Pre GE2025 Peter Kibatala: Nitawaalika Mabalozi na Jumuiya za Kidiplomasia kwenye Kesi ya Lissu Aprili 24, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani wewe mwenzetu ujaona bado US Aid hadi mabango ya ofisi huko marekani Elon Musk keshayatoa.

Sasa hivi US itatumia soft powers zipi Tanzania. IMF and WB hazipo directly chini ya serikali zao.

CDM ijifunze kupambana vita yake sio kukimbilia viongozi wa dini, mabalozi, kulaumu Simba na Yanga etc.

Sasa sijasema mahakamani Lissu asitendewe haki.

..CCM nao wajifunze kupambana vita vyao wenyewe na sio kukimbilia kwa jeshi la Polisi, na kuzitumia vibaya mahakama.
 
..CCM nao wajifunze kupambana vita vyao wenyewe na sio kukimbilia kwa jeshi la Polisi, na kuzitumia vibaya mahakama.
Tatizo labda ni overlapping (maana kuna kwa ukweli fulani hapo).

Lakini aiondoi uhalisia saa zingine viongozi wa CDM wanavunja sheria na malalamiko kwa jeshi la polisi yanakuwa generalised tu.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Halafu ata wakienda watasaidia nini.

Donald Trump ameshakata mirija ya nyonyo Tanzania.

Nchi kama US hana tena tools za kutumia ‘soft powers’ Tanzania ku-influence government behaviour.

Sisemi huko mahakamani haki isitendeke, ila hao wazungu wenu hawana kitu cha kuitishia nacho serikali tena kama misaada washakata tayari.
mnapenda sana misaada
 
Sijui kuhusu uhaini hiyo charge kama too dramatic kwa wafungua mashtaka.

Lakini maneno ya uchochezi Lissu amekuwa akiyarudia mara kwa mara kwenye majukwa.

Mengine ni quality ya prosecutor na defence team ya Lissu; kwenye mizania ya mahakama.
Ni kweli, ni maneno ya uchochezi,na sheria hizo zimetungwa ili kuwa kinga kwa chama kilichoko madarakani. Sio maneno ya uchochezi kama uchochezi, bali ni maneno ya kinga dhidi ya wenye madaraka, ambayo huyapata kwa njia chafu.
 
Halafu ata wakienda watasaidia nini.

Donald Trump ameshakata mirija ya nyonyo Tanzania.

Nchi kama US hana tena tools za kutumia ‘soft powers’ Tanzania ku-influence government behaviour.

Sisemi huko mahakamani haki isitendeke, ila hao wazungu wenu hawana kitu cha kuitishia nacho serikali tena kama misaada washakata tayari.
Sijui unazungumzia wazungu gani wewe. World Bank, IMF, vyote ni mali zao. Hata vibengwe wa EU na vi-nchi choka kama Lithuania viongozi wa CCM wanaviabudu; wakijuwa bila mchango wao kwenye Bajeti yetu, hata wizi wa hao CCM wa tozo zetu utakuwa mashakani!
 
Tatizo labda ni overlapping (maana kuna kwa ukweli fulani hapo).

Lakini aiondoi uhalisia saa zingine viongozi wa CDM wanavunja sheria na malalamiko kwa jeshi la polisi yanakuwa generalised tu.

..kinachotokea ni Ccm kuvunja haki za Chadema, halafu Chadema wakizidai, wanashtakiwa kwa kuvunja sheria.

..Mfano mzuri ni jinsi Ccm walivyowanyima fomu za kiapo mawakala wa Chadema na kusababisha maandamano.

..Wakati Polisi wakizima maandamano hayo, mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Dsm akauwawa. Baada ya hapo serikali ikawashtaki Chadema.

..Hata hii kesi inayomkabili Tundu Lissu, chanzo chake ni malalamiko ya Chadema kuhusu kudhulumiwa haki zao wakati wa uchaguzi.
 
Ni kweli, ni maneno ya uchochezi,na sheria hizo zimetungwa ili kuwa kinga kwa chama kilichoko madarakani. Sio maneno ya uchochezi kama uchochezi, bali ni maneno ya kinga dhidi ya wenye madaraka, ambayo huyapata kwa njia chafu.
Cha msingi katika kulalamika kwakwe kuhamasisha vurugu sheria inatafsiri huo ni uchochezi.

Kazi kwake huko mbeleni achague maneno yake kwa makini au kila siku atajikuta yupo lupango.
 
Lakini aiondoi uhalisia saa zingine viongozi wa CDM wanavunja sheria na malalamiko kwa jeshi la polisi yanakuwa generalised tu.
Sheria zipi zimevunjwa? Polisi ndio sasa wamekuwa mahakama? Polisi wanatunga sheria na kuzi-'enforce' wenyewe?
Ni mara ngapi polisi wametumia nguvu tu na kubambikia watu kesi; kama inavyofanya serikali yenyewe sasa!
Ni mara ngapi serikali imekanyaga Katiba yenyewe na siyo sheria tu?

Kuwa kwenye madaraka hakuidhinishi kukiuka sheria zilizopo ili kulinda maslahi ya viongozi serikalini.
 
Jaribio lolote la kutomfikisha Mahakamani Antipas Tundu Lissu Mughwai tarehe 24 Aprili 2025 litakutana na upinzani mkali wa kisheria. Tunaamini kuwa wale walio na dhamana hawatajishughulisha na mipango ya kipuuzi ya aina hiyo.

Tunataka Antipas Tundu Lissu Mughwai ashtakiwe hadharani kabisa; aibu iwabebe wanaostahili. Bila shaka tunafahamu upande upi utabeba mzigo huo. Kama kawaida, muda ndio mwamuzi wa mwisho.

Kesho, tarehe 22 Aprili 2025, nitaandika rasmi kwa Mabalozi wa Jumuiya ya Kidiplomasia waliopo Tanzania, nikiwaalika maafisa wao kuhudhuria kesi ya Bw. Lissu iliyopangwa, ili wajionee kwa macho yao jinsi haki inavyotendeka nchini Tanzania.

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Aidha, nitaandika kwa Viongozi Wakuu wa Madhehebu Makuu ya Dini, nikiwaalika pia kuhudhuria na kushuhudia kinachofanyika kwa jina la Taifa.

Kesi hii ina athari za Kitaifa na Kimataifa; na tunahitaji uwazi wa hali ya juu.

Tunataka Dunia nzima ijionee jinsi Jeshi la Polisi la Tanzania litakavyoshughulikia haki ya Kikatiba ya Umma kuhudhuria mashauri ya jinai ya aina hii yenye uzito mkubwa; na wajifunze kwa dhahiri maana halisi ya kosa la uhaini.

Jaribio lolote la kutomfikisha Mahakamani Antipas Tundu Lissu Mughwai on 24th April 2025 will be met with stiff legal resistance;We trust that those responsible will not partake in any such hare-brained schemes.

We want Antipas Tundu Lissu Mughwai to be tried in full Public view; let the burden of shame be carried by the deserving side, of course we know which side that will be. Time is,as always,the final victor.

Tomorrow, 22nd April 2025, I will officially write to the Embassies of the Diplomatic Corp in Tanzania;inviting their Officers to attend Mr. Lissu's scheduled case,and witness Tanzanian Justice at play.

I will also write to the Heads of all major religious denominations:similarly inviting them to witness what is being done in the name of the Nation.

The case has intra-National, and International implications;and we require complete apparency.

We wish the whole World to witness how the Tanzania Police Force will be dealing with the statutory right of the Public to attend such momentous criminal proceedings;and learn for themselves what Treason actually entails.
Freedom is coming.🇹🇿
#freetunduLissu
#noreformsnoelection
 
Sijui unazungumzia wazungu gani wewe. World Bank, IMF, vyote ni mali zao. Hata vibengwe wa EU na vi-nchi choka kama Lithuania viongozi wa CCM wanaviabudu; wakijuwa bila mchango wao kwenye Bajeti yetu, hata wizi wa hao CCM wa tozo zetu utakuwa mashakani!
Ina maana uamini TRA wakikwambia mapato yameongezeka na budget kila mwaka deficit inayohitaji donors contribution inapungua.

Si unamsikilizaga Mwigulu au? Halafu ata hela zenyewe wazungu wanazo ahidi uwa awatoi zote na nchi inadunda tu.

Serikali ya Tanzania inajifunza kujitegemea, CDM nao waanze kufuata hiyo njia sio kulilia wazungu katika changamoto zao. Ukiwa tegemezi unadumaza akili kuwa bunifu uwezo ambao upo ndani ya ubongo tayari sema autumiki.
 
Tatizo labda ni overlapping (maana kuna kwa ukweli fulani hapo).

Lakini aiondoi uhalisia saa zingine viongozi wa CDM wanavunja sheria na malalamiko kwa jeshi la polisi yanakuwa generalised tu.

..wakati mwingine tuangalie madhara ya Ccm kulazimisha mambo yao wakitumia Polisi.

..wakati wa kutengeneza kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe kuna ex-commando alikamatwa na hajulikani alipo mpaka leo.

..Ccm kulazimisha kuwanyima fomu Chadema, kulikopelekea maandamano, ndio chanzo cha kifo cha Aquilina Akwilini.

..Kuna watu wengi sana wasingeathirika kama HAKI ingekuwa inatendeka kwa wadau wote wa siasa za Tanzania.
 
Back
Top Bottom