Paul Makonda: Watu wa Arusha wanaweza kwenda popote kupambana, iko mikoa unakuta waganga wengi wa kienyeji. Kutambulisha polisi wa kitalii

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,663
8,795
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais Samia kumteua mkuu wa mkoa wa Arusha kuongoza wananchi wenye akili nyingi na wapambanaji wasiokata tamaa na wanaojua hatma ya nchi. Ameyasema hayo kwenye kumbukizi ya waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika mjini Arusha.

Makonda amesema mji huo ni wa wajanja wanaoweza kutoka na kwenda popote kupambana na kujenga uchumi. Makonda amesema watu wa mkoa huo wametambulisha umahiri wao katika utafutaji ilhali kuna baadhi ya mikoa waganga wa kienyeji ni wengi lakini si kwa mkoa wa Arusha.

Kwenye hatua nyingine, Makonda amesema jiji la Arusha litafungwa camera na kuhakikisha taa zinawaka na kuwa na polisi wa kitalii watakaokuwa wanaendesha baiskeli kuhakikisha ulinzi umeimarika.

Makonda: Ifike hatua watu wakija jiji la Arusha wajisikie raha na kupiga picha na polisi wao ambao ndio wanaimarisha ulinzi katika jiji la Arusha.

Pia tumekubaliana kuondoa mabango yote yanayochafua sura ya jiji la Arusha na kuhakikisha tunakuwa na muonekano mzuri ili watalii watakapokuja wasione kama watu tusioweza kujipanga, tunatembelea miji yao tunaona namna ilivyo.

Pia Makonda amemuomba Rais Samia kilomita 20 za barabara za lami kwani katika ya mji wa Arusha kuna barabaraba mbovu, amedai kuwa wananchi wa mkoa huo wamemtuma akamuombe 'mama yake' barabara na wanampima kama ni mama yake kweli.

PIA, SOMA:

Uteuzi wa Ukuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
 
Ameenda na gundu huko arusha
Wa Rufiji naye? Vipi hanang alienda pia?

Mwache Mungu akupeni ujumbe wake wajinga nyiyi

Mafriko ya rufiji badala ya kusema ni hali tu inayoweza kutokea popote, nyinyi mkaenda mbali sana kusonya mradi wetu wa umeme

Je Arusha nako kuna JKNHP?

Jinga sana
 
Mjinga mwenyewe. Kwenda huko kama imekuuma si uitoe
 
Pia tumekubaliana kuondoa mabango yote yanayochafua sura ya jiji la Arusha na kuhakikisha tunakuwa na muonekano mzuri ili watalii watakapokuja wasione kama watu tusioweza kujipanga, tunatembelea miji yao tunaona namna ilivyo.
Kuna mabango ya kusifiasifia kindezi yako ile barabara mpya ya Tengeru-Sakina, yanatia kinyaa sana.
 
Anaongelea kolomije?
Mkoa unaoongoza kwa wachawi na waganga wa kienyeji ni huko anakotoka yeye. Nakumbuka lile jopo la waganga 900 toka kijiji cha Gamboshi walioapa kupamshughulikia yoyote atakayempinga Magufuli.
 
Hana akili huyooo ati atawataja wanaomtukana mama kwenye mitandao ????? Huyu alisoma wapi jamani . Hajui hata uteuzi wa maneno hajui anapuyanga tuu
Tumia lugha ya staha Mkuu, kwanza habari iliyopo ni nzuri we unaingiza jambo ambalo halipo... be positive mkuu au ndo wewe unaetukana ndomana unaogopa kutajwa?
 
Pia tumekubaliana kuondoa mabango yote yanayochafua sura ya jiji la Arusha na kuhakikisha tunakuwa na muonekano mzuri ili watalii watakapokuja wasione kama watu tusioweza kujipanga, tunatembelea miji yao tunaona namna ilivyo.
Kati ya mabango hayo ni yale yenye picha ya Samia, yaondolewe mapema!
 
Ila ni kweli kuna mikoa ukienda nchi hii Waganga wa kienyeji ni wengi sana πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„,uswahili kibao
 
Ni kweli kuna mikoa yenye waganga wengi wa kienyeji: Geita, Shinyanga, Simiyu, n.k.
 
Sifa yake kubwa ya kuwa karibu na JPM ni kumpeleka kwa wagangq, JPM kipindi kile alikuwa hakauki chato japo ni Rais, jioni anawasha mashine kwenda kibirizi, asubuhi asharudi, hata SSH anajaribu kumsogelea amuonyeshe waganga. Ila SSH mjanja, halishwi kasa hivi hivi, ukimpa neno hili, analihakiki kwa huyu na yule.

Waganga ndio walifanya JPM ajikute peke yake na makonda. Wakienda kupiga ramli, Makonda anakuwa kashampanga mganga, na kumpa maadui ambao JPM aone ni wa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…