Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,067
- 32,216
PICHA KUTOKA GAZETI LA MAMBO LEO LA MWAKA WA 1934 WATAZAME MANGI WALIOPAMBANA NA RAJABU KIRAMA - MANGI NGILISHO NA SHANGALI
Katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama Mangi wa Kibosho Ngilisho Sina alimwandikia barua kali Mzee Rajabu kuhusu msikiti aliokuwa anataka kujenga Kibosho.
Nakuwekea hapo chini maelezo ya kisa hicho kama nilivyokiandika katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama na picha ya Mangi Ngilisho (wa pili kutoka kulia safu ya mbele) akiwa na machifu wengine wa Uchaggani:
''Juu ya haya yote msikiti ulijengwa na kwa mara ya kwanza Machame Nkuu pakawa panaadhiniwa mara tano kila siku kuwaita Waislamu kwenye sala mara tano kwa kutwa.
Halikadhalika kengele ikawa inapigwa kanisani ambayo kwa takriban miaka mia moja ilikuwa inasikika kote kijijini hapo.
Pale Machame kwa Mangi kutoa amri ya kuvunjwa kwa misikiti lilikuwa jambo la kawaida na kadri Wachagga walivyozidi kusilimu na kuwa Waislamu, matukio ya kuvunjwa misikiti iliyokuwa inajengwa ikawa kitu cha kawaida.
Kufikia mwaka wa 1945 Kibosho kulikuwa na jumla ya Waislamu 500 na hawa Waislamu walihitaji kuwa na msikiti kwa ajili ya sala na pia kama sehemu ya madrasa kutoa elimu kwa watoto wao. Ikasadifu pia hapo Kibosho kuwa Waislamu walikuwa katika kipindi hicho wakivunja mawe kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Waislamu hawa walijenga msikiti lakini Mangi Ngilisho Sina wa Kibosho alitoa amri msikiti uvunjwe.
Mzee Rajabu akiwa ameongozana na wazee 18 kutoka Kibosho walikwenda kuonana na Mangi Ngilisho Sina kwa ajili ya shauri la kiwanja cha msikiti maombi ambayo yalipelekwa siku nyingi lakini majibu hayakutoka.
Mzee Rajabu ikawa sasa anarudi nyuma kwenye historia yake na ujenzi wa msikiti wake wa Machame mwaka wa 1930 ulioibua uhasama mkubwa baina yake na Mangi Abdieli Shangali (safu ya mbele wa tatu kutoka kushoto).
Kama alivyokuwa anamfahamu Chifu Abdieli Shangali ni hivyo hivyo ndivyo walivyokuwa anafahamiana na Mangi Ngilisho Sina.
Mzee Rajabu alikuwa kalelewa Kibosho ndani ya nyumba ya Mangi Sina pamoja na mtoto wa Mangi Sina, Ngilisho Sina.
Hii ilikuwa baada ya baba yake Muro Mboyo kwenda uhamishoni Old Moshi kama ilivyokwishaelezwa huko nyuma na mama yake kurudi kwao Kibosho kwa wazazi wake na kwa Mangi Sina.
Rajabu Ibrahim Kirama na Mangi Ngilisho Sina walikuwa wamelelewa ndani ya nyumba moja.
Wakibosho wakimfahamu kama Rajabu Ibrahim Kirama kwa majina yake ya udogoni ya Kirama Muro lakini sasa amewatokea akiwa Rajabu Ibrahim Kirama na yale mavazi waliyozoea kumuona akivaa udogoni hakuwanayo tena.
Amewatokea akiwa kavaa kama Mswahili kavaa kanzu na kapiga kilemba.
Lakini ingawa alisharudi kwao Machame kwa baba yake miaka mingi lakini ile lafudhi ya Kikibosho haikumtoka.
Mzee Rajabu aliweza kuyatupilia mbali yale mavazi yake ya zamani ya kawaida yaliyokuwa yanavaliwa na takriban kila mtu lakini lafudhi ya Kikibosho ilikuwa imemganda na kama humjui utasema huyu ni Mkibosho.
Mangi Ngilisho alikuwa ameshalitolea uamuzi mapema suala la kujenga msikiti.
Katika barua kali iliyoandikwa kwa hati ya mkono na kuambatanishwa na karatasi iliyokuwa na majina hayo 18 yameandikwa maneno haya yakieleza msimamo wa Mangi Ngilisho Sina:
“Waissiramu walio Kibosho ni 500 waliyokwenda kwa mangi kutaka mahali pakujenga mussikiti walipomuuliza Mangi wao amesema hamwezi kupata hata mkifika kwa District Officer [Afisa Mtendaji wa Wilaya] Moshi na Arusha kwa pissii hamuwezi kupata maana mimi Mangi Ngilisho c/s Sina nimeweka sahihi mbele ya Bwana pissii Arusha wakati nilipovunja mussikiti ule wa kwanza ndipo nilipoweka sahihi kama katika nchi yangu ya Kibosho sitakubali kujenga mussikiti haya ndiyo majibu Mangi aliyowajibu wazee waliopelekwa na jamiaya waissiram wa Kibosho wazee waliyokwenda majina yao ni haya...”
(Taarifa haina jina la mwandishi iliyoandikwa kwa hati ya mkono katika karatasi mbili moja ni taarifa na karatasi ya pili ina majina ya wazee 18 tarehe 1 Novemba, 1945: Mhamed bin Makwini, Sofiani bin Ngelechi, Ali bin Nangeda, Hassani bin Kisamu, Salim bin Choloi, Abubakali bin Tira, Abudian bin Ngelechi, Hamissi bin Mchomba, Salim bin Urawe, Rashidi bin Maimbi, Ali bin Mzuli, Rashidi bin Ngowiya, Salehe bin Mangale, Omali bin Mkenya, Ali bin Tuta, Hassana nin Mangale, Asumani bin Mbonika, Ramazani bin Mota. Angalia barua ya tarehe 5 Novemba, 1945 kutoka kwa Rajabu Kirama, Jamiatu Islam, Machame kwa Sulemani Rajabu inayoeleza kuwa alikwenda na wenzake kwa Mangi tarehe 27 Oktoba, 1945 kusadikisha kuwa Kibosho kuna Waislamu 500 ambao hawana msikiti kwa hiyo apatiwe kiwanja cha kujenga msikiti). Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama).