kutoka kinafiki,vinginevyo unahitaji kuchekiwa akili,hata mkeo au mumeo akikwambia wewe ni bora kuliko mamaake kuna uwezekano mkubwa kwamba anakuongopea,ni kweli mke ana nafasi yake na tunawapenda sana wake zetu but to be frank NOTHING COMPARES TO MAMA.
 
Kichwa cha habari kulikuwa kiwe
Siku ambayo Rais Magufuli alinunua PHD yake akiwa waziri
 
mimi nimependa kipande hiki...

baada ya kufanya utafiti kuandika na kufanikiwa kuitetea tasnifu (thesis) inayohusu matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu. Tasnifu hiyo inahusu uwezo wa tabaka jembamba linalojipanga lenyewe la aside ya anakadi itokanayo na kioevu cha maganda ya kokwa za korosho kama njia ya mpako wa kuzuia kutu.
 
Back
Top Bottom