Pemba sasa si Shwari tena: Vifaru vimeanza kuranda maeneo ya mji wa Chake Chake Pemba

usijali mkuu , wanasema ukiona giza totoro uje karibia kunakucha .
Sijui nini kimetokea mimi ni mwanaume ila machozi yameishia kunitoka
Nimejikuta naangalia documentaries
Ghost of Rwanda
Darfur now
The story of blood diamonds

Mungu akasimame na Zanzibar
 
Safari hii Tanzania itatokea maajabu haijawahi tokea duniani. Tusubiri. Hata hizo karatasi za utambulishi wagombea wamezi"print" kimakosa. Nafikiri mumeziona. Majina ya wagombea yameandikwa tafauti na 2015 na nambo ya chama fulani imebadlika pia. hahhaha kazi ipo kwa ccm.
 
Magufuli kazi anayo. Siasa za Zanzibar zina histoty ndefu, CCM ikubali kuachia nguvu fulani nayo ni kumpa Maalim umakamu wa Urais na CUF nayo ikubali kupokea nafasi hiyo. wakae meza ya mazungumzo ya muafaka kuokoa hali isije kuwa mbaya zaidi dalili za mvua ni mawingu. CUF ikumbuke wao wameshika makali ya kisu na CCM Imeshika mpini. wakivutana zaidi raia ndio watakao kuwa kafara wa hali yoyote itakayojitokeza.. haya ni maoni tu
 
Ndugu hata jogoo alikuwa yai usione anawika hivyo dakika ikifika hakuna kisichotekelezeka
Miaka yote hii licha misuko suko tuliyopitia Mungu alitupitisha salama ,Na imani tu na hili tutapita salama ,inaumiza sana kupeleka jeshi la wananchi wa Tanzania kupambana na raia wake
 
Mbona Mtwara vilienda wakati wa masuala ya gesi!
Yote hayo matumizi yasiyo na maana ya kutumia Jeshi la wananchi wa Tanzania kupiga raia wake ,Jeshi la polisi limechafuliwa na wanasiasa sasa chuki hizo wanazipeleka JWTZ ,
Naimani Mwl Nyerere angekua hai kamwe hili la JWTZ asingekubali
 
Yote hayo matumizi yasiyo na maana ya kutumia Jeshi la wananchi wa Tanzania kupiga raia wake ,Jeshi la polisi limechafuliwa na wanasiasa sasa chuki hizo wanazipeleka JWTZ ,
Kwahiyo haukuwa sahihi uliposema kuwa haukutegemea kuwa TZ tutafika huku, kwani tukio kama hili lilifanyika Mtwara!
 
Hawajiamini ndio maana wameleta vitoi vyao, acha watu wavizoee ipo siku yatageuka, na ivi madereva wote walevi.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
ndiyo maana mliambiwa mtu akileta fyokofyoko atakumbuna na nguvu kubwa sana ya dola.
 
Magufuli kazi anayo. Siasa za Zanzibar zina histoty ndefu, CCM ikubali kuachia nguvu fulani nayo ni kumpa Maalim umakamu wa Urais na CUF nayo ikubali kupokea nafasi hiyo. wakae meza ya mazungumzo ya muafaka kuokoa hali isije kuwa mbaya zaidi dalili za mvua ni mawingu. CUF ikumbuke wao wameshika makali ya kisu na CCM Imeshika mpini. wakivutana zaidi raia ndio watakao kuwa kafara wa hali yoyote itakayojitokeza.. haya ni maoni tu
Kukaa mezani kila siku kisha kuwapa CUF umakamu? Kwa nini ccm wao wasipewe huo umakamu? Mungu hakuiumba Zanzibar ili iwe ya ccm pekee
 
Magufuli naye amejiunga na slogan ile ile ya wanaccm wenzake kuwa Zanzibar kamwe haitakuja kutolewa kwa vikaratasi vya kupigia kura.

Magufuli huyo huyo ameikana Zanzibar kuwa mambo ya huko hayamuhusu na wala hatayaingilia.

Sasa inakuwaje kwa mambo ya nchi nyingine ambayo hayamuhusu halafu yeye kama Amiri Jeshi Mkuu anapeleka vifaa vya kivita kwa ajili ya kuwanyamazisha watu wote wanaoleta fyoko fyoko huko nchi jirani ya Zenji?!
 
Halafu anatokea mtu anasema yeye ni mzalendo sana,eti Nassari asipumbazwe na maVyama wakati yeye analinda liChama lake lililoshindwa uchaguzi!
 
Back
Top Bottom