RIGHT MARKER
Member
- Apr 30, 2018
- 99
- 360
📖Mhadhara (68)✍️
Katika mizunguko yangu ya leo tarehe 27/11/2024, majira ya saa 14:20 nilifika kwenye duka la nguo la dada mmoja mwenye umri kati ya miaka 30 - 40. Wakati nachagua nguo dada huyo akiwa na mwenzake walikuwa wanazungumza jambo. Kwenye mazungumzo yao dada mwenye duka anamshauri mwenzake kama ifuatavyo-
(NANUKUU): "......... Kubali jina lako lililopo kwenye NIDA hata kama limekosewa ili kuepuka mchakato mrefu wa kurekebisha jina kwenye ofisi ya NIDA. Mimi nilitaka kukosa haki zangu kwasababu jina moja kwenye NIDA limekosewa, na nilipowaomba NIDA wanirekebishie jina nilitajiwa hela kubwa ambayo ilinishinda kutoa. Hivyo niliamua kulikubali jina (ambalo sio sahihi) lililopo kwenye NIDA ili niweze kupewa haki zangu......".(MWISHO WA KUNUKUU).
Baada ya kusikiliza mazungumzo ya hao wadada wawili nilipata picha kuwa pengine kuna watu wengine wengi wanakosa haki zao sehemu mbalimbali kwasababu ya majina yao ya kwenye NIDA kukosewa, na wanapohitaji kurekebisha majina yao mlolongo (kwenye ofisi za NIDA) unakuwa ni mrefu sana ikiwemo kuombwa hela.
Mbali na hao wadada, kwa upande wangu nakiri kwamba kuna watu majina yao hayako sawa kwenye vitambulisho vyao vya NIDA. Wengine majina yao ya kwenye NIDA yamepishana na vyeti vyao (vilivyotangulia) vya shule, ndoa, kuzaliwa, n.k.
Pengine ni makosa ya kibinaadam kwa wananchi wenyewe au mawakala wa NIDA wakati wa kujiandikisha, lakini ni vyema mamlaka husika (NIDA, UHAMIAJI, N.K) kuitazama hii changamoto kwa jicho la tatu - ama kwa kuweka utaratibu wa haraka/rahisi au kuondoa vikwazo pindi watu wanapohitaji kurekebisha majina yao.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM